Monday, January 22, 2007

Mahalu

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, akitoka kizimbani ambapo alipandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, wizi na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni. Picha ya Deus Mhagale.

Balozi Mahalu kizimbani

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, wizi na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Balozi Mahalu alitiwa mbaroni na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takuru) pamoja na watu wengine wawili waliokuwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzani nchini humo ambao nao wanaohusishwa na tuhuma hizo. Wengine ni Steward Migwano ambaye alikuwa Mtunza Fedha na Grace Martin ambaye alikuwa Afisa Utawala ubalozini hapo.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo ya Kisutu asubuhi ya leo wakiwa kwenye gari la Takuru aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili T385 ALK na kusomewa mashtaka hayo yanayohusiana na upotevu wa Euro 2,065,827.60 wakati wakiwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia. Euro ni sawa na Sh1,692.74.

Friday, January 19, 2007

Masikini tulie tuu hatuna chetu!

UNAWEZA kutuita jina lolote unalotaka, na kisha ukatudharau na kutupachika kila unaloona linafaa. Mara sisi ni wavivu wa kufikiri, mara eti mikopo ipo ila tumelala hatuichukui. Ebo tutaichukuaje wakati hali yenyewe ndiyo hii. Nasikitika nazungumzia sisi masikini.

Masikini katika ardhi yetu hii ya mama yetu Tanzania, tutaendelea kuwa masikini hata iweje na mipango yote inayoanzishwa wala haiwezi kutulenga kamwe, bali itakuwa inawalengeni ninyi wenye unafuu wa maisha.

Na itawafanya muwe matajiri wa kufuru kwa mgongo wetu, na siyo mgongo wetu tu, bali hata jasho letu la damu na machozi yetu, na hamtakaa mkajua tunateseka vipi hadi na nyinyi muwe kama sisi jambo ambalo haliwezekani. Soma zaidi kwa kubonya hapa:

Thursday, January 18, 2007

Monday, January 15, 2007

Mama Migiro safarini

Kuna mdau mmoja alibahatika kusafiri ndege moja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro, na huu ndo ulikuwa ujumbe wake katika safari hiyo kama nilivyoukuta katika kwa kubonya hapa: ina headline ACHA HIZO MRS MIGIRO

Mama Migiro hongera sana kwa kuteuliwa kuwa deputy UN sec. general. Lakini kitendo chako cha kuichelewesha KLM for more than one hour pale DIA eti unagoma na unatia mkwara ndege isiondoke kisa one of your staff aliekuwa akiku-accompany awe upgraded to business class la sivyo ndege haiondoki sio cha kiungwana kabisa. Maskini ilibidi abiria mmoja wa business class ajitolee kukaa economy ndio staff wako akenda b-class na ndege ikaondoka but tukachelewa for more than one hour. bila hivyo sijui ingekuwaje.
Mbona nimepanda ndege mara nyingi tu na former prezo Clinton from DC-JFK tena anakaa economy?
be careful kwani hata NYC mayor tunapanda nae subway on top of that he's a billionaire.
Jamaa anaitwaDaddy Yankee

Thursday, January 11, 2007

Doha moja kwa moja hadi Bongo


Pichani dege la Quartar Airlines lenye uwezo wa kubeba watu 110 sasa linafanya safari za moja kwa moja toka Doha hadi Dar mara nne kwa wiki. Karibuni Bongo usafiri simple sasa. Picha ya Deus Mhagale.

Mchezo wa nyoka


Mmoja wa wanakikundi wa Simba Theatre akicheza na nyoka katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKNyerere(Picha yaDeus Mhagale)

Monday, January 08, 2007

Rais Kikwete na mstaafu Mkapa


Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. Nchi nyingine ni nadra sana kufanya hivi, akimaliza madaraka Rais anakuwa na mgogoro na anayefuata.

JK na BMWMarais Jakaya Mrisho Kikwete na Mstaafu Benjamin Mkapa katika Mazishi. (Picha ya Mpoki Bukuku)

Saturday, January 06, 2007

Waziri Migiro ateuliwa Naibu Katibu Mkuu UNWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa.

Kutokana na uteuzi huo, tayari Rais Jakaya Kikwete amemruhusu Asha-Rose kwenda kuchukua nafasi hiyo haraka iwezekanavyo, hiyo ikimaanisha kuwa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa sasa imebaki wazi.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jioni ilisema kuwa uteuzi huo umefanywa na Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ambaye amechukua nafasi ya Koffi Annan, akianza kazi hiyo mpya mwezi huu.

Taarifa hiyo imemkariri Rais Kikwete akisema anayo furaha kubwa kwa Mtanzania kupewa nafasi kubwa kama hiyo ya kuutumikia Umoja wa Mataifa ambao ndiyo chombo cha juu kabisa duniani.

"Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni wizara nyeti kwangu, lakini uteuzi huu pia ni heshima kubwa kwa Tanzania na kwa Migoro mwenyewe," ilisema sehemu ya taarifa hiyo, ikimariri Rais Kikwete.

Mapema kabla ya uteuzi huo, Moon alizungumza kwa simu na Rais Kikwete kumweleza juu ya uamuzi wake kutaka kufanya kazi na Waziri Migiro, na yeye mwenyewe akampigia simu Migiro kumjulisha juu ya uteuzi huo.

Wakati akiteuliwa kupewa nafasi kubwa namna hiyo katika Umoja wa Mataifa, Migiro alikuwa hayupo nchini kwani alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Lesotho.

Migiro anakuwa Mtanzania wa pili kupewa wadhifa mkubwa katika Umoja wa Mataifa baada ya mwanamke mwingine, Profesa Anna Tibaijuka, kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Makazi ya Umoja wa Mataifa (UN- Habitat) yenye makao yake makuu Nairobi, Kenya.

Tuesday, January 02, 2007

Maalim Seif na Rais Karume


Ni urafiki tuu au kuna mashaka ndani yake hapa viongozi hawa walikutana siku ya Idd El Hajj.