Sunday, May 31, 2009

PAMBANO LA CHEKA NA NADILOV


MSAIDIZI wa bondia Ramil Nadilov akimfuta damu bondia wake mara baada ya raundi ya kwanza kumalizika hata hivyo bondia huyo akuweza kumaliza pambano hilo lililokuwa la raundi 12, kutokana na jeraha hilokatika jicho.

KATIBU tawala wa Mkoa wa Tanga, Paulo Chikira (kushoto na Promota wa Pambano hilo Zumo Makame wakimnyanyua mikoa Francis Cheka mara baada ya kumchapa kwa KO ya raundi ya pili Bondia Ramil Nadilov na kutwaa wa mabara wa UBO.


Francis Cheka akipambana na Ramil Nadilov katika pambano la kimataifa la kuwania ubingwa mabara wa UBO lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga jana,Cheka alishinda pambano hilo katika raundi ya pili kwa KO na kutwaa ubingwa huo, Picha zote na Samuel Msuya, Tanga.


Dr Salim kumbukumbu ya Tajudeen
DK Salim Ahmed Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) akiwaongoza wasomi mbalimbali waliojitokeza katika kumbukizi la kumkumbuka aliyekuwa mwanaharakati wa masuala ya kijamiii Dr. Tajudeen Abdul Raheem aliyefariki dunia kwa ajali ya gari. Kumbukizi hilo lilifanyika katika ukumbi wa COUNCIL CHAMBER Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumbukizi liliandaliwa na "THE MWALIMU NYERERE FOUNDATION In collaboration with UDASA.

Majenerali Waitara na Sayore ndani ya golf


Majenerali hawa wawili George Mwita Waitara na mtangulizi wake Gideon Waitara ni miongoni mwa wachezaji wa golf waliokuwapo katika michuano ya Golf ambapo zaidi ya 120 toka vilabu mbalimbali vya mchezo huo nchini, wanashiriki katika mashindano ya wazi ya Lugalo yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji hao wa ridhaa na wale wa kulipwa, wanatoka katika vilabu vikubwa vya mchezo huo vilivyopo Mufindi mkoani Iringa, TPC Moshi, Gymkhana Morogoro, Dar es salaam pamoja na wenyeji JWTZ Lugalo.

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Husein Mwinyi ndie aliyefungua rasmi michuano hiyo, kwa mujibu wa katibu mkuu wa klabu ya golf ya Lugalo JWTZ John Nyalusi

Mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya zaid kwa kitita cha shilingi milioni saba, ambapo meneja masoko wa zain Costantine Magavila, amesema msisimko wa mashindano hayo ndio umewasukuma kujitosa katika kuyadhamini

Mashindano ya golf ya wazi ya Lugalo, ni miongoni mwa mashindano makubwa ya mchezo huo yanayotambuliwa na chama cha mchezo wa golf cha taifa TGU.

Diamond Musica si mchezo!!!


Hawa ni Diamond Musica wakishambulia jukwaa.

Hawa ni Diamond Musica wakishambulia jukwaa.


Kundi la akina dada linaloongozwa na mwadada WAHU kutoka Kenya alipagawisha wageni kwa mapigo yake na umahiri wa kuimba katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jana. Picha na Fidelis Felix

Miss Universe huyu hapaMiss universe Tanzania 2009 Illuminata James, pose the group pictures with second run up Hidaya Maeda (Left) Fist run-up Evelyne Almasi after announced the winner’s in Dar es Salaam on Saturday evening at Milimani City Hall. Photo/ Fidelis Felix

Kikwete azindua mradi mkubwa wa maji
RAIS Jakaya Kikwete amezindua mradi mkubwa wa maji kuliko yote Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Ziwa Victoria ambao umegharimiwa na Serikali ya Tanzania bila ya msaada wa wahisani kwa zaidi ya Sh bilioni 200.

Uzinduzi huo ulionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa,TBC1.

Katika hotuba yake ya uzinduzi uliofanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza jana, Rais Kikwete alisema uzinduzi huo ni sehemu tu ya utekelezaji wa ahadi za serikali yake kwa wananchi .

Alisema mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake za kuwapatia wananchi maji safi na salama.

Aidha alimsifu Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyekuwapo katika uzinduzi huo kwa uthubutu wa kuamua kuanzishwa kwa mradi huo.

“Ndani ya Ilani ya CCM, mradi huu ulipaswa kukamilika mwaka 2010, Rais Mkapa alituachia na akaamini tutaweza na kweli Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha mradi huo kabla ya wakati uliokuwa umepangwa.

“Hii inadhihirisha CCM inaweza. Tumewaweza Busanda na bado tutaendelea kushinda, na mradi huu ni ushahidi,” alisema Rais Kikwete.

Pichani:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza msichana Martha Philipo kutoka katika kijiji cha Iselamagazi,Shinyanga, mara baada ya kuteka maji na kumtwisha ndoo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kuchotea maji iliyofanyika kijijini hapo jana jioni.Kituo hicho cha kuchotea maji ni moja kati ya vituo vingi vya kuchotea maji vilivyo katika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga.Pembeni ya Rais ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.

Picha nyingine Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua bomba la maji katika kituo cha kuchotea maji katika kijiji cha Iselamagazi wakati wa hafla ya kufungua kituo hicho iliyofanyika katika kijiji hicho jana mchana.

Pia Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Waziri wa Majui Profesa Mark Mwandosya wakizungumza wakati wakikagua mitambo mikubwa ya kusafisha maji iliyopo katika kijiji cha Ihelele Wilaya ya Misungwi jana mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa nmdiye aliyeasisi mradi huo mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga (Picha zote na Freddy Maro)

Meli yapinduka Zanzibar, watatu wafariki dunia 
MELI ya mizigo ya inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul, Mv Fatih imepinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar usiku wa kuamkia jana na maiti za abiria watano zimepatikana huku juhudi za ukoaji zikiendelea.

Meli hiyo inayodaiwa kuwa na watu 27 na mizigo yenye uzito wa tani 76 ilipinduka na kuzama ikiwa tayari imekaribia kutia nanga katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar ikitokea Dar es Salaam.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Bakari Khatib Shaaban amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo alisema ilipinduka saa 4.00 juzi usiku katika bandari ya Malindi na abiria waliokuwemo walikuwa wanataka kushuka lakini ghafla ilipinduka na kuzama baharini.
 
Kamanda Shaaban alisema hadi jana mchana ni maiti tatu tu ndizo zilizoonekana ikiwamo ya mtoto mdogo wa kiume, na mwanamke na mwanaume ambao hawakuweza kufahamika majina yao kamili.
 
Waliookolewa katika ajali hiyo ni Machano Mkinai Mkaazi wa Mkwajuni na Kitiba Mussa Kitiba, Gamba Mkoa wa Kaskazini 'A' Unguja, Halima Mussa wa Arusha, Hassan Omar, Maulid Abdallah, wote wa Kisiju Mkoa wa Pwani.
Salma Said, Zanzibar soma kinagaubaga taarifa hapa
upate habari hizi kwa kina pia tutakuwa tukikuletea taarifa zinazoendelea kutokea visiwani humo

Friday, May 29, 2009

Ruling CCM Dominates Tanzania Politics(Angus Reid Global Monitor) - The Revolutionary State Party (CCM) is clearly the dominant political party in Tanzania, according to a poll by REPOA, Michigan State University, and Afrobarometer. 79 per cent of respondents would vote for the nominee of the CCM in the next presidential election.

The candidates representing the Civic United Front (CCW) and the Party for Democracy and Progress (CHADEMA) are far behind, with four per cent each. Only one per cent of respondents would support the candidate of the National Convention for Construction and Reform (NCCR).

Tanzania held presidential and legislative elections in December 2005. The CCM’s Jakaya Kikwete won the ballot with 80.2 per cent of the vote. His party also won most of the seats in the legislature, followed by the CCW.

On May 21, Kikwete met with United States president Barack Obama and U.S. state secretary Hillary Rodham Clinton in Washington. The Tanzanian president told Clinton before his meeting with Obama: "I’m here to reaffirm our commitment for continued cooperation and friendship. We have excellent relations on a political level, a bilateral level. We see eye-to-eye on many international issues. We work together at the multilateral level. I’m here to give you that assurance for continued cooperation efforts."

Polling Data

If a presidential election were held tomorrow, which party’s candidate would you vote for?

Revolutionary State Party (CCM) 79%
Civic United Front (CUF) 4%
Party for Democracy and Progress (CHADEMA) 4%
National Convention for Construction and Reform (NCCR) 1%
Source: REPOA / Michigan State University / Afrobarometer
Methodology: Face-to-face interviews with 1,208 Tanzanian adults, conducted in June and July 2008. Margin of error is 2 per cent.

Liyumba sasa mambo yake supa


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa masharti mapya ya dhamana kwa Mkurugenzi zamani wa Utawala na Utumishi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 221 bilioni.

Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba alisema mahakamani hapo jana kuwa amekubaliana na hoja za upande wa utetezi kwamba kifungu namba 148 hakiingiliani na kesi hiyo.

“Hakuna ubishi kwamba mshitakiwa ana haki ya kupata dhamana kwa sababu kifungu walichokitaja upande wa mashitaka hakiingiliani na kesi hii,” alisema Hakimu Nyigulila.

Katika masharti hayo, Liyumba anatakiwa kutoa Sh 300 milioni au hati ya mali yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa, kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 50 milioni kila mmoja, kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuwasilisha polisi hati yake ya kusafiria.

Awali Liyumba alipewa dhamana katika mazingira ya utatanishi baada ya hati zake nyingi kuonekana zina kasoro, lakini akaruhusiwa kurudi uraiani kwa hati ya mali ya Sh882 milioni kati ya Sh55 bilioni zinazotakiwa kwa dhamana.

Upande wa utetezi ulisema mahakamani hapo kuwa uko tayari kwa ajili ya dhamana, lakini upande wa mashitaka ulidai kutokuwa na muda, hivyo Hakimu Mwaseba akaahirisha kesi hiyo hadi Juni Mosi mwaka huu itakapoendelea kwa ajili ya dhamana.

Upande wa mashitaka juzi uliiomba mahakama kutumia kifungu namba 148 (5) (e) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) ambacho kinaeleza wazi kwamba mshitakiwa anaweza kutoa nusu ya pesa zilizoibwa au hati ya mali.

Hata hivyo upande wa utetezi kupitia kwa wakili Majura Magafu ulidai kuwa kifungo kilichotajwa na upande wa mashitaka hakistahili kutumiwa katika kesi hiyo kwa madai kwamba mashitaka ya mteja wake ni ya matumizi mabaya ya ofisi ambayo katika kifungu hicho hayapo.

Jeetu Patel akiri kampuni yake kuchota mabilioni ya EPAWAFANYABIASHA Jayant Kumar maarufu kama Jeetu Patel na Devendra Patel wamekiri mahakamani kuwa kampuni ya Bencon Internatinal Limited inayodaiwa kujipatia fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni ya kwao.

Wafanyabiashara hao walikiri hayo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana wakati walipokuwa wakisomewa maelezo ya awali ya kesi yao.

Maelezo hayo yalisomwa na wakili wa serikali Timon Vitalis mbele ya jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo Ruwaich Meela, Grace Mwakipesile na John Kahyoza.

Washitakiwa hao walikiri kuwa wao ni kati ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ilianzishwa hapa nchini Aprili 4 mwaka 2005.

Pia Jeetu Patel na mshitakiwa mwingine Amit Nandy walikubali kuwa kampuni hiyo ilianzishwa hapa nchini Aprili 4 mwaka 2005 na kwamba wao ndio waliokwenda kufungua akaunti benki. Imeandikwa na Nora Damian.MBIO ZA MWENGE HIZOOOOOOO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasha Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo kwa ajili ya kukimbizwa katika Mkoa yote ya Tanzania ambapo jumla ya miradi 138 itakayoharimu jumla ya shilingi 8.6 Bilion itazinduliwa katika mbio za Mwenge mwaka huu, ujumbe wa mwaka huu ni pinga ukatili wa kijinsia wa watoto na Albino. Kulia ni waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof Juma Kapuya.

Thursday, May 28, 2009

Dk Mwakyembe akasirishwa na taarifa ya polisi

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA KYELA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimesikitishwa na kufedhesheshwa na taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Iringa Jumatatu iliyopita na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini James Kombe na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mazingira ya ajali ya gari niliyopata tarehe 21, Mei 2009, saa 1 na dakika 10 eneo la Ifunda, mkoani Iringa.
Taarifa hiyo ya Polisi inakanusha maelezo yangu yote na ya dereva wangu kuhusu ajali ilivyotokea na kunitaka nijiepushe kutoa matamshi kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba sina utaalamu na masuala ya ajali. Taarifa hiyo nimeipata kupitia gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 26, 2009 na kwa kuwa uwasilishwaji wake haujalalamikiwa na Jeshi la Polisi, naichukulia taarifa hiyo kuwa sahihi.
Pamoja na kwamba bado naumwa na niko nyumbani nikipumzika kwa ushauri wa madaktari, nimelazimika kuvunja ukimya na kutoa taarifa hii fupi kuzuia upotoshaji wa makusudi unaofanywa na magazeti, hususan gazeti la Tanzania Daima, na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi kwa sababu wanazozijua wenyewe kuhusu suala hili.
Aidha nataka kuelezea masikitiko yangu kuhusu hatua hiyo ya Jeshi la Polisi ambayo ina mwelekeo zaidi wa kisiasa kuliko utaalamu wa upelelezi na uendeshaji mashitaka kama ifuatavyo soma kinagaubaga taarifa hapa

Wednesday, May 27, 2009

Kenya, Uganda hatarini kuzichapa

BUNGE nchini hapa limempa baraka Rais Mwai Kibaki kuchukua hatua za kijeshi iwapo juhudi za kidiplomasia zinazoendelea katika mvutano kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo katika Ziwa Victoria zitashindikana.

Bunge hilo pia limemruhusu Rais Kibaki kuomba msaada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo mvutano huo utaonekana kutishia usalama wa kanda ya Afrika Mashariki.

Katika hoja hiyo iliyopitishwa na Bunge, wabunge walimtaka Kibaki ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu kutumia mamlaka yake na kufanya kila linalowezekana kulinda ardhi ya Kenya.

Hoja hiyo ambayo juzi ilikosa nguvu baada ya baadhi ya mawaziri kujaribu kuipinga, jana iliweza kupitishwa baada ya serikali kukosa idadi ya kura za kutosha kuipinga.

Wabunge hao walionyesha hisia za wazi wakati wa kujadili suala hilo, wakieleza umuhimu wa kuingia vitani iwapo itabidi, huku wakimtaka Rais Kibaki kuchukua mamlaka kuhusu mipaka ya nchi.

Juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula na Waziri wa Habari, Samuel Poghisio kujaribu kupinga hoja hiyo na kujaribu kutafuta upatanishi zaidi zilishindikana. Source: Daily Nation

Liyumba afutiwa mashitaka, PCCB wamnyaka


Aliyekuwa Mkurugenzi wa utumishi wa BoT, Amatus Liyumba na Meneja mradi wa benki hiyo Deogratias Kweka wameachiwa huru na Mahakama ya Kisutu leo baada ya kubaini kuwa hati ya mashitaka ina makosa ya kisheria.

Uamuzi huo ulitolewa leo na Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema anayesikiliza kesi hiyo. Baada ya kutolewa uamuzi huo saa 5:20 asubuhi washitakiwa hao walishuka kizimbani na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Washitakiwa hao walipelekwa katika moja ya vyumba vilivyoko mahakamani hapo na saa 5:34 asubuhi walichukuliwa na Defender la polisi lenye namba T 337AKV.

Wakati wa kesi hiyo ulinzi uliimarishwa mahakamani hapo kwani kulikuwa na askari polisi zaidi ya watano waliokuwa wamevaa kiraia huku wakiwa wameshikilia bunduki.

Mmoja wa mawakili wanaowatetea washitakiwa hao Hudson Ndusyepo alisema wateja wao wamepelekwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Pia mawakili hao wanataka shitaka la tatu linalowakabili wateja wao la kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 221 bilioni liondolewe kwani halijawekwa wazi kwamba washitakiwa wamefanya kosa gani.

Katika hoja za upande wa Jamuhuri kupitia kwa wakili wa serikali Boniface Stanslaus ulikiri mahakamani kukosewa kwa hati hiyo lakini uliiomba mahakama iwaruhusu ili waweze kuwabadilisha hati mpya.

Monday, May 25, 2009

Mshindi ni Lorecia Bukwimba CCM Busanda


Mbunge mpya wa Jimbo la Busanda Lolensia Bukwimba,
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukwimba Dan Mollel ametangaza matokeo rasmi ambapo mgombea wa CCM ameibuka kidedea.
matokeo ni kama ifuatavyo:
Waliojiandikisha kupiga kura ni 135,000 na ushee
Waliojitokeza kupiga kura 55,000 na ushee
CCM wamepata kura...............29,242
CHADEMA..................22,764.
UDP.......................271
CUF.........................607.

Sunday, May 24, 2009

matokeo ya awali uchaguzi wa Busanda

Matukio yaliyotufikia yanaonyesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendeshwa puta na mchuano ni mkali kati ya mgombea wa CCM na yule wa Chadema ambapo katika maeneo ya mjini Katoro Chadema kilionekana kuongoza kwa kura nyingi dhidi ya CCM huku CCM chenyewe kikipimana nguvu katika maeneo ya nje ya mji kwa kuzidiana kura.

Katika maeneo hayo ya vijijini baadhi ya vituo vilivyofikiwa na Mwananchi vilionyesha Chadema kuwa juu sana na CCM kura chache, wakati huo huo vituo vingine vikionyesha CCM ikiwa juu sana na Chadema kupata kura chache.

Katika mji wa Katoro wananchi walikuwa wakishangilia mfululizo huku wakikishangilia chama cha Chadema kwa ushindi, hali hiyo pia ilitokea katika maeneo ya vijijini kwa wafuasi wa CCM.

Hata hivyo Mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hawezi kusema lolote kwa wakati ule kwani alikuwa akisubiri kwanza matokeo kutoka maeneo ya vijijini ili waweze kujumlishana kumpata mshindi.

Akizungumza na Mwananchi jana Mbowe alisema anasubiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo kwasababu ndiyo utakapo toa mshindi wa uchaguzi huo.

Uchaguzi wa leo umetawaliwa na vituko vya aina mbalimbali, vikiwemo vilivyotokea kwenye mji mdogo wa Katoro, katika eneo la posta ‘B’ kituo cha Ludete ‘B’ ambako wananchi walilizuia gari la Halmashauri ya Wilaya ya Geita (namba za usajili SM 5179) ambalo lilikuwa likitokea kituo cha Shule ya Msingi Mkapa.

Wakiwa wamezuia gari hilo, baadhi yao waliwasiliana na viongozi wa Chadema ambayo ilimtuma mgombea wake, Finias Magesa aliyemkagua mratibu huyo.

“Nimemkagua, hamna taabu. Nimemkagua na nimeridhika hana kitu mwacheni,” alisema Magesa.

Tatizo la miundombinu yetu
Tanzania yetu tuna mambo yetu tuna kila jambo letu kila kitu ni chetu na hivyo kila jambo na kila shida na kila raha ni zetu, pichani waweza kuona namna mbavyo barabara zetu bomu, ingawa tuko mbele kimiundombinu kuliko DRC lakini pia tuko nyuma kuliko mataifa mengine ya hapa Afrika, tunaziona jitihasa zinazoendelea ktukomboa lakini hazitoshi, Waziri wa zamani wa miundombinu bwana John Pombe magufuli alituahidi kuwa ifikapo mwaka 2010 mtu aweza kodi kutoka Mwanza hadi Mtwara, 2010 ndiyo hiyoo mambo baaado kabisa

Ushindi kwenda kwa nani leo

CHADEMA: Finias Magessa
CUF: Oscar Ndalahwa
UDP: Beatric Lubambe
CCM:Lolesia Bukwimba
Picha kwa hisani kubwa ya rsmiruko.blogspot.com

Friday, May 22, 2009

Kikwete alipokutana na Obama


The US President Barack Obama Welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete to his Oval office in the White House this afternoon.The two Presidents and their close assistants held talks concerning bilateral relations between the two countries.President Kikwete is on weeklong working tour of United States.President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with his host The US President Barrack Obama at the Oval Office in the White House, in Washington this afternoon.President Jakaya Mrisho Kikwete signs a visitors book shortly after he arrived at The White House in Washington DC where he held talks with the US President Barrack Obama this afternoon(photos by Freddy Maro)

Thursday, May 21, 2009

Dk Mwakyembe apata ajali mbaya
Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe aliyepata ajali leo asubuhi mkoani Iringa karibu na eneo la Mafinga akiwa njiani akitoka Kyela kuelekea jijini Dar es Salaam.

Walioshuhudia tukio hilo wanaeleza kuwa gari la Dk Mwakyembe lilipata ajali baada ya kukwepa lori na kisha kutumbukia katika korongo ambapo tairi lilichomoka gari limeharibiwa vibaya na Dk Mwakyembe mwenyewe amekimbizwa hospitalini mkoani humo, na taarifa za karibuni kabisa zinasema kuwa Bunge limetoa ndege na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Dk Mwakyembe apata ajali mbaya


MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amepata ajali mkoani Iringa karibu na eneo la Mafinga akiwa njiani akitoka Kyela kuelekea jijini Dar es Salaam, walioshuhudia tukio hilo wanaeleza kuwa gari la Dk Mwakyembe lilipata ajali baada ya kukwepa lori na kisha kutumbukia katika korongo ambapo tairi lilichomoka gari limeharibiwa vibaya na Dk Mwakyembe mwenyewe amekimbizwa hospitalini ambapo anaendelea na matibabu na anaweza kuzungumza kama, lakini haijajulikana ni kiasi gani ameumia.

Tutaendelea kuwaleteeni taarifa zaidi kadri muda unavyokwenda kuhusiana na maendeleo ya kiafya ya Dk Mwakyembe, ambaye amejitokeza siku za karibuni kukabiliana vikali katika vita dhidi ya ufisadi, vita vilivyomuingiza katika malumbano makali na wana- CCM wenzake pamoja na baadhi ya wafanyabiashara.

Tuesday, May 19, 2009

Waandamana kupinga eneo la makabuei kuuzwa


Wakazi wa eneo la Ununio wilayani Kinondoni wakiandamana kupinga kuuzwa kwa eneo la makaburi kwa mwekezaji ambaye anadaiwa kutaka kuanza shughuli za ujenzi, hata hivyo uongozi wa eneo hilo uliwapoza wakazi hao ukiwaeleza kuwa watarejeshewa eneo lao. Picha na Tumaini Msowoya.

Wanajeshi wamtwanga Trafiki

Picha ya Silvan Kiwale.

ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo asubuhi wamemshambulia na kumpiga askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Thomas Mayapila, wakidai aliwachelewesha kupita eneo la Ubungo.

Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati Thomas akiwa kazini kuongoza magari katika makutano ya Barabara ya Morogoro, Sam Nujoma na Mandela, Ubungo, eneo ambalo kwa kawaida huwa na misururu mirefu ya magari nyakati za asubuhi na jioni.

Tukio hilo lilitokea saa 1:35 asubuhi wakati trafiki huyo akiendelea na kazi yake ya kuongoza magari katika eneo hilo, akionekana kutofahamu kuwa kulikuwa na magari matatu ya JWTZ yaliyokuwa yakitokea Barabara ya Sam Nujoma na kuelekea Buguruni. habari zaidi soma Mwananchi.

Sunday, May 17, 2009

Confession!

A girl went to the priest for a confession and this is how it went:
Girl "Forgive me father for I have sinned"
Priest "What have you done my child?"
Girl "I called a man a son of a bitch."
Priest "Why did you call him a son of a bitch?"
Girl "Because he touched my hand."
Priest "Like this?"(as he touched her hand)
Girl; "Yes father."
Priest "That's no reason to call a man a son of a bitch."
Girl "Then he touched my breast."
Priest "Like this?"(as he touched her breast)
Girl "Yes father."
Priest "That's no reason to call him a son of a bitch."
Girl "Then he took off my clothes; father."
Priest "Like this? (as he takes off her clothes)
Girl "Yes father."
Priest "That's no reason to call him a son of a bitch."
Girl "Then he stuck his "you know what "into my "you know where"
Priest "Like this? (as he stuck his " you know what "into her "you know where")
Girl "YES FATHER;YEES FATHER ;YEES FAAAATHER!!"
Priest "(after a few minutes) That's no reason to call him a son of a bitch"
Girl "But father he had AIDS!
Priest "SHIT! THAT'S SON OF A BITCH!!!

IS TI POSSIBLE TO CONFESS OUR SINS TO A HUMAN BEING?
Chriss!

Friday, May 15, 2009

Vodacom miss IFM 2009


Baadhi ya washiriki wa shindano la kumtafuta Vodacom Miss IFM 2009 wakipozi kwa picha wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana kuhusu shindano hilo linalotarajiwa kufanyika leokatika ukumbi wa New Msasani Club jijini humo. Kutoka kushoto ni Diana Mhenga, Beatrice Lukindo na Francisca Mansilo.

Thursday, May 14, 2009

Buzwagi waanza mavuno


Tanzania last week dug deeper into its golden era, after Barrick Gold's new Buzwagi mine in Kahama District, Shinyanga Region, started production. Buzwagi mine is now one of the country's largest mining operations and Barrick Gold, the world's largest mining house, has expressed excitement on its first gold pour.

In 2009, Buzwagi is expected to produce approximately 200,000 ounces of gold at total cash costs of $320-$335 per ounce. The Buzwagi project is a catalyst for economic growth, with an initial investment of 500bn/- during its construction phase and over 1.5trillion/- when it becomes operational. kwa habari za kina tembelea http://www.marketwire.com/press-release/Barrick-Gold-Corporation-NYSE-ABX-983701.html

Wednesday, May 13, 2009

Hivi Rais Karume kwanini haudhurii vikao baraza la mawaziri


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha baraza la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi, hakika hiki ndicho chombo kikubwa kabisa humu nchini mwetu lakini cha kushangaza hebu angalia vizuri hiyo picha utaona kiti cha Rais wa Zanzibar Abeid mana Karume hakina mtu , mwenyewe hayupo sababu hatujui, na hatukuelezwa hivyo tunajiuliza hivi kwanini Rais Karume haudhurii vikao vya baraza la mawaziri??? maswali mengi yanaibuka kwetu (picha ni ya Freddy Maro)

Usafiri wetu


Hebu cheki hapa usafiri wa jijini kwetu ulivyo kero, gari imechoka ile mbaya, barabara nazo hoi ili mradi kila kitu hapa jijini kwetu ni balaa, sukuma sukuma kila sehemu. Foleni kila kukicha hebu mtanzania mwenzetu tuambie.

Jeshi lapewa vifaa

Mkuu wa kamandi ya Afrika wa Jeshi la Marekani, Jenerali William Ward akisalimiana na kiongozi wa kikosi cha Tanzania kinachotarajiwa kwenda nchini Sudan kulinda amani, Luteni Kanali Ally Katimbe wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kijeshi yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wapiganaji 800 kutoka Tanzania, wanatarajiwa kujiunga na vikosi vya Umoja wa Mataifa na Afrika katika kazi hiyo. Chini wapiganaji wetu wakiwa tayari kufanya mambo huko Darfur!! PICHA YA MPOKI BUKUKU.