Showing posts with label biashara. Show all posts
Showing posts with label biashara. Show all posts

Wednesday, January 15, 2025

MAC AND JAK: THE NEW HOME OF REVIVAL IN BAGAMOYO

Bagamoyo has always been a destination steeped in history, culture, and beauty. However, finding the perfect blend of luxury, tranquility, and modern amenities has often been a challenge for travelers and business professionals alike.

The town deserved a space where comfort meets sophistication — a retreat that feels like home but better.

Imagine arriving in a place brimming with potential, only to find accommodations that lack personality and fail to connect with the local spirit. A promising getaway, overshadowed by uninspired menus, cramped facilities, and outdated decor, leaves you longing for something more.

For many visitors, the longing for an elevated experience has been unmet. 

You deserve a destination where you’re welcomed with more than just a smile — a space designed to revive your soul and inspire your senses.

Mac and Jak Getaway is Bagamoyo’s answer to the ultimate luxury retreat.

At Mac and Jak, nomadic traditions blend seamlessly with modern comforts, crafting a haven that’s truly one of a kind. Whether you’re seeking leisure, business productivity, or a mix of both, this is where your journey to revival begins.


A Taste of Mac and Jak’s Offerings

Whether you’re looking to unwind and escape the hustle and bustle, or eager to explore the stunning scenery, reach Bagamoyo culture, and exotic cuisine, our resort offers a wide range of activities to suit every preference.

Accommodation

Each room at Mac and Jak tells its own story. 

Inspired by the rich heritage of Bagamoyo, all our rooms are named after iconic streets and landmarks, offering you an authentic taste of the local culture.

Designed with meticulous attention to detail, our accommodations feature plush beds, spacious layouts, and a perfect blend of local artistry and contemporary elegance.

Wake up to breathtaking views of Bagamoyo’s coastline and let the refreshing ocean breeze greet you as you start your day.

Bar and Restaurant

The restaurant is where culinary artistry takes center stage. From fresh seafood delicacies to international classics with a Tanzanian twist, every dish is crafted to perfection. 

Pair your meal with a cocktail from the bar, where mixologists turn drinks into unforgettable experiences. It’s more than dining — it’s a feast for your senses.

Private Villas

For those seeking ultimate privacy and indulgence, the private villas at Mac and Jak are second to none. Spacious, secluded, and equipped with every amenity you could desire, these villas redefine luxury. 

Think private terraces, personal pools, and interiors that blend comfort with opulence.

Gym and Swimming Pool

Revive your body and mind in the state-of-the-art gym, complete with modern equipment to suit all fitness levels. Afterward, take a refreshing dip in the crystal-clear swimming pool. 

It’s the perfect place to unwind or soak up the African sun.

Conference Facility

Mac and Jak isn’t just for leisure travelers. Its cutting-edge conference facilities make it an ideal destination for business events, seminars, and team retreats. 

With fully equipped meeting rooms, high-speed internet, and impeccable service, your event is set to impress.


Explore Bagamoyo

Mac and Jak is more than just a hotel; it’s a gateway to Bagamoyo’s wonders. 

From historical sites like the Old Fort and Kaole Ruins to vibrant local markets, there’s so much to explore.

The hotel offers guided tours, to make sure you don’t miss a thing. 

Whether you’re tracing the steps of Bagamoyo’s storied past or soaking in its coastal charm, your adventure starts here.

Why Mac and Jak?

1. Personalized Service: Every guest is treated like family, with attention to detail that ensures your stay is unforgettable.

2. Unmatched Comfort: From the smallest rooms to the grandest villas, every space is designed to make you feel at home.

3. Prime Location: Situated in the heart of Bagamoyo, Mac and Jak is the perfect base for exploring the area.

Lastly, welcome to Mac and Jak.

Mac and Jak isn’t just a hotel — it’s an experience. It’s where luxury meets tradition and every detail is designed to create unforgettable memories. 

When you’re ready to escape the ordinary and embrace the extraordinary, Mac and Jak are waiting to welcome you.

For inquiries and bookings, contact us at info@macjak.co.tz or call +255 768 364 583. Early booking are available for honeymoon and holiday season events.

Sunday, January 12, 2025

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA TAWI LA NMB WETE, APOKEA VIFAA TIBA VYA MIL. 12

 








NA; MWANDISHI WETU, PEMBA

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hemedi Suleiman Abdulla, amezindua Tawi la NMB Wete, lililopo Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, huku akiahidi kuwa SMZ itaendeleza ushirikiano wake na NMB, benki aliyoitaja kama kinara wa kusapoti jitihada za utekelezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati.

Uzinduzi wa NMB Tawi la Wete umefanyika Januari 10 na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, akiwemo Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) – Kanda ya Zanzibar, Ibrahim Malogoi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Saada Mkuya Salum na Afisa Mkuu wa Fedha NMB, Juma Kimori.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais alisema tawi hilo ni muhimu sana kwa ustawi na maslahi mapana ya wananchi wa Kaskazini Pemba na Zanzibar kwa ujumla na kwamba mwitikio wa haraka wa wateja 1,800 waliofungua akaunti zao baada ya kufunguliwa unaakisi kiu ya maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.

“Uzinduzi huu wa NMB Wete, ni jambo muhimu kwa maisha maslahi ya wananchi wa Kaskazini Pemba na Wazanzibar, Takwimu zimetolewa hapa kuwa siku chache kabla uzinduzi huu wateja 1,800 wamefungua akaunti, hii ni kuthibitisha kiu yao ya huduma zenu, ndio maana nasisitiza wananchi wachangamkie fursa.

“Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB ameeleza fursa nyingi na huduma nyingi watakazotoa hapa, nami nieleze kuwa wananchi karibieni tawini mjue huduma na fursa hizo na mzitumie, nasisitiza hilo huku nikiwaomba NMB waendelee kusambaza na kuboresha huduma zao kwa wananchi, hasa suala zima la huduma za kidijitali,” alisema Makamu wa Rais.

Aliongeza kuiwa SMZ Inaahidi ushirikiano mkubwa na NMB katika kufanikisha ustawi na maisha bora kwa Wazanzibar, akibainisha kuwa ubora wa kihuduma unaooneshwa na benki hiyo unatokana pia na mazingira mazuri na uwekezaji mzuri wa teknolojia uliofanywa.

“Ujio wa NMB Wete utaleta na kuchachua ushindani wa taasisi za fedha Kaskazini Pemba kihuduma, ambazo hazihitaji ushawishi wa maneno, bali huduma zenyewe ndio mshawishi mkuuu,” alisisitiza Abdullah huku akituma salamu za pongezi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wake Ruth Zaipuna kwa kazi kubwa na nzuri anayofanya.

“Kwa dhati kabisa shukrani zetu zimfikie CEO wa NMB, na salam zimfikie, tunamshukuru kwa ushirikiano wake na sapoti zake kwa SMZ n ahata Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hakika amekuwa mfano wa kuigwa, kazi kubwa anaifanya na tunampongeza kwa juhudi zake, utumishi na mashirikiano yake.

“Mambo mbalimbali yamesemwa jinsi waliyosaidia hapa Pemba, lakini ukiacha vifaa vya elimu na vifaa tiba vilivyotajwa, ipo ‘Ultra Sound’ moja haijatajwa, mliyotoa katika Hopsitali ya Kendwa ikiwa nma thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 53, kupitia kifaa kile hospitali ile inafanya kazi kubwa kuliko hospitali ya wilaya,” alimalizia.

 Awali, Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna, aliishukuru SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano bora inaoonesha kwa NMB na mazingira wezeshi inayoyaimarisha kila uchao katika kuziwezesha Taasisi za Fedha kuhudumia wananchi kwa ufanisi.

“Tuko hapa kuthibitisha kwa vitendo kaulimbiu yetu ya Karibu Yako, NMB Wete inaenda kumaliza adha ya wakazi wa hapa kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 30 kwenda Chakechake kufuata huduma za kibenki na sasa watapata huduma zote hapa tawini ikiwemo mikopo, kuweka na kutoa pesa, bima na kubadilisha fedha.

“NMB Wete ni tawi la 241 kote nchini Tanzania, likiwa ni tawi la tisa kwa Visiwani Zanzibar. Hii maana yake ni kwamba mtandao wetu wa huduma unaojumuisha ATM 720, kati ya hizo 22 zikiwemo hapa Zanzibar, unaendelea kukua kwa kasi na ahadi yetu ni kuzidi kusogeza huduma kwa Watanzania wote, kote nchini.

“Tunaahidi kuendelea kusafiri pamoja na serikali zote, hasa SMZ katika meli yake ya Uchumi wa Buluu, sera ambayo ni muhimu mno kwa ustawi wa Wazanzibari. Sambamba na uzinduzi huu, tunakabidhi vitanda 10 vya kulaza wagonjwa, vitano vya kujifungulia na mashuka 80 kwa Hospitali ya Mzambarauni, vyenye thamani ya Sh. Mil. 12.

“Vifaatiba hivyo tunavitoa kupitia fungu letu la Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ambayo tunatumia asilimia moja ya faida yetu kurejesha kwa jamii kama tulivyofanya katika uezekaji wa mapaa ya Skuli ya Tasini na Kiwani tulikopaua shule na Kituo cha Afya Kendwa, ambako tumetumia zaidi ya Sh. Mil. 110,” alisema Kimori.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa BoT – Kanda ya Zanzibar, Ibrahim Joseph Malogoi, aliipongeza NMB kwa jitihada kubwa inazofanya katika kusambaza huduma za kibenki kwa jamii na kwamba NMB ni benki ya 14 Zanzibar na ya nne kufikisha huduma kwa Wananchi wa Pemba, huku Tawi la Wete likiwa ni tawi la 9 la benki.“

Kama msimamizi wa Serikali katika huduma za kibenki, nafarijika sana kuona ustawi wa Sekta ya Fedha Zanzibar ukikua kwa kasi na ongezeko hili la Taasisi za Fedha kwa Wazanzibar, linaakisi jitihada za dhati za kuimarisha ukuaji wa Uchumi na ndio maana halisi ya Mapinduzi,” alibainisha Malogoi.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Bi. Saada Mkuya Salum, aliipongeza NMB kwa kuzindua tawi jipya Wete, alioutaja kama muendelezo wa taasisi hiyo kusapoti Sera ya Ujumuishwaji wa Wananchi katika masuala ya fedha, ambayo kiwango cha Watanzania wanaotumia huduma hizo imeongezeka kwa kasi.

Alisema kupitia Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar, miradi kadhaa mikubwa na ya kimkakati imezinduliwa, akisema imetokana na fedha ambazo Serikali imekopa kutoka kwa NMB na NBC, ambao kwa pamoja wameikopesha Sh. 470 na kwamba Ofisi ya Rais Fedha na Mipango inatambua na kuthamini mchango huo na inaahidi ushirikiano endelevu.

Sunday, January 05, 2025

Benki ya NBC Yazindua Hati Fungani ya Sh Bilioni 27.2 Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya NBC - Theobald Sabi.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi Kiwango cha kwanza cha sehemu yake ya pili ya Hati Fungani ya NBC Twiga, yenye thamani ya shilingi bilioni 27.2, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha sekta ya biashara ndogo na za kati nchini.

Hatua hii ya kimkakati ya benki hiyo inatajwa kuwa inalenga kuthibitisha jitihada za benki hiyo katika kurahisisha upatikanaji wa mitaji miongoni mwa wafanyabiashara hususani wajasiriamali ili kukuza maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo mwishoni mwa wiki, hati fungani hiyo ya miaka mitano tayari imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).


“Fedha zitakazopatikana kupitia Hati Fungani hii ya NBC Twiga zitatumika kuwezesha mikopo rafiki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao kimsingi tunawatambua kama uti wa mgongo wa uchumi wetu kama taifa,’’ alisisitiza Bw Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, katika taarifa hiyo.

Bw Sabi alisisitiza kuwa kwa kuboresha upatikanaji wa mitaji hiyo muhimu kwa wajasiriamali, benki ya NBC inadhamiria kufungua uwezo mkubwa wa ukuaji kwa biashara hizo, hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla nchini.

“Malipo ya riba kwa wawekezaji yatafanywa kila nusu mwaka wakati wote wa hati fungani hii itakayohitimishwa mwezi Oktoba, 2029. Jambo la msingi pia ni kufahamu kwamba mapato yatokanayo na hati fungani hii hayatozwi kodi ya zuio (withholding tax), na hivyo kuongeza mvuto wake kwa wawekezaji wa ndani na kimataifa,” aliongeza.

Akizungumza kuhusu faida zinazoambatana na hati fungani hiyo, Bw Sabi alionesha kuridhishwa na mchango wake katika kuimarisha sekta ya ujasiriamali nchini. “Hati Fungani hii ya miaka mitano itaimarisha si tu sekta ya ujasirimali —ambayo inawaajiri watu wengi katika nchi—bali pia itapanua upatikanaji wa mitaji na kufungua fursa mpya za ukuaji wao,” alisisitiza.


Maoni ya Bw Sabi yanaakisi dhamira ya NBC ya kuendeleza maendeleo ya uchumi endelevu kupitia ujumuishaji wa kifedha na msaada wa biashara zinazochipukia.

Uzinduzi wa Hati Fungani hiyo unakuja kama muitikio chanya kutoka kwa Mfuko wa Dhamana za Sarafu za Ndani za Kiafrika (ALCB Fund) ambao ni mpango wa Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) unaolenga kuwekeza katika hati fungani za kampuni na mashirika kupitia sarafu za ndani.

Hivi karibuni, Mfuko wa ALCB ulifanya uwekezaji mkubwa wa fedha kiasi cha sh bilioni 27.2 (takribani Dola za kimarekani milioni 10) katika hati fungani hiyo ya NBC Twiga, hatua iliyoonesha imani ya mfuko huo katika kuuunga mkono mikakati ya kifedha ya NBC.

Katika hatua inayoongeza imani na matarajio zaidi ya mpango huo, uwekezaji huo wa Mfuko wa ALCB umewezeshwa kupitia ruzuku kutoka kwa Mfuko wa Kubadilisha Sarafu (TCX) iliyotolewa kupitia Kituo chake cha Bei za Uundaji wa Soko la Umoja wa Ulaya. Kituo hiki kinakusudia kuhamasisha matumizi ya sarafu za ndani katika fedha za maendeleo, jambo ambalo ni muhimu katika kukuza utulivu wa kiuchumi na ukuaji nchini.

“Hati Fungani ya NBC Twiga inatarajiwa kuchochea ukuaji wa mabadiliko, ikinufaisha wajasiriamali na uchumi kwa ujumla, na hivyo kufungua milango kwa siku nzuri zijazo katika mzunguko wa kifedha nchini.’’

“Tunapoendelea na mpango huu, tunabaki imara katika dhamira yetu ya kuimarisha mifumo ya uchumi wa Tanzania, kuhakikisha kwamba wajasiriamali wanapata msaada stahiki ili kuweza kustawi na kuchangia katika ajenda ya maendeleo ya kitaifa,” alihitimisha.

Wednesday, January 01, 2025

NMB yadhamini kombe la Mapinduzi 2025, yafadhili Siku ya Mazoezi Kitaifa Z'bar

 






BENKI ya NMB, imetangaza udhamini wa Sh. Milioni 50 wa michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar (Mapinduzi Cup 2025), inayotarajia kuanza Januari 03, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani visiwani Pemba, ambayo itashirikisha timu za Taifa, badala ya klabu za Tanzania Bara na Zanzibar kama ilivyozoeleka


Sambamba na udhamini huo, NMB pia imekabidhi 'tracksuit' 100 zenye thamani ya Sh. Mil. 9 za kuvaa viongozi wa Serikali ya Zanzibar katika Siku ya Kitaifa ya Mazoezi (Januari 1, 2025), ambayo ni sehemu ya Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo inafanyika chini ya kaulimbiu: 'Amani, Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo Yetu - Mapinduzi Daima.'

Hafla ya makabidhiano ya hundi ya udhamini na 'tracksuit' hizo, imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, ambako Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar, Ahmed Jumaa Nassor, alimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Fatma Hamad Rajabu, mbele ya Meneja Uhusiano wa NMB Zanzibar, Jaha Khamisi.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo baada ya kupokea hundi, Bi. Fatma aliishukuru NMB kwa mchango wao, ushirikiano na umoja wanaoonesha kwa Serikali ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, na kuitaka kudumisha mashirikiano hayo kwa ustawi wa Zanzibar na maendeleo ya Wazanzibar kwa ujumla.

Alibainisha kuwa mchango na ushiriki wa NMB sio tu katika Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, bali iko mstari wa mbele daima kuchagiza maendeleo ya visiwa hivyo na wakazi wake na katika nyanja nyingi, ikiwemo michezo, ambako imejitoa vya kutosha kudhamini Kombe la Mapinduzi kwa miaka kadhaa na kuchangia ongezeko la ajira kupitia michezo.

"Wazanzibar wengi wanahudumiwa na NMB na uwingi wao unalenga kuiwezesha benki kukuza pato lao ili nao wanufaike na mchango wa maendeleo ya Zanzibar na watu wake. Tunawapongeza kwa kufadhili Siku ya Mazoezi Kitaifa, lakini pia kwa udhamini wenu mnono katika Kombe la Mapinduzi 2025.

"Tofauti na miaka yote ambako klabu hushiriki Kombe la Mapinduzi, mwaka huu zitacheza timu za Taifa, ikiwemo Zanzibar Heroes. Wito wetu kama Serikali, tunawataka Wazanzibar wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Gombani Pemba, kuisapoti timu yao iweze kubakisha nyumbani taji la mashindano hayo," alisema Bi. Fatma.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar, Ahmed Jumaa Nassor, alisema benki yake inajisikia fahari kuwa sehemu ya Shamrashamra za Mapinduzi ya Zanzibar kwa miaka 12 sasa na kwamba inatambua na inathamini mchango wa Serikali ya Zanzibar katika kuweka mazingira wezeshi ya wao kuhudumia Wazanzibar na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya wananchi.

"NMB imekuwa mshirika mkubwa wa Serikali zote (Zanzibar na Tanzania), hivyo ni heshima kuendelea kuwa sehemu ya Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

"Tuko hapa kufanya mambo mawili, yote yakihusiana na sherehe hizo zinazoanza Januari Mosi na kufikia ukomo wake Januari 13, siku moja baada ya kilele cha Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Leo tunakukabidhi 'tracksuit' 100 za kuvaa washiriki wa Siku ya Mazoezi Kitaifa Zanzibar Januari Mosi, tukiamini kuwa mchango huu utatumika kama chachu katika muendelezo wa hamasa ya mazoezi miongoni mwa Wazanzibar, pia tunakabidhi kwako hundi ya udhamini wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi, wenye thamani ya Sh. Milioni 50," alisema Ahmed na kuongeza:

"Udhamini huu pamoja na vifaa hivi, ni kilelezo na uthibitisho wa dhati kuwa NMB inathamini michezo, kwani afya zetu zinaimarika zaidi kupitia michezo na uimara wa afya ndio chachu ya kukua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

"Ni fahari kubwa kwetu kuendelea kushirikiana na Serikali kwa miaka 12 ya NMB kuwa sehemu ya ukamilifu wa matukio hayo kwa kipindi chote hicho," alisisitiza Ahmed katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na maafisa wa wizara hiyo ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo pamoja na Wajumbe wa kamati ya kombe la mapinduzi 2025.

Saturday, December 28, 2024

Mil. 76/- kati ya Mil. 300/- za NMB MastaBata zaenda kwa wateja 712

 


NA MWANDISHI WETU

WATEJA zaidi ya 700 kati ya 2000 wa msimu wa sita wa promosheni ya kuhamasisha malipo na manunuzi kwa njia ya kadi inayoendeshwa na Benki ya NMB ‘NMB MastaBata – La Kibabe,’ wameshajizolea kitita cha jumla cha zaidi ya Sh. Mil. 76.4, kati ya zaidi ya Mil. 300 zinazoshindaniwa kupitia droo za kila wiki.

NMB MastaBata – La Kibabe ni kampeni inayochagiza matumizi yasiyo ya pesa taslimu, ambako wateja wa NMB wanaotumia Kadi za MastaCard kuchanja kulipia huduma kwa njia ya QR Code, PoS na NMB Pay by Link, ambapo benki hiyo huwazawadia kila wiki, kila mwezi na ‘grand final’ itakayofanyika Februari 12, 2025.

Idadi hiyo ya washindi na kiasi hicho cha pesa walizoshinda, kimekuja baada ya kufanyika kwa droo ya saba, iliyofanyika Ijumaa Desemba 27, kwenye Ofisi za NMB Tawi la Tegeta, ambako Meneja wa Tawi, Bi. Magreth Lwiva, alichezesha akisimamiwa na Pendo Mfuru kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

Akizungumza kabla ya droo hiyo, Bi. Magreth alisema jumla ya washindi 2000 watajishindia zawadi mbalimbali zilizotengwa na benki hiyo zikiwa na thamani ya Sh. Mil. 300 na kwamba kila wiki wateja 100 hujinyakulia kiasi cha Sh. 100,000, huku wengine 40 wakishinda zawadi za papo hapo, zikiwemo vocha za manunuzi ‘shopping challenge.’

“NMB MastaBata pia hutoa zawadi za kila mwisho wa mwezi kwa miezi miwili, ambako washindi 15 hujinyakulia Sh. 500,00 kila mmoja, washindi watano hujishindia safari ya kutembelea Mguga za Wanyama za Mikumi na Ngorongoro na wengine watano kujishindia pesa hadi Sh. Mil. 4 za ada zao au watoto wao.

“Katika droo ya mwisho yaani grand finale, wateja wetu sita watajishindia tiketi za kusafiri Kwenda Dubai wao na weza wao, ambapo wataka huko kwa siku tano kwenye Hoteli ya Nyota Tano, safari ambayo itagharamiwa kila kitu na NMB,” alibainisha Bi. Magreth mbele ya Afisa wa Idara ya Biashara ya Kadi NMB, Salehe Nkuruvi.

Kwa upande wake, Bi. Pendo Mfuru kutoka GBT, alisema Bodi yake inaishukuru NMB kwa namna inavyoendesha droo zake kwa uwazi na haki, huku akiwataka wateja wa benki hiyo kuwa huru wanaposhiriki droo mbalimbali, kwani inazingatia sheria, kanuni na miongozi wanayopewa na GBT.

“Niko hapa kwa niaba ya GBT, uwepo wangu hapa unalenga kuhakikisha droo inachezeshwa kwa kuzingatia vigezo na masharti yanayosimamia michezo hii, ili kupata wateja kihalali, ambalo ndilo jukumu mama la taasisi yetu. Hivyo tunawahakikishia wateja wa NMB kwamba, haki, vigezo na masharti vinazingatiwa,” alisema.











TASHICO YAFAFANUA MELI MV SERENGETI KUZAMA ZIWA VICTORIA




 NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

KAMPUNI ya Meli Tanzania (TASHICO) imefafanua tukio la kuzama kwa meli ya MV Serengeti katika Bandari ya Mwanza Kusini,Ziwa Victoria, baadaa ya kukumbwa na tatizo la kuegemea upande wa nyuma na kutitia chini ndani ya maji.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASHICO, Wakili Alphonce Paul Sebukoto, ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Disemba 26, majira ya saa 8:00 usiku, ambapo meli ilionekana kulalia upande wa nyuma na kuzama majini.

Amesema kuwa walipokea taarifa ya meli hiyo kuingiza maji na hivyo kuzama upande wa nyuma baada ya kuelemewa na maji , ikiwa imeegeshwa katika ghati eneo la Bandari ya Mwanza Kusini, wilayani Nyamagana.

“Meli haijafanya biashara muda mrefu ilikuwa imeegeshwa tangu mwaka 2016, ikisubiri kufanyiwa ukarabati mkubwa. Hii ni meli ambayo ilisitisha kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo na abiria,” amesema Wakili Sebukoto.

Amesema MV Serengeti, imetengewa fedha za ukarabati ni moja ya meli nne zilizokuwa zimesimamishwa na serikali ili kufanyiwa ukarabati mkubwa,zingine ni MT Ukerewe, MV Nyangumi na ML Wimba na zinakaguliwa kila mwaka na wataalamu wa kiusalama ili kuhakikisha usalama wa meli hizo.

“MV Serengeti haikuwa na matatizo yoyote ya kiusalama,iko katika mpango wa matengenezo mwaka huu wa fedha 2024/25.Meli hii inakaguliwa kila mwaka na wataalamu wa usalama na siku chache kabla ilikaguliwa na kuonekana iko salama.”

Wakili Sebukoto ameongeza kuwa chanzo cha meli hiyo kujaa maji bado hakijajulikana, na kuna uwezekano wa kuchakaa kwa baadhi ya vyuma vya meli, au kupigwa mawimbi makali ambayo yanaweza kuleta tatizo hilo.

Amesema bado ni mapema kusema nini kimesababisha meli ilemewe na maji hadi kuzama upande wa nyuma, hivyo baada ya kunyayuliwa utafanyika uchuguzi wa kitaalamu kuibaini tatizo.

“Meli hii iliyojengwa mwaka 1988 ina uwezo wa kubeba abiria 500 na tani 250 za mizigo. Ni meli muhimu yenye faida kwa TASHICO na serikali, hasa katika maeneo yasiyo na miundombinu ya bandari, ikiwemo visiwani,” amesema Wakili Sebukoto, akisisitiza umuhimu wa ukarabati wa meli hiyo.

Akijibu maswali kuhusu tukio lingine la meli ya MV Clarias, Wakili Sebukoto amefafanua kuwa, hilo halihusiani na la MV Serengeti na kubainisha wazi kuwa MV Clarias ililalia upande mmoja ikiwa ghatini baada ya kutoka safari katika visiwa vya Gana na Goziba.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini ikiwa kulikuwa na uzembe au hujuma katika matukio yote mawili,endapo uchunguzi utaonesha uzembe au makosa ya watu, hatua kali zitachukuliwa ikiwemo watu kufikishwa mahakamani.

“MV Clarias ilikuwa na tatizo la matundu (Stain tube) yaliyo na upana usio wa kawaida, ya kuruhusu maji kuingia ndani ya meli na kupumua kwa kiwango kinachotakiwa.Uchunguzi unaendelea na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika,” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TASHICO.

Naye, Said Sekiboto wa Kitengo cha Uokoaji Ndani ya Maji cha Jeshi la Zimamoto ya Uokoaji, Mkoa wa Mwanza, ameeleza kuwa hatua za dharura zinaendelea kuchukuliwa ili kuinyanyua meli ya MV Serengeti.

Amesema kuwa walifika katika tukio majira ya saa 8:00 usiku (Disemba 26,) baada ya kupata taarifa za meli hiyo kuzama, lakini walishindwa kufanya operesheni ya kuinyanyua mara moja kutokana na changamoto za vifaa.

“Vifaa tulivyokuwa navyo havikuwa na uwezo wa kuinyanyua meli kwa haraka, lakini sasa tumeimarisha vifaa hivyo na tunaendelea na operesheni ya kuinyanyua.Tutatumia vifaa vya ziada kuendelea na kazi ya kuinyanyua meli na kufyonza maji yaliyokuwa yamejaa ndani pamoja na kwenye Chelezo,”alisema.

Sekiboto ameongeza kuwa, licha ya meli hiyo upande wa nyuma kuzama hakuna madhara, sehemu ya mbele inaendelea kuelea juu ya maji, kazi ya kuondoa maji ndani ya meli itafanyika kwa siku nzima ili kuhakikisha usalama wa meli na kuirejesha hali yake.
Hivyo, TASHICO na vyombo vingine vya usalama, likiwemo Jeshi la Zimamoto, vinaendelea na operesheni hiyo kwa umakini mkubwa kuhakikisha meli inarejeshwa kwa usalama na kuondoa hatari yoyote inayoweza kutokea kwa umma na mali za serikali ili kusubiri uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Wednesday, December 11, 2024

BENKI KUU YA TANZANIA KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATEJA KIDIGITALI

  Kaimu Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha BoT, Ms Nangi Massawe, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha maalum kwa watoa huduma za kifedha, iliyofanyika leo Disemba 10, 2024.

  Kaimu Meneja wa kumlinda mtumiaji wa Huduma za Fedha, Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, BoT, Dkt. Khadija Kishimba, akifafanua jambo alipokuwa akizungumza katika Warsha hiyo, iliyofanyika katika Ofii za BoT Jijini Dar es Salaam. 

Meneja Msaidizi Idara ya Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Kifedha, Benki Kuu ya Tnzania BoT, Violet Luhanjo, akizungumza katika warsha hiyo.

  

 Meneja Msaidizi Idara ya Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Kifedha, Benki Kuu ya Tnzania BoT, Violet Luhanjo, akizungumza katika warsha hiyo.

.









Monday, November 11, 2024

BENKI YA DCB KUONGEZA MTAJI WA SH BILIONI 10.7

BENKI ya Biashara ya DCB, imezindua zoezi ya uuzaji wa Hisa za Upendeleo, ikitarajia kupata zaidi ya sh bilioni 10.7 ili kuongeza kiasi cha mtaji wake unaofikia sh bilioni 15 kwa sasa, ili pamoja na mambo mengine kukidhi vigezo vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pamoja na kuwaletea wanahisa wake na watanzania kwa ujumla tija za kiuchumi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji wa hisa hizo jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro alisema uamuzi huo unaenda sambamba na mikakati yao ya maendeleo ya miaka mitano katika kuongeza mtaji wake kutoka ulipo sasa hadi kufikia sh bilioni 61.

“Bodi ya Wakurugenzi ya DCB iliidhinisha mpango mkakati wa miaka mitano ukijikita kwenye mambo makuu Matano; Kwanza kukuza mtaji wa benki kutoka shs bilioni 15 (2024) hadi kufikia shs bilioni 61 ifikapo mwaka 2028, pili ukusanyaji wa amana nafuu za benki kupitia wanahisa wakuu na wateja wetu, tatu kuongeza wigo wa mikopo bora itakayotolewa kwa ufanisi na umahiri, nne utaoaji wa mikopo kwa wateja wadogo wadogo na wa kati ili kuendelea kutimiza lengo la kuanzishwa kwa benki yetu na tano, kuboresha njia za utoaji huduma na kuongeza bidhaa zinazotolewa kwa njia za kijiditali.

“Tukio la leo linaenda kuandika historia ya benki na kuanza kutimiza mkakati wa kwanza wa kuongeza mtaji wa benki, hivi sasa, mtaji wa benki uko kwenye kima cha chini kilichowekwa na Benki Kuu ya Tanzania, na ili kuweza kusimama imara kama benki, ongezeko la mtaji ni muhimu sana, benki inadhamiria kufanya biashara kubwa ambapo ili kufanikisha lengo hili, kuna ulazima wa kuongeza mtaji”, alisema Bi. Zawadia.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ili kuweza kuhakikisha mtaji wa benki unaendelea kukua mwaka hadi mwaka baada ya zoezi hili na pia kutumiza malengo ya benki, Bodi ya Wakurugenzi iliona ni muhimu kufanya mabadiliko machache ya kiutawala katika menejimenti ya benki yetu, na kumteu Ndugu Sabasaba Moshingi kama Mkurugenzi Mtendaji wa benki mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika tansia ya benki, huku mabadiliko mengine yakifanyika katika idara ya biashara, mikopo na uendeshaji na teknolojia, idara zote hizi kwa ujumla ni nguzo muhimu katika biashara ya benki.

Alisema uuzaji wa Hisa za upendelo unatarajia kuwaletea wanahisa na watanzania kwa ujumla tija za kiuchumi, baada ya kuongeza mtaji wa benki ambapo unalenga kukuza biashara na kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati mitaji ya kukuza biashara zao na upande mwingine umiliki wa hisa za benki ya DCB unaunga mkono juhudi zinazoendelea za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi shupavu wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watu wake maendeleo.

“Bodi ya DCB pamoja na Menejimenti ya benki ilipendekeza na kuidhinisha uuzaji wa Hisa za Upendeleo 97,646,913 zenye thamani ya shs 10,741,160,430 kwa bei ya punguzo ya shs 110 kwa kila hisa moja, kinyume na shs 160 iliyopo sokoni, ni matumaini yetu zoezi hii litapata muitikio mkubwa kutoka kwa wanahisa wetu, ambao wana imani na benki hii, bodi na menejimenti yake kwa ujumla.

“Benki imerahisisha ununuzi wa hisa kwa kuruhusu ununuzi kwa njia za kidigitali ili kuongeza wigo wa ushiriki wa wanahisa, natoa rai kwa wanahisa kuchangamkia fursa hii ya kununua hisa kwa njia za kidigitali, au kupitia mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam au kwa kufika kwenye matawi yetu ya benki”, aliongeza Bi. Nanyaro.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius aliipongeza Benki ya DCB kwa uamuzi huo uliofanyika kwa weledi na ufanisi mkubwa na kupata idhini kutoka CMSA.

Akimwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo, CPA Nicodemus Mkama, Bwana Julius alisema, serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.

“Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma, hatifungani za miundombinu, hatifungani rafiki za mazingira, hatifungani za bluu, hatifungani za jamii na hatifungani za taasisi za serikali”, alisema Bw. Julius.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi alisema, yeye pamoja na menejimenti yote ya DCB wamejipanga kuhakikisha hadi kufikia Mwaka 2028 wanaandika upya historia ya benki hiyo sambamba na mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya benki hiyo wa kuhakikisha benki inaendelea kukua na kupata faida.

Alisema kwa kuthibitisha hayo, benki hiyo imeweza kutengeneza faida katika robo ya pili na ya tatu huku ikiendelea kutoa huduma za kibenki bila kusahau jukumu la kuanzishwa kwake takribani miaka 22 iliyopita ikiweka mkazo mkubwa katika huduma zake za kidigitali ili kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

“Tumejipanga kuhakikisha benki yetu inaendeleza maono ya kuanzishwa kwake ambayo ni kusaidia miradi ya kupunguza umasikini kwa kutoa mikopo ya mitaji kwa wajasiriamali wadogo na wa kati waliokosa huduma hizi kutokana na kutokidhi vigezo vya benki ya kibiashara za wakati ule.

“Uuzaji huu wa Hisa za Upendeleo ambao sasa benki yetu inafanya kwa mara ya nne kwa vipindi tofauti utasaidia kuongeza uwezo wa benki yetu katika kuwahudumia wateja wetu na ni imani yetu pia kuanzia mwakani wanahisa wetu wataweza kuanza kupata gawio hivyo tunaomba waendelee kutuunga mkono”, alisema.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius (katikati), akikata utepe, kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la uuzaji wa Hisa za Upendeleo za Benki ya Biashara ya DCB, jijini Dar es Salaam leo. Wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro na wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi pamoja na wawakilishi wa taasisi nyingine waliohudhuria.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Exaut Julius (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi (wa tatu kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, wakionesha kitabu chenye taarifa muhimu kuhusu Hisa wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la uuzaji wa Hisa za Upendeleo za Benki ya DCB, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa DCB, Bi. Regina Mduma, pamoja na wawakilishi kutoka taasisi nyingine waliohudhuria hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga, akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo.



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Hisa za Upendeleo za benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Alisema Bodi na  Menejimenti ya benki ilipendekeza na kuidhinisha uuzaji wa Hisa za Upendeleo  97,646,913 zenye thamani ya shs 10,741,160,430 kwa bei ya punguzo ya shs 110 kwa kila hisa moja. Huku bei ya soko ikiwa shs 160. 

WAZIRI JAFO AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA KUJA KUJENGA VIWANDA TANZANIA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu fursa za ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.

Na.Mwandishi Wetu-ETHIOPIA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka Mazingira bora na wezeshi yanayovutia wafanyabiashara kuja kuwekeza nchini hususani katika kuanzisha viwanda ili kutiumiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayolenga kujenga uchumi shindani na jumuishi wa viwand kwa lengo la kuongeza ajira na pato la Taifa .

Waziri jafo ameeasema hayo Novemba alipotembelea na kuzungumza na uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern Industry Park) iliyopo Addis Ababa, Ethiopia yenye jumla ya viwanda takribani 257 ikiwemo viwanda vya chuma, nguo, na dawa na yenye nia ya kuja kuwekeza Tanzania kwa kujenga Kongani kubwa ya Viwanda.

Waziri Jafo akiwa ameambatana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia pamoja na wataalamu kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) utakaofanyika Novemba 9-10, 2024, mjini humo ameikaribisha kampuni hiyo na kuahidi kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Taasisi husika itaipa ushirikiano wa katika kuanzisha kongani hiyo.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern Industry Park) Bi Ma Futao amesema Kampuni yake iko tayari kuwekeza Tanzania kwa kuwa mazingira ya ufanyaji biashara yanavutia ikiwemo Sera nzuri za biashara, bandari na miundombinu ya barabara na reli ya kisasa inayoinganisha na nchi jirani zisizo na bahari

Naye Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amebainisha kuwa Kongani ya Viwanda ya Eastern ikijengwa Tanzania itaongeza ajira hususani kwa makundi maalum kama wananwake na vijana, pato la Taifa na hatimaye kukuza biashara na uchumi kwa ujumla.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) wakipeana mkono wa heri na Mmiki wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia Bw Bw.Lu Qixin mwenye nia ya kuwekeza Tanzania baada ya kutembelea Kongani hiyo ambapo amemkaribisha mwekezaji huyo kuja kuwekeza nchini ili kuongeza ujenzi wa Viwanda ambavyo vitatoa ajira nyingi kwa watanzania na kujenga uchumi wa nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakitembelea viwanda katika Kongani ya Eastern Industry iliyopo Addis Ababa, Ethiopia kujionea shughuli za uzalishaji kwa Mwekezajih uyo mwenye nia ya kuwekeza Tanzania.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu fursa za ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Tirita General Trading ya Djibouti Bw. Abiy Araya kuhusu fursa za ufanyaji biashara Tanzania katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia ambapo Dkt. Abdallah amemukaribisha Mfanyabiashara huyo kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...