Saturday, December 19, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA MITAMBO YA GESI YA TEGETA JIJINI DAR.

Majira ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo alifika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi iliyoko  Tegeta jijini Dar es Salaam inachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo. 

Waziri Muhongo amekagua  mitambo jana  na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.
 
Pia Muhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na nishati hiyo  hapa nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri huyo kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mitambo hiyo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mitambo hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo jana jijini Dar es Salaam.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZIBLOG

No comments: