Monday, June 26, 2017

DKT SHEIN AONGOZA BARAZA LA EIDD EL FITRI MJINI UNGUJA,ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya Eidd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya ElIdd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
 Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga   alipokuwa akitoa khutba baada ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi  leo.
 Waislamu wanawake wakiwa katika Swala ya Eid  el fitri iliyoongozwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjni Unguja leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo  Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali walihudhuria [Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
 Baadhi ya waislamu wanaume waliohudhuria katika swala ya EId elfitri wakimsikiliza  Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Fadhil Soraga aklipokuwa akitoa khutba ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI KILIMANJARO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya Eid Elfitr itakayo fanyika Kitaifa mjini Moshi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, June 22, 2017

OFISI YA MANISPAA YA ILALA YAHAMIA KWA MUDA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUWAHUDUMIA WANANCHI KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na mmoja wa wazee waliofika kupatiwa huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo ofisi nzima ya Manispaa hiyo imehamia viwanjani hapo kwa ajili ya kuhudumia watu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akiwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto wakitoa huduma kwa wadau waliofika kutaka msaada juu ya mambo yanayowakabili . Ofisi za Manispaa hiyo zimahamia hapo kwa muda kwa ajili ya kuhudumia watu, ikiwa ni sehemu ya mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela akimuhudumia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika katika viwanja vya mnazi mmoja.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni ya kuuza vifaa vya kuzimia moto inayojulikana kwa jina la Zima Moto  
 Afisa mkaguzi  Msaidiz wa jeshi la Zima Moto , akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema wakati wa maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ilala ambo wanatoa huduma kwa wananchi katika Viwanja vya mnazi mmoja 

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ,IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA ZANZIBAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza na maafisa wakuu wa Jeshi la Polisi alipofanya kikao na maafisa hao akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kabla ya kwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Ali Mohamed Shein. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani makame. Picha na Hassan Mndeme.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Hassan Mndeme.

ZIARA YA RAIS DK. MAGUFULI MKOA WA PWANI, AZINDUA MIRADI UKIWEMO WA MAJI WA RUVU JUU

Rais Dk. John Magufuli akilijaribu kuliwasha Trekta katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta ya URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani, wakati akizindua Kiwanda hicho, akiwa katika ziara ya siku tatu katika mkoa wa Pwani, jana.
Rais Dk. John Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza  matrekta ya URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani, jana.
Rais Dk. JohnMagufuli akiweka jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza  matrekta ya URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani. 
 Rais Dk. John Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani, jana.
 Rais Dk. John Magufuli  akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ya TRL kusafirisha nondo kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani, jana.
 Rais Dk. John Magufuli   akishirikiana  na viongozi wengine kukata utepe wakati akifungua kiwanda hicho cha nondo. 
 Rais Dk. John Magufuli akishirikiana na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole (kushoto),  na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali kukata utepe kuzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani, jana.
 Rais Dk. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge baada ya kuzindua rasmi Mradi wa upanuzi wa Mitambo ya kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani.
 Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa  baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji
 Rais Dk. John Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji cha Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo
 Rais Dk. John Magufuli akishirikiana na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya kupiga ngoma, baada kuzindua mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa ajili ya miji ya Pwani na Dar es Salaam.
 Rais Dk. John Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa kwa njia ya mdandao na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga kabla ya kuzindua Mradi huo wa maji
 Rais Dk. John Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani.
 Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
 Rais Dk. John Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani. PICHA ZOTE NA IKULU.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUTARISHA CHATO , AKIWA NJIANI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIGONGO FERI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki  katika swala ya magaharibi katika  futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu mjini  Chato, mkoani Geita, Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuturu pamoja na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC)  Dayosisi ya Geita (kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alhaj Yusuph Kabaju(kulia) katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli, mjini  Chato, mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli  mjini  Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza  na wananchi wa eneo la Kigongo feri Wilaya ya Misungwi, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ziara ya siku mbili  Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,  Ezekiel Kyunga wakati alipowasili mjini Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017 kwa ziara ya siku mbili mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Ahimiza nyumba za ibada zisitumiwe vibaya 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba waumini wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wahakikishe nyumba zao za ibada hazitumiki kuleta migogoro. 

Ametoa ombi hilo jana usiku (Jumatano, Juni 21, 2017) wakati akizungumza na mamia ya waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu pamoja na viongozi wa dini walioshiriki ibada ya futari wilayani Chato, mkoani Geita. 

Akizungumza na waumini hao kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Mheshimiwa Rais alishapanga kufika Chato ili kushiriki nao ibada ya iftar lakini ametingwa na majukumu ya kitaifa akaona ni vema amtume yeye ili amwakilishe.

“Mheshimiwa Rais alishapanga kuja Chato kufuturu pamoja na wana-Chato lakini kadri siku zinavyozidi kwenda anajikuta anabanwa na majukumu mengi ikiwemo kukutana na wageni wa kimataifa, kwa hiyo akaona ni vema nije kumwakilisha katika shughuli hii,” alisema.

“Mheshimiwa Rais anawaombea heri katika siku zilizobakia za mfungo wa Ramadhan ili mmalize salama na Mungu akijalia muweze kusherehekea pamoja, na pia anawatakia heri wale watakaoendelea na sita tushawal.”

Akisisitiza kuhusu amani na utulivu nchini, Waziri Mkuu alisema: “Hatupendi kusikia kuwa msikiti fulani wamechapana viboko kwa sababu ya kugombea uongozi au kwenye kanisa fulani waumini wamepigana wakigombea mchungaji wao.”

“Tutumie nyumba zetu za ibada kudumisha amani na mshikamano wetu. Napenda niwahakikishie kuwa Serikali yenu chini ya Rais John Pombe Magufuli itaendelea kuheshimu dini zote.”

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waumini hao kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhan ni wa toba kwa kila muumini. “Huu mwezi mafundisho yake yanasisitiza amani, uvumilivu na kusameheana. Nipende kuwasihi kwamba tuendelee kudumisha utulivu tulionao,” aliongeza.

“Nipende kusisitiza kwenu wana-Geita na wana-Chato kwamba jukumu kubwa mlilonalo ni kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, busara na uongozi wa kimungu katika maamuzi yake. Niwasihi ndugu zangu Waislamu na Wakristo, tuendelee kuwaombea viongozi wote wa kitaifa kila siku ili wafanye kazi kwa kuongozwa na Mungu,” alisema.

Awali, akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Chato, Sheikh Ally Moto alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa fursa ya kuweza kushiriki ibada ya iftar pamoja na watoto yatima na wajane.

Alisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na ili kudumisha amani wilayani humo, waumini wa Kiislamu na Kikisto wameunda Kamati ya Amani ya wilaya hiyo inayojulikana kama Interfaith Committee. 

Naye Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuandaa futari hiyo ambayo imejumuisha wana Chato kutoka pembe nne za wilaya hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Geita, Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Magufuli na kuwapongeza viongozi wakuu wa kitaifa kutokana na utendaji wao unaogusa mioyo ya Watanzania.

“Ninyi wote watatu ni viongozi ambao Mungu amewaweka kuongoza nchi yetu. Katika miezi hii 18, mmefanya mambo makubwa, ni imani yetu kuwa ataendelea kuwaongoza katika utendaji kazi wenu,” alisema.

Akitoa shukrani, Sheikh wa Mkoa wa Geita, Sheikh Yusuph Kabaju ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa fursa wana-Geita kujumuika pamoja katika futari hiyo na kuahidi kudumisha amani ya Tanzania.

“Tunakushukuru kwa kutuunganisha wana Geita katika futari hii japo umeamua kufanyia ibada hii hapa Chato. Maneno ya Quran tukufu yanasema malipo ya waliofunga anayapata pia yule aliyefuturisha waliofunga,” alisema.

Sheikh Kabaju pia alisoma dua ya kumuombea Mheshimiwa Rais Magufuli pamoja na viongozi wa kitaifa. Pia aliombea amani kwa ajili ya Taifa la Tanzania.IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

ALHAMISI, JUNI 22, 2017.

WANAWAKE VIONGOZI KATIKA MASOKO WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUTEMBELEA KATIKA MASOKO AONE MIUNDOMBINU ILIVYO

Ofisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Suzan Sita (kulia), akitoa mada katika Warsha ya Siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa Umoja wa Wanawake Masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na shirika hilo inayoendelea katika Hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi hao wakiwa katika warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Warsha hiyo. Kulia ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Irene Daniel.
Taswira katika ukumbi wa mikutano.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas, akichangia mada. (kulia) ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma na kushoto ni Verdiana Gervas kutoka Soko la Ilala.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Ilala Mchikichini, Bupe George akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akichangi mada.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele akichangia jambo.
Mfanyabiashara kutoka Soko la Gongolamboto, Elika Mwakyusa akichangia.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Johanitha Katunzi akichangia mada.
Mshiriki wa warsha hiyo  akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Kiwalani Kigilagila, Bisura Juma akichangia jambo.

Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI Wanawake katika masoko jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk.John Magufuli atembelee masoko wanayofanyia shughuli zao ili aone changamoto ya miundombinu katika masoko hayo.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas  wakati akichangia mada kwenye warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa umoja wa wanawake masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

Alisema wafanyabiashara wakiwemo wanawake wamekuwa wakilipa ushuru kila siku katika masoko hayo lakini manispaa husika zimeshindwa kuwajengea miundombinu kama vyoo bora, umeme na maji hivyo kuwa changamoto kubwa kwao.

"Tumekuwa tukitoswa ushuru wa shilingi 500 kwa siku kwa kila mfanyabiashara lakini hatuoni jitihada zozote zinazochuliwa na hizi manispaa zetu za kutuwekea miundombinu bora ndio maana tunamupomba Rais wetu afanye ziara katika masoko tunayofanyia kazi ili tuzungumze naye na kuiona changamoto hii tuliyonayo" alisema Cleophas.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele alisema wakati ufike manispaa ziweke wazi sheria ya ulipaji wa ushuru kwa mfanyabiashara ambaye hakufika sokoni kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kuumwa kwani anapo pona na kurudi katika eneo lake la kazi anatakiwa kulipa ushuru wa muda huo wote ambao hakufanya biashara wakati alipokuwa akijiuguza.

"Tunaomba manispaa zetu ziweke wazi jambo hili kwani limekuwa ni changamoto kubwa sana kwetu" alisema Mtewele.

Mwezeshai wa Sheria katika Soko la Kigogo Sambusa Mariam Rashid alisema zabuni za uzoaji taka katika masoko zinapaswa kuangaliwa kwa karibu kwani wengi wanaozipata hawana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo kusababisha masoko mengi kuwa na changamoto ya mlundikano wa takataka ambapo alishauri kuondoa mfumo dume katika masoko unaotoa tenda hizo na badala yake zitolewe fursa kwa wanawake ili waweze kuingia katika kamati za masoko ili nao waweze kuchangia katika mambo mbalimbali.

Elika Mwakyusa aliomba manispaa ya Ilala kutenga eneo la soko Gongolamboto ambako hakuna soko kwani eneo wanalofanyia biashara zao ni la mtu binafsi hivyo wamekuwa na changamoto kubwa ikiwemo kumlipa ushuru mkubwa mtu huyo.

Mwezeshaji sheria wa Soko la Vingunguti wa Simba, Maimuna Mungi alisema ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi mbalimbali katika soko hilo hakuna kutokana na kuwepo kwa mfumo dume jambo ambalo limechangia wanawake wafanyabiashara katika soko hilo kushindwa kuzipatia kusaidiwa changamoto walizonazo.

Mwezeshai Sheria kutoka Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa aliomba asilimia 10 ya fedha za makusanyo ya ushuru zibaki katika masoko husika ili zisaidie ujenzi wa miundombinu.

Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG Suzan Sitha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwaongezea uelewa viongozi wanawake masokoni kuhusu ukatili dhidi yao pamoja na kupanga mikakati ya kuendeleza kampeni za kupunguza ukatili dhidi ya wanawake masokoni baada ya mradi kuisha.

Alitaja lengo lingine ni kutambua haki za wanawake na wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake pamoja na kuwakumbusha viongozi juu ya wajibu wao na utunzaji wa kumbukumbu za vikundi.

Sitha alisema warsha hiyo imewashirikisha viongozi wanawake kutoka masoko  ya Manispaa ya Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam, ambayo ni Ilala Boma, Gongolamboto, Mombasa, Kiwalani, Mchikichini, Kigogo Fresh, Kigogo Sambusa, Chamazi, Kiustu, Kinyerezi, Feri, Temeke Sterio, Buguruni, Gezaulole, Tabata Muslim na Vingunguti kwa Simba.

Alisema karibu changamoto zote zilizopo katika masoko zinalingana kubwa ikiwa ni miundombinu mibovu licha ya  wafanyabiashara kulipa ushuru na kuwa mradi huo wa Mpe Riziki Si Matusi upo katika Wilaya ya Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ambapo mradi mkubwa wa Sauti ya Mwanamke Sokoni  upo katika mikoa tisa hapa nchini.