Thursday, March 31, 2016

BARABARA YA KIGOMA-NYAKANAZI KUKAMILIKA MWEZI MEI.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kigoma tayari kuanza ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika mikoa ya ukanda wa magharibi.
2Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) kuhusu ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na China Railway 50 Group.
3Ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 inayojengwa na Kampuni ya  China Railway 50 Group ukiendelea.
4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa ujenzi wa kampuni ya China Railway 50 Group baada ya kukagua mitambo yao ya kupima na kutafiti udongo kabla ya kujenga barabara.
5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa kofia) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu mara baaada ya kukamatwa kwa vijana wawili (waliokaa chini) kutokana na wizi wa nyaya za mkongo wa taifa, mkoani Kigoma.
6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa koti la kaki) akiangalia athari za mmonyoko wa udongo zilizoathiri mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Kidahwe mkoani Kigoma.
……………………………………………………………..
Makandarasi wanaojenga barabara ya Kidahwe-Kasulu Km 50 na Kibondo-Nyakanazi Km 50 wametakiwa kukamilisha ujenzi huo mwezi Mei mwakani badala ya Novemba ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara za lami.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo uliyogawanywa sehemu mbili, Kidahwe-Kasulu inayojengwa na China Railway 50 Group na Kibondo-Nyakanazi inayojengwa na Nyanza Road Works.
Prof. Mbarawa amewataka makandarasi hao kuongeza kasi ya ujenzi, vifaa na  wafanyakazi wenye sifa ili barabara hizo zikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Tutahakikisha ifikapo Juni mwaka huu tutakuwa tumelipa madeni yote mnayoidai Serikali hivyo fanyeni kazi kwa uhakika kwa kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano tayari tumeshawalipa makandarasi zaidi ya shilingi bilioni 725”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kwamba nia ya Serikali ni kuifungua mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa kwa barabara za lami ili kufungua ukanda wa magharibi mwa nchi kibiashara kutokana na ukanda huo kuwa sehemu muhimu ya nchi katika uzalishaji na kiungo kikuu kwa nchi za Congo DRC, Burundi na Rwanda.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), kulinda miundombinu ya reli na kujiepusha na vitendo vya hujuma ili kuliwezesha shirika hilo kupata shehena kubwa ya mzigo kufuatia wadau mbalimbali kuonesha nia ya kusafirisha mizigo kwa njia ya reli.
“Serikali imewekeza vya kutosha katika Shirika la Reli hivyo mfanye kazi kibiashara ili mpate mzigo mkubwa wa kusafirisha”, amesisitiza Prof. Mbarawa
Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma na taasisi zilizo chini ya wizara yake Prof. Mbarawa amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuzuia uvamizi na uhujumu wa miundombinu ya barabara, reli, na mkongo wa taifa wa mawasiliano na wote watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua za haraka na za kisheria.
Prof. Mbarawa ametoa wiki moja kwa taasisi zilizo chini ya wizara yake kuhakiki wafanyakazi ili kubaini kama kuna wafanyakazi hewa.
Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa wa Kigoma umejipanga vizuri katika kudhibiti uvamizi wa miundombinu ya barabara na wale waliojenga ndani ya mita 22 kwenye barabara kuu wataondolewa maramoja bila kulipwa fidia.
Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya kukagua miundombinu katika mikoa ya kanda ya magharibi ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa uiboreshaji wa miundombinu ya kanda hiyo ili kuiwezesha kufanya biashara kiurahisi na mikoa mingine ya Tanzania na nchi za Congo DRC, Rwanda na Burundi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AFPIF 2016

IMG_7655
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. (Picha naModewjiblog)
Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika bara la Afrika.
Amesema taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji wa mitandao kwa bara zima la Afrika.
“Tunatambua kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika huduma ya intaneti.
Amesema kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani wataboresha huduma kwa wateja.
“Nchi yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.
IMG_7593
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
IMG_7596
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary, Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
IMG_7603
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.
IMG_7613
Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30 – Septemba, 1
IMG_7617
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7629
IMG_7631
IMG_7645
IMG_7622
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7667
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

“KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUFUTA HATI MILIKI YA ECO ENERGY”


 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injinia Ramo Makani kulia akiteta
jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili,Ardhi na Utalii,Meja Jenerali
Gaudance Milanzi katikati kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wa Shirika la
Hifadhi za Taifa(TANAPA),Ibrahim Mussa wakati wa ziara ya siku moja ya
kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utalii kwenye hifadhi ya Taifa ya
Saadani,
Wajumbe wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii wakiingia kwenye hifadhi ya
Taifa ya Saadani jana

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii Atashasta
Justus Nditiye akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kuitembelea
hifadhi ya Taifa ya Sadani wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa kamati
hiyo,Marry Chatanda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Injia Ramo Makani akizungumza wakati wa ziara hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa (TANAPA),Ibrahim Mussa akizungumza wakati za ziara ya kamati ya Bunge
Maliasili,Utalii na Ardhi Mazingira ilipotembelea hifadhi ya Taifa ya
Saadani.

Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Meja Jenerali Gaudance
Milanzi akizungumza wakati za ziara ya siku moja ya Kamati ya Bunge ya
Maliasili,Utalii na Ardhi

 Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Tanapa,Mtango Mtaniko akizungumza
wakati wa ziara ya kamati ya Bunge Maliasili,Utalii na Ardhi walipofanya
ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mjumbe wa Kamati ya Bunge Maliasili,Utalii,Ardhi na Mazingira,Pauline Gekule
akiulizwa swali wakati ziara hiyo

MJUMBE wa Kamati ya Bunge,Maliasili,Ardhi na Utalii,Shabani Shekilindi ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga akiuliza swali wakati wa ziara hiyo

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini,Marry Chatanda ambaye pia  ni mjumbe wa kamati
hiyo akichangia hoja kwenye ziara hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudance Milanzi kulia akiteta jambo na Meneja wa Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete wakati kamati ya Bunge Maliasili,Ardhi na Utaliiwalipotembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani
Picha kwa Hisani ya Tanga Raha Blog