Thursday, February 28, 2013

‘Wafuasi 54 wa Ponda wana kesi ya kujibu’


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imetathmini ushahidi wa upande wa mashtaka yanayowakabili watu 54, wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na kubaini kuwa wana kesi ya kujibu.Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya maandamano yaliyozuiliwa na polisi, kukusanyika isivyo halali , uchochezi na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo ambaye alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka na vielelezo , mahakama imeona kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na kwamba wanapaswa kutoa utetezi wao. 
Mapema wakili wa washtakiwa hao, Mohammed Tibanyendera aliiomba mahakama iwaachie huru washtakiwa kwa madai kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, umeshindwa kuthibitisha makosa dhidi ya washtakiwa. 
Wakili Tibanyendera alidai kuwa, mashahidi wa upande wa mashtaka wote walikiri kuwa hakuna hata mmoja aliyewahi kuona tangazo la kuzuia maandamano.
Pia alidai kuwa hakuna ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ukionyesha kuwa kulikuwa na maandamano na kwamba mashahidi wote waliithibitishia mahakama kuwa walishiriki katika kukamata washtakiwa kwa njia ya simu ya upepo ya polisi. 
Wakili huyo pia alidai kuwa mikusanyiko haikuwa ya kuvunja amani na kwamba wala hakuna shahidi hata mmoja aliyeieleza mahakama kuwa alishuhudia uvunjifu wa amani ama malalamiko kutoka kwa majirani kuhusu hofu.
“Hii inadhihirisha kuwa mkusanyiko waliokuwa nao washtakiwa ulikuwa halali na hakukuwa na amri yoyote ile ya kuzuia watu kukusanyika katika Jamhuri ya Tanzania hapo Februari 15, mwaka huu,” alidai wakili huyo.
Pia wakili huyo wa kujitegemea alidai kuwa hakukuwahi kutolewa wakati wowote ule, amri ya kuzuia mkusanyiko na kwamba walizuia maandamano.

Wakili Tibanyendera alidai kuwa ukamataji wa wateja wake, ulifanyika baada ya Swala ya Ijumaa, na kwamba watu walikamatwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Mkunguni na Makunganya.

Alifafanua kuwa waliokamatwa katika maeneo ya Mkunganya walikamatwa umbali wa mita 100 kutoka msikitini, DIT walikuwa karibu na kituo cha daladala na waliokamatwa katika eneo la Mkunguni walikuwa karibu na misikiti takriban mita tatu.
“ Huu ni uwiano mkubwa wa kimazingira, tulitarajia tutapata ushahidi tofauti baina ya watu waliotenda kosa na waliokusanyika katika nyumba za ibada,” alidai wakili huyo wa utetezi.

Baada ya kumaliza kutoa hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola aliiomba mahakama iwaone washtakiwa kuwa wana kesi ya kujibu.
Hakimu Fimbo aliiahirisha kesi hiyo hadi leo washtakiwa watakapoanza kujitetea.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya upande wa mashtaka kupitia mawakili wa Serikali waandamizi, Benard Kongola, Nassor Katuga na Joseph Mahugo kufunga ushahidi wao.

Upande wa mashtaka ulifunga ushahidi wake baada ya kupeleka mashahidi 10 mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya washtaka wakiambatanisha pia vielelezo 12.
Alidai kuwa Februari 11, mwaka huu alipokea barua kutoka katika Shura ya Maimamu, ikimwomba kibali cha kufanya maandamano ya kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Alidai kuwa barua hiyo ilisainiwa na Sheikh Juma Idd na kwamba ndani yake pia ilikuwa inahoji sababu za kutokumpatia dhamana Sheikh Ponda .
Pia walikuwa wakitaka maandamano hayo, yafanyike Februari 15, mwaka huu baada ya Swala ya Ijumaa na waandamanaji watakuwa wakitokea katika misikiti mbalimbali.
ACP Msangi alidai kuwa yeye na maofisa wenzake, walitafakari barua hiyo ili kujua uzito wa maandamano hayo.
Alidai kuwa Jeshi la Polisi lilibaini kuwa halikuwa na askari wa kutosha kuwapeleka katika kila msikiti kwa ajili ya kuwalinda waandamanaji.
Habari na Tausi Ally
Chanzo - Mwananchi

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Al Youseif Sheikh Abdullah Mohamed Alyouseif, Azungumza na Dk Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na  Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Al Youseif Sheikh Abdullah Mohamed Alyouseif, alipofika Ikulu Mjini
Zanzibar kuzungumza na Rais leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na  Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Al Youseif Sheikh Abdullah Mohamed Alyouseif, alipofika Ikulu Mjini
Zanzibar kuzungumza na  Rais leo.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Azindua Mpango Mkakati wa GS1 Tanzania kwa miaka 5

Kaimu Mkurugenzi wa GS1 Tanzania, Fatma Kange akizungumza wakati wa kikao cha tatu cha wadau wa GS1 Tanzania katika Hotel ya Blue Pearl,Ubungo Plaza,jana Feb,27,2013. 
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho cha GS1 Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa GS1 Tanzania,Yakub Hasham akizungumza na wadau  mbalimbali waliohudhuria kikao cha tatu cha washika dau na kikao cha pili cha mwaka cha GS1 Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Joyce Mapunjo akifafanua jambo juu ya umuhimu wa Barcodes katika kuinua soko la bidhaa zetu.
Salum Awadh akiwasilisha  mpango mkakati wa GS1 Tanzania wa kipindi cha mwaka 2013-2018 kama Mtaalamu Mshauri ( Consultant) wa GS1 Tanzania.
Mwenyekiti wa Amsha Institute of Rural Entrepreneur ,Biubwa Ibrahim Malengo akizungumzia mafanikio ya kikundi chake kutoka Lindi Vijijini.
Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua Kikao cha tatu cha washika dau katika Hotel ya Blue Pearl, Ubungo Plaza,jana,Feb 27,2013
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia washika dau wa GS1 Tanzania jana

BOHARI YA DAWA (MSD) YAONESHA VIFAA TIBA VYA KISASA KATIKA MAONESHO YA WADAU WA HUDUMA ZA AFYA KUSINI MWA AFRIKA

 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Florida Sianga (kulia)) akiwaelekeza Monica Gofrey (kushoto) na Geofrey Kandi kifaa tiba aina ya sterilizer inayotumia gesi katika maonesho ya Shirikisho la Wadau wa Huduma za Afya Kusini Mwa Afrika, leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
                                              Wageni hao wakiendelea kupata maelezo

 Kitanda cha wagonjwa ambacho ni baadhi ya vifaa tiba vinavouzwa na MSD
                                              Kifaa Tiba aina ya kitasishaji 'Starilizer' inayotumia gesi
                                                                 Kitanda cha kujifungulia
 Kabati la kusambazia dawa wodini 'Dispensing Trolley'
                                           Banda la MSD linavyoonekana kwenye maonesho hayo


(PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF KUFANYIKA MACHI 7 NA 8 JIJINI DAR

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
TAARIFA KWA UMMA
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano Mkuu wa wadau utakaofanyika tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF - Golden Jubilee Towers , Dar es Salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es Salaam au Ofisi za PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.
“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,
Golden Jubilee Towers, Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
Central Area, Kiwanja Na. 8, 9, 12 na 15,  S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255 22 2120912/52 au +255 22 2127375 /6
Nukushi: +255 22 2120930.

Rais Jakaya Atembelea Makao Makuu ya JKT Dar

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea jana February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa  uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake jana February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yao jana February 27, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea jana February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea jana February 27, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka kwenye uwanja wa sherehe baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa  uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake jana  February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.Picha na IKULU

Wednesday, February 27, 2013

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Afungua Warsha ya Wadau Bagamoyo

 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akifungua Warsha ya Wadau ya Kupitia na Kujidili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Nihgu Warsha imefanyika kwenye Hotel ya Palmtree Village Bagamoyo.
 Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Richad Muyungi akimwambia jambo Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Daniel Nkondola Mara baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Wadau wa Kujidili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini Warsha imefanyika Hotel ya Palmtree Village
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akimsikiliza jambo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Raisi Bw Richad Muyungi mara Baada ya Ufunguzi waWarsha ya Wadau wakupitia na Kujadili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Warsha ya Kupitia na Kujadili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini.Picha na Ali Meja

Spika Makinda akutana na Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack

 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot)  akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano  na Bunge la Namibia kwani kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
  Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa  nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele.Picha Na Prosper Minja-Bunge.

Benedict XVI to hold final papal audience in Vatican

Crowds have begun gathering in St Peter’s Square in the Vatican for the Pope’s final general audience before his resignation on Thursday.
Papal audiences are normally held inside a Vatican hall in the winter.
But such is the level of interest that the event is being held outdoors and 50,000 tickets have been requested.
 As many as 200,000 people may attend.
After Benedict XVI steps down on Thursday, he will become known as “pope emeritus”.
There has been no papal resignation since Pope Gregory XII abdicated in 1415.
The surprise announcement of Benedict’s abdication has required the rules of electing a successor to be changed to allow the next pope to be chosen before Holy Week, which leads up to Easter.
On Wednesday, the Pope, 85, will be making one of his last public appearances – using his trademark white “popemobile” to greet pilgrims in St Peter’s Square.

WAMA WAKABIDHI VIFAA VYA AFYA MKOANI RUKWA

 
Na Anna Nkinda-Sumbawanga
 Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imeikabidhi hospitali ya mkoa wa Rukwa - Sumbawanga kontena la  urefu wa futi 40 lenye mitambo ya kisasa na vifaa vya huduma ya afya ilivyochangiwa na Shirika linayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu la  Project C.U.R.E la nchini Marekani vyenye thamani  ya zaidi ya shilingi milioni mia saba .

Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika viwanja vya Hospitali hiyo ambapo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo aliwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuvitunza na kuvitumia vifaa hivyo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi na si vinginevyo.

Akiongea na wananchi wa mkoa huo pamoja na wahudumu wa afya waliohudhuria hafla hiyo  Mama Kikwete alisema kuwa kupatikana kwa vifaa hivyo ni kutokana na changamoto mbalimbali alizokuwa  ameelezwa katika ziara zake za mikoani ambazo zilimpa  msukumo mkubwa wa kwenda mataifa mbalimbali kwa kuwa  aliona anao wajibu wa kufanyia kazi matatizo aliyoelezwa yakiwemo ya upungufu wa vifaa vya kutolea huduma za afya. 

 “Bila ya shaka yoyote vifaa na mitambo ninayoikabidhi leo vitafanya kazi kubwa katika kutoa huduma bora zaidi ya afya  na kuokoa maisha ya wananchi wetu katika hospitali ya Sumbawanga”, alisema Mama Kikwete.

Akisoma taarifa ya Hospitali hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. John Gurisha alishukuru kwa mitambo na vifaa tiba walivyopewa  na kuahidi kufanya kazi kwa uwezo wao wote ili kufanikisha azma ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dk. Gurisha  alisema kuwa hospitali hiyo inahudumia wakazi wa mkoa huo na Katavi wapatao 1,760,639  na wanatoa huduma za tiba, kinga na ushauri wa kitaalamu. Inauwezo wa kuwa na vitanda 450 na wastani wa kulaza wagonjwa 300 kwa siku  lakini kwa sasa inavitanda 270 na inalaza wagonjwa 160 kwa siku. 

“Baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo ni upungufu wa watumishi wenye ujuzi, ucheleweshaji wa matengenezo ya vifaa mara linapotokea tatizo na hivyo kusababisha wagonjwa kutopata huduma inayostahili kwa wakati na  imani na mila potufu katika jamii imekuwa ni kipingamizi kikubwa katika utoajia wa huduma bora za afya kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakichelewa kufika hospitali mpaka wapitie kwanza kwa waganga wa jadi”, alisema Dk. Gurisha. 

Aliyataja mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kuwa ni kuajiri madaktari saba na wauguzi 11, wamepata wateknolojia watano wa maabara kutoka Taasisi ya Benjamini William Mkapa, wamejenga chumba cha kuhifadhi dawa za chanjo, wodi ya wagonjwa wa akili, wodi moja ya daraja la kwanza , maabara ya kisasa kwa msaada wa Serikali ya Marekani, chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Project C.U.R.E Dk. Abdul Kimario alimpongeza Mke wa Rais kwa jitihada alizozifanya kwa muda mrefu za kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vimefika nchini na kuwaomba watanzania wamuunge mkono kukabiliana na upungufu wa vifaa tiba mahospitalini kwani jitihada alizofanya ni kubwa na  amepanda mbegu ambayo itaota kwa miaka mingi.

Dk. Kimario alisema kuwa kabla ya kutumwa kwa vifaa hivyo nchini alikuja kufanya tathimini na kuangalia ni Hospitali gani inamahitaji makubwa zaidi na kugundua kuwa hospiatali za Rukwa (Sumbawanga) na Lindi zinamahitaji makubwa ukilinganisha na zingine.

 “Shirika letu linafanya kazi katika nchi 125 zinazoendelea, tumieni nafasi hii kwa kushirikiana na WAMA ili muweze kupata vifaa tiba katika Hospitali zenu za wilaya na mikoa kwani vifaa tunavyo vingi  na baadhi ya nchi tulizozipelekea vifaa ni Jamuhuri ya watu wa Kongo, Malawi, Nigeria, Ghana, Tunisia, Mauritania, Ethiopia, Sudani, Kenya na Uganda”, alisema Dk. Kimario.

Kupatikana kwa vifaa hivyo ni jitihada ya Mama Kikwete za kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua hapa nchini kutokana na hilo Shirika la Project C.U.R.E ilifanya harambee ya kumuunga mkono mwezi wa nne mwaka 2011 na kumchangia  makontena matano ya vifaa vya afya vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni tatu sawa na shilingi bilioni 4.5 za kitanzania.

Kabla ya kutumwa  kwa vifaa hivyo wataalamu kwa afya kutoka Project C.U.R.E walikuja  nchini kufanya tathimini ya vifaa vinavyohitajika katika Hospitali na Kliniki ambazo zilipendekezwa  na wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ili kutambua mahitaji mahususi, tecknolojia na nishati iliyopo kwani  kila kifaa kilichotolewa kinahitajika mahali husika  na kinaweza kutumika katika mazingira na tecknolojia iliyopo.

Baadhi ya mitambo iliyokabidhiwa ni  mashine ya  Ultra sound, vifaa  vya X-ray, mitambo na vitanda maalum cha ICU kwajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa mahututi, vifaa vya upasuaji mkubwa na mdogo, vifaa vya upasuaji na tiba ya macho ya kisasa (laser), mitambo, viti  na vifaa vya huduma ya tiba ya kinywa na meno, vifaa vya tiba, mitambo na tiba ya mgongo na mifupa na  taa ya meza maaluma ya upasuaji na  mashine ya usingizi (anaethetic machine) 

Kontena moja lenye  mitambo na vifaa tiba limeshakabidhiwa kwa Hospiali ya mkoa ya Lindi Sokoine na mengine yatapelekwa katika  Hospitali za mikao ya Simiyu, Tabora, Tumbi na Mtwara .

Chakula cha Jioni kwa Ujumbe wa Oman huko Zanzibar

IMG_0217
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini, (kulia)  akimkabidhi
zawadi ya Kasha  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman  Yussuf bin Alawi bin
Abdullah,akiwa kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,baada ya
 hafla ya chakula maalum,kilichoandaliwa kwa ujumbe huo,katika Hoteli
ya Serena Mjini Zanzibar jana.
IMG_0164
Baadhi ya Viongozi wa Ujumbe wa Nchini Oman na
Viongozi wa Taasisi mbali mbali hapa Zanzibar wakiwa katika  hafla ya
chakula  maalum kwa ujumbe wa wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa
na Waziri Yussuf bin Alawi bin Abdullah,(hayupo pichani) katika Hoteli
ya Serena Mjini Zanzibar jana.
IMG_0172
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi bin
Abdullah,akichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa  kwa
ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri Yussuf,katika
Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.
IMG_0174
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,na Mawaziri wengine
walipoungana katika hafla ya chakula  maalum kwa ujumbe wa wa Serikali
ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri Yussuf bin Alawi bin
Abdullah,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.
IMG_0177
Viongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Watu wa
Oman,wakichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa  kwa
ujumbe huo,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.
IMG_0186 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,(kushoto) akiwa na mgeni
wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman  Yussuf bin Alawi bin
Abdullah,akiongoza ujumbe wake katika hafla ya chakula
maalum,kilichoandaliwa kwa ujumbe huo,katika Hoteli ya Serena Mjini
Zanzibar jana.

FLAVIANA MATATA kazini


 Backstage Blonds Fall 2013; Red eyes, black liners, big blonde wigs and  funky nails!
See more images after the jump