Sunday, December 20, 2015

WAZIRI KITWANGA, DKT. MWAKYEMBE WATEMBELEA MAGEREZA MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM, WAAHIDI KUBORESHA HUDUMA KWA WAFUNGWA NA MAHABUSU

kitw1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Kamshina Jenerali wa Jeshi la Magereza,. John Minja wakati alipokuwa anawasili Gereza la Mahabusu Keko kwa ziara ya kikazi. Mwenye mawani ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo.
kitw2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga  akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Gereza Keko alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea Magereza Makuu ya Mkoa wa Dar es Salaam.
kitw3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na mahabusu na wafungwa waliopo Gereza la Wanawake Segerea, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Gereza hilo kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Magereza. Kulia kwake ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Maimuna Tarishi. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja.
kitw4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kushoto) na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) wakikagua  jiko linalotumia gesi asilia kupikia vyakula vya wafungwa katika Gereza la Mahabusu Keko, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja.
kitw5
Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ukiwasili katika lango Kuu la Gereza Kuu Segerea, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Magereza.
kitw6
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakitoka Gereza la Wanawake Segerea baada ya kuzungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza hilo lililopo jijini Dar es Salaam.
kitw7
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa wa kike wa Gereza la Wanawake Segerea ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa program ya urekebishaji magerezani. Pembeni yake ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Abdalah Kiangi. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.
kitw8
Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto aliyevaa suti) akipokea heshima kutoka gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji cha Jeshi la  Magereza mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kikazi ya kutembelea Magereza Makuu ya Mkoa wa Dar es Salaam.
kitw9
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akitoa majumuisho kwa waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam. Katika ziara yake hiyo Waziri Kitwanga aliambatana na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati). Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.,
Post a Comment