Tuesday, November 29, 2016

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

mchec1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kwenye chumba cha watu mashuhuri cha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini  Dr es salaam Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kwenye uwanja wa ndge wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI NAPE NNAUYE APOKEA PICHA YA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI ILIYOCHORWA NA KIKUNDI CHA ANGAVU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia)  jijjini Dar es Salaam. Picha hiyo imechorwa kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group.
Muonekano wa picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyoichora kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group ambapo imekabidhiwa  jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye kwa niaba ya Mheshimiwa Rais.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyochorwa na kikundi cha Angavu Youth Group  jijini Dar es Salaam. Picha hiyo imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba ya Mhe. Rais. kushoto ni Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na kulia ni Katibu wake Bi. Oliver Charles.Picha na Anitha Jonas – MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth Group Bi.Oliver Charles (katikati) wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.

WAZIRI LWENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MABOMBA NCHINI

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kinachotengeneza mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.

“Nimeridhishwa na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.“Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.

Inj. Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) alisema nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.

Alisisitiza bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA RAIS DKT.MAGUFULI ALIPOMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wimbo wa Taifa 
 Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa
 Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 
 Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama
 Viongozi wakiwa wamesimama
 Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia
 Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa
 Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria
 Wageni mbalimbali
 Mabalozi mbalimbali
 Mabalozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje 
 Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali
  Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje
 Viongozi wa taasisi mbalimbali
 Viongozi wa kidini na wageni mbalimbali

 Makatibu wakuu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuma
 Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia
 Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza

 Mrisho Mpoto akighani wimbo maalumu
 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 


 Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 
 Rais Edgar Lungu akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
 Rais Edgar Lungu akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Rais Edgar Lungu akisindikizwa na mweyeji wake Rais Dkt Magufuli
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakiondoka baada ya dhifa

Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt.  Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Saturday, November 26, 2016

JAMII YATAKIWA KUWAHESHIMU NA KUWASAIDIA WAZEE NCHINI

Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania  Mathias Canal akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza baadhi ya mahitaji kwa ajili ya wazee waishio kituoni hapo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary akimsikiliza kwa makini mzee aliyelala kutokana na homa kali inayomsumbua
Kushoto ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa akisisitiza jambo kwa Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni katibu wa TAWSO Mwanza Bi Abigali Mhingo
 Meneja Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein Sungura akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya uongozi wa METDO Tanzania katika kituo cha Wazee KIILIMA Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera
 Hiki ndicho Choo kinachotumiwa na wazee waishio kambi ya KIILIMA-Bukoba
Moja ya Mzee katika Kituo cha Wazee KIILIMA akiwa amelala kutokana na homa kali iliyokuwa inamsumbua
 Mahitaji yamepokelewa kwa furaha na wazee wote kupitia uongozi wao
Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu, Kushoto kwake ni Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Ndg Charles  Mafimbo, Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Hussein Sungura Meneja Mradi METDO Tanzania na Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ndg Ashrafu Omary
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary akifanya usafi katika jiko la watumishi wa kituo cha wazee KIILIMA
 Mjadala ukiendelea baada ya kazi kumalizika Kijijini KIILIMA kambi ya wazee
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza akipanda mti kwa ajili ya kumbukumbu
Tafakuri pana kwa Mzee Wilson Ziraimanikabla ya kukabidhiwa mahitaji na uongozi wa METDO Tanzania
 Nyumba ya kulala wazee wa kituo cha KIILIMA kilichopo Kata ya Nyakato Mkoani Kagera
 Viongozi wkibadilishana mawazo mara baada ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA
Kijana ni mzee ajaye na Mzee ni kijana aliyekuwa
Hili ndilo jiko linalotumiwa na viongozi wa kituo cha KIILIMA kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba
Katikati ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa akipata maelezo ya awali kwa Moja ya mzee aishie kambini KIILIMA kabla ya kumfanyia vipimo
Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania akipanda mti wa matunda aina ya Mlimao kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA
 Majadiliano ya namna ya kuchimba mashimo kabla kupanda miti
 Moja ya nyumba anayoishi Mtumishi wa Kituo cha wazee KIILIMA Kilichopo Mkoani Kagera
Mkurugenzi wa METDO Tanzania Bw Ashraf Omary mwenye Jembe akimsaidia kazi Mzee Wilson Ziraimani, Mzee huyu alikuwa anafanya kazi za kilimo katika mashamba mbalimbali nchini, yeye ni mkazi wa Ngara na wakati akiwa mtoto alikuwa analelewa na Mama wa kambo.
Aliwasili katika kituo cha kulelea Wazee cha KIILIMA Mwaka 1986 hapo alipo anatambaa kwani alivunjika kiuno enzi za ujana wake baada ya kuanguka mtini wakati alipokuwa anakata kuni kwa ajili kupikia.
Viongozi wa METDO Tanzania, Kiongozi wa TASWO, na Viongozi wa kituo cha Wazee KIILIMA wakipanda mti wa matunda aina ya Parachichi kwa ajili ya kumbukumbu na kampeni ya upandaji miti

Na Mathias Canal, Bukoba

Kukosekana kwa huduma bora na msingi kwa wazee nchini imetajwa kuwa changamoto kubwa kwa Wazee waishio katika kambi mbalimbali za serikali na zile za binafsi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary wakati akikabidhi mahitaji kwa wazee wa kituo cha KIILIMA kilichopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Bw Omary alisema kuwa Asasi hiyo yenye usajili No. ooNGO/08317 inajishughulisha na kutoa Elimu ya Mazingira kwa wananchi wanozunguka migodi pamoja na wafanyakazi wa migodini ambapo pia imejikita kuwasaidia wazee waishio katika kambi mbalimbali nchini katika huduma za kuwapatia mahitaji ya msingi ya kila siku kama vile (Chakula, na Mavazi) sambamba na kutoa huduma ya upimaji wa afya zao kupitia wataalamu wa tiba na kuwapatia dawa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali.

Alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la wazee kutopatiwa huduma bora ikiwemo chakula na matibabu jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia wazee wengi kufariki pasina huduma yoyote ya kitabibu sambamba na kukosa Lishe Bora.

Bw Omary ameushukuru uongozi wa kampuni ya ZONGII PUMBLING LTD ya Jijini Mwanza kwa kushirikiana na METDO Tanzania kufanikisha kupatikana mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wazee wa kambi ya KIILIMA sambamba na kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa ushirikiano ulioonyesha ikiwa ni pamoja na kuruhusu madaktari kwa ajili ya kwenda kuwapima afya wazee hao.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein Sungura amebainisha kadhia zinazowakumba wazee katika kituo cha KIILIMA sambamba na vituo vingine nchini kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za usafiri ili kurahisisha wazee kufikishwa haraka hospitalini pindi wauguapo, Ufinyu wa Bajeti, Ukosefu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya usafi na ucheleweshaji wa Ruzuku ya serikali.

Sungura alisema kuwa Mpaka sasa Asasi hii ya METDO Tanzania imesaidia katika maeneo mbalimbali ikiwemo tukio la Agosti 13, 2016 la kumuenzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika Makao ya wazee wasiojiweza BUKUMBI Mwanza, Tukio la Octoba Mosi 2016 SIKU YA WAZEE DUNIANI katika wilaya ya Shinyanga ambapo jamii ilishirikishwa kutambua changamoto zilizopo katika kituo cha Wakoma na Wazee wasiojiweza cha KOLANDOTO pamoja na Kituo cha Wakoma na  Wazee wasiojiweza cha NYABANGE BUTIAMA  na kuwa sehemu ya kuzitatua changamoto hizo.

Kutokana na kazi hiyo ya wito inayofanywa na METDO Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salim Kijuu ametoa wito kwa Asasi hiyo kuwekeza Mkoani Kagera katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo ili ushirikiano wa kusaidia wazee uweze kukomaa na kusaidia wazee wote nchini kirahisi sambamba na kutoa fursa kwa vijana kutambua umuhimu wa kufanya kazi sawia na kujiajiri.

Kijuu alisema kuwa kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na hali nzuri ya hewa na udongo wake kuwa na rutuba ni vyema Asasi ya METDO Tanzania ikafanya kazi yake kwa misingi ya katiba lakini pia inapaswa kuwasaidia vijana wengi nchini ili kuachana na uvivu walionao badala yake kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuisimamia na kutekeleza kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

Akisoma taarifa ya kituo hicho Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza alisema kuwa Kituo hicho kina jumla ya wahudumiwa 24 ambapo kati yao kuna watoto 6 waliokuwa kwenye mazingira hatarishi baada ya kutelekezwa na wazazi wao huku wengine wakipokelewa baada ya wazazi wao kufariki kutokana na janga la UKIMWI lililotokea mwaka 1984.

Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwachukua watoto hao kwani kuendelea kubaki katika kituo hicho sio jambo jema kwao kwani wanachanganyikana na wazee ambao wengi wao wana matatizo ya akili.

Lwiza amesema kuwa kufuatia uharibifu wa majengo kutokana na Tetemeko lililotokea hivi karibuni Mkoani Kagera na kuharibu majengo mengi kituoni hapo imesababisha kukosekana kwa nyumba za watumishi, na choo kwa ajili ya matumizi ya wazee pamoja na watumishi wa kituo hicho.

Naye Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa ameiomba serikali kusaidia upatikanaji wa sehemu maalumu ya kuhifadhia dawa, kutolewa mafunzo ya tiba kwa wahudumu waliopo kituoni hapo sambamba na kupatikana kwa vifaa tiba kwa ajili ya kupima damu, Sukari, MRTD, Presha na wingi wa damu.

Kituo cha Wazee KIILIMA kilichopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kilicho chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni moja kati ya vituo vya kulelea wazee hapa nchini ambapo awali kilikuwa chini ya kanisa la Roman Catholic na baadaye kilikabidhiwa rasmi kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1974.

Baada ya kutembelea vituo vyote vya Wazee kanda ya Ziwa METDO Tanzania inataraji kuzuru Mikoa ya Kanda ya kati kwa ajili ya kujionea changamoto za wazee mbalimbali waishio kambini na kuzifikisha sehemu husika wakiwemo viongozi wa dini, Wafanyabiashara, Serikali na Wadau mbalimbali nchini.