Tuesday, December 31, 2013

JAMAA AKWEA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO AKATAA KUSHUKA HADI AONANE NA RAIS HATIMAYE ASHUSHWA

 
Jamaa mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana leo majira ya saa 5 na nusu asubuhi alipanda juu ya mnara wa kampuni ya simu Vodacom mkabala na ofisi ya Tbs,alipokuwa juu ya mnara alikua na picha pamoja na document mbalimbali ambazo alisema hashuki mpaka Rais Jakaya Kikwete afike eneo hilo.

Baadhi ya mashuhuda wanasema kuwa jamaa ni mpiga debe maeneo ya ubungo na madai yake alifungwa jela miaka 6 bila hatia hivyo moja ya sababu zilizofanya apande juu na kuhitaji kuonana na rais kwa ajili ya kuzungumza nae.
 Kikosi cha Zimamoto na uokoaji walifanikiwa kumshusha majira ya mchana huu na kumpeleka moja kwa moja kituo cha polisi.

Sasa Soma Kwa Makini Rasimu Yote Ya Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Iliyokabidhiwa Rasmi Kwa Rais Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akipokea rasmi Rasimu ya Katiba Mpya ambayo itajadiliwa hapo baade na Bunge maalum la Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba katika Makabidhiano yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam jana.

JK amteua Ernest Mangu IGP mpya


Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu,
Na Mwandishi Wetu,Mwananchi

Rais Jakaya Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa jana usiku na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini aliyestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza kesho, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika jeshi hilo la Polisi. Pia taarifa hiyo ilisema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).  

Tazama Picha ya Mwisho Kupigwa IGP, Said Mwema akiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania muda mfupi kabla ya Rais Jakaya Kikwete Kumteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu Kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Nchini


Picha juu ndio picha ya Mwisho kupigwa IGP, Said Mwema akiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania. Picha hii ilikuwa jana katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Picha na Mroki Mroki

Rais Jakaya Kikwete Katika Hafla Ya Kukabidhiwa Rasmi Ya Katiba Kwenye Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar es Salaam

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba mara baaada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Hall kupokea Rasimu ya Pili ya Katiba. Kulia ni Mhe. Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu huku Jaji Mkuu wa Tanzania Bara Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Muungano Mhe Anne Makinda na Spika wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho wakisubiri zamu zao
 Rais Kikwete akimuamkia  na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 Rais Kikwete akimuamkia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya
 Meza kuu
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Jukwaa kuu la pili
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiwa na wajumbe wenzie wa Tume na maofisa wa serikali
 Dkt Asha Rose Migiro, Mama Amne Salim na Mama Warioba
 Sehemu ya wananchi walioshuhudia tukio hilo la kihistoria
 Wananchi wakiwa katika hafla hiyo
 Wananchi wakifuatilia hafla hiyo
 Watangazaji wa TBC wakiwa kazini kurusha live tukio hilo
 Baadhi ya wazee mashuhuri katika hafla hiyo. 
 Wadau mbalimbali
 Wadau katika hafla hiyo
 Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa
 Wadau wa habari 
 Wanasheria nguli, Mzee Mark Bomani na Profesa Issa Shivji wakiwa miongoni mwa wadau
 Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe Alfani Mpango akijumuika na wadau
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na mabalozi
 Wadau na maafisa wa serikali
 Maafisa wa ofisi wa Masajili wa vyama
 Wadau
 Wadau na maafisa mbalimbali
 Makatibu wakuu
 Mawasiri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Mawaziri wa Bara na Zanzibar
 Mawaziri, wabunge na maafisa wa serikali
 Sehemu ya mawaziri wa bara na wa Zanzibar
 Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi (wa tatu kushoto) akiwa ameketi na wabunge na viongozi wa vyama mbalimbali 
 Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo
 Meza kuu ikimsikilia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba 
 Rais Kikwete akimkabidhi Sir George Kahama nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais Kikwete akiwakabidhi Mzee Hassan Nassoro Moyo na Jenerali Sarakikya nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akisoma hotuba yake
 Rais Kikwete akihutubia
 Wabunge na wadau wengine wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume kwa kazi nzuri
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu na wajumbe wa Tume
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu, wajumbe wa tume 
 Viongozi wakuu, viongozi wa vyama vya siasa na wajumbe wa Tume
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mhe Tundu Lissu
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba 
 Rais Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia
Nikiripoti kutoka hapa katika viwanja vya Karimjee ni mimi.... wa Mlimani TV.Picha Zote na IKULU