Monday, April 30, 2018

NHC YAFIKIA MAKUBALIANO NA HALMASHAURI YA MONDULI KUHUSU NYUMBA ZILIZOJENGWA MJINI HUMO

Shirika limefikia makubaliano na Halmashauri ya Monduli kuhusu nyumba tulizojengwa mjini Monduli. Katika makubaliano hayo yalioongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara, Ndugu William Genya, Baraza la Madiwani limeafiki kununua nyumba 10 zenye thamani ya Sh.1.1bn/- na kuruhusu Shirika kuuza nyumba 10 zilizobaki kwa watu wengine. Picha hapo inamwonyesha Mwenyekiti wa Halmashauri, Ndugu Isack J. Copriano akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi William Genya. Wanaoshuhudia ni baadhi ya madiwani pamoja na Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Ladislaus Bamanyisa
Picha ya pamoja mbele ya nyumba mojawapo iliyokamilika tayari kwa kukabidhiwa kwa Halmashauri wakati wowote. Ujumbe wa Shirika ulimshirikisha pia Katibu wa Shirika, Ndugu Martin Mdoe (hayuko pichani).Picha ya pamoja mbele ya nyumba mojawapo iliokamilika tayari kwa kukabidhiwa kwa Halmashauri wakati wo wote. Ujumbe wa Shirika ulimshirikisha pia Katibu wa Shirika, Ndugu Martin Mdoe (hayuko pichani).Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Ladislaus Bamanyisa akipeana mkono na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha, Isack Joseph (kulia) Wengine kwenye picha ni Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli,  Mama Rose Mhina na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha, Ladislaus Bamanyisa.

Kikao cha maamuzi kati Shirika na Baraza la madiwani kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri. Karibu nae ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Mama Rose Mhina. Kushoto ni ujumbe wa Shirika ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara. Wengine ni Meneja wa Mkoa na Mwanasheria wa Shirrika, ndigu Martin Mdoe.

Friday, April 27, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
  Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma-PICHA NA IKULU

MTOTO WA MIEZI TISA AFA AJALINI BAADA YA BASI LA POLISI, NOAH KUGONGANA USO KWA USO MOROGORO

 Pichani ni  gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro.
Pichani ni  Baadhi ya Askari wa JWTZ na Jeshi la Polisi wakishiriki kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali ya gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro. 
 Baadhi ya Askari wa JWTZ wakitoa msaada kwa majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea.*Dereva wa Noah naye afariki, askari JWTZ, Polisi wajeruhiwa

Na Ripota Wetu,Morogoro 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitha kufariki dunia kwa watu wawili akiwamo mtoto wa miezi tisa Amina Hassan baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha gari ndogo aina ya noah pamoja na basi la Jeshi la Polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu na Michuzi Blog jioni hii kuhusu ajali hiyo Kamanda Matei amesema imetokea saa saba mchana eneo la Mikese Maseyu mkoani humo, ambapo Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo lilikuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam.

Amefafanua mbali ya kufa kwa mtoto huyo dereva wa Noah hiyo iliyopata ajali ambaye amemtaja kwa jina la Zimbao Cornel huku akielezea kujeruhiwa kwa askari Polisi wanne na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) nao wanne na wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa kwenye Noah amesema bado haijathibitika walikuwa wangapi lakini wanaendelea kufuatilia na kisha watatoa taarifa kamili.

Kuhusu hali za majeruhi Kamanda Matei amesema wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika, hivyo kikubwa ni kuwaombea ili wapone haraka na kurejea kwenye ujenzi wa nchi.

Kabla ya kuthibitishwa na kamanda kuhusu ajali hiyo, Ripota Wetu ameshuhudia gari hiyo ya Noah ikiwa imeharibika vibaya na baada ya ajali kutokea waliopoteza maisha na majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa upande wa Muuguzi wa zamu kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoani Edwine Damas amekiri kupokea mwili wa mtoto huyo na majeruhi na wanaendelea kuwapatia matibabu.Friday, April 20, 2018

TANZANIA KUNADI VIVUTIO VYA UTALII DUNIANI KUPITIA TAMASHA LA URITHI WA UTAMADUNI WA MABARA NCHINI UFARANSA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.

...........................................

Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu.

Tanzania inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.

“Kimsingi tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali pamoja na nyimbo.

“Baada ya tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na ninaamini hata zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa wingi  zilizopo Bara la Asia zitaanza kuja,’’. alisema Kigwangla.

Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kuhusisha takriban nchi zote za bara la Afrika, zaidi limelenga kutangaza tamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika mataifa yote yatakayoshiriki  huku likitajwa kuwa tamasha bora na kubwa  la utalii pengine kuliko matamasha mengine yote kutokana na kila nchi kujitokeza kuonyesha vivutio vinavyopatikana katika mataifa yao.

“Tanzania tunavyo vivutio mbalimbali tunavyotarajia kwenda kuvionyesha katika tamasha hilo, ukiacha vivutio vya mambo kale, tuna bonde la Olduvai Gorge na mengineyo, tunayoamini kuwa  kupitia tamasha hilo tutaweza kuyatangaza na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini” alisema Dkt. Kigwangalla. 

Hata hivyo alisema baada ya kukamilika kwa tamasha hilo, Septemba mwaka huu hapa nchini kutakuwa na tamasha la ‘Urithi wa Mtanzania’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka kuadhimisha urithi wa Mtanzania.

Alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi
mzima, pia litatoa fursa kwa kila wilaya kutangaza vivutio vyake, huku akizitaka kila wilaya kujiandaa na tamasha hilo, litakalotoa fursa pia kwa mikoa na wilaya hizo kukuza utalii wa maeneo yao.
 Waziri Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
 Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asngya Bangu akiongoza zoezi la utambulisho.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

 Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax mabula akizungumza katika mkutano huo.
 Picha ya pamoja ya Waziri Kigwangalla na washiriki wa mkutano huo.
 Waziri Kigwangalla akifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom yaingia ubia wa kibiashara kampuni ya iflix

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua apllication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (kulia) akikabiziwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiteta jambo na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja mtandao wa wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akikabiziwa zawadi na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, (wapili kushoto) wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja mtandao wa wa Vodacom watapakua aprication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi.

Kutana na burudani bila kikomo: Vodacom Tanzania yaingia ubia na iflix

Dar Es Salaam, 19 Aprili, 2018 – Kampuni yenye mtandao wa simu za mkononi unaoongoza, Vodacom Tanzania PLC leo imetia saini mkataba wa ubia na kampuni ya iflix, yenye kutoa huduma ya burudani inayoongoza katika nchi zinazoendelea ili kuwapa wateja wa Vodacom huduma hiyo ya iflix bila kikomo. Kampuni hii ya burudani inawapa wateja wa Vodacom uwezo wa kuangalia maelfu ya vipindi bora duniani, sinema na mengine mengi kwenye kila kifaa walicho nacho.

Mteja anatakiwa kupakua App ya iflix, ambapo hakutakuwa na malipo ya aina yeyote. Lakini kuna vifurushi maalum Mteja atabonyeza *149*01# kisha chagua intanet halafu kifurushi ikifuatiwa na iflix. Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 na cha mwezi kwa shilingi 18,000.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Hashim Hendi alisema: “Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini imedhamiria kuiingiza Tanzania katika dunia ya kidijitali na njia mojawapo ya kudhihirisha hili ni kwa dhamira yetu ya kuwapatia wateja burudani isiyo na kifani ya kidijitali. Leo hili linahakikishwa kwa ubia wa kihistoria na kampuni ya iflix. Kuwahakikishia lengo letu la kutoa huduma inayomlenga mteja, siyo tu kuwa tunawapa wateja wetu uwezo wa kufikia burudani bora duniani lakini pia tunajenga jukwaa ambalo wasanii wataweza kutumia kuuza kazi zao. Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom ikielekea kuwa kampuni ya kidijitali inayoongoza barani Afrika ambayo inawezesha maisha ya kidijitali ya wateja wetu. Tunafurahia sana kuwaleta wateja wetu zaidi ya milioni 12 kwenye huduma za iflix.”

Makubaliano haya yanakuja wakati wa mabadiliko makubwa kwenye vyombo vya habari duniani, mabadiliko yanayoleta ongezeko la uhitaji wa maudhui bora kwenye mifumo mbalimbali. Ikiwa imeshasaini makubaliano na zaidi ya kampuni 240 za usambazaji duniani, iflix inawapa watazamaji wake chaguo kubwa la vipindi vya TV vinavyosifika pamoja na sinema zinazopendwa na mashabiki kitaifa na kimataifa kama vile ICE, Saints I Sinners, Riviera, Britannia, Tin Star, Being Mary Jane, Medici Masters of Florence na Luther, pamoja na nyinginezo. Hii ikiambatana na sinema kubwa za Bollywood kama Love Shagun, Sharafat Gayi Tel Lene, Golmaal Returns and Dedh Ishqiya.

Muanzilishi wa iflix na Mkurugenzi Mkuu Mark Britt alisema: “Leo ni siku muhimu kwa iflix. Tunafurahi sana kufikisha huduma yetu yenye ubora wa kimataifa nchini Tanzania na kuingia ubia na Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini. Sisi iflix tunashauku kubwa kuwahudumia wateja wa ndani ya nchi ya Tanzania. Tumedhamiria kuwapatia chaguo kubwa kabisa la vipindi vya burudani, kwa uhitaji na matakwa yao wenyewe waweze kutazama au kupakua kwenye kifaa chochote atakachopenda mteja.”

Upande wa maudhui ya KiAfrika, iflix inatoa sinema za Bongo kama vile Akili  Nyingi, Mama Kubwa, Mapenzi Yamerogwa, Family, Perfect Command, Omega na nyingine nyingi huku kukiwa na sinema na vipindi vitakvyokuwa maalum kwa iflix ambavyo vitatangazwa baadae.

Mkuu wa iflix Afrika Mashariki, Bw. Paul Coogan aliongeza “Tumefurahishwa sana kuileta huduma ya kimataifa ya iflix nchini Tanzania. Ikiwa na vipindi bora kabisa vya TV na sinema kutoka duniani kote, iflix iko tayari kubadilisha kabisa namna ya upatikanaji wa burudani nchini Tanzania. Tunauelewa mkubwa wa watazamaji wa Tanzania na tuna mategemeo mazuri katika ubia wetu na Vodacom kuwafikishia hayo. Huduma yetu nchini Tanzania inawalenga watazamaji wa KiTanzania! Kuanzia uchaguzi wa maudhui hadi jinsi inavyonadiwa, mteja ni kiini wa yote tunayoyafanya.”

Kwa sasa ikiwa inapatikana katika nchi 27 barani Asia, Mashariki ya Kati na  Afrika Kaskazini pamoja na barani Afrika kusini mwa Sahara, iflix inawapatia watazamaji maudhui mengi ya sinema kubwa za Hollywood na vipindi vya TV vya kikanda na kitaifa, nyingi kati ya sinema na vipindi vikiwa ni vipya na ndiyo vinarushwa kwa mara ya kwanza. Kila mteja atakapojiandikisha ataweza kuipata huduma hii kwenye vifaa vitano, ikiwa ni pamoja na simu za kiganjani, laptop, tablet na kwenye TV za nyumbani ili aweze kutazama popote na wakati wowote.

SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA SHILINGI TRILIONI 1.5

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi hapa nchini kinapimwa ili kuchochea maendeleo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali shilingi trilioni 1.51 leo Bungeni mjini Dodoma. 
Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu maboresho yanayopaswa kufanywa katika sekta ya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika Mkoa wa Kagera na katika hosipitali zote za umma. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifutilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO

Serikali leo imelithibitishia Bunge na umma kwa ujumla kuwa kufuatia maneno ya baadhi ya watu yaliyosheheni upotofu, siasa na yenye nia ya kuchafua taswira ya nchi kwamba kuna Shilingi trilioni 1.5 zimepotea, ukweli ni kwamba hakuna upotevu huo na mchanganuo wa matumizi uko wazi.

Akitoa taarifa hiyo ya kina Bungeni leo, huku akiainisha mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesisitiza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, fedha za umma ziko salama na wanaojaribu kufanya ufujaji hatua kali zinachukuliwa. Taarifa kamili yenye aya 12 ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari 2016, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Kauli ya Serikali juu ya madai ya kutoonekana kwa matumizi ya shilingi trilioni 1.51 kwenye matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kuandaa hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (International Public-Sector Accounting Standards – IPSAS Accrual). 

Katika kipindi hicho, Serikali iliendelea kukusanya taarifa mbalimbali kwa kutumia mfumo huu ili kutuwezesha kutambua kikamilifu hesabu za mali, madeni pamoja na mapato yanayotokana na kodi.

 “IPSAS Accrual” ni mfumo wa kiuhasibu ambapo mapato yanatambuliwa baada ya muamala husika kukamilika na sio wakati fedha taslimu inapopokelewa; na matumizi yanatambuliwa wakati muamala wa matumizi umekamilika na sio wakati fedha inalipwa. Mfumo huu ni mzuri na una faida nyingi ikiwa ni pamoja na miamala ya Mapato na Matumizi kutambuliwa wakati husika na siyo wakati wa fedha taslimu inapopokelewa au kulipwa. 

Mheshimiwa Spika, matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa uandaaji wa hesabu kwa mfumo wa “IPSAS Accrual” umeiwezesha Serikali na taasisi zake kutoa taarifa za kina na zinazoonesha uwazi na uwajibikaji wa taasisi husika, hususan katika usimamizi wa mali na madeni ya taasisi. Kuongezeka kwa uwazi, kumewawezesha watumiaji wa hesabu kupata taarifa zinazowasaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kutokana na matumizi ya mfumo huu wa viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika sekta ya umma, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kwamba hakuna fedha taslimu ya shilingi trilioni 1.51 iliyopotea au kutumika kwenye matumizi ambayo hayakuidhinishwa na Bunge. Hivyo basi, madai ya baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu na Serikali yetu ya Awamu ya Tano hayana msingi wowote wenye mantiki. Haya yanadhihirishwa na aya zifuatazo kwenye tamko hili la Serikali.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeeleza jumla ya mapato yote ya Serikali kwa mwaka 2016/17, yalikuwa shilingi trilioni 25.3 ambapo fedha hizi zinajumuisha mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, mikopo ya ndani na nje pamoja na misaada na mikopo nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kuanzia mwaka 2016/17, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianza rasmi kuyatambua mapato kwa mfumo wa Accrual. Hivyo basi, kati ya mapato haya ya shilingi trilioni 25.3, yalikuwemo pia mapato tarajiwa (receivables) kama mapato ya kodi yenye jumla ya shilingi bilioni 687.3 pamoja na mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya jumla ya shilingi bilioni 203.92 (transfer to Zanzibar).

Mheshimiwa Spika, katika uandishi wa taarifa ya ukaguzi, CAG alitumia taarifa za hesabu na nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti (Budget Execution Report) ambapo hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017, mapato yalikuwa jumla ya shilingi trilioni 25.3 na matumizi yalikuwa shilingi trilioni 23.79. Matumizi haya hayakujumuisha shilingi bilioni 697.85 zilizotumika kulipa dhamana na hati fungani za Serikali zilizoiva. Matumizi haya yalikuwa hayajafanyiwa uhamisho (re-allocation) wakati ukaguzi unakamilika. Hivyo basi, baada ya kufanya uhamisho jumla ya matumizi yote kwa kutumia Ridhaa za Matumizi (Exchequer issues) yalikuwa shilingi trilioni 24.4.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ufafanuzi huo, shilingi trilioni 1.51 zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali zilitokana na mchanganuo ufuatao:Maelezo Shilingi Trilioni
Matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva 0.6979
Mapato tarajiwa (Receivables) 0.6873
Mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya Serikali ya Zanzibar 0.2039
Jumla 1.5891
Fedha iliyotolewa zaidi ya mapato (Bank Overdraft) (0.0791)
Fedha zilizodaiwa kutoonekana kwenye matumizi 1.51

Mheshimiwa Spika, hii inamaanisha kwamba, baada ya kupunguza mapato ya Zanzibar ya shilingi bilioni 203.92 na kupunguza mapato tarajiwa ya shilingi bilioni 687.3, mapato halisi kwa mwaka 2016/17 yalikuwa shilingi trilioni 24.41. Aidha, baada ya kujumlisha matumizi ya dhamana na hati fungani zilizoiva za kiasi cha shilingi bilioni 697.85 kwenye matumizi ya shilingi trilioni 23.79 yaliyooneshwa katika Taarifa ya CAG, ridhaa za matumizi zilizotolewa zilikuwa shilingi trilioni 24.49 na kuleta ziada ya matumizi ya shilingi bilioni 79.07 ikilinganishwa na mapato. 

 Kwa mchanganuo huu, ni dhahiri kwamba kwa mwaka 2016/2017 matumizi ya Serikali yalikuwa makubwa kuliko mapato kwa shilingi bilioni 79.09 ambazo ni Overdraft kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Utaratibu wa kutoa fedha zaidi ya mapato (Overdraft facility) uko kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

Hitimisho

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepata mafanikio makubwa katika uandaaji wa Hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo huo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS Accrual). Itakumbukwa kwamba, katika Afrika, Tanzania ndio nchi pekee iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa kuandaa hesabu kwa kuzingatia matakwa ya IPSAS na kufanikisha kuandaa hesabu za Majumuisho kwa kuzingatia mfumo huo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo haya ya Serikali, napenda kulitaarifa Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumla kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ipo makini na haiwezi kuruhusu upotevu wa aina yoyote wa fedha za umma. Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuona kwamba, kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo na kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, na naomba kuwasilisha.