DIAMOND AFUNIKA KAMPALA, UGANDA JANA

2Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani usiku wa kuamkia leo katuka Uwanja wa Lugogo Cricket Oval, Kampala, Uganda.
4 
Diamond akiimba kwa hisia.5
Madansa wa Diamond wakiendelea na makamuzi.
index 
...Akiwauliza jambo mashabiki wake wa Uganda (hawapo pichani).
9...Akicheza sambamba na madansa wake.rr 
...Akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
uuDiamond akiwa amesimama na madansa wake baada ya shoo.
USIKU wa kuamkia leo katika Uwanja wa Cricket wa Lugogo, Uganda, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' alifunika kwa kupiga shoo kubwa na ya kihistoria. Diamond aliyekuwa ameongoza na madensa wake, muda mwingi aliwakosha mashabiki hao kwa kuwapigia nyimbo zake zote kali zinazotamba kama vile Kesho, Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyingine kibao. Baada ya kufunika shoo hiyo.

 Diamond atarejea jijini na moja kwa moja kujiandaa na shoo nyingine kubwa na ya kihistoria itakayofanyika Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live, Diamond atapiga live kwa kutumia vyombo nyimbo zake zote kali ikiwa ni pamoja na hii ya Utanipenda ambayo ni habari ya mjini kwa sasa. Mbali na Diamond katika shoo hiyo pia atakuwepo mkali wa nyimbo za Singeli, Msagasumu ambaye tagonga nyimbo zake zote kali zinazobamba kama vile Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Naipenda Simba na nyingine nyingi. 

Baada ya Msagasumu, Mashabiki pia wataburudika na shoo kutoka kwa wakali wa kucheza nyimbo Afrika Mashariki, Wakali Dancers ambapo watakinukisha mwanzo mwisho kwa kutoa burudani ya kucheza ngoma zote zinazobamba ndani na nje ya nchi kwa staili za kipekee. Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Comments