Thursday, March 29, 2007

Katikati ya jiji la Dar es Salaam


Mtaa wa Samora karibu kabisa na mnara wa saa.

Antena


Hizi antena zimeingia kwa kasi bongo moja inauzwa hadi 30,000. zinaona hizooo.

barabara

ukishuka katika mawe yale unapita katika hii barabara.

Mawe

mawe haya yapo nje kidogo ya mji wa Shinyanga, ndiyo yanakukaribisha katika mkoa huo.

hawa ni wangu


mbuzi mbuzi mbuzi.

tiba


Daktari wa mifugo, Paschal Alphonce akiwapatia tiba mifugo wa wilaya yake. Mbuzi pamoja na tiba walitolewa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Oxfam.

shambani


Shamba la mahindi yapo makini vipi huko.

Monday, March 19, 2007

Watoto wa bongo

Watoto halisi wa bongo hawa wakiwa kwao.

Tembe

Nyumba aina ya matembe ambazo ni maarufu sana katika maeneo mengi nchini. Hapa ni kijiji cha Mangu, Shinyanga.

Barabara


Pichani mojawapo ya barabara za vijijini ikiwa imekarabatiwa tayari kwa matumizi. Hii ni sehemu kijiji cha Mangu kilichopo huko Meatu mkoani Shinyanga.

Monday, March 12, 2007

Kama tumekosa kauli, basi tunyamaze tusijiabishe

KAULI ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu yeyote awaye. Kauli yaweza kuchonganisha. Inaweza pia kufurahisha, kutoa matumaini, kuleta balaa wakati mwingine na hata kuleta madhara makubwa.

Kauli ndizo huweza kumtambulisha mtu na kutambua yukoje mbele ya wenzake. Huweza kuwafanya watu wengine watambue ni kiasi gani mtu wanayezungumza naye kaiva au kukomaa au vinginevyo.

Kwa jumla, kauli humchonganisha au kumkutanisha mtu na watu wengine. Kisiasa, kauli hujenga mtaji kwa mwanasiasa kukubalika na hasa kama anajua namna ya kuzipangilia hoja kimantiki, lakini hasa zikiwa zenye kubeba ukweli na uhalisia wa mambo.

Kwa kawaida, imezoeleka kuwa kauli nyingi zinazotoka midomoni mwa wanasiasa kuwa ni za uongo, huchukuliwa hivyo kwa sababu mara nyingi hutolewa ili kutumika kama chambo cha kuwavuta wananchi kuwachagua na kisha wakishawachagua wanawasahau. Lakini, si kweli wakati mwingine kuna ukweli fulani.Soma kwa urefu zaidi hapa