Thursday, December 24, 2015

RAIS DK. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAWAZIRI KUJAZA NAFASI ZILIZOKUWA WAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika utawala wake wa awamu ya tano.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

 Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano


 Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Profesa Jumanne Maghembe – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
 Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu. Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

No comments: