Thursday, January 31, 2013

Kocha Kim Paulsen ateua wachezaji 21 kuivaa Cameroon

Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Katika kikosi hiki, Poulsen hajamuita Jerry Tegete ambaye siku za karibuni amefufua makali yake wakati ameita washambuliaji halisi wawili tu, Ulimwengu na Samatta. 

DR. ASHA ROSE MIGIRO ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini , Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.


Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013

IGP SAID MWEMA APATA AJALI MOROGORO


Mkuu wa jeshi la polisi Igp Said Mwema amenusurika kifo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Dodoma, kupata ajali eneo la Mkundi ndani ya Manispaa ya Morogoro jana majira ya saa 12 jioni, hata hivyo katika tukio hilo hakuna aliyeumia na walibadilisha gari na kuendelea na safari, kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia blog hii www.jumamtanda.blogspot.com

Wednesday, January 30, 2013

RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU MOJA

 Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana wa leo Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA:UWEZEKANO WA MATUKIO YA MVUA KUBWA NCHINI KUTOKANA NA KUWEPO KWA KIMBUNGA ''FELLENG''
Tafadhali pokea taarifa hii kuhusu uwezekano wa matukio ya Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) katika baadhi ya maeneo ya mikoa  ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara  na maeneo jirani ya mikoa hiyo kati ya tarehe 30 Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013.
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa.

Ahsante

Public Weather Service,
 Tanzania Meteorological Agency.
Ubungo Plaza,
Morogoro Road, P.O.Box 3056,
 Dar es Salaam:
Tel: +255 22 2460706-8;Fax: +255 22 2460735
 :Website: www.meteo.go.tz 

VODACOM NA FASTJET WAINGIA KATIKA UBIA WA USHIRIKIANO, WASAFIRI WA FASTJET SASA KUANZA KUNUNUA TIKETI KWA M-PESA

fastjet and the fastjet crew
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa, (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubia wa ushirikiano baina ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom na Shirika la Ndege la FastJet uliofanyika Dar es Salaam, utakaowawezesha wasafiri wa shirika hilo kuanzia sasa kulipia tiketi za safari zao kwa njia ya M-Pesa. (Kulia ni Meneja wa Biashara wa FastJet, Jean Uku).
 

Elizabeth Michael ‘Lulu’ Akiondoka Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam Muda mfupi Baada ya kukamilisha Taratibu za Dhamana


  Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililomleta Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana
 Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
 Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza
 Lulu akiingia mahakamani.
 Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
 Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
 Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.
 Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
 Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.Picha Zote na Mdau Dande Francis

Tuesday, January 29, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana na Sekretarieti Nzima ya CCM Watembelea ujenzi wa daraja la Malagarasi

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana akihutubia ngaruka
 Dk Asha-Rose akihutubia Nguruka
Nape Nnauye akihutubia Ngaruka
Kinamama katika mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wakipokea kwa shangwe msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
 Juma Kilabuka na Hasani Kankwi wa mjini mdogo wa Nguruka wakifurahia msafara wa Kinana ulipofika katika mji huo
Kinana akisalimia wananchi katika mji mdogo wa Nguruka , Uvinza mkoani Kigoma baada ya msafara wake kuwasili  katika mji huo kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka,  Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili Nguruka mkoani Kigoma, Januari 28, 2013.
Kinana akiaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka, wilayni Uvinza mkoani Kigoma. Kushoto kwake ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
Dk. Asha Migiro akiwa katika matembezi kuingia mjini mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM. Kushoto ni Asha Baraka.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kwenda kwenye mkuytano wa hadhara wa CCM, Nguruka, Januari 28, 2013. Pembeni yake ni Asha Baraka
Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akimtembeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na ujumbe wake kushuhudia hali ya ujenzi wa daraja hilo ilivyo, Januari 28, 2013, wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa You mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika  Aprili mwaka huu. Wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kushoto) . Kinana na ujumbe wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Januari 3, 2013.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Khalidi wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kushoto ni  Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Yong.Picha Zote na Bashir Nkromo-Idara ya itikadi na Uenezi-CCM
----
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema kuwa wananchi wa Mtwara wanayo hoja hivyo Serikali inatakiwa kuwasikiliza na kutoa majibu sahihi.

Pamoja na hayo chama hicho kimesema kuwa kinachoonekana hivi sasa nyuma ya sakata hilo kuna watu wanafanya uhaini, uhalifu na kila aina ya hujumu jambo ambalo wanaitaka Serikali kuchukua hatua kali za kuhakikisha wote wanojihusisha na uhalifu huo wanachukuliwa hatua.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ikiwa ni msimamo wa chama chao katika sakata hilo.

Mjadala wa gesi ya Mtwara kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam umekuwa gumzo kubwa huku wananchi wakiitaka Serikali kuwaeleza watanufaika vipi na gesi hiyo kabla ya kunufaisha maeneo mengine.

Kinana alisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuhakikisha inatumia nafasi yake kuzungumza na wananchi wa Mtwara katika kupata suluhu ya suala hilo kwani wana hoja za msingi ambazo zinataka majibu.

“Msimamo wetu kama chama, tunataka Serikali kukaa na wananchi hao na kuwasikiliza.Tunahitaji kuona Serikali inatoa majibu ambayo yatakuwa sahihi na kumaliza tofauti iliyopo sasa,”alisema Kinana.

Pamoja na hayo alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona hali ya uvunjifu wa amani inayofanywa na baadhi ya watu ambao wameamua kuingia mtaani na kuiba, kupora mali na kuharibu nyumba za watu kwa kuzichoma moto.

Alisema kuwa CCM inaona ni wakati mzuri kwa Serikali kuwadhibiti wote ambao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu huo ambao haukubaliki huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kusikilizwa.

Alisema mtazamo wa chama chao ni kwamba kuna jambo ndani ya suala hilo maana gesi inatakiwa kujadiliwa kwa njia ya amani kupata suluhu kuliko mali za watu kuharibiwa na kufanywa kwa uhalifu ambao hauvumiliki.

Rais Jakaya Kikwete Arejea Nchini Kutoka Addis Ababa


Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik Muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana usiku akitokea nchini Ethiopia ambapo alihudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za umoja wa Afrika(AU) uliofanyika jijini Addis Ababa.Picha na Freddy Maro-IKULU

Chadema kwenye Kikao Cha Dharura Cha Baraza Kuu la Chadema Jijini Dar es Salaam

  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanchama wa chama hicho aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Clemence Tara baada ya kujiunga na chama hicho.
 Katibu Mkuu Dk. Willbroad Slaa akizungumza katika mkutano huo.
 bungo John Mnyika akitete jambo na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa (kulia) wakati wa Kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
  Katibu Mkuu Dk. Willbroad Slaa akisalimiana na baadhi ya wajumbe katika mkutano huo.
 Mbunge Kigoma, Zitto Kabwe akiwasikiliza kwa makini wajumbe wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Chadema kutoka mkoa wa Mtwara.
 Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei akiingia katika ukumbi wa mkutano huku akifuatana na Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe.
 Picha juu na Chini sehemu ya wajumbe wakiitikia  Peoples Power
Sehemu ya Wabunge wa Chadema
  Wajumbe wa mkutano.
 Baadahi ya wabunge wa Chadema wakiwa katika kikao hicho.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika(katikati) akiwa amepozi na baadhi ya wajumbe.Picha zote na Mdau Dande Francis