Tuesday, March 15, 2011

Flaviana Matata is Arise Magazine’s Model of the Year!

Model of the Year: Flaviana Matata

Lagos. Tanzanian model Flaviana Matata has won the Model of the Year award by Arise Magazine Lagos Fashion Week. It's been a good year for Flaviana who has been featured in numerous United States editorials including Dazed & Confused, Glass Magazine, L'officiel and soon to be in ID Magazine.

She has also walked the runways of some of fashions most influential designers, including Vivianne Westwood, Tory Burch, Suno, and Louise Gray and was featured in the Alexander McQueen film tribute and Topshop Spring 2011 ad campaign. Sky is the limit for her.

The event, that took place in Lagos, starting 13th March, also saw designer Mustafa Hassanali showcase his latest collection.

BRIEF BACKGROUND: ABOUT THE MODEL

Flaviana Matata (born 1987) is a Tanzanian beauty queen and fashion model. She won the first edition of the Miss Universe Tanzania pageant in 2007, and went on to represent the contest in the Miss Universe pageant the same year, where she placed among the Top 15 semifinalists and ended up in 6th place after the evening gown competition. Recently she modeled print advertisements for Sherri Hill.Habari zaidi waweza kubonya hapaUpate tukio hilo kwa kina.Sunday, March 13, 2011

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Rais Jakaya Kikwete, akiangalia ndege ya kijeshi JW 9242 F 7 G wakati alipotembelea kikosi cha Anga cha JWTZ Airwing Dar es salaam jana.Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mtaalamu msaidizi wa rubani wa ndege za kijeshi za Jeshi la China,aliyetambuliwa kwa jina moja la Gao, akimwonesha Rais Jakaya Kikwete namna urushaji wa ndege ya kijeshi kutoka China wakati Rais alipotembelea Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiteremka kutoka kwenye ndege ya kijeshi ya JWTZ JW 9242 F 7 G kutoka china wakati alipotembelea kikosi cha Anga Dar es Salaam Jana

Lema azitungia wimbo vurugu za Arusha


Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alipoonyesha CD iliyobeba wimbo alioutunga kuelezea vurugu na vifo vya Arusha, kulia ni Katibu wa Kanda ya Kinondoni Chadema Henry Kilowo. Picha na Venance Nestory.

Wednesday, March 09, 2011

Siku ya wanawake dunianiWanamuziki wa bendi za The African Stars na Msondo Ngoma baba ya muziki wakitumbuiza jana katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kuadhimisha miaka 100 inayofanyika kila mwaka March 8.


Siku ya Wanawake Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1911 wakati makundi ya wanawake nchini Marekani yalipokusanyika na kupinga udhalilishaji, ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa kijinsia hususani sehemu za kazi. 


Sunday, March 06, 2011

Maelfu yafurika kutibiwa magonjwa sugu Loliondo

misururu ya magari mbali mbali iliyoleta wagonjwa na wasio wagonjwa kwenda kunywa dawa dawa ya Mugariga katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, aliyooteshwa na Mzee Mwasapile mwaka 1991.

Mchungaji Ambikile Mwasapile akifuata dawa katika nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Samunge.Dawa hiyo ikishachemshwa huingizwa ndani na kuiombe kisha kuwanywesha wgonjwa.

Gari inayoonyesha namba za usajili SM, ni mali ya Manispaa ya Arusha. Gari hili ni moja ya magari ya Serikali yakiwa nayo yanasonga mbele kwenye foleni ya kunywa dawa inayogawiwa na mchungaji Mwasapile kwa kikombe abiria wakiwa humohumo ndani ya gari.
watu wakiwamo waasia mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha, Manyara na sehemu kadhaa za Tanzania na nje ya Nchi wakisubiri dawa ya Mugariga kwa ajili ya kujitibu.


*NI KWA MCHUNGAJI ANATIBU KISUKARI, PUMU, SARATANI NA UKIMWI

MAELFU ya watu, wakiwemo vigogo wa serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa nchini, wamefurika katika Kijiji cha Samunge Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata 'dawa ya maajabu ya Mungu' inayodaiwa kutibu magonjwa mengi sugu ikiwamo Ukimwi.

Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1,000 yakiwamo magari ya serikali, binafsi na mashirika ya kimataifa ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yamefurika katika kijiji hicho kilichopo umbali ya takriban kilometa 400 kutoka Jiji la Arusha.

Dawa hiyo, inatolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76), ambaye anasema alioteshwa na Mungu kuitumia kutibu tangu mwaka 1991.

Mchungaji Mwasapile ambaye alifanya mahojiano na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake wakati akiendendelea kutoa dawa kwa wagonjwa wake, anasema ndoto hiyo aliendelea kuota mara kadhaa hadi Agosti 26 mwaka jana alipoanza rasmi kutibu.

Anasema dawa hiyo inatokana na mti aina ya mugariga na yeye pekee ndiye anaweza kukupatia na kunywa kikombe kimoja pekee na ukinywa tu inaanza kazi ya kutibu maradhi sugu ya ukimwi, kisukari, pumu na saratani.

Mchungaji Mwasapile anasema gharama za dawa hiyo ni Sh500 tu na dozi yake ni kikombe kimoja tu na hairuhusiwi kurudia kuinywa. Kabla ya kukamilika mchungaji huyo huiombea dawa hiyo na kuichemsha katika majisafi.

“Mungu ameniotesha kutoa dawa hii kwa Sh 500 aliponiambia hata mimi nilishangaa. Kwanza aliniambia niwape watu wapone saratani, kisukari, pumu na magonjwa mengine na baadaye akanionyesha kuwa dawa hii niwape hata wagonjwa wa ukimwi na watapona,“ anasema Mwasapile. Habari hii imeandikwa Mussa Juma na Daniel Sabuni, Loliondo.Habari zaidi waweza kubonya hapaUpate tukio hilo kwa kina.