Friday, January 31, 2014

MAKABIDHIANO A ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

IMG_6612Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Goodluck Ole Medeye(kushoto) akimkabidhi ofisi Naibu Waziri mpya katika Wizara hiyo George Simbachawene (Kulia)leo kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni. Picha/ Clarence Nanyaro/Ardhi GC
IMG_6615

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM PHILIP MANGULA AWASILI MKOANI MBEYA

1Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya tayari kwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM zinazofanyika jumapili kwenye uwanja wa Sokoine mkoani humo, Katika sherehe hizo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dr. Jakaya Kikwete. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA2Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi. Siasa na Uenezi wakati alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Mbeya leo katikati ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi3Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Abdallah Bulembo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa.4Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya.6Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akiongozana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi. Siasa na UeneziIMG_2076Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangulaakisaini kitabu cha wageni

RAIS AONDOKA KWENDA NCHINI INDIA KWA ZIARA RASMI

TA1A1303Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake (katikati) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shei,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A1310Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A1324Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi  wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake, pichani akipeana mkono na Brigedia Jenerali Sheikh Sharif Othman .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A1339Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi mbali mbali katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A1349Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake,[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

DK ASHA ROSE MIGIRO AITEMBELEA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA

akipokea mauaWaziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (kushoto) akipokea maua kutoka kwa Afisa Tawala wa Tume Bi. Suzan Magotiakisalimia watumishiMh. Migiro akisalimiana na Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Caritas MushiAsha rose akiongeaWaziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rose Migiro akizungumza wakati wa kikao chake na uongozi wa TumeBaadhi ya WatumishiKikao cha pamoja baina ya Mhe Waziri wa Katiba na Sheria na Uongozi wa TumeCM akimpokea MigiroMwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanazania Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akimpokea WazIri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro alipotembelea ofisi za TumeCM akiongeaMwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza wakati Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe Asha Rose alipoitembelea TumeKM akiongeaWashiriki wa KikaoMakamishnasehemu watumishiSehemu ya Watumishi na ugeni wa Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha pamojawakiwa kikaoKatibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Korosso akiwasilisha taarifa fupi ya Tume kwa  Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Asha Rose Migiro

KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA WATEMBELEA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

SONY DSCMwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Mhe. William Mganga Ngeleja akizungumza na watendaji na menejimenti ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakati Kamati yake walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kukagua utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu.
Picha na Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

WAZIRI MKUU WA FINLAND ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

DSC_0132Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), jana asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.DSC_0142Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo jana asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.DSC_0151Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland,  Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo jana asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.DSC_0166Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada wakati wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jana asubuhi kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo.DSC_0169Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Finland,  Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

MWILI WA SHEKH WA MKOA WA MARA WAWASILI UWANJA WA NDEGE MUSOMA

NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
 RUBANI WA NDEGE AKIELEKEZA NAMNA YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema  wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.
Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
   INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII, WATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII, RUNGEMBA IRINGA. RUNGEMBA

imageNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (mb.) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa,Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii leo wametembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.  Lengo la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika utoaji wa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kupitia chuo hiki. Katika ziara hii, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea taarifa ya chuo na kutembelea maeneo / miradi mbalimbali ya chuo.image_1Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Saidi Mtanda (Mb.) wakikagua maeneo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika baadhi ya maeneo yenye kuhitaji maboresho.image_2Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Kati) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, (Kulia, mwenye nguo ya kahawia) Bibi Santina Mbata wakiwapitisha Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Majengo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.

UNIC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MATESO YA KAMBI ZA WAYAHUDI

DSC_0014
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
DSC_0005
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
DSC_0044
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.
Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
DSC_0051
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.
“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
DSC_0077
DSC_0075

UBALOZI WA CHINA NCHINI WASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO WA MOROGORO

Mkurugenzi  wa Idara ya  Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali kutoka kwa  Balozi wa Mhe. Lu Youqin.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Eliphace Marwa-Maelezo
Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya watu wa China nchini   wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko mkoani Morogoro toka kwa  Mhe. Lu Youqing ,vyenye thamani ya sh. milioni 30.
Msaada huo  umetolewa  na  Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing na ulikabidhiwa kwaMkurugenzi  wa Idara ya  Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali amesema kuwa anaishukuru Serikali ya China kwani imekuwa mstari wa mbele  pale Tanzania inapopata maafa mbalimbali.
Aidha Luteni Jenerali Rioba aliongeza kuwa  mafuriko hayo ya aina yake hayajawi kutokea yalianzia milima ya Kilosa na Mvomero na kupelekea kufurika kwa mto Mkundi.
“Mheshimiwa Balozi mvua hizi zilikuwa kubwa  ambazo hazijawahi kutokea wilayani Mvomero na kupelekea kuharibu daraja la Dumila ambalo ndiyo  kiunganishi cha Mkoa wa Morogoro na Dodoma,” alisema Luteni Jenerali Rioba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Antony Mtaka akiongea kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  amesema kuwa mamia ya nyumba ikijumuisha madarasa, majengo ya mahakama ya mwanzo, mashamba na barabara zimeharibiwa vibaya na mafuriko hayo.
“Kwa niaba ya Serikali napenda kushukuru Serikali ya China  kupitia Mhe. Balozi Lu kwa msaada huu na ningependa kuahidi kuwa msaada huu utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa, ”alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wake Balozi wa china ametoa pole kwa waathirika wa mafuriko na kusema kuwa watu wa Jamhuri ya China wako pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.
“China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu hivyo kampuni ya ujenzi ya CCECC ilichukua hatua za haraka katika kushiriki ujenzi wa daraja hilo kwa kushirikiana bega kwa bega  na ndugu zao Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana na kumaliza ujenzi huo kwa muda wa siku mbili,” alisema Balozi Youqing.
Ubalozi wa China kwa kushirikiana na makampuni ya China nchini umetoa vitu mbalimbali ikiwemo Chakula, mashuka, madawa na maturubahi ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa waathirika hao wa mafuriko mkoani Morogoro.

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR

01Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo. Picha na OMR02Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR03Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR04Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR05Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR06.Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
07Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR