Friday, February 27, 2015

SERIKALI KUFUFUA BANDARI 14 ZA ZIWA NYASA – WAZIRI MKUU


*Apewa jina la Chifu wa Wanyakyusa, aitwa Mwakabulufu 
WAZIRI MKUU Mizengo amesema Serikali imeamua kufufua bandari ndogo 14
kwenye mikoa mitatu inayozunguka Ziwa Nyasa ili kuimarisha usafiri wa
majini kwa wakazi wa Ruvuma, Njombe na Mbeya.
 
“Tangu mwaka 2006 bandari za kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya
zilikufa na hivyo kuleta shida ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo
lakini Serikali imeamua kuzifufua bandari hizo na Itungi itakuwa ndiyo
kituo kikuu cha bandari zote katika Ziwa Nyasa,” alisema Waziri Mkuu.
 
Alikuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kyela kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika jana jioni (Jumatano, Februari 26, 2015) kwenye
uwanja wa michezo wa Mwakangale na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa
wilaya hiyo.
 
Alizitaja bandari hizo kuwa ni Ndumbi, Lundu, Njambe, Mkili, Liuli, na
Mbamba bay ambazo ziko mkoani Ruvuma. Nyingine ni Lumbila, Ifungu,
Nsisi, Lupingu na Manda ambazo ziko Njombe wakati bandari za Mbeya ni
Itungi, Kiwira na Matema.
 
Alisema ili kufanikisha hilo, Serikali imehamisha chelezo (Dry Dock)
kutoka bandari ya Mwanza na kwamba mkandarasi kutoka Kampuni ya
Songoro Marines, ameshaanza  ujenzi wa chelezo hiyo.
 
“Baada ya kukamilika, Chelezo hiyo, itatumika kutengenezea meli mpya
yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo na kufanya
ukarabati wa meli pindi zinapohitaji matengenezo. Nimeambiwa na
mkandarasi kutaka watamaliza hii kazi ifikapo Juni, mwaka huu,”
alisema huku akishangiliwa na umati huo.

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

mam10 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.mam9
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015
.mam4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki.mam11 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA WILAYANI KYELA

ky1Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kyela baada ya kufungua ukumbi wa  Halmashauri hiyo wakiwa katika ziara ya wilaya  hiyo Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky14Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, MizengoPinda wakati aliozungumza baada ya kufungua mashine ya kukoboa nakuchambua mpunga mjini Kyela Februari 26, 2015. (PIcha na Ofisi  yaWaziri Mkuu)
ky11Daraja la Mwaya  wilaya ni Kyela ambalozo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, mizengo Pinda.
ky7Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakitazama  eneo itakapojengwa chelezo na bandari ya  Itungi  wilayani Kyela wakiwa katika ziara ya wilaya hiyo, Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)ky6Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na watalaamu wa kampuni ya kichina ya CHICCO kabla ya kufungua daraja  la Mwaya lililojengwa na kampuni  hiyo wilayani Kyela Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky4Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Mama Mlemavu, Lesia Kambungwe baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Kyela akiwa katika ziata ya wilaya hiyo Februari 26, 2015<(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky3Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari  26, 2015. Wapili kulia ni mkewe Tunu na wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kyela anayeoondoka, Margareth Malanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky5Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa chelezo ya kuundia meli kwenye bandari ya Itungi,  Kyela akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo  Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky8Mwendesha baiskeli akipita katika daraja la zamani la Mwaya wilayani Kyela huku wakitazama daraja jipya  (kulia) lilozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)ky12Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Zamani wa Mbeya Mzee  John Mwakipesile baada ya kuwasili kwenye  makazi ya  Mkuu wa Wilaya ya Kyela kwa ziara ya siku moja wilayani humo Februari 26, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)ky15Wanafunzi wakimpungia mkono Waziri Mkuu Mizengo Pinda hayupo pichaniky16Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  Katibu wa CAHDEMA wa kata ya Mwaya, Ageni Pamesa  kabla ya kufungau maabra ya  shule ya sekondari ya  Mwaya akiwa katika ziara ya Mkoa wa  Mbeya Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)ky17Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (wapili kulia) akitazama mafunzo kwa vitendo wakati alipokagua maabara ya Kemia katika shule ya seondari ya Mwaya wilayani Kyela Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE AHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU LEO

kj1Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima
zao za mwisho kwa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa
Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Msaki jijini Dar es
salaam leo.
kj2Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji
Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea Msaki jijini Dar es
salaam leo walipofika heshima zao za mwisho kwa mama yake mzazi
Marehemu Esther Gigwa Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo.
kj3Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na Makamu
wa Rais Dkt Mohamed Ghariv Bilali, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni
Sefue wakiwa pamoja na wafiwa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther
Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward
Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo.
kj4Sehemu ya wafiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Marehemu

Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt
Edward Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo.
PICHA NA IKULU

AJALI YA NDEGE YA JWTZ MKOANI MWANZA

jw1Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.
Hata hivyo, rubani wa ndgevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .
Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu.
 Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
jw2jw3jw4jw5jw6jw7jw8

JAJI KIONGOZI ATOA SOMO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA, VYAMA VYA WAAJIRI NA WAAJIRIWA.

JA1
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akifungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini.
JA2
Baadhi ya washiriki wa mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) wakifuatilia masuala mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
JA3
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano maalum wa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Chama cha waajiri Tanzania (ATE) na Wafanyakazi (TUCTA) leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaaban Lila ametoa wito kwa watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini  kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, viwango na uadilifu ili mahakama hiyo iendelee kuwa kimbilio la wananchi wanaotafuta haki.
Akizungmza wakati wa wakati wa kikao cha wadau wa Mahakama kujadili uboreshaji wa utendaji kazi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kilichowahusisha watendaji wa Mahakama ya Kazi , Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) leo jijini Dar es slaam, Mhe.Shaaban Lila amesema kuwa  msingi mkuu wa Mahakama ya Tanzania nikuhakikisha kuwa inatoa maamuzi kwa wananchi kwa haki na wakati.
Amesema  iwapo waajiri na waajiriwa kote nchini haki watazingatia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao kulingana na kanuni na taratibu zinazosimamia maeneo ya kazi migogoro  mingi inayopelekwa mahakamani baina ya waajiri na waajiriwa itapungua nchini.
 “Kila upande ifanye kazi yake kwa haki ,kumekuwa na mrundikano wa mashauri  ya kazi yanayokwenda mahakamani kwa ajiri ya utatuzi na usuluhishi ,mengi ya mashauri hayo hayahusiani na kufukuzwa kazi isipokuwa yale ya kukosa uaminifu, wizi na ubadhirifu sehemu za kazi” Amesisitiza.
Amebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania lazima iheshimiwe kutokana na misingi yake kwa kuweka msisitizo katika kushughulikia masuala ya msingi na kutatua kero za wananchi hususan usimamizi na utoaji wa haki kwa wakati.
Mhe. Shaaban amefafanua kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya maboresho na mabadiliko katika kushughulikia mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani huku akieleza kuwa mkakati wa sasa ni kupunguza umri wa mashauri ya muda mrefu ya miaka 5 hadi 10 yanayofikia 265  na yale ya umri wa miaka 3 yapatayo 201 yaweze kushughulikiwa ndani ya mwaka 1 hadi 2 ifikapo June 2015.
“Lengo letu ni kushughulikia mashauri haya haraka kwa muda mfupi, muhakikishe mashauri haya mnayamaliza kwa sababu yanagusa uzalishaji na maisha ya watu, kuchelewa  kuyasikiliza  kunaathiri  uchumi ” Amesisitiza.
Aidha,amewataka wadau wanaoshiriki mkutano huo kujipima katika malengo wanayojiwekea pamoja na kusimamia utekelezaji wa hukumu na maamuzi yanayotolewa na mahakama na kueleza kuwa ofisi yake inaandaa mkakati wa usimamizi wa suala hilo.
 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mulimuka akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwaweka pamoja wadau  hao kwa maana ya Mahakama, Waajiri (Serikali) na waajiriwa unalenga kuangalia na kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazohusu maslahi ya wafanyakazi na mashauri yanayopelekwa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi nchini.
Amesema asilimia 70 ya mashauri yanayokwenda  mahakama Kuu Divisheni ya Kazi yanahusu migogoro ya waajiri  kuwasimamisha kazi wafanyakazi wao kutokana na makosa mbalimbali na kuongeza  kuwa mengi ya makosa hayo hayasababishi mtu afukuzwe kazi.
Ametoa wito kwa pande zote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kufuata haki ili mashauri yote yanayopelekwa mahakamani yaweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuondoa migogoro ya kazi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.

BLOGGERS KUKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO KATIKA PATI YA KIHISTORIA

 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
 Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

KIPINDI CHA “JICHO LETU MKURANGA” CHA REDIO UPENDO CHASAIDIA JAMII YA WENYE MAHITAJI MUHIMU MKURANGA

DSC_2663Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKTDayosisi ya Mashariki na Pwani akikabidhi madawati kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaam pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo sare za shule, madaftari na viatu kutokana na msaada mkubwa wa kipindi cha “Jicho letu Mkuranga” kinachorushwa kila siku na kituo cha Redio cha Upendo Media cha jijini Dar es salaam kwa kuibua changamoto hizo na kuhamasisha taasisi na wananchi mbalimbali wenye uwezo kusaidia jamii masikini na zenye mahitaji muhimu, katika picha wa pili kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA Flow na katikati ni Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLCDSC_2664Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la KKKT akikabidhi sare za shule  kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye zililzotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaamDSC_2667Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLC akitoa shukurani zake kwa wageni mbalimbali mara baada ya kukabidhi madawati na vifaa mbalimbali vya shule kwa mkuu wa wilaya ya Mkuranga.DSC_2642Nang’ida Johanes Lairumbe Mkurugenzi wa Upendo Media akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali waliofika katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika jengo la Luther House jijini Dar es salaam, Kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA FlowTraidinga, Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani na Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo .DSC_2652Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKTDayosisi ya Mashariki na Pwani akitoa shukurani zake kwa Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding kwa msaada wa madawati na vifaa mbalimbali vya shule walivyovitoa kwa wilaya ya Mkuranga.DSC_2658Picha ya pamoja viongozi hao wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyokabidhiwa kwa wilaya ya Mkuranga.