Saturday, December 19, 2015

KIGOMA UJIJI YAPATA MEYA TOKA ACT WAZALENDO

Madiwani wa Manispaa ya Kigoma ujiji wakiwa katika picha ya pamoja .
Mwenyekiti wa uchaguzi wa Meya na Naibu meya mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoa maelezo ya awali kabla ya uchaguzi.
 Meya wa Manispaa ya kigoma Ujiji Hussein Ruhavi akimweleza jambo makamu meya  Athuman Mussa wa manispaa hiyo kushoto ni mbunge wa Kigoma mjini ndiye alikuwa mwenyeti wa uchaguzi
 Mmoja wa Madiwani akipiga kura ya kumchagua meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Kigoma Ujiji  limemchagua Diwani wa kata ya Bangwe Hussein Ruhavi kuwa meya wa Manispaa hiyo.

Mbunge Zitto Zuberi Kabwe alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo alimtangaza diwani Ruhavi kutoka chama cha ACT wazalendo kuwa mshindi wa kiti cha umeya kwa kupata kura 19 kati ya kura 21 zilizopigwa na akamshinda mpinzani wake Masudi Kassim kutoka chama cha mapinduzi(CCM).

Pia Zitto alimtangaza diwani wa kata ya Buzebazeba Athumani Mussa kupitia chama cha ACT wazalendo kuwa naibu meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji alimshinda Mussa Maulid wa CCM aliyepata kura moja.

Baada ya kutangaza matokeo Zitto ambaye ni mbunge wa jimbo la kigoma mjini alisema kuwa watasimamia mipango ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa usawa.

"Diwani yeyote ambaye kwa makusudi ataamua kukwamisha michakato mbalimbalu ya maendeleo tutamshughulikia lwa namna tutakayojua sisi"alisema Zitto

Naye meya Hussein Ruhavi akizungumza baada ya kuchaguliwa aliwashukuru madiwani kwa imani yao waliyoionyesha kwake kwa kumchagua kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Alisema atafanya kazi kwa kushirikuana na madiwani wote ili kuwaletea wananchi maendeleo,pia aliwataka madiwani kufanya kazi pamoja bila ya kujali itikadi zao

No comments: