Friday, July 31, 2009

Majambazi yakupua mamilioni NMB Dar



Majambazi yaliyotumia gari zilizokuwa na nambari za usajili zinazofana na za magari ya serikali kuvamia benki ya Benki ya NMB tawi la Temeke mida ya saa tano na dakika 13 asubuhi ya leo, kufanya mashambulizi na kupora fedha zaidi ya Sh150 milioni.

Katika heke heka hizo majambazi hayo yalimuua mlinzi mmoja, kuwajeruhi watu zaidi ya kumi wengine wakiwa mahututi waliokimbizwa hospitali Temeke na Muhimbili.

Majambazi hao walifika wakiwa na silaha kali pamoja na mabomu mengine yakiwa kwenye vifuu vya nazi walikuja na magari mawili moja yenye namba za usajili STJ aina ya Prado yenye rangi ya kijani na Vitara yenye namba SU.

Walianza mashambulizi katika kibanda cha mlinzi kwa kupiga risasi hovyo iliyowajeruhi askari na kuamua kurusha bomu lililomfikia mlinzi wa benki hiyo aliyetambulika kwa jina la Seif Mwikwike wa kampuni ya Moku Security Service iliyomjeruhi vibaya katika maeneo ya kichwani, kifuani na mguuni na kupoteza maisha yake.

Hali ya mashambulizi yaliendelea wakati majambazi hao walipoingia ndani ya benki hiyo kwa kuanza kuwajeruhi baadhi ya watunza fedha (Cashiers) kwa kurusha bomu lingine ambalo lilimjeruhi mhasibu iliyosababisha kusambaa kwa damu ndani ya benki. Taarifa kwa mujibu wa Felix Mwagara wa Mwananchi

Mzee wa Mshitu ndani ya Bunge






Mzee wa Mshitu (mwenye suti jeusi) akisalimiana na Mheshimiwa Spika Samuel Sitta, pia waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi , John Pombe Magufuli katika viwanja vya Bunge, alipotembelea taasisi hiyo Jumatatu wiki hii. Wengine wanaoangalia ni Kisima Cha Fikra (mwenye suti ya kahawia) na Bakari Machumu, Mhariri Mtendaji wa The Citizen (tall). (picha na Jube Tranquilino)

Thursday, July 23, 2009

Hatimaye Mkonga wazinduliwa rasmi


Rais Jakaya Kikwete akizindua rasmi Mkongo wa Kimataifa mawasiliano uliopita chini ya bahari uliowekwa na kampuni ya Seacom Dar es Salaam leo hii ambao utatuunganisha na dunia kimawasiliano kwa urahisi na gharama nafuu zaidi.

Wednesday, July 22, 2009

Some shots from Bagamoyo



Mambo ya Bwagamoyo haya hapa wanaonekana vijana wa "YOMnet" wakiwa mitaa ya Bwagamoyo baada ya kupata somo kali hivi karibuni, jengo kwa upande mwingine ni mojawapo ya maboma yaliyopo wilayani humo. Wilaya hii ni wilaya tajiri mno kwa utalii ingawa kuna mambo kadhaa yanaikwamisha kuendelea katika kiwango kinachostahili. Picha za Yomnet.

Spika akiwa majuu


Spika Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati Maalum ya maspika wa Jumuiya ya Mabunge duniani (IPU) iliyofanya mkutano wake mjini Geneva tarehe 16 hadi 17 Julai 2009 ili kufanya maandalizi ya mkutano wa maspika wa dunia utakaofanyika Geneva mwaka 2010. (Picha na Ofisi ya Bunge)

Tuesday, July 21, 2009

ONYESHO LA USIKU WA KANGA DODOMA!!





Onyesho lao la mavazi lililofanyika kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma Julai 17, onyesho hilo lilipambwa na bendi ya Kalunde inayoongozwa na mwanamuziki Deo Mwanambilimbi huku wabunifu kadhaa wakishiriki kuonyesha nguo zao, wabunifu hao ni Asia Idarous mwenyewe, Gymkana na Grace Matovolwa na Mbunifu Gymakana (Paka Wear), hakika show ilikuwa ya nguvu watu kibao, waheshimiwa kibao walikuwapo

Sunday, July 19, 2009

Jua kupatwa keshokutwa


wataalamu wanatuambua jua litapatwa mnamo julai 22 mwaka huu ambapo kuna sehemu mbalimbali duniani watashuhudia kupatwa kamili kwa jua. wadau mlio maeneo hayo tunasibiri taswira. maeneo yanayotabiriwa kuwa na kupatwa kamili kwa jua ni India, Nepal, Bangladesh, Bhutan, Myanmar, China, Japan na juu ya Kiribati. Vile vile sehemu za Marshall islands katika bahari ya Pacific.
Sehemu zingine ni Surat, Varanasi, and Patna in India, Thimphu huko Bhutan, Chengdu, Chongqing, Wuhan, Hangzhou na Shanghai huko China. Nchi karibu zote za Kusini Mashariki mwa Asia na visiwa kibao vya bahari ya Pacific. Visiwa vya Iwo Jima Kaskazini ndiko inasemekana wataona kupatwa kwa jua kwa muda mrefu kuliko sehemu nyingine.

Giraffe Ocean View



Hii ni sehemu mojawapo ya ukarabati mkubwa unaoendelea hivi sasa pale kwenye hoteli ya kitalii ya Giraffe Ocean View.

Friday, July 17, 2009

Mdigrii



kwa waliowahi kusoma hapa mlimani nadhani watakuwa wanaufahamu vizuri mti huu maarufu kama MDIGRII. Chini ya mti huu vichwa vilikuwa vikiumia na mambo mengi wakati huo hakika nimeukumbuka mdigrii, hivi sasa ndivyo unavyoonekana mti huu kama ulivyokutwa na mdau wetu, zamani tulikuwa tukibeba viti baadaye vikajengwa vijiwe tulivyovifahamu kama VIMBWETE kutokana na umaarufu wa aliyeanzisha mpango wa mabadiliko ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Tolly Mbwete ambaye wakati huo alikuwa kitivo cha Uhandisi sasa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Rais Kibaki ndani ya Bongo


Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha nchini Rais wa Kenya Mwai Kibaki kwa ziara ya kiserikali.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakilakiwa na akinamama wakazi wa Dar es Salaam baada ya Rais Kibaki kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana kwa ziara ya kiserikali.

Wednesday, July 15, 2009

Daftari la Kudumu la Wapiga kura

Rais wa Usalama Barabarani akiwa katika kituo cha kuandikisha wapiga kura skuli ya Wingwi kusimamia zoezi hilo la uandikishaji. Licha ya hali kuwa shwari, kuna askari wengi wa vikosi vya usalama na ulinzi katika maeneo ya vituo vya uandikishaji wakiwemo hata askari wa barabarani kama alivyoonekana huyu jana Julai.

Wazee wakiwa wamejipanga chini kusubiri zamu zao za kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha skuli ya Wingwi, wilaya ya Micheweni Pemba leo. Picha kutoka kwa salim said, Pemba

Tuesday, July 14, 2009

Gesi kuanza kutumika kwenye magari


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (wa pili kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Ethur Mwakapugi na kushoto kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.

Mfanyakazi wa PanAfrican Energy (T) LTD ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akimuonyesha Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) jinsi ya kuweka gesi katika gari maalum wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama kulia kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akimsikiliza mkazi wa Ubungo Maziwa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kuhusiana na maombi yao ya kulipwa fidia ili waweze kahama eneo hilo na kupisha ujenzi wa mitambo kupeleka gesi majumbani, kwenye taasisi na kwenye magari. Waziri Ngeleja alifika katika eneo hilo leo kwa ajili ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagane wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliopo Ubungo jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Msitu wa Nyumbanitu




Kijiji cha jadi cha Nyumba Nitu kilichopo Kata ya Mdandu Wilaya ya Njombe. Kijiji hiki ni muhimu sana kwa utalii na ni muhimu sana kwa utunzaji wa mimea na hifadhi ya mazingira.
Msitu huu ni wa maajabu sana kwani miti yake na mimea yake iko pale kwa karne nyingi na hata wanafunzi wetu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine huenda pale kwa kujifunza aina za mimea.
Mbali ya msitu kuna kuku weusi wa ajabu na kuna mapango makubwa pale Nyumbanitu ambayo watu zaidi ya mia moja wanaweza kuishi kwenye mapango hayo yalikuwa yanatumika wakati wa vita. Maajabu hayo ni sawa kabisa kama yalivyo nchini Japan. Picha imepigwa na mdau Tumaini Msowoya aliyekuwapo ndani ya msitu huo kwa siku nzima amenieleza mambo mengi kuhusu msitu huu si mchezo.

Monday, July 13, 2009

Irene Uwoya mambo safiii



Hamad Ndikumata akitia saini shahada ya ndoa huku bibie Irene Uwoya akishuhudia kwa makini mkubwa

Mitaa ya Mbauda



Mambo ya Arusha hayo hebu cheki wakazi wa vitongoji vya Mbauda, Mianzini na Sanawari wakipata shule kuhusu namna ya kupanga uzazi iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali linalotoa Elimu ya Afya kwa jamii nchini (PSI-Tanzania), Shirika hilo la kimataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii linaendesha programu ya matumizi ya uzazi wa mpango. Picha kwa hisani ya PSI.

Daftari la kudumu la wapiga kura


Akinamama wa Wingwi wasioona wakiwa katika hali ya kukata tamaa baada ya kufukuzwa kutoka kituo cha kuandikisha kura huko mitaa ya Wingwi baada ya kukosa vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi. Picha ya Salim Said.

Friday, July 10, 2009

Kempinski nyingine yazinduliwa


President Jakayas Mrisho Kikwete and the owner of the Bilila Lodge Kempinski Mr.Ali Al Bwardy unveils the plaque to signal the official opening of the Bilila Lodge Kempinski in Serengeti this morning(picture by Freddy Maro)

President Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the official opening of the world class five star Bilila Lodge Kempinski located in Serengeti National park.The hotel can accomodate up to 160 guests in the 80 rooms.

Across section of the invited guests who particpitated in the ceremonies for the official opening of a five star Bilila lodge Kempinski in Serengeti,Mara Region this morning.

Morogoro leo




Mfanyabiashara wa kuuza machungwa katika Manispaa ya Morogoro akitayarisha machungwa kwa kumenya maganda huku mteja akirufuhaia kula tunda hilo katika eneo la uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchuuzi wa kuuza nguo za mitumba mjini Morogoro akifurahia jambo huku mteja wake wakati akichagua nguo hicho alizoweka katika beka jirani na stendi ya daladala mjini hapa. (Picha na Juma Mtanda.

Wednesday, July 08, 2009

Mtoto wa Michael Jackson aliza wengi


Mwili wa mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson ukiwa kwenye jeneza lenye kuta za dhahabu uliagwa na maelfu ya washabiki wake waliohudhuria kwenye ukumbi wa Staples Center wakati mamilioni ya washabiki wake wengi duniani walifuatilia tukio hilo kwenye luninga na internet. Picha za hafla ya kuuaga mwili wa Michael Jackson mwisho wa habari hii.
Akiongea kwa mara ya kwanza mbele ya halaiki ya watu, mtoto wa kike wa Michael Jackson , Paris, mwenye umri wa miaka 11 aliwaliza watu wengi pale alipopewa nafasi ya kuongea.

"Tangia nilipozaliwa, baba amekuwa ni baba bora ambaye hana mfano, ningependa kusema kwamba nampenda sana" alisema Paris na kuanza kuangua kilio huku akikumbatiwa na shangazi yake Janet Jackson.

Awali akiongea katika hafla hiyo ya kuuaga mwili wa Michael Jackson, mchungaji Al Sharpton aliwaambia watoto watatu wa Michael Jackson kuwa wasijali habari mbaya zinazosambazwa juu ya baba yao.

"Nataka watoto watatu wa Michael Jackson wajue kwamba baba yao alikuwa si mtu wa ajabu kama anavyoandikwa" alisema Sharpton na kuongeza "Vitu vya ajabu ni vile ambavyo baba yenu ilimbidi avikabili".

Safari ya Michael Jackson ilianzia kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti ya Forest Lawn ambapo familia yake na ndugu zake walikusanyika kwa maombi na kulichukua jeneza lake tayari kwa safari ya kuelekea kwenye ukumbi wa Staples Center ambako watu 20,000 walikuwa wakisubiri.

Baada ya hapo jeneza la dhahabu la Michael Jackson lilipandishwa kwenye gari la kifahari huku helikopta 20 za waandishi wa habari zikifuatilia tukio kutoka angani.

Msafara wa magari mengi ya kifahari ulianza kuelekea kwenye ukumbi wa Staples Center ambako familia , marafiki na watu maarufu walijumuika na washabiki wa Michael Jackson ambao walibahatika kushinda bahati nasibu ya tiketi za kuhudhuria hafla hiyo.

Monday, July 06, 2009

CCM yashinda Biharamulo

CHAMA cha CCM hatimaye kimeshinda uchaguzi wa jimbo la Biharamulo Magharibi na kukibwaga chama pinzani cha Chadema kwa kra si zaidi ya 1,000.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Zuberi Mbyana alisema kuwa CCM wameibuka washindi kwa tofauti ya kura 861 baada ya kupata kura 17561 dhidi ya 16,700 wakati chama cha TLP kikiambulia kura 198.

Alisema katika uchaguzi huo jumla ya watu 87,188 walijiandikisha kupiga kura lakini waliopiga kura walikuwa ni 35, 338 hivyo kura halili zilikuwa ni 35,459 na kura zilizoharibika 879.

Wakati msimamizi akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa oganaisheni na mafunzo Benson Kigaila naye alikuwa akiwatangazia wanachama wake kuwa wao bado wanaamini matokeo yao kuwa wameibuka washindi lakini msimamizi ameamua kuwasaidia CCM kwa kutangaza matokeo wameshinda.

Kila mfuasi wa chama alikuwa akishangilia matokeo yake na kujinadi kuwa kashinda hatua ambayo ilivuta mvutano kwa viongozi wa vyama hivyo na kulazimika kuhakiki matokeo yote kwa kupitia kata zote nane wakiwa mbele ya msimamizi wa uchaguzi. Imendaliwa na Fredrick Katulanda.

Kigamboni ya leo




Kijijini kwetu huku Kigamboni mambo yetu ni shega tuu yaani kila mmoja na mambo yake kila mmoja na kibanda chake cha kujificha hebu cheki mbavu hizo ambazo nyinyi mnaziita mbavu za mbwa kwetu sisi hizi ni sawa na matofali tuu hali ya hewa ndani ya nyumba zetu hizi ni coool sana kisha ukiona maji tunayokunywa utasema nini sijui hebu cheki katika picha maji ya kufa mtu hahahahahaha ilimradi maisha ni kama kawa. Picha ni ya mdau.

Sunday, July 05, 2009

Matokeo Biharamulo

MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Biharamulo Magharibi yameonyesha Chama cha Chadema kikikaba koo chama cha CCM kwa kura chache ambazo hata hivyo zinaweza kufikiwa na CCM.

Mpaka sasa asilimia 84 ya kura zimeshahesabiwa na matokeo yanaonyesha kuwa Chadema kimezoa asilimia 51.2 ya kura zote huku CCM kikipata asilimia 48.8 ya kura na TLP kimiambulia asilimia 0.65. Matokeo haya ni ya awali na hayajathibitishwa na tume ya uchaguzi.

Matokeo kamili yatatolewa kesho hivi sasa wanakusanya masanduku ya kura na matokeo kutoka bush na vyama vimekubaliana matokeo kesho. Tofauti na uchaguzi uliopita, matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Biharamulo yamekuwa ni ya kushangaza, kwani katika maeneo ya vijijini ambako ndiko kunakotarajiwa kuwa ngome ya chama tawala cha CCM baadhi ya kata zinaonyesha kuwa na kura nyingi za mgombea wa Chadema.

Lakini pia maeneo ya mijini ambayo yanaonekana kuwa ni ngome kubwa ya vyama vya upinzani, lakini kwa Biharamulo CCM ilionekana kuchuana vikali katika vituo na kata mbalimbali huku vituo vingine vyama hivyo vikilingana kwa kura. Matokeo kamili tutawaletea kesho.

dawa za kukuza matako, matiti



Pichani Meneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza akionyesha mojawapo ya dawa za kuongeza matako na matiti kwenye viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere (DITF), dawa hizo zimeelezwa kuwa na athari zinazosababisha kansa.

Wakati huo huo TFDA imewatahadharisha wanawake wanaotumia vipodozi vya kuongeza makalio na matiti kwamba wanaweza kupata madhara ya figo, ubongo na kansa ya ngozi.

Mkaguzi wa dawa vipodozi na vifaa vya tiba wa TFDA Kissa Mwamwita alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake wanaotumia vipodozi hivyo ambavyo havijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwamwita alisema vipodozi hivyo vimekuwa vikiingizwa nchini na kuuzwa kwa kificho huku ikidaiwa kuwa wateja wake wakubwa ni wanafunzi wa sekondari na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Mwamwita aliwataka wanawake wanaotumia vipodozi kuwa makini wakati wanaponunua vipodozi kwa kuangalia kama vimesajiliwa kwani vipo vipodozi vinavyouzwa kwa kificho.

“Matumizi ya vipodozi hivyo vinavyoongeza ukubwa wa makalio na matiti ni hatari kwa afya na pia yanawaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya saratani,” alisema Mwamwita.

Alisema watumiaji wa vipodozi wanatakiwa kuwa makini wanapotaka kununua bidhaa hizo ili kuepuka kununua vipodozi vyenye viambata vya sumu.

Hata hivyo TFDA imetoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kutumia vipodozi vyenye viambata vya sumu zikiwemo ‘losheni’ kuacha kutumia kwa kuwa kiafya vina madhara makubwa.

Mwamwita alitaja baadhi ya vipodozi vyenye viambata kuwa ni Chloqinone,Chloroform na Mercury Compound.

Foleni Ndefu


Baadhi ya wakazi wa mjini Biharamulo wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura ya kumchagua mbuge wa Jimbo la Biharamulo Mgharibi kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katika kituo cha Shule ya Msingi Umoja Mjini Biharamulo Mkoani Kagera jana wa kutafuta mirithi wa kiti hicho kilichoachwa wazi na Marehemu, Phares Kabyeu. Picha na Salhim Shao

Uchaguzi Biharamulo





Wananchi katika Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera leo wanapiga kura kumchagua mbunge wao baada ya kampeni za uchaguzi huo kukamilika jana huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali kati ya vyama vya Chadema na CCM.

Leo wanapiga kura kumchagua mbunge wao baada ya kampeni za uchaguzi huo kukamilika jana huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkali kati ya vyama vya Chadema na CCM.

Katika uchaguzi huo, ambao kampeni zake zilitawaliwa na vurugu, kila chama kilifanya kampeni ya nguvu kutupa kete yake ya mwisho kujinadi kwa wapigakura.

CCM ilihitimisha kampeni zake Biharamulo mjini katika Uwanja wa Sokoni, huku Chadema ikihitimisha kampeni zake katika uwanja wa mpira mjini hapa.

Wanaochuana ni Dk Anthony Gervas Mbassa wa Chadema, Oscar Rwegasira Mukassa wa CCM na Mpeka Buhangaza wa TLP.

Katika uchaguzi huo vituo 238 vimetengwa kwa ajili ya kupigia kura na waliojiandikisha kupiga kura ni watu 87,189.


Lwakatare naye yumo Chadema.