Sunday, December 13, 2015

WAHITIMU TIA WAMEASWA KUTUMIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA SOKO LA AJIRA NCHINI

ti1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akitoa hotuba wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI2
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua kutoa hotuba wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI3
Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo inayojumuisha pia idadi ya wahitimu 3,169 ambao kati yao wanawake ni 1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7 wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI4
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasili viwanja vya mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI5
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkbidhi Mwanafunzi Cosmas Ephraim zawadi ya kufanya vizuri katika masomo yake ya  shahada ya Uhasibu wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI6
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI7
Baadhi ya wahitimu wakisiliza Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisoma tamko la kuwatunuku vyeti wahitimu hao wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI8
TI9
TI10
Baadhi ya wahitimu washangilia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
TI11TI12
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo (kushoto) wakiondoka eneo la mahafali mara baada ya kuatunuku vyeti wahitimu 3,169 wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda
……………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wameaswa kutumia mafunzo ya ujasiriamali waliyoyapata chuoni hapo katika kukabiliana na changamoto ya soko la ajira na kuelekeza mawazo yao katika kujiajiri badala ya kuajiriwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati mahafali ya 13 ya taasisi hiyo kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
“Mafunzo ya ujasiriamali mliyoyapata yawe chachu ya ufanisi wenu katika kufanyakazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu, umakini na weledi wa hali ya juu ili kujiletea maendeleo yenu wenyewe yenye na yenye tija kwa taifa”,
“Msingi wa mafanikio na kuhifadhi ajira ni kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, jiepusheni na vitendo vya rushwa na ubadhirifu mkitabua kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo” alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.
Mahafali hayo ya 13 yanajumuisha wahitimu kutoka fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusianao wa Jamii na Uhasibu wa Fedha za Umma ambazo msingi wake ni kendesha uchumi wa taifa katika kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma kwa kutumia wataalamu mbalimbali ambao wengi wao ni tunda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania.
Aidha, Dkt. Mwinyimvua aliwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata vema katika kuendeleza uchumi wa taifa, kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka pamoja na kupambana na kupambana na changamoto zinazolikabili taifa kwa kudhibiti ubadhirifu na matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali za taifa.
Awali akitoa taarifa fupi kwa Mgeni Rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda alisema kuwa wapo jumla ya wahitimu 3,169 kati yao wanawake ni 1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7.
Idadi hiyo inajumuisha wahitimu 441 kutoka kampasi ya Mtwara na wahitimu 2,728 kutoka kampasi ya Dar es salaam kwa ngazi ya cheti, stashahada, shahada na shahada ya uzamili.
Dkt. Kihanda alisema kuwa kwa mwaka wa masomo 2014/2015 Taasisi ya Uhasibu Tanzania ina jumla ya wahitimu 6,949 kutoka kampasi za Dar es salaam, Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza na Kigoma.
Kati ya wahitimu hao idadi ya wanawake ni 3,458 ambao ni sawa na asilimia 49.8 na idadi ya wanaume ni 3,491  ambao ni sawa na asilimia 50.2, wahitimu kutoka kampasi ya Kigoma ni wa kwanza tangu taasisi hiyo ianzishwe mkoani humo.
Dkt. Kihanda aliongeza taasisi bado inaendelea na zoezi la udahili kwa mwaka wa masomo 2015/1016 kwa ngazi ya shahada ya kwanza pamoja na wanafunzi katika ngazi ya cheti cha awali kwa awamu ya pili mwanzoni mwa mwaka 2016.
Taasisi hiyo inatarajia kudahili wanachuo wapatao 10,500 katika kampasi zake zote na kufanya idadi ya wanafunzi kuongezeka kutoka 12,899 ya sasa hadi 17,739.
Kwa upande wake mwanafunzi Cosmas Ephraim alisema kuwa amefarijika kuhitimu masomo ya shahada ya Uhasibu mbayo ameahdi kuitumia elimu hiyo ili kutoa mchango wake katika kuendeleza taifa liweze kuwa na maendeleo yenye tija kiuchumi kwa Watanzania wote.
Post a Comment