VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA JKT WATAKIWA KUACHANA NA VITENDO VYA UHARIFU NA WAWE WAZALENDO NA NCHI YAO
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA DESEMBA 29
VIJANA hapa nchini wanaomaliza mafunzo ya awali ya kujitolea ya jeshi la kejenga Taifa (JKT) yanayofahamika kwa jina la Operesheni Kikwete wametakiwa kutojihusiha kabisa na vitendo vya uharifu wa kutumia siraha na badala yake sasa kupitia mafunzo waliyoyapaya ya kijeshi kuwa
wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na sio vinginevyo.
wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yao na sio vinginevyo.
Hayo yamesemwa na Bligadia General Francia Njau kutoka JKT Makao makuu wakati wa sherehe za ufungaji wa mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea Francis Njau yaliyofanyika katika viwanja cha mabatibini mlandizi katika kikosi cha jeshi 832.
Bligadia Njau amesema kwamba anatambua vijana hao wamejitolea katika kupata mafunzo mbali mbali hivyo wanapaswa mafunzo hayo waliyoyapata wayatumia vizuri na kuwasisitiza kutoitumia vibaya kauli mbiu ya Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli inayosema hapa kazi tu kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
Aidha Njau aliwataka vijana hao kutokuwa na fikra potofu ya pindi wanapomaliza kuhitimu mafunzo hayo ya awali wanakwenda kupata ajira na kuwaomba wajitahidi kadri ya uwezo wao kutumia mafunzo ya waliyoyapata ya ujasirialiamali na ufundi stadi kama fursa za kuweza kujiajiri wao wenyewe kuliko kuitegemea serikali pekee.
Naye mwakilishi kutoka JKT Mkao Makuu Luteni Kanali Piace Kapello amesema kwamba jukumu kubwa la jeshi la kujenga Taifa ni kuhakikisha inatoa mafunzo na malezi bora kwa vijana ambao wataweza kulilinda Taifa lao liwe katika hali ya amani,utulivu na usalama.
Kwa upande wao mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ambaye alisoma risala kwa mgeni rasmi pamoja na Mkuu wa kikosi cha 832 JKT Ruvu Luteni Kanali Charles Mbunge walikuwa na haya ya kusema kuhusina na mafunzo hayo.
MAFUNZO hayo ya awali ya kujitotolea yanayojulikana kama Operesheni Kikwete wamewajumuisha vijana wapatao 1187 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania na yamechukua muda wa miezi sita kwa kujifunza mambo mbali mbai ya ujasiriamai, stadi za kazi, ufugaji, kilimo, usafi, nidhamu juu ya ulizni na usalama pamoja na jinsi ya matumizi ya siraha.
Comments