Friday, May 30, 2008

Zombe afoka mahakamani

MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge,mkoani Morogoro na dereva teksi mmoja wa jijini Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, amewafokea waendesha mashtaka kwa madai kwamba wanachelesha kesi yake.

Zombe alitoa tuhuma hizo jana wakati kusikiliza kesi yake inayoendelea katika Mahakamu Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Mbali na malalamiko hayo, pia aliilaumu mahakama hiyo kuwa haimtendei haki, kwa kukubali kusikiliza mashitaka yake kinyume cha sheria.

Alifafanua kuwa alipokamatwa awali, alishitakiwa na kufikishwa mahakamani bila kupewa nafasi ya kutoa maelezo kuhusiana na mashitaka hayo.

Zombe alitoa malalamiko hayo baada ya mawakili wa utetezi kupinga shahidi namba 11, D8790 koplo John kutoka Kituo Kikuu cha Polisi kutoa ushahidi wake kutokana na kutokidhi masharti ya kisheria ya kutoa ushahidi. cheki MWANANCHI KWA KINA

miss universe 2008


Miss Universe TZ 2008 Amanda Sululu akipozi muda mfupi baada ya kutangazwa kwenye Ukumbi wa Movenpick usiku kuamkia leo. Huyu ndiye mrithi wa Flavian Matata ambaye mwaka jana aliingia tano bora kwenye mchuano wa dunia. amanda si mgeni sana kwenye ulimbwende kwani mwaka jana alishiriki Miss TZ

Miss Universe Tanzania, Amanda Sululu,katikati, akipozi muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi kwenye Ukumbi wa Movenpick Da es Salaam juzi,kushoto ni mshindi wa pili Jamila Nyanga na Eva Babuely. Picha za braza Michuzi.

Waziri Mkuu asifu maandalizi ya Sullivan

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema ameridhishwa na maandalizi kwa ajili ya mkutano wa
nane wa kimataifa wa Leon Sullivan unaotarajiwa kufanyika Arusha kuanzia Jumatatu
ijayo.

“Tumekuwa na maandalizi ya muda mrefu, lakini kama Serikali ilibidi tufike kuona
hali halisi na kujiridhisha na jinsi kazi inavyokwenda… kwa kweli mambo yanakwenda
vizuri, kuna mabadiliko makubwa nimeyaona na mfano ni hapa AICC,” alisema Waziri
Mkuu.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Ijumaa, Mei 30, 2008) wakati akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ukumbi wa mikutano wa AICC ambako mkutano
huo utafanyika.

Kabla ya kukagua ukumbi huo, Waziri Mkuu alitembezwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambako wajumbe wa mkutano na wageni mashuhuri (VIPs)
watafikia kuanzia kesho (Jumamosi).

Alisisitiza haja ya kutowakawiza wageni hasa katika maeneo ya idara za Uhamiaji na
Forodha. “Sisemi kwamba muwaachie tu, hapana, nataka taratibu zifuatwe lakini zisiwe
kero…” alisisitiza.

Akiwa njiani kuelekea Arusha mjini, alikagua maeneo ya hoteli ya Ngurdoto ambako
wageni mashuhuri watafikia na ambako dhifa ya kitaifa itafanyika. Pia alifanya
mazungumzo na Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo pamoja uongozi wa mkoa wa Arusha.

Waziri Mkuu amerejea Dar es Salaam leo jioni.
 
Ends

AICC SULLIVAN


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi
Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya (kulia) jana Arusha alipotembea
kujionea ukumbi utakaofanyika mkutano wa Sullivan kuanzia Jumatatu.
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Isidory Shirima. Picha na Edwin
Mjwahuzi

Mkapa leaves for UK

Former President Benjamin William Mkapa in his capacity as the Co-Chair of Investment Climate Facility for Africa (ICF) will be leaving Dar Es Salaam on Sunday 01st of June 2008, for London (United Kingdom).

Former President Mkapa and Mr. Niall FitzGerald (KBE) will Co-Chair the Board of Trustees and the Annual General Meetings from 2nd to 3rd June 2008.

The Investment Climate Facility for Africa (ICF) of which the headquarters is in Dar Es Salaam, seeks to help Africa to create a more attractive business environment and realize its potential as global player and trading partner.

The ICF works toward removing real and perceived obstacles of domestic and foreign investment by assisting Africans to prepare and promote the continent as an investment destination.

Today, ICF has a number of projects in different African countries. One example, two weeks ago the ICF signed an agreement with the Judiciary to expedite and facilitate court process in Tanzania. The priority areas for the ICF support are in (i) Property rights and contract enforcement (ii) Business registration and licensing, (iii) Taxation and customs (iv) Financial Markets (v) Infrastructure Facilitation (vii) Labour Markets, and (viii) Competition.

MUGABE


IF ANYONE HAS SEEN THIS CHILD PLEASE CALL 10111 URGENTLY, HIS PARENTS ARE LOOKING FOR HIM 

Wanamuziki wa Marekani ndani ya Bongo

Wanamuziki wa Jazz kutoka Marekani AMP Fiddler na N'dambi Blue waliopo nchini wakiwa katika pozi mbalimbali mara baada ya kuwasili nchini kufanya maonyesho kadhaa kwa udhamini wa Zantel, e bwanaa wako makini hawa si mchezo ndugu. Picha ya mdau Kassim Mbarouk.

Thursday, May 29, 2008

Mwenge choma


Mkuu wa Mkoa wa Pwana Dk Christine Ishengoma akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo mwaka huu, Shames Nungu tayari kwa kuukimbiza katika wilaya sita za mkoa wake jana. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kijiji cha Msoga, Bagamoyo mkoani Pwani baada ya kuwashwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) kijiji hicho ndio alipozaliwa Rais Jakaya Kikwete.

TATIZO LA USAFIRI


KWELI MAISHA NI SAFARI NDEFU, WATOTO HAWAWAPO NJIANI KATIKA SAFARI YA MAISHA WAKITAFUTA ELIMU, USAFIRI TATIZO, WANAKAA VITUONI MASAA MENGI, WAKIFIKA SHULENI WAMECHOKA NA WANAPOREJEA NYUMBANI MAMBO NI YALE YALE, HIVI TATIZO HILI LA USAFIRI LITAISHA LINI???

Kipanya Leo

Wanachama wafungia ndani uongozi Saccos


MGOGORO wa Chama cha Akiba na mikopo cha Lumumba Saccos Ltd umechukua sura mpya baada ya wanachama wake kuwafungia ofisini viongozi wa chama hicho, baadhi ya wanachama, Mrajisi wa ushirika mkoani Dar es Salaam na Mrajisi wa ushirika wa Wilaya ya Ilala.

Kitendo hicho kilitokea jana saa 4.45 wakati Mnajisi wa Mkoa aliyetambulika kwa jina moja la Mgoe na Mrajisi wa Ilala ambaye jina lake halikupatika walipokuwa wakizungumza na uongozi wa chama hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi, wanachama hao walisema mazungumzo hayo yalitokana na maandamano yao kwa Mkuu wa Mkoa Abass Kandoro, juzi, kumuomba aingilie kati mgogoro wao ambao kiini chake ni kukosa imani na uongozi wa chama hicho.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake, Emmanuel Mwambeta alisema maandamano hayo hayakuwawezesha kuonana na Kandoro ingawa waliahidiwa kuwa tatizo lao litapatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia uamuzi wa kuwafungia viongozi na wawakilishi wao ofisini alisema ni kutokana na kukosa imani hali iliyotokana na kuzungushwa kwa muda mrefu bila kukopeshwa fedha au kukubaliwa kujiondoa katika chama hicho.

Dakika 40 baada ya viongozi hao kufungiwa ofisini, walijaribu kutoka nje kwa kupitia mlango wa ofisi ya pili ambayo inaingiliana na ofisi ya chama hicho hali iliyosababisha vurugu kubwa kiasi cha kuwafanya wamiliki wa ofisi hiyo ya pili kurudisha ndani.

Polisi wanaodiwa kushirikiana na Zombe watajwaWATUHUMIWA wawili katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini waliouwa Januari 14, 2006 jijini Dar es Salaam wakidhaniwa kuwa ni majambazi jana wametambuliwa kuwa ni miongoni mwa askari polisi waliohusika kuwakamata marehemu hao kabla ya kuuawa.

Shahidi wa sita katika kesi hiyo, Mjatta Kayamba mkazi wa Sinza C, Palestina, alimtambua mtuhumiwa namba tatu ASP Ahmed Makele na mtuhumiwa wa tano WP.4593 Jane Andrew kwamba walihusika katika tukio hilo.

Akitoa ushahidi huo mbele ya Jaji Salum Masatti wa Mahakama Kuu ya Tanzania, anayesikiliza kesi hiyo, shahidi huyo alidai askari hao ni miongoni mwa askari watatu waliofika Sinza Palestina karibu na nyumbani kwa Mathew Ngonyani ambako wafanyabiashara hao walikuwa wamekwenda.

Kayamba alidai kuwa, siku hiyo akiwa nyumbani kwake, aliwaona wafanyabiashara hao wakielekea nyumbani kwa Ngonyani wakiwa na gari dogo na kusalimiana na mke wa Ngonyani na muda mfupi baadaye wakati wafanyabiashara hao wanataka kuondoka ilifika gari aina ya Toyota Stout na kuzuia gari ya wafanyabiashara hao kuondoka kwenye eneo hilo.

Kikwete ateua wanawake saba majaji

KATIKA hatua ambayo inaonyesha azma ya kuziba pengo la majaji nchini, Rais Jakaya Kikwete, ameteua majaji 11 wapya ambao saba ni wanawake.

Uteuzi huo wa Rais licha ya kujaribu kuziba pengo la majaji, lakini pia umezidi kuongeza uwiano wa wanawake na wanaume katika nafasi za juu za maamuzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ikulu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, uteuzi huo umeanza Jumamosi iliyopita, Mei 24, 2008.

Rais amefanya uteuzi huo pia ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu ateue majaji wengine 20, ambao alifanya baada ya bunge la bajeti la mwaka jana.

Luhanjo katika taarifa hiyo ya Ikulu, aliwataja wanawake walioteuliwa kuwa majaji ni Sophia Wambura, Crecencia William Makuru, Zainabu Goronya Muruke na Upendo Hillary Msuya.

Wengine ni Atuganile Florida Ngwala, Rose Aggrey Teemba na Rehema Kiwanga Mkuye.

Majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Kassim M. Nyangarika, Gabriel Kamugisa Rwakibarila, Ibrahim Sayida Mipawa na Lawrence Kisenge Nziajose Kaduri.

Katibu Mkuu Kiongozi ametangaza pia kwamba, Rais Kikwete amemteua Ferdinand Leons Katipwa Wambali, kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Wambali anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi wake, Wambali alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani.

Wednesday, May 28, 2008

Usafiri wa bongo balaa


Abiria waendao maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, kutoka Posta Mpya, wakipanda gari kupitia mlango wa nyuma na wale wanaoshuka kutumia mlango wa kawaida kutokana na shida ya magari yaendayo maeneo hayo nyakati za mchana jana. Picha ya Kassim Mbarouk.

Mama wa Ballali awekwa chini ya ulinzi mkali

MAMA wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Ballali amewekwa chini ya ulinzi katika nyumba ya mtoto wake iliyopo Boko, wilayani Kinondoni, nje kidogo ya Jiji la Dares Salam.

Ulinzi huo ambao umewekwa kwa wiki nzima tangu kutokea taarifa za kifo cha Ballali kwa maelekezo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), unazuia watu mbalimbali kuingia, wakiwemo waandishi ili wasikutana na mama huyo wala yeye kuzungumza chochote.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema benki hiyo haijatoa maelekezo ya kuwepo ulinzi nyumbani kwa mama huyo.

"BoT haijatoa maelekezo ya kuwepo ulinzi, kwa nini itoe maelekezo ya kuwepo ulinzi, au kwa nini iingilie mambo ya familia?" alihoji Profesa Ndulu.

Kwa mujibu wa profesa Ndulu, BoT imekuwa ikiwezesha kufanyika mambo manne ambayo ni ubani, viti, mahema na vinywaji.

"Inachofanya BoT ni kusaidia matanga kwa vitu vinne, ambavyo ni ubani, viti, mahema na vinywaji, lakini hayo mambo ya ulinzi hatuyajui," alisisitiza.
Gavana Profesa Ndulu aliongeza kwamba, suala la ulinzi katika nyumba hiyo ni la familia.

Alifahamisha kuwa ulinzi katika nyumba hiyo ulikuwepo kabla ya matanga na kutaka watu wasiitwishe BoT mzigo ambao si wake.

Profesa Ndulu alifafanua kwamba, BoT itaendelea kusaidia familia hiyo hadi itakaposema kwamba matanga yamekwisha.

"Jamani, msiivishe BoT gunia la moto, sisi hatuhusiani na hayo mambo ya ulinzi, ila tunasaidia na tutaendelea kusaidia matanga hadi familia itakaposema imemamiliza matanga," alisema. habari ya Ramadhan Semtawa wa Mwananchi.

Tuesday, May 27, 2008

Kesi ya Zombe yaanza kunguruma Mahakama KuuKESI ya mauaji kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake 12, imeanza kusikilizwa jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania na mashahidi 50 upande wa mashitaka wanatarajia kutoa ushahidi.

Kesi hiyo ambayo ilivuta umati mkubwa wa watu, ambao walifika katika mahakama hiyo ili kuisikiliza, ilianza saa 4.15 asubuhi mbele ya Jaji Salum Masatti wa mahakama hiyo.

Shahidi wa kwanza kupanda kizimbani, alikuwa Mathew Alex Ngonyani, ambaye alieleza mahakama kuwa alipata taarifa za kukamatwa na kuuawa kwa wafanyabiashara hao, wakati akiwa kwenye machimbo ya madini huko Mahenge, ambao walikwenda kuuza madini Arusha na Dar es Salaam.

Alisema mwishoni mwa Desemba mwaka 2005, marehemu Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo, alipata madini na kumwomba Ngonyani amsindikize kwenda kuyauza, Dar es Salaam au Arusha.

Alisema kabla ya kuondoka Mahenge, walipata taarifa kuwa wakaguzi wa migodi wangefika kukagua migodi hiyo, hivyo wakaamua kubaki ili kuwasubiri wakaguzi hao.

Alifafhamisha kuwa Marehemu Jongo aliondoka pamoja na Ephraimu Chigumbi, Mathias Lugombi na Protas Mchami wakiwa wanaendesha gari ya Jongo aina ya Landcruser Prado, kwenda Dar es Salaam na baadaye kuelekea Arusha, ambako waliuza madini kidogo kutokana na soko kuwa baya na mengine waliyauza Dar es Salaam.

Ngonyani alidai kuwa wakiwa Dar es Salaam walifikia katika Hotel ya Bondeni, iliyoko Magomeni na kwamba kabla ya kuondoka aliwaagiza wafike nyumbani kwake Sinza Palestina ili kumsalimia mkewe na kumpa fedha za matumizi. Imeandikwa na James Magai

Sunday, May 25, 2008

Waliouawa Afrika kusini sasa 50People displaced by xenophobic violence in Cape Town listen as police brief them on safety at a community hall where they have taken refuge May 24, 2008. The violence started in Johannesburg's Alexandra township on May 11, and has spread to Cape Town and the eastern port city of Durban. REUTERS/Mark Wessels (SOUTH AFRICA )

Rais Kikwete safarini Japan

Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 08) kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe, Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman, Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami na Mbunge wa Muleba Kusini na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.


Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam
25.05.08

Askofu Mokiwa


Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza askofu Mpya wa kanisa Anglikan Tanzania Dk. Valentino mokiwa mara baada ya kutawazwa rasmi kwa askofu huyo kuwa askofu wa tano wa kanisa hilo kwenye sherehe iliyofanyika leo katika kanisa kuu la Anglikana mjini Dodoma. Picha ya ofisi ya Makamu wa Rais.

Rais Mugabe kampeni kijiji kwa kijiji


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace wakiwasalimu wafuasi wao wakati rais huyo alipozindua kampeni za uchaguzi wa marudio katika jiji la Harare jana. Mugabe anamtuhumu Balozi wa Marekani nchini mwake James McGee kwa kuingilia siasa za ndani ya nchi hiyo na akatishia kumfukuza kutoka katika taifa hilo la kusini mwa Afrika. PICHA YA REUTERS.

Bemba anaswa UbelgijiTHE HAGUE, Uholanzi
MMOJA wa makamu wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba amekamatwa hii jana nchini Ubelgiji.

Kiongozi huyo wa chama cha Movement for Liberataion of Congo MLC anashikiliwa kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita vilevile uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kwa mujibu wa Beatrice le Fraper mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Bwana Bemba alikamatwa juzi jioni mjini Brussels.

Mahakama hiyo inataraji kuwa Bemba atafikishwa mahakamani nchini humo Ubelgiji katika kipindi cha siku chache zijazo kisha kuhamishwa kwenye mahakama ya ICC majuma machache yatakayofuatia.

Hati ya kukamatwa kwa Jean Pierre Bemba ilitolewa tarehe 16 mwezi huu wa Mei japo kiongozi huyo wa zamani hakuwa na taarifa yoyote kwani hatua hiyo haikutangazwa hadharani.

Mama Kikwete


Nahodha wa Timu ya mpira wa Pete ya Towna Star ya Nzega akijaribu bila ya mafanikio kumzuia mke wa Rais Mama Salma Kikwete asifunge golki wakati wa uzinduzi wa fainali za mchezo wa pete kati ya timy ya Town Star na Chief Ntinginya.Katika mchezo huo Timu ya Chifu Ntinginya iliibuka mshindi katika fainali hizo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga mpira wa miguu kuzindua fainali za mchezo huo kati ya timu ya Nzega Football club na Shule ya Sekondari Uchama iliyopo Nzega.Katika mchezo huo Nzega FC iliibuka kidedea kwa kushinda Uchama kwa penalti.

Friday, May 23, 2008

IGP atibua safu ya jeshi

JESHI la Polisi nchini limefanya mabadiliko makubwa ya uongozi, ambayo yamefanya Kamanda wa Polisi Mbeya, Suleiman Kova kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuchukua nafasi ya Alfred Tibaigana aliyestaafu.

Kamishna Tibaigana, ambaye atastaafu rasmi Julai, mawaka huu ni wa kwanza kuongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya Jeshi la Polisi baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuanzisha kuzifanya wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke kuwa mikoa katika operesheni za polisi .

Mabadiliko hayo ambayo yameacha furaha na majonzi kwa baadhi ya maafisa wa jesh hilo, yanagusa nafasi za makamanda wa polisi mikoa (ma-RPC), Wilaya (Ma-OCD) na Wakuu wa Upelelezi (Ma-RCO) na wengine walio katika nafasi mbalimbali.

Kufanyika kwa mabadiliko hayo kunatokana na kujaza nafasi za maafisa ambao wanastaafu akiwemo Kamishna Tibaigana, ambaye amestaafu baada ya kutimiza umri wa miaka 60.

Pamoja na Tibaigana, askari wa ngazi za chini 700 ambao kwa pamoja watatimiza miaka 55 wamestaafu, huku maafisa wengine wakirudishwa makao makuu, ifikapo Julai mosi, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Clodwig Mtweve alisema nafasi ya Kamanda Kova itachukuliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Zelothe Stephen.

Kwa mujibu wa Mtweve, katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi (ACP) Jamal Rwambo anakwenda Mwanza kuchukua nafasi ya Stephen.

Mtweve alifafanua kwamba, Mamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi (ACP) David Saibullu anastaafu na nafasi yake itachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACP) Leberatus Barlow ambaye alikuwa ni Afisa Nadhimu, Utawala na Fedha wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Nafasi ya ACP Rwambow itachukuliwa na Kamishna Msaidizi ( ACP) Mark Kalunguyeye kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, huku Kamishna Msaidizi (ACP) Ray Karama, kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akiteuliwa kuwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo ambako Makao Makuu yake yako Arusha.

Katika mabadiliko hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi (ACP) Abdallah Msika anarejeshwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, ambako haikuelezwa atafanyakazi gani huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACP) Selewi kutoka Mkoa wa Pwani.

Kamishna Msaidizi (ACP) A, Mwakyomba kutoka Makao Makuu anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi (ACP) M. Msafiri analetwa Makao Makuu ya
Kurugenzi ya Upelelezi (CID).

Mazishi Rasmi ya Daudi

Daudi Timothy Said Ballali
Viewing: PrivateService: May 23, 2008 @ 10AM
Location: St. Stephen The Martyr
Daudi Timothy Said Ballali On May 16, 2008 of Washington, D.C.
Husband of Anna Ballali
Mass of Christian Burial will be offered on May 23, 2008 at 10AM at St. Stephen,Washington, D.C.Interment Gate of Heaven Cemetery
View the guest book for Daudi Timothy Said BallaliSign the guest bookhttp://www.devolfuneralhome.com/index.asp?sid=6&formid=102&serviceid=960
R.I.P
*Courtesy-Chemi-Chemponda

Thursday, May 22, 2008

Afrika kusini hakukaliki sasa
MAELFU ya wahamiaji wameanza kuikimbia Afrika Kusini kutokana kushambuliwa na makundi ya raia wa nchi hiyo kwa siku kadhaa sasa. Mashambulizi hayo yamesababisha mauaji na inadaiwa mpaka Mei 22,2008 watu 42 ambao ni wageni wamepoteza maisha.
Msumbiji imeandaa mabasi maalumu kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani raia wake na hadi Me1 21,2008 wananchi wake 9,000 wamekwisha kurejeshwa nyumbani wiki hii.
Baadhi ya raia wa Zimbabwe pia wanarejea kwao, wameona ni bora wakakumbane na vurugu za nchini mwao kuliko kuhatarisha maisha yao katika Afrika Kusini.
Wakati watu 42 wamekwisha kuuawa na wengine 15,000 wameomba hifadhi kukimbia mashambulio na vijana hao ambao wanawalaumu wageni kwa uhalifu na kusababisha ukosefu mkubwa wa kazi nchini Afrika Kusini.
Jeshi la nchi hiyo linatumika kusaidia kukabili vurugu hizo – ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994. Lakini polisi wa Johannesburg ambako vurugu hizo zilianzia wamesema hivi sasa hali ni tulivu kwa kiasi fulani.
Polisi walitumia risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi kuyatawanya makundi ya vijana waliokuwa wanafanya vurugu. Raia wa Zimbabwe wapatao milioni tatu wanaaminika wako Afrika Kusini hivi sasa baada ya kukimbia njaa na vurugu nchini mwao.

KIvuko kipya cha Kigamboni


Kivuko kipya kiwa katika matengenezo ya kukiungisha kama kinavyoonekana jana wakati Waziri wa Miundo Mbinu, Dk Shukuru Kawambwa alipofaya ziara ya ukaguzi wa ujezi wa kivuko hicho jijini Dar es Salaam, ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa Picha na Salhim Shao
Kivuko hicho kipya ambacho ni cha tatu cha Kigamboni, Dar es Salaam (Magogoni-Kigamboni) ambacho kimekuwa kwenye ujenzi kwa takribani miezi 15 sasa, kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi Septemba mwaka huu.
Kwa sasa matengenezo ya kivuko hicho yamefikia asilimia 60 na mkandarasi wa kampuni ya Neue Ruhrorter Schiffswerft Gmbh ya Ujerumani ameomba kuongezewa miezi miwili aweze kukamilisha sehemu iliyobakia.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho Mei 22,2008 wakati Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alipokagua kivuko hicho Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ufundi wa Umeme wa wizara hiyo, John Ndunguru alisema kivuko hicho kitakachojulikana kama Magogoni-Kigamboni kikikamilika kitasaidia kuondoa kero ya usafiri Kigamboni.
Kivuko hicho ambacho kimeigharimu Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2006/2007, Sh bilioni 8.8 kina urefu wa mita 74.5 na upana wa mita 17.44 na kina uwezo wa kubeba tani 500, yaani magari madogo 60 na abiria 2,000.

Mke wa Ballali asema anamwachia Mungu

WAKATI bado kukiwa na kiwingu kizito katika chanzo cha kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu (BoT) Daud Balali, mkewe Anna Muganda, ameunguruma kwamba kilichotokea anamwachia Mungu.

Kauli hiyo ya Muganda ni ya kwanza kuitoa kwa kuzungumza na chombo cha habari cha Tanzania, tangu kutokea kwa msiba wa mumewe.

Muganda katika mazungumzo hayo na mwandishi wa habari hii kutokea Marekani, ambayo yalifanyika jana 1:30 usiku kwa saa za Tanzania ambayo ni asubuhi Marekani, alisema kilichotokea ni mipango ya Mungu.

"Mimi namwachia Mungu, Mungu atajua mwenyewe, tumeshapoa nashukuru sana kwa pole," alisema Muganda, huku akikataa kuzungumza kwa undani kuhusu msiba huo. Kwa taarifa za kina Soma Mwananchi. habari hii inaletwa kwenu kwa hisani ya Ramadhani Semtawa aliyezungumza moja kwa moja na mama Muganda.

Wednesday, May 21, 2008

Rais Kikwete Bagamoyo


Rais, Jakaya Kikwete akiongozwa na Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani jana wakati Rais alipokwenda kufunga mkutano wa siku tatu wa majaji mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Picha na Salhim Shao

AMERICAN VISITORS NOW #1 MARKET FOR TANZANIA WORLDWIDE

For the first time ever, American visitors represent the largest single tourism market for Tanzania, attracting a record high of 58,379 in 2007. Taking over from the traditional place held by the UK market, the number is even greater when the US is combined with Canada (North America), 83,930 in 2007. Supporting this growth of tourism from North America to mainland Tanzania and the spice islands of Zanzibar, is the fact that the number of American and Canadian tour operators offering Tanzania as a stand-alone destination has also soared.

“The jump in US and Canadian visitors can be attributed to several factors,” said Hon. Shamsa Selengia Mwangunga, Minister of Natural Resources and Tourism for the United Republic of Tanzania. “One is Tanzania’s aggressive promotion, particularly in the past year. Significantly, so successful have these efforts been that Tourism now exceeds Agriculture as Tanzania’s leading economic sector. A total of 750,000 tourists in all are expected in Tanzania this year. They are predicted to bring in revenue of about $950 million dollars. Second, but of major importance for tourists, is the fact that Tanzania is a peaceful and stable country, with a democratically elected government, strong ties with the US and warm friendly people.”

Peter Mwenguo, Managing Director, Tanzania Tourist Board, added, “we are confident that this trend will continue as we begin to see the results of our first ever TV Broadcast campaign, launched in September 2007, on CNN USA.” The campaign, Tanzania – Land of Kilimanjaro, Zanzibar and the Serengeti” appeared on CNN, CNN Headline News, CNN Airports and CNN.com. It culminated in a Tanzania Sweepstakes on CNN.com in March which resulted in 39,000 plus entries.

Simultaneous to the TV Campaign targeting the American travelers, TTB launched a Tanzania Travel Agent Specialist program through Travel Agent University. More than 500 travel agents completed the course earning certificates qualifying them as Tanzania Specialists.

Balali kafariki dunia
MAMBO ni ya ajabu ajabu kuhusiana na taarifa za Dk Daud Balali, wengine wanasema Mzee Daudi Balali (pichani) amefariki, wengine wanasema amejificha Boston au Washington D.C. huko Marekani!

Kuna habari iliyotoka jana kwenye African Baraza kuwa Mzee Balali anasakwa na wapepelezi kuhusiana na wizi wa dola $133 milioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati huo huo imethibitishwa hapa Bongo kwa Balali, amefariki dunia.Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Patrick Mombo, alithibitisha kifo hicho baada ya kupata taarifa rasmi kutoka Balozi wa Tanzania Ombeni Sefue.

Balozi Mombo aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam kwamba, Balozi Sefue alipata taarifa hizo juzi saa 4:00 usiku kwa saa za Marekani.kwa taarifa zaidi soma mwananchi kesho.

Tuesday, May 20, 2008

Foleni ya mkate


People in Zimbabwe are fed-up

Zimbabwe mambo si mambo hebu cheki hapa wananchi wamejipanga kusubiri mkate ambao ni dili kubwa sana nchini humo hivi sasa. habari kwa kina hebu cheki hapa

Mkuu wa FAO


Louise Setshwaelo Mwakilishi wa FAO nia Tanzania wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa FAO
Dkt Jacques Diouf wakati wakiongea na ujumbe kutoka zanzibar kwenye hotel ya
Kilimanjaro Kimpiski jana Picha kwa hisani ya Wizara ya Kilimo na Chakula.

Maandalizi ya Sullivan

Eneo la mzunguko wa barabara ya Makongoro,Goliondoi na Afrika mashariki ikiwa
inazidi kupendeza katika kuelekea mkutano wa kimataifa wa Sullivan mwezi ujao.PHOTO/GEBO ARAJIGA)

Mkurugenzi wa FAO ndani ya Bongo


Waziri Stephen Wassira (kushoto) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Dk
Jacques Diouf alipowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere hivi karibuni. Picha ya Wizara ya Kilimo na Ushirika

Sunday, May 18, 2008

Kumekucha vijana CCMKINYANG'ANYIRO cha kugombea Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), kimeanza kushika kasi, baada ya mmoja wa wanachama wake maarufu, Hussein Mohammed Bashe, kujitokeza na kutangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 13, mwaka huu.

Bashe (30), ambaye ana Shahada ya Kwanza ya Biashara na Masoko kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, mkoani Morogoro, alitangaza nia yake hiyo alipozungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Millenium Towers, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema amefikia hatua hiyo, ili apate fursa ya kupambana na changamoto zinazoikabili UV-CCM kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini na duniani na kusababisha ishindwe kukidhi mahitaji na matarajio ya vijana wa Kitanzania kwa nyakati za sasa, habari ya Muhibu Said

Masikini MboweMwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe akitoka katika ukumbi wa M-9 wa chuo
kikuu cha SAUT baada ya kumalizika kongamano la vijana kuhusu utunzaji wa
raslimali za nchi pamoja na dhana ya Utawala wa Majimbo lililoandaliwa na Chama
chake, inaelezwa kuwa Mbowe alianguka baaada ya kuteleza na hivyo kuumia mguu ambao
umewekewa P.O.P Picha ya mdau Frederick Katulanda

Friday, May 16, 2008

Wahaini wa Pemba waachiwaSIKU moja baada ya wazee wa Pemba walioshiriki kupeleka barua Umoja wa Mataifa kutishia kuwa watu 10,0000 waliiotia sahihi, watajisalimisha katika vituo vya polisi iwapo wenzao walikamatwa hawatoachiwa, wameachiwa kwa dhamana baada ya kuchukuliwa maelezo yao.

Akithibitisha hilo Kamishna wa Polisi Zanzibar Khamis Mohammed Simba alisema watu saba waliokuwa wamewashikilia katika vituo vya polisi kisiwani Unguja wamechiwa uhuru na kwamba watapewa usafiri wa kuwarejesha kwao Pemba.

“Ni kweli leo Ijumaa tumewaachia watu saba tuliokuwa tumewakamata na
tunaandaa utaratibu wa kuwarejesha kwao wote,” alisema. Kamishna.

Alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuwahoji na kukamilika kwa ushahidi wa awali na kuongeza kuwa iwapo kutahitajika maelezo zaidi watachukuliwa tena na kuhojiwa kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa bado uchuguzi unaendelea. Habari zaidi soma Mwananchi kesho.

Hata hivyo taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Marshed Ahmed Marshed (mtoto wa mmoja wa wazee waliokamatwa) zinasema kuwa wapemba hao hawajaachiwa mpaka sasa bali ni janja ya serikali iliyofanya na Usalama wa Taifa kujaribu kuficha ukweli.

Thursday, May 15, 2008

Mambo ya Israeli


Mdau Sanga amedrop majuzi tu toka huko Israeli ana michapo kibao ametueleza na bila shaka msomaji utapata mambo mengi hivi kesho kuna habari moto mota za kutoka huko kumbe Waisraeli mambo yao shega sana. Picha hizi kazipiga mwenyewe.

Mvua bongo ni balaa


Bongo bwana ni balaa tupu iwe kiangazi iwe mvua, sasa hebu cheki hapa hii mvua iliyonyesha kidogo tu juzi kila kona watu wanahangaika. Majumbani hakukaliki, barabara hazipitiki ili mradi kila kona balaa, kuna msemo hapa Dar kuwa watu wanaogopa mvua zaidi kuliko magari. Picha hizi za mdau zinaonyesha hilo.

Wednesday, May 14, 2008

Simba wamsimamisha Kaduguda


Katibu Mkuu wa klabu ya soka ya Simba, Mwina Kaduguda amesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa utovu wa nidhamu na kamati ya utendaji ya klabu hiyo iliyokutana juzi.

Habari za kuaminika toka ndani ya klabu hiyo na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo zinasema kuwa, Kaduguda amesimamishwa na kikao hicho cha dharura kufuatia kitendo chake cha kumkashfu mfadhili wao mkuu.

Wajumbe wa kamati ya utendaji chini ya Mwenyekiti wake, Hassani Dalali wamedaiwa kufikia uamuzi kwa kinachodaiwa kushindwa kuendelea kuvumilia tabia za katibu mkuu wao huyo kwa muda mrefu.

Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa, kwa muda mrefu katibu huyo amekuwa `akiharibu` lakini wenzake walikuwa wakimvumilia na kwa kitendo cha juzi cha `kumghasi` na kumkera mfadhili huyo wenzake wameamua kumgeuka.

``Yapo mambo mengi ukiambiwa yanafanywa na kiongozi huyu msomi huwezi kuamini, lakini wenzake wamekerwa na kuamua kumtia adabu, hadi hapo atakapoitwa kwenye mkutano mkuu ili kujitetea kwa adhabu aliyopewa,`` chanzo hicho kilisema.

Nipashe lilimtafuta mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, ambaye alikiri kuwepo kwa maamuzi hayo, lakini akisema yalikuwa bado ayajabarikiwa mpaka kwanza kikao hicho kilichokuwa kikiendelea kimalizike. Picha ya Mrocky Mrocky

Tuesday, May 13, 2008

Wapinzani wambeza PindaVIONGOZI wa vyama vya upinzani wamepinga kauli zilizotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu dhamira ya serikali kukabiliana na ufisadi wakisema kuwa kauli hizo ni hewa na hazina uzito wa kuuma mafisadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema amesema serikali inafanya kiini macho katika kushughulikia suala la ufisadi na kwamba kauli aliyoitoa Waziri Pinda wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari juzi inaonyesha ni jinsi gaini imeshindwa kukabiliana na tatizo hilo na haipo makini.
Akizungumza na Mwananchi jana katika mahojiano maalumu, Mwenyekiti huyo wa TLP alisema kuwa Waziri Pinda si mkweli kwa sababu tangu amechaguliwa hajafanya chochote kukabiliana na ufisadi nchini licha ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mchakato mzima wa kutoa kwa zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond ya Marekani kutoa mapendekezo yake.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwakemea viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, akiwamo Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, kuacha kuwatumia wananchi majimboni mwao kuwatukuza kama mashujaa.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana.
Cheyo ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alisema kitendo hicho licha ya kuwa ni kinyume na utamaduni wa Kiafrika, ni cha aibu kufanywa na mtu aliyetuhumiwa kwa ufisadi. Habari na Tausi Mbowe na Muhibu Said.

Rais Karume atunukiwa shahada


Pichani Rais wa Zanzibar Aman Abeid Karume akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa cha South Carolina, Marekani, alitunukiwa shahada hiyo wakati wa mahafali ya kuwatunuku wahitimu mbalimbali chuoni hapo Ijumaa. Picha hii kwa niaba ya Ikulu ya Zanzibar.

Monday, May 12, 2008

Kikwete amaliza mgogoro DRC, UgandaRAIS Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa AU amewapatanisha Rais wa Uganda Yoweri Mseveni na Joseph Kabila wa DRC Congo katika mgogoro wa kugombania mpaka kati ya DRC na Uganda uliodumu kwa muda sasa.

Wakizungumza katika tamko la pamoja lililotiwa saini na mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Mbusa Nyamwisi na mwenzake wa Uganda Isaack Musumba viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda sasa.

Mgogoro huo ulianza Desemba 5 mwaka jana na waliitisha mkutano mwingine Desemba 12 hadi 15 mwaka huo huo Jijini Kampala wakisimamiwa na Rais Kikwete.

Marais Museveni na Kabila wamekubaliana kutoa ushirikiano muhimu kwa kamati ya pamoja inayoshughulikia mgogoro huo ili iweze kumaliza mgogoro huo.

Kuhusu visiwa vya Rukwanzi, wakuu hao wamekubaliana kimsingi kwa pamoja kuharakisha utawala wa pamoja wakati mchakato wa kuweka mipaka mipya ikiendelea.

Kwa upande wa usalama, wakuu hao wa nchi wamemtaka Kiongozi wa chama cha waasi cha LRA, Joseph Kony atie saini makubaliano ya mwisho ili kuharakisha mchakato wa amani wa Juba.

Sunday, May 11, 2008

bwana harusi Reginald SimonReginald Saimon mwanablogu mwenzangu huyu, ameamua kuondoka ghafla katika klabu ya mabachelor na mkewe Winifrida Kokwenda wakimeremeta jana baada ya kufunga ndoa kanisa la Mtakatifu Yosefu na baadaye kwenye bonge la pati Land Mark Hotel, Ubungo, dar

Friday, May 09, 2008

Ze Comedy nje ya EATVKUNDI la sanaa za vichekesho nchini maarufu 'Ze Comedy' limemaliza mkataba wake wa miezi minane na Kampuni ya IPP na kwa sasa wasanii wake wana mapumziko kwa ajili ya kujipanga upya.

Kundi hilo lililojizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo wao wa 'The Comedy Show' limemaliza mkataba wake kupitia Televisheni ya East Africa na kwa sasa wanajipanga upya kwa ajili ya kutoa burudani zaidi kwa wapenzi wao.

Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo, Isaya Mwakilasa au 'Wakuvanga' alisema kwa muda usiopungua miezi minane walikuwa wakifanya kazi na IPP na kutokana na mkataba wao kumalizika kwa sasa wako katika mapumziko kwa ajili ya kujipanga upya.

"Tumefika kipindi sasa tunataka kufanya vitu tofauti na vya kipekee ili kuleta msisimko zaidi kwa mashabiki wetu na sasa tunataka kuja kivingine na kipekee ikiwa ni moja ya kuinua sanaa yetu hapa nchini," alisema Mwakilasa.

Naya kiongozi wa kundi hilo, Sekioni Gideon au Seki alisema yeye yupo pamoja na kundi hilo na kwa sasa watakua pamoja mapumzikoni kwa ajili ya kuja kitofauti zaidi na kuendeleza sanaa ya Tanzania ndani na nje.

Alisema mara baada ya kupumzika wao kama kundi wataamua kuweka mkataba na kituo chochote cha televisheni endapo watafikia muafaka ua kurudi katika kituo chao cha awali.