Friday, December 18, 2015

KAMATI YA URATIBU YA SHIRIKISHO LA VYUO ELIMU YA JUU YAANZA VIKAO VYA SIKU MBILI

 
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah
(MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu
ya juu, kulia ni Katibu Mtendaji Ally S. Hapi
 Mwenyekiti
wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah
(MNEC) akijadiliana jambo pamoja na  Daniel
Zenda (katikati) na Ally S. Hapi wakati wa kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu
ya juu.
 Wajumbe wa kikao wakichambua mambo mbali mbali.
Kamati ya Uratibu taifa ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu leo
imeanza kikao cha siku mbili kinachofanyika makao makuu ya CCM Ofisi
Ndogo Lumumba jijini Dar es salaam
chini ya Mwenyekiti wake bi Zainab Abdallah(Mnec). Viongozi wengine
wanaohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho Ndg. Hamid
Mhina (Mnec), Katibu Mtendaji Ally S. Hapi, Katibu mtendaji Daniel
Zenda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa kutoka Shirikisho Joseph
Chitinka,Katibu uchumi na Fedha Richard Luhende, katibu wa siasa na
uenezi Fikiri Mzome na katibu wa uhamasishaji Mganwa Nzota.

No comments: