Thursday, November 29, 2007

Shule ni nini????

Moja jumlisha moja = 3, nimepatia au ??? hebu cheki vitegemezi vinavyofunzwa shule ya awali halafu ucheki wengine hawa wakubwa wanavyofunzwa madarasani, picha hii imetolewa na mdau, wadau wengine mna maswali. Wengine wanasema shule ni sehemu wanayofeli watu, wengine wanadai shule ni sehemu ambayo bongo za watu zinanolewa, hebu nipe definition yako.

Mv Kigamboni


Huu mzaha mzaha matokeo yake bila shaka siku moja tutaja yaona na kisha eti watakuja hawa viranja wetu wajidai wanatoa machozi ya simba kujifanya wanaona huruma saana jamani , Kivuko hiki cha Kigamboni na kile kingine kidogo havifai kabisa kwa matumizi ya binaadamu wa kawaida, hebu cheki lilivyosheheni jana, mdau Salhim Shao kanirushia hii.

Tuesday, November 27, 2007

Waziri Mkuu wa Canada nomaaa

Hebu cheki hizi taarifa huyu jamaa Waziri Mkuu wa Canada aliyekuwapo jana hapa nchini kumbe ana soo, hivi karibuni
alipokuwapo huko Santiago, Chile alilazimika kuingilia mlango wa nyuma wa ofisi za kampuni ya Barrick Gold kukwepa kuzomewa.

Ilimbidi achelewe saa mbili huku akiwa chini ya ulinzi mkali uliojumuisha maboard guard, polisi na vikosi malumu, Stephen Harper (Waziri Mkuu wa Canada) aliwasili katika ofisi za Barrick Gold na akaingia kupitia mlango wa nyuma majira ya mchana akikwepa umati wa wananchi waliokuwa wakiandamana tangu saa mbili asubuhi.

Harper, anadhaniwa kufanya madudu kibao katika ziara yake hiyo ambayo amelazimika kuingia bongo akazungumza mawili matatu, lakini kwa baadhi ya madudu yake hebu mcheki hapa THE DOMINION NEWSPAPER eeee bwana noma kweli.

Question in the House on Mining and Corporate SocialResponsibility/Barrick

Gold: Thursday Nov 22nd 2007 (Hansard)

Mr. Paul Dewar (Ottawa Centre, NDP) :

Mr. Speaker, the Prime Minister is developing a habit of visiting the
offices of Barrick Gold when he travels abroad. First in Chile and now
tomorrow in Tanzania the Prime Minister will lend credibility and
promote the business interests of Barrick. This Canadian company is
operating in a most erratic way.

Why is the Prime Minister promoting the practices of Barrick Gold?

Answer
Mr. Deepak Obhrai (Parliamentary Secretary to the Minister of Foreign
Affairs, CPC) :

Mr. Speaker, the Prime Minister is in Tanzania because we have a great
relationship with that country and the promotion of Canadian businesses
working in Tanzania. As far as we are concerned, the roundtable
conference on social corporate responsibility of which the government
will be giving its response pretty soon and we are very proud of
Canadian businesses that comply with the regulations that are in Canada.

* * *

Mr. Deepak Obhrai (Parliamentary Secretary to the Minister of Foreign
Affairs, CPC) :

Mr. Speaker, the Prime Minister is always promoting Canadian businesses.

We expect all Canadian businesses to follow Canadian practices, Canadian
laws and Canadian regulations and we expect that company to do the same
thing. That is why that company participated in corporate social
responsibility and we are positive that all Canadian companies follow
the rules that have been laid down in Canada.

* * *

Duhhh ktika pita pita yangu nimekutana na huyu jamaa mtandaoni hakika amekuja na ubunifu wa ajabu ambao haujawahi kuwapo katika ulimwengu wetu wa mablogu, huyu jamaa hakika anachokifanya si cha kupuuza hata kidogo, amebuni na sasa bila shaka atavuna matunda ukitaka kumcheki unaweza kumtembelea kibandani kwake anaitwa KENNEDY eeee bwana anatisha kweli kweli kweli.

Canada backs Dar's Mining Review moveBy Pius Rugonzibwa-The Citizen
The government of Canada has assured Tanzania of a maximum support in the country’s efforts to benefit from the mining sector and it is looking forward to see Tanzania achieving this goal.

The assurance has been given by the visiting Canadian Prime Minister Mr. Stephen Harper during a press briefing he made when he addressed Journalists at the State House yesterday.

Mr Harper was responding to a question about how Canada see the initiative of Tanzania in the Mining sector and his views on the loyalty collected from Mining companied in the country. Mr. Harper was in the one day state visit in the country.

In his address, the Prime Minister added that Canada is keen to see cooperation with Tanzania growing with more initiatives in encourage more investors not only in the Mining sectors but also in other sectors like Telecommunication and energy.

“We are looking forward to extend our relationship in various sectors but as far as mining as concerning Canada is really willing to help Tanzania achieve its goals and targets in the sector,” said Mr. Harper.

Earlier President Jakaya Kikwete said that Tanzania is intending to review the Mining Law so that the country gets the required share in the sector and not posing a threat to investors. President Kikwete was answering to a question as asked by a Journalist from Canada who wanted to know the position of the Canadian companies in on going enquiries.

Saturday, November 24, 2007

Mambo si mambo Uganda


British Prince Charles chats with a local resident during his visit at a barber shop in a slum area in Kampala, Uganda, Nov 23, 2007. Prince Charles arrived here Nov. 22 for a Royal visit in Uganda. (Xinhua/pool) (hdt/lhn)
A supporter of the opposition party Forum for Democratic Change (FDC) speaks during a protest against the Commonwealth Heads of Government Meeting in Kampala, Uganda, Nov. 23, 2007. Dozens of demonstrators took part in the protest on Nov.23. (Xinhua/Hou Dongtao) (hdt/lhn)

Friday, November 23, 2007

Ripoti ya muhimbili


Duhhh limeibuka soo jingine, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii , Profesa David Mwakyusa ameitosa ripoti iliyoundwa na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) na kuunda. Picha ni ya Edwin Mujwahuzi.

Mkurugenzi wa Tanesco afuta uamuzi wake

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) amefuta uamuzi wake wa kujiuzulu baada ya kukaa na kutaf akari maauzi yake ya juzi na kwamba anarejea kazini bila ya masharti yoyote. Maamuzi haya yamethitishwa na bodi ya Tanesco. Jamani Mna maswaaliiiiii?????

Mkutano wa Jumuiya ya Madola umefunguliwa leo

Head of Commonwealth, Queen Elizabeth II take a group photo with the commonwealth Head of Government soon after she opening the meeting. Photo/ State House


Head of Commonwealth, Queen Elizabeth II take a group photo with the commonwealth Head of Government soon after she opening the meeting. Photo/ State House.British Queen Elizabeth II (R) and President of Uganda Yoweri Kaguta Museveni (L) attend the opening ceremony of the 2007 Commomwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) in Kampala, Uganda, Nov. 23, 2007. Delegates from 53 Commomwealth member states are present at the 3-day meeting. (Xinhua/Wang Ying)

Commonwealth Secretary-General Don McKinnon (standing) speaks during the opening ceremony of the 2007 Commomwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) in Kampala, Uganda, Nov. 23, 2007. Delegates from 53 Commomwealth member states are present at the 3-day meeting Photo by Xinhua.

Wakuu wa nchi 53 waanza mkutano Kampala

KAMPALA, Uganda

MKUTANO wa Viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola (Chogm) umeanza rasmi jana mjini Kampala,k ikihudhuriwa na Malkia Alizabeth II wa Uingereza na mumewe Duke wa Edinburg.
Mkutano huo wa siku tatu unaowakutanisha viongozi 53 wa nchi wanachama wa jumuia hiyo ulifunguliwa rasmi jana na Malkia Eizabeth II kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kampala.
Taairfa zinasema kuwa hata hivyo mkutano huo ambao kwa mujibu wa ratiba ulitakiwa kufunguliwa rasmi saa 3.00 asubuhi ulichelewa kuanza kwa takribani saaa nzima.
Malkia wa Uingereza Nni mkuu wa moja wka moja wa Jumuia hiyo hasa kutokna na wadhifa wake, alifika nchini Uganda juzi, pamoja na mambo mengine alweza kuhutubia Bunge la nchi hiyo.
Ni utaratibu uliozoeleka kwa Malkia kutembelea nchi mwenyeji wa mkutano huo unaowakutanisha viongozi wa nchi 53 nyingi zikiwa ni zile zilizowahi kuwa makoloni ya Uingereza kila unapofanyika mara moja kila baada ya miaka miwili.
Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Don McKinon alisema pamoja na uamuzi uliotolewa jana asubuhi juu ya Pakistan, mkutano huo unatarajiwa kutoka na majibu juu ya namna ya kuimarisha Demokrasia, Biashara ya Kimataifa, Malengo ya Milenia yanayotakiwa kufikiwa mwaka 2015 na kupata taaarifa ya uitendaji kwenye makubaliano walioyofikia katika mkutano uliopita uliofanyika mwa 2005 Visiwa vya Malta.
Pia viongozi haoo watajadili suala la Uanachama wa nchi rafiki na jirani wa Uganda, Rwanda baada ya maombi yaliyofikishwa ikiomba kuwa mwanachama, huku Rais Kagame akiwa ni miongoni mwa viongozi walioshiriki hatua za awali za maandalizi ya mkutano huo wa wakuu wa nchi.
Hata hivyo taarifa za awali zinasema pamoja na uwezekano uliopo. Suala hilo ltaweza kuthibitishwa rasmi kwenye mkutano wa mwaka 2009, baada ya suala hilo kujadiliwa kwenye mkutano huu na kufikia uamuzi.
Pia katika mktano ao huo, viongozi hao watamchagua Katibu Mkuu mpya wa Jumuia hiyo atakayemrithi Don McKinon ambaye anamaliza muda wake Machi mwaka kesho. Miongoni mwa wanaowania naffasi hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Malta Michael Frendo, Mwakilishi wa India nchini Uingereza Kamalesh Sharma na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Jumuia hiyo Mohan Kaul.

Tiba MOI:Aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa, afarikiJackson Odoyo na Andrew Msechu wa Mwananchi

EMMANUEL Mgaya (19), aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa Jumatatu wiki hii baada awali kufanyiwa wa mguu kimakosa, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), amefariki dunia jana asubuhi.


Mara baada ya Mgaya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kisha kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hadi mauti yalipomfika jana saa 2:30 asubuhi.


Awali Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na Emmanuel Didas ya kichwa badala ya mguu, Novemba mosi mwaka huu katika taasisi hiyo.


Akizunguza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu muda mfupi baada ya Mgaya kufariki dunia, mmoja wa wauguzi wa MOI, alisema hali ya mgonjwa huyo, ilianza kuwa mbaya juzi mchana. Soma MWANANCHI kwa taarifa zaidi.

Thursday, November 22, 2007

Mkurugenzi Tanesco ajiuzulu


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Dk Idriss Rashid amejiuzulu wadhifa wake jana jioni muda mfupi mara baada ya kutokea mtafaruku katika kikao cha bodi ya Shirika hilo kubwa likiwa ni suala la Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kudaiwa kuiba umeme na kutumia njia za mkato kujifaidisha, jingine ni suala la mvutano wa upandishaji gharama za umeme ambapo Mkurugenzi alivutana sana na bodi.

Dk Rashid aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu katika bodi ya shirika hilo muda mfupi baada ya kupishana kauli, taarifa hizi tayari zimethibitishwa na Televisheni ya Taifa (TvT) na Gazeti la Mtanzania.

Wednesday, November 21, 2007

mambo yanaendelea Uganda

Commonwealth Secretary General Donald Mckinnon, invited guest Rwandan President Paul Kagame, Ugandan President Yoweri Museveni and Dr Mohan Kaul, director general of the Commonwealth Business Council, attend the opening ceremony of the Commonwealth Business Forum (CBF) 2007 in Kampala, capital of Uganda, Nov. 20, 2007. The three-day forum attended by over 1000 delegates from more than 40 commonwealth member states, opened here on Tuesday. The theme of the forum is "The Commonwealth: The Untapped Potential". (Xinhua/Wang Ying) (lhn)

Tuesday, November 20, 2007

Mambo yameiva kampala


Waandishi wa habari wanao-cover Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya madola (CHOGM) wakiwa katika kituo cha habari jijini Kampala. Kituo hicho kilifunguliwa rasmi kwaajili ya waandishi wa habari kuanza kukitumia jana, waandishi wa habari takribani 1,000 kutoka kona zote za dunia wamekusanyika mjini hapo kusakanya habari za mkutano huo unaoanza Ijumaa na kumalizika Jumapili Picha ya Xinhua

Mambo ya Kusini sasa safi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alikagua barabara  ya Lindi – Kibiti hadi Mingoyo pamoja na Daraja la Mbwemkuru, wakati akitoka Lindi kwenda  Kilwa.

Kabla ya ukaguzi huo, Rais alipata taarifa ya maendeleo ya barabara hii muhimu kwa mikoa ya kusini na Daraja la Umoja (ambalo hakulikagua) kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Bw. Omar A. Chambo; ambaye amemueleza Rais kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa barabara hiyo.  Ujenzi wa barabara ambao unafanyika kwa awamu, utakamilika mwishoni mwa mwaka huu wakati Daraja la Umoja linatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwaka 2008. 

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,

20 Nov, 07.

 

Monday, November 19, 2007

Hivi wanataka Zitto ajitoe ili iweje


Inatia mashaka huu mjadala unaoendelea wa kuvutana oooh mara Zitto ajitoe , mara sijui hakutakiwa kuingia katika kamati, mara atajimaliza kisiasa, duhhh kazi kweli kweli, sasa wengine wanadai kwamba kuvurugika kwa amani ndani ya Chadema kunatokana na pesa chafu kumwagwa ndani ya Chadema ndo maana hawaelewani. Lakini swali linabakia pale pale hivi Zitto Zuberi kabwe ajitoe katika kamati kwa lipi hasa baya.

Friday, November 16, 2007

Richard yupo kwetu leoMshindi wa Big Brother House II Richard Buzenhout akiwa kijiweni kwetu leo, kwa juu yuko na Yahya Charahani wa charaz.blogspot.com na picha ya ya kati yuko na Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Theophil Makunga na chini yuko na Mkurugenzi wa Mwananchi Communications Sam Sollei. Wote kwa pamoja tumefurahishwa sana na ushindi wake. Picha kwa hisani ya mdau Erick KalungaMdau Mrocky Mrocky katika pozi na Richard

Thursday, November 15, 2007

Nyama ya nyoka ni tamu!!!

Na Nora Damian wa Mwananchi

UBISHI makali ulizuka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana wakati wa mahojiano kati ya Wakili Gabriel Mnyele kwa upande wa wadaiwa na shahidi wa pili Daudi Kamugisha (40) kwa upande wa wadai katika kesi ya madai ya kashfa ya inayosikilizwa na Jaji Augustino Shangwa.

Katika kesi hiyo, wadai ni waumini wa dhehebu la Katoliki wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Afrika, wanaopinga habari iliyoandikwa Mei 29 mwaka 2005 katika gazeti la Majira zikidai kuwa wafuasi wa shirika hilo wanalazimisha kuwinda na kula nyama ya nyoka na kutembea pekupeku.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, anayayedaiwa kuwashurutisha wafuasi hao ni mwanzilishi wa shirika hilo, Padre Riccarido Enrico, mwenye asili ya Italia ambaye sasa ni raia wa Tanzania na amekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka 20 akitoa bure huduma za elimu ya sekondari mbali na huduma za kiroho. Soma MWANANCHI kwa taarifa zaidi

Eti Bunge kuamshwa kwa wimbo wa Taifa

Na Muhibu Said wa Mwananchi aliyepo Dodoma

BUNGE la Jamhuri ya Muungano, limeridhia mabadiliko ya kanuni zake ambapo sasa vikao vya kwanza na vya mwisho vya mkutano wake, vitakuwa vikianza kwa wimbo wa taifa kabla ya kusoma dua na pia vitakuwa vikifungwa kwa kufuata utaratibu huo.

Katika mabadiliko hayo, Spika na Naibu wake watakuwa wakiapa viapo vilivyowekwa kwa mujibu sheria, viongozi wa Bunge wanaokalia kiti cha Spika kuendesha shughuli za Bunge kwa haki bila upendeleo, Bunge kutambua haki ya raia ya kujitetea na kujisafisha kutokana na kauli zinazotolewa bungeni na Kamati za Bunge kufanya kazi zake kwa uwazi.

Pia Kamati za Hesabu za Serikali na za Serikali za Mitaa, zitakuwa na wenyeviti kutoka Kambi ya upinzani bungeni, Bunge litakuwa na Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria, wenyeviti wa Bunge watakuwa watatu badala ya wawili wa sasa na uchaguzi
wao utazingatia jinsia na pande za Muungano.

Mabadiliko hayo pia yanahusu kanuni ya kutosema uongo bungeni kufanyiwa marekebisho, taarifa za kamati za kudumu za Bunge kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni, pia kuweka mpangilio mzuri, kuunganisha baadhi ya kamati hizo pamoja na majukumu yake
na kuziweka chini ya Nyongeza ya Sita, kuweka utaratibu mzuri kuhusu usalama wa maeneo ya Bunge na Bunge kuwa na uwezo wa kuamua iwapo Muswada wowote wa Sheria unaowasilishwa kwa dharura unastahili kupitishwa na Bunge kidharura. Kwa taarifa zaidi soma MWANANCHI

Richard ndani ya Bongo

Mshindi wa Big Brother II Africa Richard akiwa katika kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam leo, kulia ni meneja wa Multichoice hapa nchini (Lucy Kihwele) na kushoto ni mmoja wa maafisa wa Multi choice aliyefahamika kwa jina la Shelukindo.


Baba mzazi wa Richard Bezuidenhout naye alikuwepo katika uwanja wa Ndege wa Jk Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati wakimpokea mwanae baada ya kushinda Big Brother Africa II.
Ndugu wa Richard,Louis naye alikuwa ni miongoni mwa Watanzania waliofurika kumpokea Mshindi huyo.

Ama kweli Richard ameleta mambo Mabaunsa , familia baba, kaka na dada zake , wabongo kibao walijaaa uwanjani hapo kuhakikisha usalama wa kutosha unapatikana na baadaye leo kazungumza na vyombo vya habari. Picha za Richard Bukos wa Global Publisherz na Mpoki Bukuku.

Wednesday, November 14, 2007

Said Kubenea ndani ya nyumba


Jamani eeehhh kijiji chetu kimevamiwa na hivi sasa ameingia mvamizi wa nguvu anatisha kama ukoma mwanamapinduzi Said Kubenea (pichani) jamaa asiyeogopa wala kutishwa kanambia yuko fiti katika hili anga la blogu, anashuka na zote kali tupu h ebu mcheki hapa KUBENEA ili mpate taarifa zaidi.

Tuesday, November 13, 2007

Breaking Newsss

RAIS Jakaya Kikwete ameteua wajumbe wa Kamati ya uangaliaji upya mikataba ya uchimbaji wa madini nchini itakayo kuwa na jukumu la kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini.

Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe kumi na mmoja itakuwa chini ya Uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine ni pamoja na:-

Zitto Kabwe- Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA),
John Cheyo -Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP),
Salome Makange- Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini
Mugisha Kamugisha- Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha
Edward Kihundwa- Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi
Dk. Harrison Mwakyembe- Mbunge wa Kyela (CCM)
Ezekiel Maige- Mbunge wa Msalala (CCM)
Peter Machunde- Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE)
David Tarimo- Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Shirika la Kimataifa la CoopersHouse
Maria Kejo- Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi ilisema kuwa pamoja na mambo mengine kamati hiyo pia itakuwa na kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Kamati hiyo iliyopewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi yake pia inajukumu la kukutana na chamber of minerals na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo.

Kuundwa kwa Kamati hiyo kunafuatia hoja binafsi ya mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa kamati itakayochunguza mikataba ya madini kufutia Waziri wa Nishati, Nazir Karamagi kutia saini makubalino ya uchimbaji wa madini katika mgodi wa Buzwagi akiwa nje ya nchi.

Monday, November 12, 2007

Richard is king of Big Brother Africa In 98 incredible days, through the magic of cellphone, TV and computer technology, fans of M-Net’s Big Brother Africa 2 turned the 24/7 daily reality series into a blockbuster bona-fide hit across the continent.

On Sunday November 11, viewer voting propelled 24-year-old film student Richard Bezuidenhout from Dar Es Salaam, Tanzania to the big prize of $100 000 (about R670 000)! With seven of the 13 voting blocks voting for Richard, he is the winner of Big Brother Africa 2.

Beating Angola’s Tatiana and Nigeria’s Ofunneka to win the series, Richard was the last person to head out of the now famous Big Brother doors, straight into the spotlight as Africa’s newest reality series winner.

During the two-hour Finale that rocked to Afro-chic fashion, music and dance beats, DStv viewers in over 40 countries watched as the popular series drew to a dramatic end.

Reliving the triumphs, tantrums and tears of the past 3 months, viewers were treated to a special packaged insert that recounted the unforgettable moments that characterised the show.

From Bertha’s leg injury, the fake eviction and the inclusion of the “moles” Victor and Ashanti, to the African themed tasks, the eviction shows and the special guests, such as Senegal’s Baaba Maal, the highlights package took viewers down memory lane.

In addition, a second insert shown during the Finale, concentrated on romance and relationships, two themes that have characterized the current season of Big Brother Africa. From Code and Maureen’s close connection to Tatiana and Richard’s relationship, which earned the couple the nickname Richiana, and including the flirtations of housemates Kwaku, Meryl and Bertha, Big Brother Africa 2 was love-struck!

Meanwhile other Finale highlights that had the live audience gathered around the catwalk-styled ramp in high spirits were electrifying performances by South African super-group Bongo Maffin, Kenyan afro-fusion legend Eric Wainaina and award-winning Nigerian hip-hop stars P-Square. Plus, with the nine previously evicted housemates all in attendance, having already enjoyed ‘heroes’ homecomings in their own countries, it seemed fitting that a duet by Zimbabwe’s Bertha and Malawi’s Code was also on the Finale menu.

Friday, November 09, 2007

Uwanja wa zamani unavyoonekana leoBaada ya kuja wataalamu wa fifa na kisha ffifa yenyewe kutupa jamvi hili la kusakatia kabumbu uwanja wetu wa zamani sasa unaonekana hivi, lakini kwa mbali unaweza kuona Uwanja mpya wa taifa.

King Kikiii akiwa na Hussein JumbeHawa jamaa sijui kama kuna asiyewajua ndiyo magwiji wa muziki wa dansi, hivi sasa Hussein yuko huko Mikumi Sound na dingi anadunda town mambo mpwitompwito muziki wa dansi oyyeeeeee!!!!!

Wednesday, November 07, 2007

Hivi tutaweza kweli????Ndivyo wanavyoonekana kujiuliza makamanda wa jeshi wakijadiliana muda mfupi mara baada kuteuliwa na kisha kuidhinishwa na Halmashauri kuu, makamanda hawa sijui wataweza vyema kupanga mashambulizi na hasa wakitumia ujanja wao wa porini, field craft walioupata sehemu mbalimbali. Off coiurse kwa kutuia makapteni wawili wa jeshi na yeye Luteni mambo bila shaka mswano, lakini wapo katika wakati mgumu, wanamtandao mtindo mmoja, ufisadi mtindo mmoja na wengi walioshinda wameingia kwa pesa kibao.

Tuesday, November 06, 2007

Makamba Katibu Mkuu tena

Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba akiwa katika ukumbi wa NEC leo karejea kama Katibu Mkuu
Rostam Aziz Kastep down
Kapteni Jaka Mwambi - Nje
Amos Makala -Mweka hazina
Aggrey Mwanri - Nje
Kidawa hamisi Swaleh -Yupo- Mipango
Salehe Ramadhan Feruz- Yumo- Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar
Kapteni John Chiligati - Katibu Mwenezi
Kapteni George Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu
Bernard Kamilius Membe -Katibu wa Siasa na uhusiano wa Kimataifa

Safu ya sekretarieti iliyopita na nyadhifa zao katika mabano ni Yusuf Makamba (Katibu Mkuu), Jaka Mwambi (Naibu Katibu Mkuu, Bara), Salehe Ramadhan Ferouz (Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar).
 
Rostam Aziz (Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa), Kidawa Hamid (Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Taifa), Aggrey Mwanri (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa), Dk Asha Rose Migiro (Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM), Kidawa hamis Swaleh.

picha kutoka kwa mdau BUKUKU

Kazi imekwisha wajumbe safariniBaadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wakijiandaa kukwea gogo ili kurejea makwao, wengine waliondoka jana na wengine wataondoka leo jioni kwa usafiri wa aina mbalimbali, kila la kheri wajumbe wa CCM.

Monday, November 05, 2007

Kila la kheri RichardMPIGIE KURA MTANZANIA RICHARD ASHINDE MILIONI 130 NA HUU NDIO UTARATIBU WA 'KUVOTI' FAINALI WIKI IJAYO!
Voting by SMS
Please SMS "VOTE NAME" of the Housemate you would like to see WIN Big Brother Africa. Nicknames, or surnames, will not be counted as a vote.

If you want Tatiana to WIN, SMS: VOTE TATIANA

If you want Ofunneka to WIN, SMS: VOTE OFUNNEKA

If you want Richard to WIN, SMS: VOTE RICHARD

If you do not include the word VOTE in your SMS, your vote will not be counted.

You can SMS your vote to the same number you use for the SMS strap. Your country’s standard rates for SMS’s will apply. If you’re lost, just look at the SMS strap at the bottom of your TV’s.

Non participating countries are also invited to vote. Details of the numbers to send your votes remain the same as the SMS number to which you send your comments. See below for a full list.

Angola 15626 (USD 0.50)
Botswana 15626 (P3.00)
Ghana 15626 (50GhP)
Kenya 15626 (Saf: Kes 30, Celtel: Kes 35)
Malawi 15626 (MK 56.00)
Namibia 15626 (N$ 3.00)
Nigeria 34626 (N75)
South Africa 34626 (R2.00)
Tanzania 15726 (Tsh 600)
Uganda UTL: 5626
Celtel: 0903015626
MTN: 15626 (U700)
Zambia 15626 (ZK2100)
Zimbabwe 15626 (Z$1,160)

Non Participating Countries can use these codes:

Gambia 15626 (15 Dal)
Sierra Leone 15626 (1550 SL L)
Liberia 15626 (50 US cents)
Togo 15626 (CFA240)
Swaziland 15626 (50 US cents)
Voting by Phone
You can also submit your vote by calling the Big Brother Africa vote line on +27-83-900-0000. There is a list of options available and all you have to do is pick one.

Win
Each week, one lucky viewer can also win an O’Botic├írio Hamper to the value of ZAR2,500.

An overall winner will win an all expenses paid trip for two to Rio.

Happy Voting and Good Luck!

Matokeo taratibu tartibuu

picha kutoka kwa mdau MPOKI ana picha nyingi huyo na kiboko zaidi.

MATOKEO ya uchaguzi wa nviongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yametoka na sasa watu wanashangilia na wengine kufuta machozi hebu cheki hawa. Wanalia.

Katika nafasi za kundi la wanawake Tanzania Bara kuna
Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki na sasa Mbunge Beatrice
Shelukindo. Pia yupo Mbunge Tatu Ntimizi na Katibu Mkuu mstaaf wa
UWT Halima Mamuya.

Kwenye kundi la Vijana kuna wagombea Hussein Mohamed ambaye
alionekana kufanya kampeni maeneo mengi ya nchi na kuonyesha kuwa
angeibuka mshindi naKiongozi katika ofisi ya UVCCM taifa, Fransis
Issack walitupwa.

Kwa upande wa Issack, hili ni pigo lingine kufuatia kupoteza nafasi zote
alizogombea mkoani Singida huku akitajwa kuwa na nia ya kusaka kiti cha
Mwenyekiti wa UVCCM ngazi ya taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Danhi Makanga, Ruth Msafiri, Thomas Ngawaiya na Tambwe Hiza wamepoteza katika kundi hili. Ngawaiya na Hiza
walitoka upinzani na walitarajiwa kupewa kura za huruma jambo ambalo
halikufanyika.

Wengine nni pamoja na wabunge Margareth Agness Mkanga, Zuhura Mikidadi na mhamasishaji wa tenzi wa CCM, Salim Shomvi Tambalizeni, Naibu Meya wa Ilala Mustafa Yakub, Mkuu wa Mkoa wa Mara Isdore Shirima na Mkuu wa Wilaya ya
Frank Uhaula walikosa nafasi hizo.

Wanasiasa wengine maarufu waliokosa nafasi baada ya kupata kura chache ni Wilson Masilingi, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Enock Chambiri, Christopher Gachuma, Charles Kagonji, Lukas Kisasa, Pascal Mabiti, Dk James Msekela, Profesa Idrisa Mtulia, Abeid Mwinyimsa na Job Ndugai.

Wengine ni wandishi wa habari Jacqueline Liana, Jeni Mihanji na Novatus Makunga.

Hawa mambo yao supa toka katika kundi gumu lenye wagombea 59 washindi ambao ni 20 ni wafuatao!
Edward Lowassa, Andrew Chenge, Yusufu Makamba, Bernard Camilius Membe, Jaka Mwambi, Juma Otman Kapuya, Abrahman Kinana, Christopher Gachuma, Stephen Masatu Wassira, Aggrey Mwanri, Milton Makongo Mahanga, Fredrick Tluway Sumaye, John Komba, Kingunge Ngombale Mwiru, William Lukuvi, John Chiligati, Amos Makalla, Samwel Wangwe, David Homeli Mwakyusa na Jackson Msome

Mambo DodomaMwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya kikwete akiingia na wasauduzi wake wa
juu, Katibu Mkuu, Yusuph Makamba (Kushoto), Makamu Bara, John Malechela na makamu
Zanzibar Amani Karume mambo yanaendelea endelea kuangalaia humu matokeo yatatangazwa muda si mrefu

Saturday, November 03, 2007

Mambo ya Dodoma

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mwakilishi wa ANC ya Afirka ya kusini Jackob Zuma katika mkutano mkuu wa 8 wa CCM uliofanyika huko Kizota mjini Dodoma leo. Mkutano Mkuu wa CCM, unafanyika mjini Dodoma kuanzia Jleo na kesho, kesho ndo unafanyika uchaguzi mkuu ndani ya chama. Picha za Ikulu

Friday, November 02, 2007

BREAKING NEWS...!! MSEKWA MAKAMU M/KITI CCM


MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI, JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA PIUS MSEKWA SPIKA MSTAAFU WA BUNGE LA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA, KUWA MGOMBEA PEKEE WA NAFASI YA UMAKAMU MWENYEKITI CCM TANZANIA BARA. Na KWAMBA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU ZIMEMPITISHA NA SASA ANAASUBIRI TU KUPIGIWA KURA ZA NDIYO AU HAPANA NA MKUTANO MKUU. KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI YUSUF MAKAMBA AMEZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA AKATHIBITISHA NA KUSEMA MAKAMU MWENYEKITI MSTAAFU MZEE MALECHELA ATAKUWA MJUMBE WA KUDUMU WA NEC NA CC. TAARIFA ZAIDI HUSUSANI JUU YA TAFSIRI YA HABARI HII ZINAKUJA.

Thursday, November 01, 2007

Hatimaye mfungwa atunukiwa shahada gerezani
HARUNA Pembe Mgombela (54) pichani juu, ambaye ni mfungwa katika Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam jana alikabidhiwa rasmi cheti cha kuhitimu shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania aliyosoma akiwa gerezani humo.

Pamoja na kukabidhiwa shahada hiyo kwenye mahafali maalum yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa Magereza Ukonga, Mgombela alisema yuko tayari kuendelea na masomo ya juu ya Shahada ya Uzamili, kama alivyoahidiwa na kupata udhamini wa Chuo Kikuu hicho.

Mgombela alisema ahadi hiyo iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Profesa Tolly Mbwette baada ya kumkabidhi rasmi cheti hicho ni changamoto kwake hivyo ataitumia vyema nafasi hiyo.

"Niko tayari kuanza shahada ya uzamili hata leo, siwezi kukata tamaa, nia yangu kubwa ni kujiendeleza na kutumia fursa hii vizuri huku nikiendelea kutumikia adhabu yangu kujirekebisha kwa mujibu wa sheria," alisema Mgombela, mzaliwa wa Kibaha mkoani Pwani.

Aliongeza kuwa matarajio yake kwa sasa ni kuendelea kujiandaa akiwa gerezani na kutumia taaluma hiyo kuwasaidia wafungwa wenzake katika masuala ya kisheria, hasa baada ya kutoa ushauri na kuandika hati za rufaa zilizowawezesha wafungwa zaidi ya 90 kushinda rufaa zao.

Alisema kwa sasa si rahisi kwake kufikiria hatma yake baada ya kutoka gerezani kwa kuwa bado ana muda mrefu wa takribani miaka 25 anayotakiwa kuitumikia katika gereza hilo ikiwa ni sehemu ya adhabu ya miaka 50 aliyohukumiwa.

Mgombela alisema katika muda wote wa masomo yake tangu alipojiandikisha rasmi mwaka 2004, hakuwahi kutoka gerezani humo kwa ajili ya shughuli yoyote ya kujisomea, lakini alikuwa akipata nafasi ya kutembelea maktaba ya gereza hilo na kupelekewa vitabu alivyohitaji.

Picha ya Faraja Jube na imendikwa na Andrew Msechu wa Mwananchi