Tuesday, September 30, 2014

Shirika la Nyumba la Taifa lakabidhi mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana Kigoma

 Meneja wa Mkoa NHC, Nistas Mvungi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mashine 32 za kufyatulia matofali ya kufungamana.
  
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji akishukuru Shirika kwa kuwapatia vijana mashine ya hydraform.
  
Wafanyakazi wa NHC na kikundi cha Vijana Kwanza Group  na wageni waalikwa wakisubiria Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Kigoma Ndg Nistas Mvungi akijadiliana na Mkuu wa Mkoa Mhe Issa Machibya jambo kuhusiana na Mashine ya matofali ya kufungamana kuhusu ufanisi wake na ajira kwa vijana.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Shirika Mkoa wa Kigoma na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Ndg. Nistas Mvungi akihutubia wananchi wa Kigoma kuhusu mradi wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana 32 zilizotolewa na Shirika kwa vikundi vya  vijana wa Mkoa wa Kigoma
 Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akikabidhi mashine za kufungamana kwa Kikundi cha Vijana Kwanza Group. Mwenyekiti wa kikundi Ndg Daniel George  na Katibu wake wakipokea mashine.

  
Picha ya pamoja ya kikundi cha vijana kwanza group na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa. 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno kwa makini kuhusiana na maelekezo yake kuhusu umuhimu wa kutumia matofali ya kufungamana na kuondokana na nyumba za matope.


ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA LEO (KESHO JUMATANO) MLIMANI CITY

expo_011
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said vMeck Sadick (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es jana juu ya kufanyika kwa maonyesho ya utalii yanayoratibiwa na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Picha: MPIGAPICHA WETU
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.
Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.
Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.
Wadhamini wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.
Pamoja na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.
Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.
Usafiri wa ardhini  utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.
Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th FloorMedia kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.
Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano.Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.
‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

USHIRIKIANO WA OMAN, ZANZIBAR UTAENDELEA KUKUA

11 064 -2
Mhe. Said Ali Mbarouk akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Habari nchini Oman Sheikh Dk. abdulla  wakati  alipofanya mazungumzo katika ofisi yake tarehe 29 Septemba 2014 akiwa katika ziara rasmi ya siku nne kutembelea sekta mbali mbali za Utalii, Utamaduni na Michezo.
MUSCAT, OMAN        30/09/2014
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk ameuelezea ushirikiano baina ya Oman na Zanzibar kuwa daima utakuwepo na utaendelea kukua kutokana na kutanuka kwa maeneo mapya ya ushirikiano katika Nyanja mbali mbali za maendeleo.
Amesema ni jambo la faraja kuona kuwa hivi sasa Zanzibar na Oman zinatambua umuhimu wa kutanua maeneo hayo ya ushirikiano katika sekta za uchumi, utalii na michezo kwa lengo la  kuwanufaisha watu wa pande zote mbili.
Mhe. Saidi Ali Mbarouk ameyaeleza hayo katika nyakati tofauti wakati alipokuwa na mazungumzo na Mawaziri  wa sekta za Habari, Michezo, Utamaduni na Utalii mjini Muscat Oman leo, akiwa katika ziara yake ya siku nne ya kukutana na viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa lengo la kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Mapema akizungumza na Waziri wa Habari wa Oman, Sheikh Dk. Abdulla Monaim Bin Mansoor Al Husani, alitoa shukrani zake kwa Serikali ya Oman kwa misaada yake kwa Zanzibar na kusifu nidhamu   ya vyombo vya habari vya nchi hiyo katika kuwaunganisha watu na kuwawezesha kujenga uchumi imara.
Alisema hatua hii ya  mfano wa kuigwa inatokana na usimamizi  madhubuti  kwa vyombo vya habari na kujali kuwajibika kwa jamii kwa vile vinatoa nafasi ya kuwapatia taarifa za kutosha juu ya harakati za kujiendeleza na kujenga ustawi na maendeleo   yao.
Ameshauri haja ya kuwepo na utaratibu wa kubadilishana wataalamu na vipindi ili kila nchi iweze kujifunza kutoka upande mwengine kwa  kutambua maendeleo yanayofikiwa na kila upande na hivyo kutoa fursa za kuwawezesha vijana na vyombo vya habari kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa pamoja hasa kwa vile ni tegemeo kubwa la taifa katika kujenga uchumi.
Katika ziara yake hiyo ya siku nne, Mheshimiwa Saidi Ali Mbarouk pia alipata fursa ya kubadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Utamaduni na Mambo ya Kale, Sheikh Hamad Hilal Al Maamari na Waziri wa Michezo, Sheikh Shallal Saad Moh’d Al Saad na kutuwama zaidi katika masuala ya kubadilishana wataalamu wa michezo na kuyahuisha majengo ya kihistoria yenye mnasaba na Oman.
Wakati huo huo,  Mhe. Said Ali Mbarouk ameitaka Oman kufungua fursa nyengine kwa kuisaidia Zanzibar katika kuanzisha Hoteli za kitalii za Halal utaratibu ambao Oman tayari imeuanzisha na kupata mafanikio yake.
Amefahamisha kuwa utaratibu wa hoteli kama hizo za Halal ni muafaka katika visiwa vya Zanzibar kwa vile zitaongeza soko la idadi ya watalii wanaohitaji kupumzika katika maeneo yenye utulivu wa maadili ya kidini na kiutamaduni.
Katika ziara yake hiyo Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alipata fursa ya kushiriki katika  karamu rasmi iliyoandaliwa kwa ajili yake  na ujumbe  wa watu watatu aliyofuatana na Mwenyeji wake Waziri wa Habari wa Oman Sheikh Dk. Abdulla Monaim iliyofanyika katika jumba la serikali la Opera mjini Muscat.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI HABARI AMELEZO ZANZIBAR 

ABDULRAHMAN KINANA NA WANA BUMBULI WATETA, DIWANI AFUKUZWA MKUTANONI NA WANANCHI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba wakati alipowasili  katika kata ya Mbuzii ambapo ameshiriki katika ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM katika kata hiyo na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kumpokea, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi mkoa wa Tanga akihimiza na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukiiarisha chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM, Kero kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kufungwa kwa kiwanda cha Chai cha Mponde ambacho wananchi wanataka warudishiwe ili wakiendeshe wenyewe ,Baada ya mwekezaji Yusuf Mulla kukiuka makubaliano ya kisheria jambo lililopelekea mmoja wa viongozi katika kata hiyo ambaye ni diwani Diwani wa Kata ya Guga Bw. Richard Mbunguni kufukuzwa mkutanoni na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa madai ya kuwasaliti katika sakata hilo, Akizungumza na wananchi katika kutano huo  Kinana ameahidi kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu akisema “Katika hili kila mtu aliyehusika abebe mzigo wake kwa kuwajibika” , ameahidi kurudi Mponde baada ya mwezi mmoja ili kuwapatia majibu sahihi wananchi yatakayomaliza kabisa mgogoro huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUMBULI -LUSHOTO)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba alipokuwa akizungumza na jambo wakati alipowasili  katika kata ya Mbuzii.3Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba  akizungumza na wanapiga kura wake wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaalipowasili  katika kata ya Mbuzii.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Mbuzii wakati  akiwa katika ziara ya kikazi katikajimbo la Bumbuli, Kulia anayeangalia ni Mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza na vijana wa kikundi cha Bodaboda cha Dule B wakati alipozindua tawi lao na kukabidhi pikipiki iliyotolewa kwa kikundi hicho na mbunge wa jimbo hilo Mh. Januari Makamba katikaki pichani na kushoto ni  Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikabidhi fungua za pikipiki kwa kiongozi wa kikundi cha Dule B Bw.Nuru ambayo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza na wanakikundi cha Maisha Plus wakati alipotembelea kikundi hicho.8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kazi ya kuponda kokoto wakati alipotembelea kikundi cha Maisha Plus ambacho hii ni moja ya kazi zinazofanywa na kikundi hicho.9Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi akishiriki kazi ya kufyatua matofari huku mbunge wa jimbo hilo Mh. Januari Makamba akishuhudia wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Plus.10Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi akiendelea na kazi ya kufyatua matofali11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akila muwa na Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha ITV Ufoo Sari wakati alipotembelea kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Plus jimboni Bumbuli leo miwa hiyo inazalishwa na kikundi hicho.12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiranda mbao huku Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akishuhudia13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ameshiriki pia kuchoma tanuri la matofari kwa kuwasha moto katika moja ya matundu ya tanuri hilo anayeangalia ni Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba .14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akizungumza jambo na mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba15Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mponde.16Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini na Mchumi wa mkoa wa Tanga CCM akiwasalimia wananchi kwenye mkutatano wa hadhara uliofanyika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli.17Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.18Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.19Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo.20Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi.21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mponde.23Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mponde jimboni Bumbuli.24Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa. Itikadi na Uenezi Chama cha Mapinduzi CCM akimtoa katika eneo la mkutano huku akiwa amemshika mkono diwani wa Kata ya Guga Bumbuli  Bw. Richard Mbuguni kulia aliyefukuzwa na wananchi katika mkutano huo wa hadhara  kwa madai ya kuwasaliti na kushirikiana na mwekezaji .

BAADA YA SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA TECH KUFUNGWA KWA VURUGU UONGOZI WA SHULE HIYO WAWAITA WANAFUNZI 28

Mkuu  wa  shule ya  sekondari ya  Ifunda  Tech  akizungumza na  wanafunzi hao  hivi karibuni
                                     Wanafunzi  wa  shule ya  sekondari ya  Ifunda  Tech
Uongozi wa shule ya sekondari ya Ifunda tech  wilaya  Iringa  mkoani  Iringa  imewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba 2 ikiwa ni baada ya  shule  hiyo  kufungwa kwa muda  usiojulikana kutokana na  wanafunzi  hao kufanya  vurugu kubwa  hivi karibuni .
 
Hatua ya uongozi wa shule hiyo kuwaita wanafunzi hao imekuja zikiwa ni zaidi ya siku 4 kupita toka shule hiyo kufungwa kufuatia vurugu kubwa shuleni hapo na  kusababisha  hasara  kubwa ya mali  za  shule  hiyo
 
Makamu mkuu wa shule hiyo  Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake .
 
Amewataja wanafunzi wanaotakuwa kufika shuleni hapo kuwa ni steven Nyiriri,petro Kalolo, Iddi shaban, John Zephania, Edwin Rwegoshora, Adinan Mrisho Mtiti, Izengo Dotto, Gaspar Manyagi, Shemson Amoni, Halid Omari, Said Sambo, Paschal Lusukanija ,Fred Kidava na Eliji Nguvila.
 
Wengine ni Stambuli Daluweshi, Jackson Mlowe, Sidi Kayombo, Yusuph Makale, Joseph Antony, Allan Laurent, Rose Kayombo, Enoce John, Rashid Kandoro, Abdul Zumo, Petro Silwimba, Joyce Nestory, Michael Kimario na Athuman Ahamad.
 
Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.

MKUTANO WA MAAFISA WANADHIMU WA POLISI MOSHI

1 (1)Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (kushoto) akielekea kufungua mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa na Vikosi vya Polisi kote Nchini unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt.Ibrahim Msengi  na Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, Matanga Mbushi. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
3 (1)Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi wakiwa wanafuatilia hotuba ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
5Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt.Ibrahim Msengi wakati wa ufunguziwa  mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa na Vikosi vya Polisi kote Nchini unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi. Kushoto ni Kamishna wa fedha na logistiki Clodwig Mtweve.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)