Friday, August 29, 2014

WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI LEO.

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni Ajali mbaya 
 
Mashuhuda 
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 
……………………………………………………………..
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
 
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
NA MBEYA YETU BLOG

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO 29 AGOSTI, 2014 MJINI DODOMA

(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
PIX 2.Mwakilishi wa Watanzania waishio Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Kadari Singo (kushoto) akifurahia jambo akiwa pamoja na waandishi wa Habari leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma
PIX 3.Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kulia ni Mhe. Stella Manyanya akiwa amefuatana na Mhe. Reuben Matango wakielekea ndani ya Bunge Singo leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma
PIX 4.Mwakilishi wa Watanzania waishio Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Kadari Singo (kushoto) akibadilishana mawazo na Mjumbe mwenzie, Mhe. Yusuph Singo leo 29 Agosti, 2014 Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.

KAMPUNI YA MATANGAZO YANAYOTEMBEA (TRIA) YAZINDULIWA RASMI TANZANIA

1qDIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA akisoma risala yake wakati wa uzinduzi wa matangazo hayo.
2qTRUSHAR KHETIA Mkurugenzi mtendaji wa TRIA akikata utepe wakati akizindua rasmi matangazo hayo nchini Tanzania wa pili kulia ni ZULFIKAR MOHAMED Meneja Mkuu wa kampuni ya TRANSPAPER EXPRESS na mwisho kulia ni DIANA LAVENDER Meneja Mauzo na Masoko kampuni ya CONICA MINOLTA na kushoto ni  AZDA  AMANI Meneja wa Huduma Shirika la ndege la PRECISION AIRLINE ambao ni wateja wakampuni ya TRIA
………………………………………………………………………
Kampuni ya matangazo kwa kutumia vifaa tembezi yaani matangazo yanayotembea  imezinduliwa rasmi jijini Dar esSalaam.
Akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageniwengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi ulifanyika katika hanga la shirika la ndege la Precision yenye makao makuu yake eneo la uwanja wa ndege jijini Dar esSalaam, mkurugenzi mtendaji na muasisi wa TRIA bw. Trushar Khetia amesema kuwa TRIA ni kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na matangazo yawekwayo juu, nje au ndani ya fifaa safirishi kama mabasi ya kusafiria ndani na nje ya miji, ndege na usafiri wa majini maarufu kama boti au meli.
“Tumezoea kuona ama kusikia matangazo malimbali ya kibiashara nay ale ya kijamii yaani matangazo yasiyo ya kibiashara yakifanyika kupitia kwenye TV REDIO magazeti na majarida hapa nchini lakini leo TRIA inawathibishia wafanya biashara wa Tanzania na wengine kuwa matangazo yanaweza kufanyika popote wakati wowote tena kwa gharama ndogo” alisema bwana Trushar na kuongeza kuwa TRIA ina lenga kuwainua watanzania hasa vijana wadogo na kuwafanya watambue fursa zao katika maisha sambamba na kuwaongezea matumaini makubwa wamiliki wa mabasi, ndege, daladala namakapuni ya usafirishaji katika kunufaika kutokana na biashara zao za usafirishaji.
Aidha bwana Trushar amesema kuwa kampuni yake pamoja na kwamba haitegemi kufanya biashara kwa hasara hailengi pia kutengeneza faida tu bali kuleta ufanisi na changamoto endelevu katika sekta ya masoko na matangazo ambapo vijana wadau na wateja wa huduma hiyo wataweza kupiga hatua za kimaendeleo kibiashara sambamba na kuongezeka kwa soko la ajira hususana kwa vijana wa kitanzania “TRIA Tanzania hailengi kutengeneza faida tu bali pia kuleta maendeleo yenye tija kibiashara kwa wale watakaokuwa wateja wetu na wadau kwa ujmla, lakini pia ajira kwa vijana wenye uwezo tofauti tofauti wa kufanya kazi pamoja na wale wenye utaalamu wa kuandaa na kutengeneza matangazo haya” alisema Khetia.
Kwa upande wake mwakili wa Conica katika hafla hiyo Bi Diana Lavender amesema Conoca imekuwa mteja mkubwa wa TRIA nchini Kenya na kwakutambua ubora wa kazi zinafanywa naTRIA Conica imeamua kuunga na TRIA kwakuendelea kufanya matangazo yake hapa chini “tumekuwa wateja wa hii kampuni mda mrefu sasa huko nchini Kenya na kutoka na mafanikio makubwa tumeweza kupata kupitia matangazo yetu yanayofanywa na TRIA tumeonelea kuwa ni vizuri kuja kufanya hayo matangazo hapa Tanzania hasa pale tuliposikia kwamba TRIA inaanzisha tawi hapa nchini” alisema Lavender na kuongeza kuwa kufanya matangazo kupitia mabasi, ndege, daladala, treni, vyombo vya usafiri wa majini ni sehemu ya mapambo ya mji na njia zake kwani matangazo haya hutengenezwa vizuri na kufanya kuvuta macho ya wengi kila ipitapo “ni ma mabasi yetu huko Kenya maarufu kama matatu ukipita ukiona vile inavutia lazima utafurahia na kwamba lazima unaweza kutaka kupanda hiyo basi” aliongeza.
Naye mwakilishi kutoka shirika la ndege la precision hapa nchini ambao ni moja kati ya wadau wa karibu kabisa na TRIA Bi Azda Amani amesema kuwa uwekezaji wa biashara mbalimbali hasa biashara ngeni kama hayo ni sehemu ya kuongeza na kukuza pato la taifa na kupitia kodi kwa kampuni husika lakini pia kwa wamiliki wa mabasi, ndege na vinginevyo pamoja na wale wamiliki wa matangazo yatakawekwa kwenye magari haya watalipia kodi “ni furaha kuona wawekezaji wakubwa na wadogo wakiingia kila siku hapa nchini kuwekeza kibiashara na kwakufanya hivi nchi yetu ina kuwa pia kiuchumi kupitia kodi kutoka kwa watoa huduma na wahudumiwa wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara nchini” alisema Amani
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Zulfikar Mohamed kutoka Transpaper ameisifia TRIA kwa hatua iliyofikia na kuwataka watanzania kuiga mfano huo muhimu na kwenda kuwekeza pia katika nchi jirani hata kimataifa “ mimi nipewa fursa ya kuzindua tawi la TRIA hapa Tanzania na kwakweli nimefurahia fursa hii.
Naomba kuwapongeza sana wahusika wote waliokaa na kuona kwamba mimi naweza kuwa mgeni rasmi wa kuzindua mradi huu muhimu lakini pia nawasifia watanzania kwa kuwa waungwana wakubwa sana kuwapokea wawekezaji kutoka pande zote za dunia bila kujali rangi kabila wa udini, kwa hili mko vizuri sana na nawapongeza sana niwaombe tu kwamba igeni huu mfano mzuri na nyinyi mkawekeze biashara zenu katika nchi nyingine kwa manufaa ya watoto wenu na watanzania wote” alisema Mohamed nakuongeza kuwa maendele ya kiuchumi katka taifa lolote huletwa na wenye nchi kupitia biashara yenye tija na inayovuka mipaka na kuleta fedha za kigeni.

JOPO LA MAJAJI LA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAENDELEA NA ZOEZI LAKE JIJINI TANGA NA WILAYA YA MKINGA

Picha Na 1
Majaji  Bw.  Venance Bahati (kushoto) na Bi.  Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kufanya tathmini ya  mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la  Mwarongo jijini Tanga. Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Picha Na 2Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw.  Mzihili Abeid (kushoto) akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo  imejengwa na  kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Picha Na 3Msimamizi wa kampuni ya  utafutaji  wa mafuta na gesi  ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia) akizungumza  na jopo la majaji na sektretarieti  kwenye maabara ya shule ya sekondari ya  Tongoni  iliyofadhiliwa na kampuni  hiyo.
Picha Na 4Jaji  Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji  wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed  Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia Gabusa.
Picha Na 5Msimamizi wa kampuni ya  utafutaji  wa mafuta na gesi  ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kushoto) akizungumza na majaji  walipotembelea maabara ya Shule ya Sekondari ya Mabokweni  jijini Tanga ambapo kwa sasa kampuni hiyo imejitolea kuwajengea maabara  ya kisasa.
Picha Na 6Mkurugenzi wa kampuni ya  Dawson Food Products Ltd iliyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga Bw. Burhani Taibali (kulia) akizungumza na majaji pamoja na sekretarieti iliyotembelea  kampuni hiyo.