WAFANYAKAZI SABA WA TPA WASHIKIRIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA UPOTEVU WA MAKONTENA MPYA 11,884 NA MAGARI 2,019
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara katika Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na kubaini uondoshwaji wa wa kontena 329 ambazo ziliondoshwa bila kulipa kodi zaidi ya sh.bilioni 12, baada ya ziara hiyo Mawakala wa Forodha walifanya ukaguzi kuona kama kuna upotevu wa mapato na kubaini jumla ya kontena 11,884 na magari 2019 yalitolewa bila malipo.
Makontena hayoo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61,DICD 491, JEFAG 1, 450, AZAM 295, PMM 779, AMI 4384, TRH 4,424 ambazo kodi yake ni zaidi ya sh.bilioni 47.
Magari 2019 yalitolewa bila kulipa kodi katika kampuni za TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SLVER 97, MASS 171, HESU 1359 kodi yenye thamani zaidi ya Tsh.bilioni moja (1) .
Akizungumza na wafanyakazi wa Bandari leo Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa wataendelea kuchukua hatua kwa wale wote watakaohusika kukwepa kodi.
Amesema kuwa wataendelea kuchukua hatua dhidi ya wale ambao wamehusika wakiwemo watumishi wanaoshiriki katika hujuma, Wafanyakazi saba wa TPA wanashikiriwa na polisi kuhusiana na upotevu wa kontena hizo na kusababisha serikali kukosa mapato.
Wanashikiriwa na jeshi la polisi ambao wengine wamekamatwa leo ni John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally ,Masoud Seleman, Benadeta Sangawe.
Wanaotafutwa kwa tuhuma za kusababisha upotevu wa kodi za serikali katika bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.
Comments