Wednesday, December 30, 2015

WAZIRI WA AFYA ,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)

UY1

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia
UY2
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo
UY3
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo ,kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo
UY4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini
UY6
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo
UY8
Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa
UY9
Waziri Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari  Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya Afya)
…………………………………………………………………………………
 Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali na hilo, waziri huyo wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.
Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya Makao Makuu, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia

No comments: