Wednesday, December 23, 2015

WAZIRI KITWANGA ATANGAZA OPERESHENI YA KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI

uh1

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uh2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uh3
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za  Kusafiria,  Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uh4
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uh5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
uh6
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uh7
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.  Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: