Thursday, February 22, 2007

Hivi tunachohitaji ni sifa tu kuitwa graduates au?

HAIWEZEKANI kupuuza jitihada zote za serikali inazofanya kuwezesha kuanzishwa kwa chuo kikuu kipya kitakachowezesha kuchukua wanachuo 40,000 huko Dodoma.

Haiwezekani pia kusema kuwa eti serikali haikufanya jambo la maana kuweza kufikia uamuzi huu mzito ilhali sekta ya elimu ya juu imekuwa ikididimia.

Pia haiwezekani kupuuza jitihada zingine zozote za kujaribu kuonyesha nia njema japo kwa kauli tu kuanzisha vyuo vikuu vingi kadri inavyowezekana.

Lakini inawezekana kuhoji na vile vile kuwa na mashaka mengi hasa kama uamuzi huu unakuja wakati kile tulicho nacho kinatushinda na tena kinakaribia kutushinda kabisa.
Unaweza kusoma zaidi kwa kubonya hapa

Friday, February 16, 2007

Kasi hii ya sasa haitufai, tutafakari la kufanya

PANGA pangua. Hili huku, lile kule, chukua huyu hamisha peleka kule, yule weka hapa, mwingine fukuza, toa matamshi ya kila aina ya kutia matumaini ya ajabu na kisha mwisho wa siku mambo yanabaki kuwa yale yale na pengine mabaya zaidi.

Hii ndivyo ilivyo Tanzania yetu, kila anayekuja anakuja na lake, anajaribu kufanya majaribio na kisha anastukia muda wake umeisha basi anaondoka na kuiacha nchi ikiwa katika hali iliyo mbaya zaidi.

Serikali yetu ilianza kwa kujiunda Baraza lake la mawaziri ambalo lilikuwa kubwa kuliko yote tangu kupatikana kwa nchi hii, ukatolewa utetezi wa kila aina, lakini baadaye muda kidogo likapanguliwa. soma zaidi hapa kwa kubonya hapa

Saturday, February 03, 2007

Mabilioni ya JK hayakupaswa kwenda benki

HAPANA shaka walalahoi wenzangu mtakuwa katika majonzi makubwa hasa baada ya kubaini kuwa kile mlichoahidiwa, ni dhahiri kuwa ni ndoto ya mchana na katu haiwezi kuwakomboa hata iweje.

Nadhani mnakumbuka kwamba Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ile ya Awamu ya Nne hivi karibuni ilitoa matumaini mapya kwa kutoa ahadi ya kugawa Sh21 bilioni katika mikoa yote nchini.

Tulipotajiwa tarakimu, hakika wengine tulifurahia sana tukajua kwamba angalau tunaweza kuambulia vijisenti na hivyo angalau kutusukuma kututoa tulipo hadi katika hatua nyingine.Soma zaidi kwa kubonya hapa

PCB msitoe tena likizo

WIKI hii kwa hakika sisi wavuja jasho, wafyeka nyasi na wasaka nyoka; (usishangae haya yote ni majina yetu sisi tusio na kitu na tusio na pa kuegemea), tulipata taarifa ambayo ilitufanya tushushe pumzi.

Taarifa hii, ilitufanya tushushe pumzi si kwa sababu tumezinduka, bali pia ni kwa sababu tumestuka na kuanza kuona 'heehh hivi tunayoyashuhudia ni ya kweli au tunaota ndoto au ni jinamizi?

Kwa hakika imetustua, kwa sababu hakuna miongoni mwetu aliyetarajia 'mabwana wakubwa' hawa wanaweza eti kukamatwa wakafikishwa kizimbani tena mbele ya hakimu.

Taarifa yenyewe ni hii ya utata wa ulaji wa pesa za ujenzi wa jengo la ubalozi kule Italia. Wiki hii aliyekuwa Balozi wetu ambaye pia ni Profesa, alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo, kama ni za kweli au la. Sizungumzii uhalali au uharamu wake. Soma zaidi kwa kubonya hapa: