Friday, July 31, 2015

TRA YAWAPIGA MSASA CTI JUU YA SHERIA MPYA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI YA MWAKA 2014

ct1
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiongea na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct2
Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Dkt. Samuel Nyantahe akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa uamuzi wa kuwakutanisha wadau wa sekta ya viwanda na kuwaelimisha kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 ili kuweza kuondoa utata kwenye baadhi ya maeneo yaliyo katika sheria hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct3
Wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct4
Wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct5
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga akimpongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade baada ya kumaliza kuwahutubia wajumbe kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), leo Jijini Dar es Salaam.
ct6
Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akiwasilisha mada kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria hiyo iliyoanza kutumika Julai 1, 2015 Leo Jijini Dar es Salaam.
ct7
Wajumbe kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakiuliza maswali kwa wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
ct8ct9ct10
Makamu wa pili wa mwenyekiti kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Pankaj Kumar akiongea wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct11
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014, wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa Kuhusu Sheria Hiyo
ct12
Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
ct13
Afisa Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Donasian Assey akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014.
ct14
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga akimueleza Jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
ct15
Afisa Mwandamizi Toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Beldom Chaula akiwaeleza jambo baadhi ya wadau kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Sheria Mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015, Leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO -MAELEZO

ZUENA MOHAMED MAARUFU KAMA “SHILOLE” KIFUNGONI MWAKA MMOJA

shilole1
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa jina la kisanii Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.
Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la Muziki nchini Ubelgiji alikiuka maadili ya kazi ya sanaa mbele ya hadhira ya  wapenda sanaa za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na jamii ya Kitanzania kimaadili.  Pia itakumbukwa kwamba mnamo mwezi Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili awapo jukwaani.
BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua  za kinidhamu kwa kitendo chake cha kudhalilisha maadili, utu na sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo.  Hivyo basi BASATA imejiridhisha kwamba alikiuka maadili ya kazi ya sanaa  kwenye onesho lake la   huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria, Kanuni  na Taratibu za uendeshaji wa Sanaa.
Hivyo basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha na kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015. 
Hivyo haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli yoyote ya onesho la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume cha hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule utakaye shirikiana naye.
Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la Taifa kwamba wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
 Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA NA MSUMBIJI IKULU DAR

01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 31, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Chirau Ali Mwakwere, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015.  Picha na OMR
unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam , leo Julai 31, 2015, wakati Balozi huyo alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi.  Picha na OMR
unnamed (1)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Dkt. Vicente Veloso, aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 31, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR

KIDOTI :VIJANA WA JIJI LA ARUSHA CHANGAMKIENI FURSA ZA KIJASIRIAMALI


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza 



 Warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti 

 Mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari

 Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A  wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao
 mabalozi wa kidoti   wakiwa kazini.

GARI LA KUBEBEA MAJENEZA LA KIPEKEE LAINGIA NCHINI

IMG_0469Pichani juu na chini ni muonekano wa Gari maalum la kukodisha kwa ajili ya shughuli za kubebea majeneza katika misiba limeingia nchini.
Kwa wanaohitaji kukodi kwa shughuli za misiba wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepekiwiaadavidson@hotmail.com au simu namba +255 715 213213, +255 713 616606 na +255 784616606
IMG_0459
IMG_0481Muonekano wa ndani sehemu maalum linapowekwa jeneza.

RAIS YOWERI MUSEVEN AFUNGUA MKUTANO WA MARAIS WASTAAFU KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda akifungua rasmi mkutano wa Marais wastaafu wa Afrka  AFRICA LEADERSHIP FORUM unaofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Mkutano huo unaojumuisha marais wastaafu  Benjamin Mkapa wa Tanzania , Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Festus Mogaye wa Botswana, Bakili Muluzi wa Malawi na Jerry Rowlings wa Ghana unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika bara la Afrika na Changamoto zinazokabili barahilo na umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Marais wastaafu Bakili Muluzi wa Malawi kulia  na Jerry Rawlings wa Ghana wakiwa katika mkutano huo. 
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kushoto na Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu Mstaafu wa AU na Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki KuuProf. Beno Ndulu wa tatu kutoka kulia na wageni mbalimbali wakihudhuria katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Marais wastaafu kutoka kushoto ni Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia,Benjamin Mkapa wa Tanzania na  Festus Mogaye wa Botswana wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  wa pili kutoka kulia pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin Mkapa akitoa mada katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda kulia akiwa katika mkutano huo pamoja na marais wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu wa Nigeria Mh. Olusegun Obasanjo.

Thursday, July 30, 2015

LOWASSA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA LEO


Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. Picks zote za issamichuzi
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.  
Rabsha za hapa na pale zilikuwepo kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya CHADEMA  yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu wakati alipofika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho tayari kwa kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalim akizungumza jambo katika kikao kifupi ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwenye makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akisisitiza jambo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwanahabari, Said Kubenea wakati akiwasili kwenye Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe na wa pili kushoto ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akitoa ufafanuzi wa kisheria wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi fomu ya kuwania Urais wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa.
 Sehemu ya Viongozi mbali mbali wa CHADEMA wakiwa kwenye shughuli hiyo.
 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akifafanua jambo.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fedha za kuchukulia Fomu ya Kuwania Urais kutoka kwa WamaCHADEMA waliojitolea kumlipia.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache mara baada ya kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 People'ssssss..........
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akizungumza machache.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu kwa wanaCHADEMA waliofurika kwa wingi kwenye Makao Makuu ya CHADEMA leo. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, Mama Regina Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar, Salum Mwalim.