Friday, January 30, 2015

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akifurahia jambo  na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Vullu katika viwanja vya bunge  walipohudhuria kikao cha pili cha mkutano wa 18 wa Bunge mjini Dodoma jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akielezwa jambo na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika  viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.

MKUTANO WA WADAU WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI WAFANYIKA JIJINI DAR


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto ) na Meneja Mradi wa Benki ya Dunia (WB) katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Oliver Braedt (kulia) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akifungua warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Dk. Lutengano Mwakahesya akifungua warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Meneja Mradi wa Benki ya Dunia (WB) katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Oliver Braedt akichangia jambo katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Wadau mbalimbali wa warsha hiyo wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (hayupo pichani) katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Baadhi ya wadau kutoka kampuni zinazojihusisha na usambazaji wa umeme vijijini wakifuatilia mada kwa makini zilizokuwa zinawasilishwa na watoa mada (hawapo pichani) kwa nyakati tofauti katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana
Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa mstari wa mbele) wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wadau mbalimbali (hawapo pichani) katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.

MKUTANO WA BARAZA LA PILI LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI WAFUNGULIWA RASMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, (katikati) akiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wakiimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi muda mchache kabla ya kulifungua baraza hilo jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa baraza hilo uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA SARAH REUBEN - OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI).

Na: Evelyn Thomas - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi - Mtwara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (Mb) amefungua mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana mkoani Mtwara.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuchika ameipongeza ofisi hiyo kwa kufanya ukaguzi wenye viwango vya juu na hatimaye kupungua kwa hati chafu au zenye mashaka katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

"Mimi binafsi najivunia sana  kutokana na jitihada na mafanikio ya kazi za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo yameijengea heshima nchi yetu na ulimwengu kwa ujumla, licha ya kupungua kwa hati chafu, hivi sasa Nchi yetu, ikiwakilishwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, inakagua shughuli za Umoja wa Mataifa jambo ambalo ni la kujivunia sana", amesema Waziri Mkuchika. 

Mkuchika ameongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni chombo nyeti sana, si hapa Tanzania tu bali katika nchi zote zinazozingatia demokrasia,uwajibikaji na uwazi,  katika mapato na matumizi  ya rasilimali za umma ili kuleta maendeleo ya watu wake.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad amesema mkutano huo una dhumuni la kutoa fursa kwa watumishi, kupitia  wawakilishi wao, kujadiliana juu ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi mahali pa kazi.

" Dhana ya kuwa na Mabaraza ya Wafanyakazi  katika sehemu za kazi, hasa katika utumishi wa umma  ina lengo la kutoa fursa kwa watumishi, kupitia  wawakilishi wao, kujadiliana juu ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi kwa upande mmoja na upande mwingine maslahi yao kama watumishi", amesema Prof. Assad.

Prof. Assad amefafanua kuwa mkutano huu wa Baraza la Wafanyakazi utatumika kujadili malengo na mipango ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ikiwa ni pamoja na Maslahi ya Watumishi kwa ujumla.

Mkutano wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi utamalizika leo jioni ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Weledi na nidhamu katika kutekeleza majukumu ya Utumishi wa Umma ni chachu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.”

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SimBanking NA FAHARI HUDUMA WAKALA


Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa benki hiyo.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wadau wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Maofisa wa Benki ya CRDB.
Wageni waalikwa pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
Maofisi wa Benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja.
Maofisa wa benki ya CRDB.
Ofisa Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Tawi la CRDB, Kijitonyama, Lucas Busigazi (katikati) kuhusu huduma za benki ya CRDB (kulia) Kulia ni Meneja wa Tawi la Msasani, Saida Francis.
Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza.
Dk. Charles Kimei akisalimiana na wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari (kushoto) akiwa na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakitoka katika Mobile Bank mara baada ya kuzindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na SimBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia) akiwa na MenejaMahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu wakiwa katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Kulia ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mtumaji wa miamala mingi katika benki hiyo atapata zawadi ya gari aina ya Passo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na wa tatu kushoto ni mjumbe wa bodi, Celina Mkoni. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo’ 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akijaribu gari aina ya Passo baada ya kuzindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’,  kupitia kwa mawakala wa ‘FahariHuduma’, ijulikanayo kama ‘Tuma pesa na simBanking shinda Passo.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’  kupitia kwa mawakala  wa ‘FahariHuduma’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

“Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.

Akielezea namna ya kushiriki  na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

“Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara,” alisema.

Kwa upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.

KINANA AZURU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM na ndugu wa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Dk.Omar Ali Juma wakiomba dua kwenye kaburi lake lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitia sahihi kitabu cha wageni kwenye kaburi la hayati Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Dk.Omar Ali Juma  lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba

Kaburi la aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Hayati Dk.Omari Ali Juma aliyefariki tarehe4 Julai 2001

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwa na Sheikh  Ali Abdala Ali pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai , Balozi Ali Karume(kushoto) wakizungumza baada ya kuzuru kabuli la aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Dk.Omar Ali Juma wakiomba dua kwenye kaburi lake lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba

MKURUGENZI MKUU WA NHC AENDELEA NA ZIARA YAKE MIKOANI


Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana cha Mshikamano Wilayani Muleba alipokitembelea kuona namna kinavtumia mashine zilizotolewa na NHC ili kuongeza ajira kwa vijana. Bw. Mchechu amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuunga mkono juhudi za NHC kwa kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia kazi zao.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Mtukula linapojengwa jingo la kisasa la biashara na NHC ili kuvutia na kuchochea ukuaji wa biashara katika eneo hilo la mpaka wa Tanzania na Uganda. Eneo hili ndipo zilipokuwa nyumba ndogondogo zilizojengwa na NHC na baadaye kuharibiwa na mabomu ya Nduli Iddi Amin alipovamia nchi yetu mwaka 1978. NHC iliiomba  Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kulirejeshea eneo hilo ili kujenga jengo hilo la kibiashara
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akimpa maelezo Mjumbe wa Bodi ya NHC Bi Subira Mchumo ya juhudi  zinazofanywa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya nchini za kuwapatia wananchi makazi bora. Ujumbe huo ulitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu Wilayani Muleba na kusisitiza matumizi ya malighafi zinazopatikana katika maeneo husika ili kupunguza gharama za nyumba hizo.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika Wilaya ya Muleba kwa ajili ya kuuzia wananchi. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji.
 Msanifu wa Majengo wa NHC Bw. Kintu akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ya jengo linalojengwa na NHC eneo la Mtukula ili kukuza biashara upande wa Tanzania.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC ulipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kujionea juhudi zinazofanywa na mwekezaji wa kiwanda hicho katika kutoa ajira kwa watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Kiongozi wa kikundi cha vijana kilichoko Wilaya ya Bukoba Mjini waliyofadhiliwa na NHC mashine za kutengezea matofali  ili kujipatia ajira