Friday, November 30, 2012

WATU WALIOMUIBIA SHARO MILIONEA KWENYE AJALI WAKAMATWA

 Gari ya Marehemu Sharo Milionea kama linavyooneka mara baada ya Ajali iliyopekea kupoteza uhai wake!

Jeshi la Polisi Mkoani Tanga na kushirikiana na wasamalia wema wamewatia mbaroni vijana wanne wanadaiwa kumpora vitu mbalimbali marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali mbaya mwanzoni mwa wiki hii.

Habari za kuaminika toka Mkoani humo zinasema kuwa vijana hao wamekamatwa baada ya kazi nzuri iliyofanbywa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kushirikiana na wasamalia wema ambapo hadi sasa vijana hao wako chini ya ulinzi mkali huku wengine wakiwa bado wanatafutwa.

Habari zaidi zilisema kuwa vijana hao wamekamatwa jana usiku na waliokamatwa wamefahamika kwa jina ya Issa Makunera,Farid Hassani,Rashidi Ayubu,Rashid Makunera na imeelezwa watuhumiwa hao wamekutwa na mali mbalimbali za marehemu.
Chanzo chetu toka mkoani humo zilisema watuhumiwa hao pamoja na mali  hizo zimekamatwa katika eneo linanaloitwa Songa Kibaoni na vitu hivyo ni SPEA TAILI,REDIO YA GARI,BETERI YA GARI,SAA YA MKONONI SURUALI AINA YA JINS PAMOJA TISHETI ,BEGI PAMOJA NA SIMU YA MKONONI.

Hata hivyo habari  ziliendelea kusema kuwa licha ya Begi hilo kupatikana ambalo lilidaiwa ndani yake kulikuwa na pesa nyinge hazikuweza kukutwa na inasemekana katika ya watuhumiwa wanaotafutwa ndio wamekimbia na fedha hizo.

Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao wananchi mbalimbali wamelipongeza  Jeshi la Polisi pamoja na wananchi waeneo waliyokamatwa watuhumiwa kwani wao ndio waliotoa msaada mkubwa hadi kukamatwa kwano.

CHANZO: http://xdeejayz.blogspot.com/2012/11/waliomuibia-marehemu-sharo-milionea.html

Thursday, November 29, 2012

Waziri Tibaijuka azindua rasmi majengo ya NHC Mchikichini

Majengo ya nyumba za makazi za NHC Mchikichini yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, yatakapokamilika yatakaliwa na familia 48, ambapo katika kila nyumba ina vyumba vitatu jiko na choo pamoja na parking ya kutosha.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba 48 za kuuza za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala Mchikichini, Dar es Salaam jana.Anayeongoza kupiga makofi kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akizindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za Makazi za  NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam kwa kuweka jiwe la msingi katika katika mojawapo ya majengo ya majengo hayo ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.
 
Msondo Ngoma walikuwapo kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Mchikichini
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akizungumza na MC maarufu nchini na Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba, Ephraim Kibonde (picha ya juu) pamoja na mtangazaji wa TBC (picha ya chini) baada ya uzinduzi  rasmi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi za  NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.

UZINDUZI WA TUSKER LITE NDANI YA USIKU WA MAAFISA MASOKO

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akinyanyua juu bia mpya ya Tusker Lite wakati wa uzinduzi wake rasmi uliofanyika mbele ya maafisa masoko wa makampuni mbalimbali nchini wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana  
Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru akizungmza mara baada ya uzinduzi wa bia mpya ya Tusker Lite wakati wa uzinduzi wake rasmi uliofanyika mbele ya maafisa masoko wa makampuni mbalimbali nchini wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon (wapili kulia) , akiwa pamoja na wafanyakazi wa SBL wakigonganisha chupa zao za Tusker Lite kuashiria furaha ya kuzinduliwa kwa  bia hiyo mpy. Tusker Lite ilizinduliwa wakati wa tafrija maalum ya ‘Markerts Night’ jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakiwa na mmoja wa washindi wa shindano maalum la uchezaji mziki lililofanyika katika usiku maalum wa Maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana. Mshindi huyo wa pili alizawadiwa Glass maalum ya Tusker Lite, bia mpya iliyozinduliwa usiku huo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Epraim Mafuru (mwenye suti kushoto) akimkabidhi zawadi ya Tusker Lite, Meneja bidhaa wa Push Mobile, Gonzoga Rugambwa  baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa shindano maalum la uchezaji mziki lililofabnyika wakati wa uzinduzi wa bia ya Tusker Lite sanjari na usiku wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati bia mpya ya Tusker Lite ilipozinduliwa sanjari na usiku maalum wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana.B
aadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati bia mpya ya Tusker Lite ilipozinduliwa sanjari na usiku maalum wa maafisa masoko jijini Dar es Salaam jana.
Wageni waalikwa
Burudani ilikuwepo kama kawaida
Ilikuwa raha tu.

Wednesday, November 28, 2012

MAMIA WAMZIKA MSANII SHARO MILIONEA LEO MUHEZA MKOANI TANGA


 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele
Sehemu Kubwa ya Umati wa watu ulikishiriki mazishi
Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono na Msanii wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu, Muheza mkoani Tanga.Picha Kwa Hisani Ya Ahmed Michuzi

Rais Jakaya Kikwete Azindua Rasmi Ukumbi Mpya Wa Bunge la Afrika Jijini Arusha Leo

Spika wa Bunge la Africa Mashariki Mhe. Margret Natongo Zziwa (kulia) akimkaribisha Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda katika jengo hilo leo.
 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiwasili katika jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha kwa lengo la kuzindua Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki ulioko katika jengo hilo.
 Spika wa Bunge Afrika Mashariki,Mhe. Margret Natongo Zziwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) ili kulihutubia Bunge la Afrika Mashariki.Kulia ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Afrika Mashariki wakati alipofika kuzindua Ukumbi Mpya wa Bunge la Afrika Mashariki ulioko katika jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.
 Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Jengo jipya la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Prosper Minja- Bunge.

Tuesday, November 27, 2012

*SHARO MILIONEA AFARIKI KWA AJALI YA GARI MUHEZA


 
Gari alilopata nalo ajali marehemu Sharo Milionea.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constatine Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali iliyosababisha kifo cha Msanii,  Sharo Milionea, aliyepata ajali usiku wa kuamkia leo mida ya saa mbili usiku katika kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga. 
*********************
MSANII mahiri wa filamu na muziki wa Bongo Flava nchini, Hussein Mkiety almaarufu, Sharo Milionea, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo majira ya saa mbili jana usiku, kwa ajali ya gari katikati ya Kijiji cha Lusanga na Maguzoni Songa, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Constatine Masawe,Sharo alikuwa peke yake garini wakati ajali hiyo ikitokea na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali Teule ya Muheza. Kamanda Masawe alisema Milionea, akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es Salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake. 


Hii ni ajali ya pili kati ya alizowahi kupata msanii huyo, Sharo kwa mwaka huu baada ya Januari 5 kunusurika katika ajali ya basi alilokuwa amepanda la Taqwa likitokea Burundi kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika eneo la Mikese, Morogoro saa mbili na nusu asubuhi.
Sharo ambaye alikuwa amekaa kwenye siti ya mbele kabisa alipoteza simu tu katika ajali hiyo ambayo ilijeruhi abiria wengine vibaya.

Kifo cha Sharo kinafuatia vifo vya wasanii wengine wawili wa filamu nchini ndani ya wiki moja, Mlopelo aliyetamba na kundi la Kaole na John Maganga aliyetamba na filamu ya 'Mrembo Kikojozi' aliyocheza na Aunt Ezekiel. 

Vifo hivyo vinakumbushia msiba wa Steven Kanumba, ambaye pia alifariki ghafla. 

Sharo atakumbukwa kwa ubunifu wake katika uigizaji akitoka kama mchekeshaji msafi tofauti na wachekeshaji wengi waliomtangulia ambao waliamini vichekesho ni lazima kuvaa kama katuni, kujaza nguo tumboni ili kuonekana na matumbo makubwa ama kujipaka masizi.

Akipendeza kwa mavazi nadhifu, Sharo Milionea alipata umaarufu kwa msemo wake wa "kamata mwizi meeen" na "Ooooh mamma!" huku akijipangusa mabega katika pozi za kibrazameni.

Katika siku za karibuni amekuwa akitawala vioo vya televisheni kutokana na kushiriki tangazo la kampuni ya huduma za simu ya Airtel akiwa na mchekeshaji mkongwe King Majuto, ambapo msemo wake mwingine wa "umebugi meen!" umetawala hasa midomoni mwa watoto.

Monday, November 26, 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI

  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za  uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za  ngoma za makabila mbalimbali  ya asili ya mkoa wa Katavi PICHA ZOTE NA FULLSHANGWEBLOG.COM.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji  cha Kibangu 
Msafara wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
 
Wazee waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho leo.

 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni  Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
 
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa  Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
 
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
 
Naibu wa Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.

 
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
 
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.

Sunday, November 25, 2012

KINANA, NAPE, KHATIB WAFUNIKA JIJINI ARUSHA

Kinana akisalimiana na Lowassa katika Uwanja wa Ndege wa Arusha. Kushoto ni Katibu wa CCM Arusha, Mary Chatanda.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Lowassa Uwanja wa Ndege wa Arusha. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda.
 
Pikipiki zikiongoza msafara wa Kinana, kutoka Uwanja wa Ndege wa Arusha.
 
Kinana akifungua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM Tawi la Nguruma, Arumeru, Arusha jana.
 
Ngoma ya Kimasai wakati wa mkutano wa Meru, jijini Arusha jana.
 
Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili Uwanja wa Usa River kuhutubia mkutano wa hadhara.
 
Nape akizungumza jambo la Lowassa kwenye mkutano wa Kinana uliofanyika Usa River, Arusha.
 
Baadhi ya vijana 150 wa Chadema waliohamia CCM wakionyesha kadi za Chadema, wakati wa mkutano wa Usa River jana.
 
Wazee wa Kimeru, wakimkabidhi vitendea kazi vya jadi, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika mkutano uliofanyika Usa River, Arusha. Anayemkabidhi ni Ezrom Sumari.
 
Kinana akivishwa mavazi ya jadi ya Wameru wakati wa mkutano uliofanyika Usa River, Arusha jana.
 
Mzee Willson Meng'atu akimvisha vazi la heshima Nape Nnauye kama ishara ya wazee wa Kimeru kutambua upambanaji wake katika kujenga Chama, wakati wa mkutano wa Usa River, Arusha jana.
 
Wazee wa Kimeru wakimvisha vazi la jadi, Katibu wa NEC Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib kumpongeza kushika nafasi hiyo ya kujenga uhai wa Chama, kwenye mkutano wa CCM Usa River, Arusha jana.
(Picha zote na Bashir Nkoromo)