Tuesday, January 27, 2009

LIUMBA NA WENZAKE WAPANDISHWA KISUTU


Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kwamba yule Mkurugenzi maarufu wa BOT na siyo BoT pekee bali katika meeneo mengine Amatus Liumba na wenzake mwenzake tayari wako wawili wameshafikishwa eneo la viwanja vya mahakama ya Kisutu wakiwa katika gari la Takukuru wanasubiri kuingizwa ndani ya mahakama muda mchache ujao.

Aliwahi kuhojiwa na Takukuru muda mrefu kuhusiana na mambo ya ajira zisizofuata taratibu

Chuo Kikuu Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa huo Kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea Chuo hicho Januari 26,2009. Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo,Profesa Idriss Kikula. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi na kuliakwake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe.

Mbunge mpya huyu Mbeya vijijini


Mshindi wa kiti cha Ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini, Mchungaji Luckson Mwanjali (wa pili kushoto), akipongezwa na baadhi ya wapiga kura wake jana, mara baada ya matokeo ya awali yasiyo rasmi kuonyesha kuwa ameshinda katika uchaguzi wa jimbo hilo uliofanyika jumapil kwa kuvishinda vyama vya CUF na SAU. Picha na Emmanuel Herman

Monday, January 26, 2009

mambo yamebadilika

HEBU cheki mvua inavyofanya mambo hapa ni katikati ya jiji leo mchana ni Kariakoo karibu na shule ya Uhuru ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema mvua zinazonyesha sasa katika ukanda wa Pwani sio za vuli bali ni za mda mfupi na zitaishi hivi karibuni..

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Philbert Tibaijuka, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa mvua hizo zitaisha kesho.

“Hali hii siyo ya kudumu itachukua takriban siku tatu, hivyo ningependa wananchi watambue kuwa hizi siyo mvua za msimu wala vuli,” alisema Tibaijuka na kubainisha kuwa hali hiyo hutokea kila mwaka katika ukanda wa Pwani na Maziwa Januari na Februari.

Alisema mvua hizo zimesababishwa na matukio mbalimbali ikiwamo mfumo unaoandamana na mfumuko wa hali ya hewa unaosababisha upande mmoja wa pepo za Kaskazini Mashariki kukosa nguvu.
“Kumekuwepo na upungufu wa mgandamizo wa hali ya hewa kuanzia Arabia mpaka kaskazini mwa Bahari ya Hindi hali ambayo imesababisha kupungua kwa upepo katika maeneo hayo na mvua kufanyika katika eneo ambalo ni jirani na mwambao wa Pwani ya Tanzania,” alisema

Friday, January 23, 2009

Rais Barack Obama- Atia saini amri ya kufungwa kwa Gereza la Guantanamo

Rais Barack Obama-Siku ya tatu tangu kuapishwa rais wa Marekani.
Rais Barack Obama-Siku ya tatu tangu kuapishwa rais wa Marekani.
Ni siku ya pili tangu kuanza kazi yake ikulu ya White House, kama rais wa Marekani. Na tayari Rais Barack Obama amekuwa na shughuli nyingi tangu kuapishwa kwake siku ya Jumanne.
Lakini suala ambalo limezua hisia kote ulimwenguni ni ile hatua iiliyotarajiwa ya kuitia saini hii leo amri ya kulifunga gereza la Guantanamo.
Nitalifunga gezera la Guantanamo ni kiwa Rais, na kweli ahadi hiyo sasa imetimia pale Rais Barack Obama hii leo kutia saini amri ya kulifunga gereza hilo hii, ambalo limekuwa kero kwa wengi duniani tangu lifunguliwe mwaka wa 2002.
Tangu atoe tangazo la kusimamishwa kwa muda wa siku 120 kwa mashtaka yote ya watuhumiwa wanaozuiliwa katika gereza hilo,na hatimaye kutiwa saini kwa amri hiyo hivi leo, maswali mengi yameibuka kuhusu nini hatima ya watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakizuiliwa kwa miaka kadhaa bila kufikishwa mahakani.
Rais Obama anaelekea kutimiza moja wapo ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeini, ambapo miongoni mwa yaliyomo kwenye amri hiyo, ni kufanyiwa marekebisho utaratibu wa idara ya ujasusi wa kuwazuia na kuwahoji watuhumiwa na hivyo kuekewa mipaka utaratibu wa kuhojiwa katika magereza yote yanayosimamiwa na Marekani kote ulimwenguni,mbali ya maeneo ya kijeshi. Jengine ni kjuzuiwa kwa shirika ujasusi kuwazuwia kwa siri wafungwa wa ugaidi katika jela za nchi nyengine.

Taka ngumu


Wakazi wa Mji wa Morogoro wakipita kwa shida kandokando ya barabara ya Makongoro huku wakikwepa takataka zilizozagaa ovyoo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kuzolewa na wafanyakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. (Picha na Juma Ahmadi, Morogoro).

LAURENT NKUNDA ARRESTED


Gen Laurent Nkunda, the leader of the largest rebel group in the eastern Democratic Republic of Congo, has been arrested, the military says.

He was arrested as he fled into Rwanda while trying to resist a joint Rwandan-Congolese military operation, the operation's joint command said.

Some 3,500 Rwandan troops entered DR Congo on Tuesday to help government forces disarm Rwandan Hutu FDLR rebels.

Gen Nkunda has been leading the rival CNDP Tutsi insurgency.

He has, says the BBC's Africa analyst, Martin Plaut, been caught in the rapidly changing diplomatic situation in Central Africa.

Gen Nkunda had been Rwanda's ally in eastern DR Congo - a Tutsi, he guarded their Western flank against attacks from the Hutu forces who fled there after the Rwandan genocide of 1994.









Thursday, January 22, 2009

ATCL yaanza kazi bila Sh5 bn



SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) linaanza tena kutoa huduma za usafiri leo huku likiwa halijapatiwa Sh5.1 bilioni lilizoomba ili liweze kuendesha shughuli zake kikamilifu.

Kuanza kwa huduma hizo leo kunatokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa Ijumaa iliyopita la kuamuru menejimenti ya ATCL, Wizara ya Miundombinu pamoja na Hazina kuhakikisha shirika hilo linarudisha huduma zake haraka iwezekanavyo.

Utekelezaji wa agizo hilo umekuja siku saba tangu lilipotoplewa Ikulu na rais mbele ya viongozi wa Wizara ya Miundombinu baada ya menejimenti ya ATCL kumueleza sababu zilizochangia kufungiwa kutoa huduma na Mamlaka ya Udhibiti wa Safari za Anga (TCAA) Desemba 8, mwaka jana.

Licha ya ATCL kurejeshewa leseni yake siku 23 baadaye na serikali kulipatia Sh2.5 bilioni, shirika hilo lilishindwa kuanza tena safari zake kutokana na kukabiliwa na mzigo wa madeni. Lilikuwa likihitaji Sh7.1 bilioni ili liweze kurejkesha huduma zake kama ilivyokuwa awali.

Wednesday, January 21, 2009

Obama na mambo yake




WASHINGTON – President Barack Obama and Congress tackled the troubled economy on Wednesday, weighing tactics for fixing the struggling financial industry and pushing ahead with a massive economic recovery package of new spending and tax cuts.
Obama, in his first full day in office, planned to meet with his White House economic advisers. On Capitol Hill, Timothy Geithner, Obama's nominee for secretary of the Treasury, told senators the country needs a "forceful course" to meet the economic crisis.
The president assumes office with access to the remaining half of a $700 billion financial bailout fund, and with Congress eager to get him a stimulus plan worth at least $825 billion within the next three weeks. In a sobering welcome to the president, stocks plunged Tuesday amid fears that governments would be forced to take over wobbly banks. Financial stocks rebounded Wednesday morning.
With a Congress that so far has acquiesced in his strategies, the combined rescue and stimulus tools would give Obama extraordinary resources to confront the recession.
A House committee was ready to put the final touches on much of the spending side of the stimulus plan, readying that portion of the bill so the House can consider the entire package next week. The House also planned a vote Wednesday afternoon on legislation setting goals and conditions for spending the financial rescue money, provisions that the Obama administration has already embraced.

ajali mbaya arusha






pichani ni Mwanajeshi mmoja ambaye hakujulikana ni wa kikosi gari akiwa anasambaza watu waliokuwa wamefurika katika eneo la ajali na hivyo kuzuwia uokowaji, na awali polisi walikuwa wakipata taabu kufukuza watu hao.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Rober Boaz akiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru katika eneo la ajali hiyo jana.

pichani ni gari aina ya Scania likijitahidi kulivuta basi dogo la abiria mara baada ya ajali hiyo ili kuendelea na ukowaji watu jana jioni.

picha zote na mussa juma


WATU 15 wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa vibaya baada ya magari matano kupata ajali katika daraja la mto Nduruma wilayani Arumeru jana mchana na moja kutumbukia ndani ya mto.

Tukio hilo la aina yake, ambalo lilisababisha kufungwa kwa barabara ya Arusha- Moshi kuanzia majira mchana hadi saa 12 jioni lilisababishwa na magari hayo kukutana katika daraja hilo jembamba na gari moja ya abiria kukosa breki.

Katika ajali mbaya iliyoyahusisha magari matano na kuthibitishwa na Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha, Robert Boaz chanzo kamili cha ajali kilikuwa bado hakijajulikana licha ya kuelezwa ni gari dogo la abiria kukosa breki na kuanza kuparamia mengine.

Magari ambayo yalihusika katika ajali hiyo, ni basi la abiria aina ya Fuso la kampuni Lim Safari lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi.

Jingine ni Land Rover lililokuwa linatoka Tengeru kuja Arusha, gari dogo la abiria lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi, Scania lililokuwa na shehena ya chupa za soda. Habari na Mussa Juma wa Arusha

Monday, January 19, 2009

Mambo magumu chuo kikuu



JESHI la polisi limelazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyokuwa yameandaliwa na serikali ya wanafunzi iliyoripotiwa kutotambuliwa chuoni hapo (DARUSO).

Maandamano hayo yaliandaliwa kwa lengo la kupinga utaratibu wa udahili unaoendelea kwa kuwarudisha wanafunzi ambao wamekamilisha malipo yao yote.

Mwananchi ilishuhudia wanafunzi wakiwa nje ya chuo wakijiandaa kuandamana huku wakiwa wameshika mabango yanayochochea maandamano, huku wengine wakiwa wanaendelea na udahili kama kawaida.

"Tumeamua kuandamana leo uongozi uone wenyewe kwamba unachokifanya sio halali kwani kumrudisha kuendelea na masomo mwanafunzi mwenye uwezo na kumuacha asiye na uwezo ni sawa na ukandamizaji,"walisikika wanafunzi hao wakiwa wameshikilia mabango tayari kwa maandaamano." Habari ya Hussein Issa na Picha ya Emmanuel Herman.

Sunday, January 18, 2009

Katuni ya leo


Zimbabwe mambo magumu


The Mabvuku well is mid-way between Ruwa and Harare, and is being used by thousands of residents there from 4am until late at night – it’s a source far from any sewage leaks but under strain with the demand being placed on a limited resource.
The rainy season is starting here. It’s a mixed blessing because rains are desperately needed for crops to feed the hungry, but rain water flowing through the streets, mingling with overflowing sewage, will cause havoc to open wells that are the residents’ only lifeline to water. Photo by Sokwanele.

Habari ya Zimbabwe


The picture shows sewerage flowing through TC Hardy High School and Chiremba Primary School. Fortunately the schools closed on the 4th of December, so children are not being ‘educated’ in the close vicinity.

But if they had still been there (and if the education system hadn’t totally collapsed already) young vulnerable people would be directly in the disease’s sights. (Photo by Sokwanele)

safari ya Obama

. U.S. President-elect Barack Obama (R) and his wife Michelle wave to the crowds gathered along the train tracks in Claymont, Deleware January 17, 2009, on his whistle stop train trip to Washington DC


U.S. President-elect Barack Obama (R) waves to the crowds from the back of a train as they roll past the station in Claymont, Delaware, January 17, 2009.

Kila mtu ni bilionea Zimbabwe


Benki kuu ZIMBABWE imetoa noti ya Bilioni HAMSINI ambayo yaweza kununua magazeti matatu tu ya siku.

Kila mutu ni bilionea nchini Zimbabwe
Last week the country's central bank began circulating Z$10, Z$20 and Z$50 billion notes - but they are no longer sufficient. A political deadlock between President Robert Mugabe and opposition leader Morgan Tsvangirai over power-sharing has done little to help Zimbabwe's failing economy.

The country is also in the grip of a cholera epidemic with food and petrol prices doubling every day.Zimbabweans often have to line up for hours outside banks to withdraw barely enough cash to buy a loaf of bread.

An official estimate put inflation at 231,000,000% in July - but some experts now believe it is much higher.In addition to the Z$100 trillion note, the Reserve Bank of Zimbabwe plans to launch Z$10 trillion, Z$20 trillion and Z$50 trillion notes, the Herald newspaper reported.

A local collects food aid But new bank notes issued in the past have done little to help the spiralling cost of living. Many blame the dire state of the economy on mismanagement by Mr Mugabe's government.

Thursday, January 15, 2009

Mwanahalisi latoka kifungoni



Gazeti la wananchi- MwanaHALISI limerejea tena mitaani baada ya kumaliza kile kilichoitwa na watawala, "Kifungo." Pata uhondo wake.

Wednesday, January 14, 2009

Kigogo wa Richmond aburuzwa kortini



SASA ni dhahiri kwamba, serikali ya Rais Jakaya Kikwete haina mzaha katika kushughulikia tuhuma za ufisadi baada ya kumfikisha mahakamani mfanyabiashara, Naeem Adam Gire kujibu shtaka la kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu uwezo wa Kampuni ya Richmond.

Tayari serikali imeshawafikisha mahakamani watuhumiwa 21 kwenye sakata la wizi wa jumla ya Sh133 bilioni, mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu wa wizara kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi; na jana ilikuwa zamu ya kashfa iliyoitikisa nchi mwaka jana kuhusu utoaji wa zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond.

Kashfa hiyo, iliyoingia hadi ndani ya Bunge la Muungano, ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata hilo. Baadaye mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, nao waliachia ngazi.

Jana, Gire alipandishwa kizimbani majira ya saa 9:00 alasiri kujibu tuhuma za kueleza uongo kuwa Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, Wariyalwande Lema, Gire alisomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Boniface Stanslaus ambaye alidai kuwa Machi 13 mwaka 2006 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alighushi nyaraka akionyesha kwamba, Mohamed Gire, ambaye ni mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani, alisaini kumruhusu Naeem Adam Gire kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini.

Tuesday, January 13, 2009

hali mbaya mafuta



Mafuta yameadimika kwenye vituo vingi jijini Dar es Salaam tangu mwishoni mwa wiki, ikiwa ni siku chache baada ya mamlaka inayohusika na nishati hiyo, Ewura kutangaza bei elekezi ambayo ni chini ya bei iliyokuwa inatumiwa na wauzaji wa mafuta.

Ewura ailitangaza kuwa mafuta aina ya petroli yauzwe hadi Sh1,166 kwa lita na dizeli iuzwe kwa Sh1,271 kwa lita tofauti na bei za awali za Sh1,450 hadi Sh1,600 kwa lita ya petroli na Sh1,300 hadi Sh1,500 kwa lita ya dizeli. Bei hiyo elekezi ndiyo iliyozua kasheshe tofauti, ikiwa ni pamoja na upungufu wa ghafla.

Kutokana na agizo hilo wafanyabiashara wa mafuta huenda wanafanya uharamia na sasa hali imezidi kuwa mbaya jana wakati vituo vingi zaidi vipositisha huduma hiyo na kusababisha kuwepo kwa misululu mirefu kwenye vituo vilivyokuwa vikiuza na hasa kituo cha BigBon kilicho Kariakoo, ambako magari yalipanga mstari mrefu iliyokuwa pembeni ya mistari ya watu waliobeba madumu.

Sehemu nyingine ambako mafuta yalikuwa yakiuzwa ni kituo cha Gapco kilicho Victoria, Mikocheni na vituo vya Engen. Vituo vya Gapco (Banana Ukonga), Oilcom (Ukonga Madafu), Oilcom (Mzambarauni), BP (Uwanja wa Ndege) na vingine vingi vilivyo wilayani Ilala havikuwa na huduma hiyo.


Monday, January 12, 2009

Wauza mafuta waanza mgomo


HALI ya upatikanaji wa mafuta jijini, hasa petroli, inazidi kuwa mbaya kutokana na vituo vingi kutouza bidhaa hiyo kwa kile kinachoonekana kuwa, ni njama za waziwazi za wafanyabiashara ya mafuta kuikwamisha serikali kudhibiti upandaji holela wa bei ya nishati hiyo.

Lakini Wizara ya Madini na Nishati imesema inasubiri kupata taarifa kutoka kwa watendaji leo asubuhi, kabla ya kuanza kuchukua hatua kwa wote waliokiuka sheria iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuhusu bei elekezi za mafuta, kwa mujibu wa naibu waziri kwenye wizara hiyo, Adam Malima.

Mafuta ya dizeli ndiyo yanayopatikana bila ya shida kwenye vituo vingi na inauzwa kwa bei iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura). Katika kile kinachoonyesha kutii agizo la Ewura, vituo hivyo vilivyokuwa vikiuza dizeli pekee, vimeweka mabango yanayoonyesha kuwa petroli inauzwa kwa bei ya Sh1,233 ikikaribiana na ya Ewura, ingawa inakuwa haiuzwi.

Hayo yametokea wakati Ewura imetangaza bei mpya ya nishati hizo kwa mikoa 21 ya bara, ikiwa imeongeza senti kadhaa kwenye bei ya awali.

Mgomo huo baridi ulisababisha vituo vichache vilivyokuwa vikiuza petroli kwa bei ya Ewura kufurika magari mengi na watu wenye madumu kwa ajili ya kununua petroli ya ziada, katika wiki ambayo bei ya mafuta katika soko la dunia imezidi kuporomoka na kufikia chini ya dola 39 kwa pipa.

Ewura imewataka wauzaji wa bidhaa hiyo kuuza petroli kwa Sh1,166 kwa lita, ingawa vituo vinavyouza bidhaa hiyo vimekuwa vikiuza kwa Sh1,233 kwa lita, tofauti na bei ambayo ilikuwa ikitumiwa awali na wafanyabiashara hao ambayo ilikuwa kati ya Sh1,450 na Sh1,600 kwa lita ya petroli.

sherehe za mapinduzi



Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume akitoka kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar . Sherehe hizo zimefanyika leo katika uwanja wa michezo wa Gombani uliopo mjini Chakechake Pemba . Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Sunday, January 11, 2009

Buriani Casian Malima




MWILI wa aliyekuwa Mhariri wa HabariLeo, Cassian Malima (44) utaagwa kesho na
kusafirishwa kesho kutwa kwa maziko mkoani Mara, imefahamika.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Emmanuel Malima, marehemu Cassian ambaye alifariki
dunia juzi katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, ataagwa nyumbani kwake
Savannah, Tabata Mawenzi, kesho kuanzia saa 5 asubuhi.

Alisema baada ya shughuli hizo, mwili huo utapelekwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, tayari kusafirishwa Jumanne kwenda Musoma, ambako
atazikwa Jumatano.

watu 27 wafariki dunia Tanga



MJI wa Tanga na maeneo mengine ya jirani, jana yalizizima kwa majonzi yaliyotokana na ajali ya basi la Kampuni ya Tashriff, iliyosababisha watu 27 kufa papo hapo na wengine 23 kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea saa 2.30 usiku wa juzi, katika eneo la mji mdogo wa Hale wilayani Korogwe, barabara kuu ya Segera-Tanga.

Habari zilisema majeruhi za wawili wa ajali hizo ni mbaya mno na wamelazwa katika Hospitali ya Teule ya Muheza.

Kwa mujibu wa habari hizo, ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Tanga.

Basi hilo aina ya Isuzu, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina
moja tu la Mdoe au kwa kwa jina la utani la Osama.

Inasemekana katika ajali hiyo, basi hilo, lililivaa kwa upande wa kushoto, lori lililokuwa limeba magogo na kuegeshwa kandakando mwa mwa barabara.

Kwa mujibu wa maelezo ya watu walioshuhudia, magogo hayo yaliwakumba abiria waliokuwa wameketi kuanzia kiti cha kwanza hadi cha mwisho katika basi la Tashriff na baadhi ya abiria waliokuwa wamesimama tayari kwa kushuka katika kituo cha Hale.

Thursday, January 08, 2009

Sophia Simba mwenyekiti UWT


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa taifa wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT).
Akitangaza matokea ya uchaguzi huo, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Seif Khatibu alimtangaza Simba kuwa alikuwa amepata kura 470 sawa na asilimia 54.5 ya kura zote zilizopigwa na kuwaacha washindani wake, Janet Kahama aliyepata kura 383 sawa na asilimia 48.4 na Joyce Masunga aliyeambulia kura 10 sawa na asilimia 1.1 kati ya kura halali 862 zilizopigwa.

Nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti ilikwenda kwa Asha Bakari Makame ambaye alikuwa mgombea pekee, aliyepata kura 736 sawa na asilimia 60.3 na kura 70 zilimkataa.

Kwa upande wa wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania bara walioshinda ni Betty Machangu, Magret Mkanga, Sifa Swai, kutoka Zanzibar ni Ratifa Nasoro, Subira Ally, Mtumwa Yusufu, Lilian Limo na Catherin Nao.

Kwa upande wa wawakilishi wa jumuiya za CCM walioshinda na Martha Mlata ambaye atakuwa ni mwakilishi kwa Jumuiya ya wazazi na upande wa vijana alichaguliwa Shy-Rose Bhanji ambaye alimshinda mbali mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Halima Dendego.

Mountain Dew Ride





Launch of the new pepsi drink, Mountain Dew a bright yellow drink and semi opaque in Kampala November 23, 2008. Piga http://www.ugandaonline.net/

Wednesday, January 07, 2009

Kilimanjaro Stars yatisha Kampala


IKICHEZA soka safi na la kujiamini lililowalazimisha Waganda kuishangilia, Kilimanjaro Stars ilitandika bila huruma Rwanda kwa mabao 2-0 na kujisafishia njia, wakati wapinzani wa Uganda wakisambaratisha Somalia 4-0.
Ushindi huo umeifanya Stars kufikisha pointi sita na kuongoza kundi kwa muda, huku kiungo wake, Athuman Idd akinyemelea ufungaji bora kwa mabao mawili aliyonayo.
Stars ambayo ilianza mchezo huo kwa kushambulia kwa nguvu, iliandika bao la kwanza dakika ya nane kupitia kwa winga wake Mrisho Ngassa ambaye alipiga 'tiktak' iliyogonga besela na kutinga wavuni.
Rwanda ambayo ilicheza soka la pasi nyingi fupi fupi na kushambulia kwa kushtukiza, ilijipanga na kupandisha shambulizi kali dakika ya 10 na kupangua ukuta wa Stars, lakini Lomani Jean akachachawa na kupaisha.
Washambuliaji wa Stars walizidi kuishambulia Rwanda, ambapo dakika 23 Henry Joseph alipiga shuti kipa akatema, lakini Mrisho Ngassa akaichelewa kumalizia.
Stars ambayo wachezaji wake walikuwa wakikaba kwa nguvu, kwa kujiamini na kutowapa nafasi Rwandakukaa na mpira, ilizidi kushambulia huku wachezajiwake wakionana vizuri na kuandika bao la pili dakika ya37 kupitia kwa Athuman Iddi 'chuji'.Taarifa ya Michael Momburi.

Mkutano wa UWT


Mke wa Rais Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,Maria wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Saba wa Jumuiya ya wanawake Tanzania(UWT) katika ukumbi wa kilimani mjini Dodoma jana. Picha na Jube Tranquilino

Monday, January 05, 2009

Bandari ya Dar es Salaam


Bandari ya Dar es Salaam kama inavyoonekana kwa juu watu wana fweza si mchezo magari kibao.

Mboma: Kitambi kimeniangusha

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.

Alisisitiza kuwa anaamini kilichochangia kutopata kura nyingi zaidi ni kitambi
hicho alichokuwa nacho na kwamba hali hiyo itamkomaza kisiasa.

Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini. alisema kkuanguka kwake katika jimbo hilo kumetokana
na wananchama wa chama hicho kumnyima kura.Imeandikwa na Hawa Mathias kutoka Mbeya

Mwinyi azindua kampeni kama baba wa taifa



RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye Chadema iliilitishia kumchafua kama angekubali kuzindua kampeni za uchaguzi za CCM mkoani Mbeya, jana alijivisha jukumu la Baba wa Taifa wakati alipotumia muda mwingi wa hotuba yake kuelezea umuhimu kwa wananchi kumchagua mtu anayeona anafaa kwenye jimbo hilo, badala ya kumpigia debe mgombea wa CCM.

Mwinyi, ambaye anajulikana kama 'Mzee wa Ruksa' kutokana na kuongoza nchi wakati wa mageuzi yaliyoruhusu ushindani wa vyama vya kisiasa, hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini.

Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi.

Mwinyi alisema vyama vyote vya siasa nchini lazima vilenge katika kutoa majibu ya kisera kwa matatizo yanayowakabili wananchi ili kuwaletea maendeleo yakayowafanya kuwa na maisha bora.

Alisema kuwa moja ya sababu kubwa za kuanzisha siasa ya vyama vingi ni kuwapa
wananchi fursa ya kushindanisha sera za vyama mbalimbali ili wananchi waweze
kuchagua sera wazipendazo na viongozi wa kuziwasilisha, kuzitetea na kuzitekeleza.

Friday, January 02, 2009

Ndanda Kossovo




Jamaa hili liko fiti ile mbaya limereje na watoto wa Tembe zamani lilitesa saana katika katika kundi la FM Academia kisha likatokomea kule Marekanmi na sasa yupo Dar huyu si mwinginen ni Ndanda Kossovo 'Kichaa"

masikini chadema

VIONGOZI na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana waliachwa wakitafakari cha kufanya baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutupilia mbali rufaa ya mgombea wao kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini.
Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu. Mgombea huyo hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Lakini jana, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo.
"Siwezi kueleza chochote kwa sasa kwa sababu tunahitaji kufanya consultations (mashauriano)," alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipotakiwa kuzungumzia hatua inayofuata baada ya Jaji Makame kutangaza uamuzi huo, habari hizi katupasha Brandy Nelson kutoka Mbeya.



Walahi mabata ushungu miye





Wananchi wa kule Tabata wakijimwaga katika ukumbi wa Da West Night Park wakifanya mavitu yao wallahi ilikuwa babu kubwa hata Peres Mwangoka alikuwapo na akatutwangia picha hizi aisee ilikuwa balaaa wacha sijui wewe ulikuwa wapi hebu nieleze mwenzangu.