Monday, July 30, 2007

Monday, July 23, 2007

Kupima tumepima Ukimwi, enhee nini kinafuata?

LAZIMA unapoanza kitu kuwe na sehemu ya kuanzia. Hilo halipingiki, unaweza kuanzia mwanzo ukaenda mwisho na pia unaweza kuanzia katikati na kisha kumalizia mwishoni, pia waweza kuanzia mwisho. Inawezekana.

Serikali yetu imeanzia sehemu fulani na sasa inasonga mbele, ndiyo maana imetangaza kampeni ya nchi nzima kupima virusi vya Ukimwi, akajitokeza shupavu huyu kwa mifano yake, Rais Jakaya Kikwete , akapima akatangaza, matokeo akaondoka.

Wakaja wengine wakapima wakaondoka. Wabunge nao wakajitutumua kupima jana, japo wengine kwa shingo upande wamekwenda, wengine nao wanaenda kupima sababu tu wenzao wamepima na kisha wanaingia mitini.

Nafurahi kwamba na sisi wavuja jasho tulikuwapo katika foleni ndefu tukionyesha kujali afya zetu, tumepima na tumeondoka, majibu yetu tunayajua wenyewe. Bonyeza hapaupate taarifa kwa kina zaidi.

Thursday, July 19, 2007

Miss Tourism Queen International 2007

Mrembo wetu Sophia Kapama, Mtanzania anayeshiriki Miss Tourism Queen International 2007 huko China anaendelea vyema na mpambano wa kuwania taji hilo litakalofikia mwisho wake Agosti 2, hapa yupo yeye na wenzake.


Ziara ya Warembo wa Miss Tourism Queen International 2007 katika ziwa maarufu la Wes Lake la jiji la Hangzhou. Marco Polo aliweka nanga ya meli yake karne moja iliyopita na alifurahishwa na mandhari ya Hangzhou West Lake. Mandhari hiyo ya West Lake sasa inapambwa na Warembo kutoka nchi zaidi ya 100 Miss Tourism Queen International 2007. Wakiwa huko warembo walifunzwa kung fu na ngoma za jadi za kichina.Niungane na Kaka Issa Michuzi kuwatafadhalisha Watanzania tumpigieni kura MTQI Tanzania ambaye yuko China kwenye mashindano.

Bonyeza http://www.misstqi.com/vote/vote_mtqi.phpupate taarifa kwa kina zaidi.

Credit card inahitajika na USD 2 hununua kura 10. Naona kuna watu wameshampigia kura lakini tunaomba tusaidiane kwani haba na haba hujaza kibaba.
Pia wapiga kura wanaweza kujishindia zawadi kama mnavyoweza kusoma kwenye website.

Hii ni picha ya muda kidogo alipokuwa akigombea Miss Sinza.

Picha za Sophia ni ngumu kupata kwani hawana website moja rasmi kwa hiyo ni kazi haswa. Update ni kwamba mpaka sasa hivi wametembelea miji ya China na jana walifanya mashindano ya Miss Best Smile ambayo ameshinda China. Wanaendelea na matokeo yatatangazwa baadaye.

Asanteni

Askofu Mkuu KKKTASKOFU Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, jana amechaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya kuwabwaga kwa kura nyingi maaskofu wawili, Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Dk Oldenberg Mdegela wa Iringa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Mkutano huo, Askofu Martin Shayo, alisema Askofu Malasusa alishinda baada ya kupata kura 132, akifuatiwa na Dk Mdegera ambaye alipata kura 35, huku Dk Munga akipata kura 17.

Awali askofu Shayo alisema mshindi wa uchaguzi huo alitakiwa apate kura theluthi tatu ambazo ni 123 kati ya wapiga kura 184.

Hata hivyo, awali kabla ya uchaguzi huo, kuliibuka hoja kadhaa baada ya aliyekuwa Msimamizi mkuu wa mkutano huo wa uchaguzi, Ibrahim Kaduma, kutangaza kuwa idadi ya wapiga kura walikuwa 216.

Hoja hiyo ilipingwa na na baadhi ya maaskofu na hivyo kulazimika kupiga kura kwa makini na safari hii watu wakipiga kura kwa majina kwa kila dayosisi.

Awali jana asubuhi, kuliibuka malumbano kadhaa kutokana na baadhi ya wajumbe kupendekeza kuwa wagombea ambao waliwahi kushindwa awali kwa kushindwa kupata kura zaidi ya theluthi moja, waenguliwe. Bonyeza hapausome Mwananchi kwa taarifa za kina zaidi. Au unaweza kumtembelea Mpoki Bukuku aliyeipiga picha hii kwa kubonyeza hapa

Wednesday, July 18, 2007

Jaji Mkuu mpya huyuRAIS Jakaya Kikwete amemteua Jaji Augustino Ramadhan kuwa Jaji Mkuu wa nne wa Tanzania, baada ya Jaji Mkuu Barnabas Samatta kustaafu rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo jana, uteuzi wa Jaji Ramadhan ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa muda mrefu sasa, unaanza mara moja.

Taarifa hiyo ilielezea kuwa Jaji Ramadhani ataapishwa kesho jioni Ikulu jijini Dar es Salaam.

Jaji Ramadhani ambaye ni mwenye vipaji vingi, kabla ya kuingia katika shughuli za mahakama, alikuwa katika jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akifanya kazi huko katika Idara ya Sheria na alitoka jeshini akiwa na cheo cha Brigedia Jenerali.

Pia amewahi kuwa Jaji katika Mahakama ya Afrika Mashariki ambako alikuwa yeye pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba, walikuwa wakiiwakilisha Tanzania.

Kwa upande wake, Kenya ilikuwa ikiwakilishwa na Jaji Moijo ole Keiwu na Jaji Kassanga Mulwa walioteuliwa na Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi.

Kwa Uganda walikuwapo majaji Joseph Mulenga na Jaji Solony Bosse, aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki.

Sambamba na hilo, Jaji Ramadhan pia ni mpiga kinanda maarufu katika kwaya ya wa Kanisa la Anglikana jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa juzi kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari (Maelezo), ilisema kuwa Mahakama ya Tanzania itafanya kikao maalum cha kumuaga kitaaluma Jaji Msataafu Samatta, ambacho kitafanyika Julai 19, mwaka huu kwenye jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo Kivukoni Front.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Jaji Samatta atastaafu ifikapo Julai 20, mwaka huu. Katika shughuli za kumuaga, atakagua gwaride la heshima mbele ya jengo hilo.

Miongoni mwa watu watakaohudhuria siku hiyo ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu akiwemo Naibu wake, Mathias Chikawe, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika ambaye atatoa hotuba.

Mbali na Jaji Samatta, Watanzania wengine wazalendo waliowahi kushikilia nafasi ya Jaji Mkuu ni Augustino Saidi na Francis Nyalali.

Hii ina maana kwamba Jaji Ramadhan anakuwa pia Mzanzibari wa kwanza kushika wadhifa wa juu katika duru za mahakama nchini Tanzania. Unaweza kumsoma zaidi katika gazeti la Mwananchi

Tuesday, July 17, 2007

Waziri Meghji, hebu tukuulize swaliNIMEPITIA magazeti ya wiki hii nikakuta habari zinazoonekana kama nzito hivi, zinanivutia kichwa chake cha habari, najaribu kuzisoma kwa undani na hata umakini kutokana na kunigusa kwa kiasi kikubwa.

Habari hizo zinazungumzia hatua inazozichukua serikali kunusuru hali mbaya inayoelezwa kusababishwa na wauzaji mafuta.

Nikadhani ni habari moto na nzito hasa. Namaliza kuzisoma naishia kutikisa kichwa. Nasikitika hasa mimi mvuja jasho , nasikitikia wavuja jasho wenzangu wengi tu waliotapakaa hapa nchini wanaoishi kwa taabu na uchungu wakitamani kupotea katika uso wa dunia. Bonyeza hapaupate taarifa kwa kina zaidi.

Monday, July 16, 2007

Tanzania bila Ukimwi Inawezekana


Mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete aliongoza wananchi na viongozi wenzake wa serikali na wa vyama vya kisiasa katika kampeni zilizoanza za kupima Virusi vya Ukimwi. Kitendo cha Rais Kikwete na mkewe (Pichani) na viongozi wengine wote ni kitendo cha kijasiri ambacho hakina budi kupongezwa na kuungwa mkono. Ingawa ni kitendo kilichochelewa lakini kufanyika kwake kumekuja wakati muafaka katika kukoleza mapambano dhidi ya ugojwa huu unaoangamiza jamii yetu na kuweka hatima ya baadaye ya taifa letu mashakani.

Ingawa pia haitoshi kwa viongozi kupima tu bali pia kutangaza matokeo ya vipimo hivyo hadharani ili wawe watakaogundulika wameambukizwa siyo tu wawe mfano wa kupima tu bali pia wawe mfano wa watu wanaoishi kwa matumaini na kuendelea na majukumu yao badala ya kuonekana kuwa kugundulika kuwa na VVU ni leseni ya kifo.

Hata hivyo, katika upande wa kauli mbiu ya 'Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana' kunaonekana kuwapo utata wa aina fulani. Moja sababu Ukimwi upo na kwa maana hiyo haujapatiwa dawa na kwa maana hiyo wenye ukimwi wapo. Kwa maana hiyo kusema tanzania bila ukimwi inawezekana ni kuwanyanyapaa wenye virusi. Je wanapopatikana na ukimwi ina maana serikali itafanyaje?

Monday, July 09, 2007

I wapi ndege yenu ya uchumi inayopaa ?TUNAJUA hata iweje, bajeti itakuja na itaondoka na sisi tutaendelea kuishi hata kama maisha yetu ni ya kubahatisha kwa kula mlo mmoja na maji na siku kuisha, haya yote ni maisha.

Tumewasikia waheshimiwa wetu walioko 'peponi' Dodoma wakiijadili bajeti ambayo kwetu sisi kadri tunavyoendelea kuufuatilia mjadala huo, unaendelea kutujaza hasira na kutuondolea matumaini ya kuondokana na machungu tuliyo nayo.

Wamekaa wakubwa na wawakilishi wetu wakaongeza ushuru katika mafuta, wakautetea uamuzi huo kwa nguvu zao zote. Wale wenzao, yaani wa upinzani waliukataa. Bonyeza hapa

Saturday, July 07, 2007

Huko Kome nako kuna mitaaMoja ya mitaa iliyopo katika nyumba zinazokaliwa na wavuvi kisiwa cha Mchagani.

Visiwa vya Kome
Kibao kinaochoonyesha kuwa ni marufuku kuingia katika hifadhi iliyopo katika kisiwa cha Kome eneo la MChagani , lakini mbele yake kuna nyumba zinazotumiwa na wavuvi katika eneo hilo, kama kilivyonaswa na mdau Julius.

usafiri majini
Watu wakishusha mizigo katika boti kubwa inayotumika kusafiri kati ya Mwanza na baadhi ya visiwa vikubwa vilivyopo katika ziwa Victoria. Picha kwa hisani ya Julius Samwel wa magodi.blogspot.com

MandhaliNyumba nyingine ya wavuvi iliyopo katika pori lililopo katika kisiwa cha Ito

Friday, July 06, 2007

Mambo ya Mwanza haya


Mdau Julius aliyekuwa jijini Mwanza hivi karibuni alitembelea baadhi ya vijiji na hii ni moja ya Centre.

Sijui ni Guest au Wash RoomMdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini?

Wednesday, July 04, 2007

Mchungaji wa Kianglikana aliponaswaMchungaji wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Central Tanganyika aliyesimamishwa kutoa huduma katika kanisa hilo,Elia Mbalaga akiwa mikononi mwa walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Dodoma Security baada ya kutokea vurugu
katika ibada ya Kipaimara na kusimika wazee wa kanisa wa kanisa kuu la roho mtakatifu. Picha ya Michael Uledi

Tuesday, July 03, 2007

Ilianza hiviMchungaji wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Central Tanganyika aliyesimamishwa kutoa huduma katika kanisa hilo,Elia Mbalaga akiwa mikononi mwa walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Dodoma Security baada ya kutokea vurugu
katika ibada ya Kipaimara na kusimika wazee wa kanisa wa kanisa kuu la roho mtakatifu. Mchungaji huyo alipelekwa kituo cha polisi kwa ushirikiano na Askari Kanzu. Kanisa la DCT linakabiliwa na matatizo makubwa sana ikiwa ni pamoja baadhi ya waumini wanashinikiza Askofu Mdimi Mhogolo ajiuzulu kwa kile wanachodai kuwa anaunga mkono ushoga kwa kuendelea kupokea misaada toka kwa kanisa la Kianglikana la Marekani (ECUSA) Picha ya Michael Uledi.