Saturday, October 31, 2015

TACCEO YALAANI KITENDO CHA POLISI KUVAMIA OFISI YAO NA KUWAKAMATA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU

Mmoja wa Wakurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Polisi kudaiwa kufanya uvamizi na kuwakamata waangalizi, vifaa binafsi na vifaa vya Kituo cha Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mbezi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio na Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Anna Henga
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

TACCEO yalaani kukamatwa waangalizi wa uchaguzi

Na Dotto Mwaibale
ASASI za Kiraia za Uangalizi wa Uchaguzi (TACCEO), pamoja na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), wamelaani kitendo cha kuvamiwa na Jeshi la Polisi, Oktoba 29, mwaka huu na lile la kukamata vitendea kazi na waangalizi wa uchaguzi  36.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda, alisema Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha LHRC, kilichopo Mbezi na kudai kuwa, waliagizwa na mamlaka husika kuwakamata waangalizi  na vifaa vya kieletroniki vilivyokuwa vikitumika katika mchakato huo.
Mwakagenda alisema polisi hao waliongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya  ya kipolisi Kawe, ASP Mgonja, ambapo  maofisa wa uangalizi walieleza kuwa, walipata taarifa kituo hicho kinakusanya na kunasambaza taarifa za matokeo zisizo rasmi.
"Katika mchakato huo, polisi walikusanya vifaa vyetu na kukamata kompyuta za mezani 24, mpakato tatu na simu za mkononi za waangalizi 25," alisema Mwakagenda.
Alisema baada ya tukio hilo, vifaa hivyo vilichukuliwa na kukabidhiwa kituo cha kati na baadaye kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi huku, baadhi ya waangalizi wakichukuliwa kwa ajili ya kutoa maelezo na baadaye kupata dhamani.
Watu hao wametakiwa kurudi kituoni hapo Oktoba 30, mwaka huu kwa ajili ya kumalizia maelezo yao.
"Mchakato huo la kurudi Oktoba 30, mwaka huu lilifanikiwa na kwa sasa waliambiwa warudi leo, kwa taratibu nyingine za kipolisi," alisema Mwakagenda.
Mwakagenda alisema uvamizi huo uliofanywa na jeshi la polisi ni wa kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini kwani, wasababisha kuwatishia wananchi kushiriki katika mambo yanayohusu mchakato wa chaguzi nchini.
"Katika hili ni kama wameondoa dhana nzima ya ushiriki kikamilifu wa sekta ya umma na binafsi   katika kutoa maoni ya kuboresha demokrasia na uchaguzi," alisema Mwakagenda.
Aidha, Mwakagenda alisema uvamizi huo uliathiri  na kuwafanya wakashindwa kukusanya taarifa za mwisho za uangalizi wa matokeo na ukusanyaji wa maoni ya wananchi.
"Uangalizi kwa kutumia tehama haujaanza mwaka huu kwani, tangu mwaka 2010 kulikuwa na utaratibu huu, mambo yaliyofanyika hivi sasa tunashindwa kuelewa tatizo ni nini," alisema

TAARIFA ILIYOTOLEWA NA UMOJA WA VIJANA WA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 31 OKTOBA 2015 MAKAO MAKUU YA UVCCM DAR ES SALAAM


Ndugu Waandishi wa Habari,

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unachukua nafasi hii kukipongeza kwa dhati Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais mteule Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupata ushindi wa kidemokrasia wa kishindo kwa kupata asilimia 58.46%.

Ushindi huo ni alama na kielelezo cha kuendelea kukubalika kwa CCM mbele ya Watanzania walio wengi kutokana na Sera zake, Mipango yake na mikakati ya kuwatumikia wananchi, kulinda amani, utulivu na kuendeleza Umoja wa Kitaifa nchini.
Ndugu waandishi wa habari,
Kwa upande mwingine tumelazimika kuwaita hapa leo kuelezea masuala muhimu kadhaa yaliyojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka 2015.
Kama ilivyotolewa taarifa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha, kwamba Uchaguzi wa Zanzibar kwa sehemu kubwa ulikumbwa na kasoro nyingi za kimsingi ambazo zimesababisha Tume kufuta matokeo kwa nafasi za Urais, Wawakilishi na Madiwani.
Ndugu waandishi wa habari,
UVCCM tumefanya tathmini ya haraka na kina ili kujua kiini cha tatizo hilo ikiwemo kukusanya taarifa toka vyanzo mbalimbali ambapo tumebaini na kugundua madhaifu kadhaa yaliyojitokeza katika hatua za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa upande wa Zanzibar.
Tumepata wasiwasi wa suala zima la namna zabuni ya karatasi za kupigia kura ilivyotangazwa na kumpata mzabuni ambae alipewa kazi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Ni ukweli usiopingika kwamba ZEC ilizidiwa nguvu na wanasiasa wa Chama cha Upinzani cha CUF ambao kwa kiasi fulani wameshinikiza Tume ya Uchaguzi kwa namna moja au nyingine kuikubali Kampuni ya ya Afrika Kusini ambayo sifa zake zinafahamika kuwa ina matatizo.
UVCCM tuna mashaka na kampuni hiyo iliyopewa kazi ya kuchapisha vifaa vya Uchaguzi ambayo kumbukumbu zinaonyesha iliwahi kuomba kazi ya kutayarisha vifaa kama hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kupewa, lakini SMZ baada ya kugundua kampuni hiyo ina matatizo, ilivunja mkataba na karatasi za kura zilichapishwa hapa hapa nchini.
Kampuni hii inalalamikiwa kuwa chanzo cha kuvurugika kwa chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika ikiwemo Cameroon, Benin, Ivory Coast na baadhi ya nchi za Latini Amerika. UVCCM tumeshangazwa sana kuona ZEC wakiikubali Kampuni ambayo tayari SMZ mwaka 2005 waliikataa na kuvunja nayo mkataba.
Kampuni hii inasemekana kwamba imekuwa inashirikiana na vyama vya upinzani hasa katika nchi za Afrika chini ya mkakati wa kuvisaidia kushinda Uchaguzi.
Pia tumepata mashaka na watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ama walizembea au walikuwa sehemu ya njama za kutaka kuvuruga uchaguzi. Kwa nini tunasema hivyo? Ni kwa sababu watendaji wa Tume ya Uchaguzi wanaifahamu vyema Kampuni hii, matatizo yake, lakini wameshindwa kuishauri Serikali na matokeo yake kuiingiza nchi katika hasara na mkanganyiko wa kisiasa.
Tunawataka watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kujipima kama wanatosha kuendelea kuwa na sifa ya kuwa Watendaji wa Tume hii sambamba na Makamishna wao ambao nao hawakujituma zaidi kujiridhisha na utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwa kuzingatia taarifa za nyuma za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa pale ilipovunja Mkataba.
Kwa mwenendo huo na mtazamo halisia ni wazi kuwa Chama cha CUF kimehusika na njama hizi za wizi wa kura na ndio maana Katibu Mkuu wake Seif Shariff Hamad akaamua kukiuka taratibu na kajitangazia ushindi kinyume na Katiba na Sheria za nchi wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea katika majimbo ya Pemba na Unguja. Ni kituko na mshangao kuona vyombo vya dola vikimtazama macho mgombea huyo aliyefanya kosa la jinai bila ya kumchukulia hatua za kisheria na kumfikisha kwenye mikono ya sheria.
Umoja wa Vijana wa CCM tunaitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kuunda Tume huru itakayochunguza kwa kina na undani wa kadhia hii ikiwemo suala zima la namna ilivyoendeshwa zabuni hadi kufikia kupatikana mzabuni na taarifa yake itolewe kwa umma.
Ndugu waandishi wa habari,
Tumekuwa tukisema mara kadhaa Chama cha CUF ni chama ambacho kimezoea kuwahamasisha wafuasi wao kufanya vurugu, ghilba, ubaguzi na masuala mengine ambayo hayaendani na kanuni za kidemokasia.
Katika kuyathibitisha haya, wakati wa kazi ya kupigakura na kuhesabu kura huko Kisiwani Pemba, wafuasi wa CUF wakiwa na jazba wamevamia vituo vya kupigia kura kinyume cha sheria na kuanza kuwashambulia kwa mapanga Mawakala wa Chama cha Mapinduzi na kuwatoa nje, huku wengi wao wakijeruhiwa vibaya.
Wafuasi hao wa CUF wakiwa katika makundi, wameyafanya hayo katika Vituo vya Majimbo ya Tumbe, Micheweni na Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Mawakala wa CCM wamewapiga na kuwajeruhi na kusababisha kusimamishwa kwa kazi za kuhesabu kura.
Hadi sasa Mawakala wetu hali zao sio nzuri bado wapo hospitalini wakiendelea kupatiwa matibabu. Tumekuwa tukijiuliza inakuwaje Pemba CUF hawataki vyama vyengine kushiriki Uchaguzi kwa kuwafanyia vitendo vya kuwapiga, kuwabagua, kuwabughudhi wakati wao wanashiriki katika kila uchaguzi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Ndugu waandishi wa habari,
Haikuishia katika Majimbo hayo tu, bali uvunjaji wa sheria uliendelea katika sehemu mbalimbali za huko Pemba ambapo wafuasi wa CUF waliokuwa wamekaa pembezoni mwa barabara karibu na Vituo vya Makangale, Kisiwani kwa binti Abeid, Chonga, Mtambwe, Wete, Kojani, Mchangamdogo wafuasi hao wa CUF waliwazuia wana CCM wasiende kupigakura.
Mbali na kufanya hivyo, pia katika huduma za usafiri wafanyakazi wa gari za abiria za kutoka Wete kwenda Gando, Konde-Wete, Chake ? Wete kupitia njia kongwe waliwashusha wana CCM na huku katika vituo vyengine vya kupanda abiria wakiwakataa wana CCM wasipande magari yao

Hivi wanataka kutuambia kuwa CCM na vyama vyengine nje ya CUF havina haki ya kushiriki katika Siasa Kisiwani Pemba? Ubaguzi huu haukubaliki na tunawaomba wapenda demokrasia wote na Jumuiya za Kimataifa kuchukia vitendo vya kibaguzi na kihuni vinavyofanywa na wafuasi wa CUF kule Pemba.
Ndugu waandishi wa habari
Tangu siku ya Jumatatu wafuasi wa CUF kule Pemba wanachanganya maji na dawa ya kusafishia chooni au kwenye masinki ya kuoshea vyombo wanawamwagia wafuasi wa CCM ama katika makazi yao au usiku wakiwa wamelala wanawamwagia maji hayo ambayo yanawaletea madhara ya kuwashwa mwilini.
Ni dhahiri kuwa Chama cha CUF hakipati kura nyingi kule Pemba kwa ridhaa ya wapigakura, bali ni kwa kuwashurutisha wapigakura , kutoa vitisho na hata katika baadhi ya Majimbo wanawake wametishiwa na waume zao wasipopiga kura CUF watapewa talaka.
Hali kama hiyo pia imejitokeza katika Shehia za Kijini na Potoa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo wanaume waliwashurutisha wake zao kwamba watakapofika kituo cha kupigia kura wadai hawajui kusoma na kuandika au wana matatizo ya kutokuona vizuri ili waume zao wapige kura kwa Chama cha CUF. licha ya sheria kuzuia mikusanyiko ya watu karibu na vituo vya kupigia kura huko Pemba wafuasi wa CUF walikusanyika karibu na vituo vya kupigia kura Katika majimbo ya Ole, kojani, Chonga, Mkanyageni, Mtambwe, Wete, Jadida, na Konde,. Vituo vya shengejuu pujini, kiuyu, Minungw'ini kulikuwa na wafuasi wa CUF waliokusanyika na hata walipotakiwa kuondoka na polisi hawakutii.
Ndugu waandishi wa habari,
Yote hayo yametendeka mbele ya macho ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi na licha ya mawakala wetu kulalamikia ukiukwaji huo wa demokrasia hakuna aliyewasikiliza. Ni wazi kuwa kuliandaliwa mazingira ya wizi wa kura na ukiukwaji wa taratibu na sheria uliopewa baraka na baadhi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi tunalaani vikali vitendo vya wafausi wa Chama cha CUF na tunaziomba pia Jumuiya za kimataifa kuungana nasi katika kulaani vitendo hivyo ambavyo havikubaliki hata kidogo.
Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka wale wote wanaohusika na uharamia huu na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria.
Sote tunafahamu kuwa misingi ya uchaguzi huru ni pamoja na masuala mazima ya kutotishwa wapigakura, kutoshurutishwa kupiga kura kwa Chama fulani kwa maana mpigakura awe huru kuchagua Chama anachokitaka , kuwepo kwa mawakala na watazamaji wengine wa Uchaguzi mambo ambayo kwa sehemu kubwa hayazingatiwi katika Majimbo mengi kule Pemba.
Wakati tukijiandaa kurejea Uchaguzi wa Zanzibar UVCCM. Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa makini na watendaji wake hasa wasimamizi wa vituo kule Pemba ambao kwa namna moja au nyingine wanashirikiana na Chama cha CUF kuvihujumu Vyama vingine hasa Chama cha Mapinduzi.
Ndugu waandishi wa habari,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na pengine ilijulikana mapema na waangalizi wa Uchaguzi, Makundi ya Waangalizi wa
Uchaguzi hasa wale wa Kimataifa walikipa kisogo Kisiwa cha Pemba. Tujiulizeni kwa nini waangalizi wengi walisalia katika Kisiwa cha Unguja na kukiacha Kisiwa cha Pemba?

Hata hivyo tunazo taarifa za uhakika kuwa baadhi ya waandishi wa habari nao waliondolewa kwa hila na vitisho huko Pemba kwa madai kuwa kungeweza kutokea machafuko ambayo yangehatarisha aidha maisha au usalama wao .
Mpango huo wa vitisho tumepata ushahidi umeratibiwa na kusimamiwa ipasavyo kwa karibu na waandishi wawili wa habari wa kike ambao ni wafuasi na mashabiki wa CUF waliokuwa wakipokea maelekezo kutoka kwa Kiongozi mmoja wa Upinzani huko Zanzibar.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU

ANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA HAPA

Baraza la Mitihani Tanzania - NECTA limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba iliyofanyika September 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini. 
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema jijini Dar es salaam kuwa  jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602 wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 56.99. 

 Dk. Monde amezitaja shule zilizofanikiwa kuingia kumi bora kitaifa mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika nafasi ya mwisho. 

 Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani hiyo.

 Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa. 
BOFYA jina la Mkoa kupata matokeo yake
ARUSHADAR ES SALAAMDODOMA
IRINGAKAGERAKIGOMA
KILIMANJAROLINDIMARA
MBEYAMOROGOROMTWARA
MWANZAPWANIRUKWA
RUVUMASHINYANGASINGIDA
TABORATANGAMANYARA
GEITAKATAVINJOMBE
SIMIYU

MAGUFULI AWASHUKURU WAPIGA KURA


 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 


 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.


 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.


 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.


 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.


Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.


 Mama Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.


 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.


 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba. Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE HAFLA YA KUKABIDHIWA CHETI CHA URAIS DKT MAGUFULI NA MAKAMU WAKE MHE SAMIA SULUHU HASSAN

 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira  na wagombea wengine wakiwa  katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
 Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Damia Lubuva wakiwa tayari katika sehemu yao
 Meza kuu
 Mke wa Rais Mteule Mama Janet Mgufuli akisalimiana na Waziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela na Jaji Joseph Sinde Warioba 
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete