Thursday, January 27, 2011

Migomo migomo tuuuu


Wanafunzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMUCCO) cha chuo kikuu cha Tumaini, ya Masoka kilichopo Mwika Moshi Vijijini wakiwa wamegomea kuingia madarasani jana wakipinga kuchelewa kupatiwa mikopo na miundombinu duni ya majengo chuoni hapo. (picha na Dionis Nyato)

Wednesday, January 19, 2011

Buriani Jaji Mapigano

Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro).
Rais Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo jioni. viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal, Waziri mkuu Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Othman Chande na waziri mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba, walihudhuria Mazishi hayo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Jaji Dan Mapigano wakati wa ibada ya mzishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo jioniTuesday, January 18, 2011

Tigo wazindua huduma ya InternetMeneja Uhusiano wa kampuni ya simu ya Tigo,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kutambulisha huduma yao mpya ya internet leo katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo.kushito ni Meneja Mradi wa Internet wa Tigo,Titus Kafuma.
=========================

Tigo the leading most affordable mobile network in Tanzania, has launched Tigo Internet that is based on the latest 3.5G technology and will offer its customers the fastest and most reliable internet services in Tanzania.

The Tigo Internet is a user friendly service that allows one to browse the web, access social networks, download and listen to music, watch videos at the touch of a button. In addition, Tigo Internet is offered in packages that meet the different internet needs of its customers. These packages allow all our customers to experience world class mobile services at the most affordable prices

Speaking at the launch of Tigo Internet, Titus Kafuma, Tigo Internet Commercial Manager said, "We at Tigo are committed to offering our customers the full range of wireless communication, and Tigo Internet is a stride in bringing the world closer to our customers. We are rapidly changing the way our customers experience their wireless communications as we continue to shape the future of mobile and broadband connectivity in the in the telecommunications industry. He added, "This is yet another value-adding service at affordable rates, benefiting our customers."

The Tigo internet packages include:
* Tigo Light for general surfing: checking emails, blogs, Facebook and other social networks.
* Tigo Standard Offering faster surfing and extra speed for a longer time, to surf the web, download music and watch videos online.
* Tigo Max for people that want to get the fastest surfing and downloading speed, having the ultimate Internet experience.

Tigo is rapidly consolidating its leading position as a multiservice provider, leading by innovation and implementing the latest technologies, a process that started last year with the launch of a robust mobile money service "Tigo Pesa", also with the expansion of network capacity, and now the launch of the first 3.5G network in Tanzania that will provide affordable and reliable internet access.

Monday, January 17, 2011

Darasa jipya alokabidhiwa Rais Kikwete leo


Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wanafunzi wa darasa la saba katika shule Mpya ya Msingi Msoga iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China.Rais Kikwete alikagua madarasa hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa na kaimu Balozi wa China Bwana Fu Jijun huko katika kijiji cha Msoga,wilayani Bagamoyo leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

Tuesday, January 11, 2011

Chuo Kikuu cha Kijeshi Kunduchi

Waziri wa Ulinzi na JKT Dk. Hussein Mwinyi na Meja Jenerali Qian Lihua kutoka nchini China wakikata utepe wakati wa makabidhiano ya Chuo cha Kikuu cha Kitaifa cha kijeshi (NDC) kilichojengwa Kunduchi Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa ameshikilia mfano wa funguo baada ya kukabidhiwa na Meja Jenerali Qian Lihua kutoka nchini China ikiwa ni ishara ya kumkabidhi chuo hicho.

Ninaugua kuongezeka uzito, nina kilo 300 sasa


UKISTAAJABU ya Musa, utayaona ya Firauni. Mambo mengine ni kama hadithi, lakini hii ni habari ya kweli, kwamba yupo mtu mwenye uzito wa Kilo 300 na zaidi, uzito unaoongezeka kila kukicha na kusababishi maumivu makali kwa mtu huyo.
Ni Tabu Kasidi mama wa makamo, mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa Tabata ambaye amejikuta akiongezeka uzito hadi kufikia hatua hiyo bila kujua chanzo cha hali hiyo. Mbaya zaidi ni kuwa uzito huo unaambatana na maumivu makali yanayotishia kukatisha maisha yake.
“Nikisikia maadhimisho ya kifo cha Nyerere na mimi nahesabu mwaka mwingine wa kukaa chini na maumivu makali, imekuwa sehemu ya maisha yangu kwani miaka 11 sasa nimeshindwa kupata ufumbuzi wa tatizo hili” anasema mama huyu akimaanisha kuwa ameanza kupata matatizo hayo kipindi kile Nyerere alipokufa.
Kasidi anasema tatizo hilo lilianza kama jambo la kawaida ambapo alianza kupata maumivu makali sehemu za kiuno na alikuwa akihisi kuvutwa na kitu kiasi cha kulazimika kukaa chini au hata kulala bila kujali mahali alipokuwa.
“Nakumbuka siku moja maumivu yalinipata nikiwa eneo la tabata relini, ambapo nililazimika kukaa chini katikati ya reli hali iliyosababisha wasamaria wema waje kunisogeza pembeni na kuniuliza sababu, lakini niliwaambia waniache kwa muda maumivu yatapungua na nitaweza kuendelea na safari yangu” anasema.
Anasema, wakati huo uzito haukuwa mkubwa sana Alikuwa na kilo 80 tu hali iliyomuwezesha kutembea kwa miguu yake na kuzunguka sehemu mbalimbali, huku akiendelea na biashara zake ndogondogo za kupika chapati, maandazi ili kuweza kujipatia riziki. Imeandikwa na Joyce Mmasi.