MKUU WA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA) AWATUNUKU SHAHADA, STASHAHADA NA VYETI WAHITIMU 691 KATIKA MAHAFALI YA KUMI NA MOJA KAMPASI YA TUNGUU.
Maandamano ya wahitimu wa Mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yakiingia katika kiwanja cha Mahafali hayo yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na Makeme Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiutangazia mkusanyiko uliokuwepo kiwanja cha Kampasi ya Tunguu kuwa ni Mahafali ya kumi na moja ya Chuo hicho, (kulia) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Said Bakari Jecha na kushoto Makamu Mkuu wa chuo Prof. Idriss Ahmad Rai.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia wanafunzi, wazazi na wageni waalikwa katika Mahafali ya kumi na moja YA Chuo hicho yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Kemia Khamis Mohammed Saidi kwenye mahafali ya kumi na moja yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
Mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi katika Mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Rauhiya Ahmed Hamdun akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana, Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohammed akimpa zawadi mwanafunzi bora wa mahafali ya kumi na moja Rauhiya Ahmed Hamdun katika Kampasi ya Tunguu.
Comments