Sunday, November 29, 2009

Nondozzzz SAUT Mwanza



Mzee wa Mshitu,Kadago, Sanga

Frank Sanga, Mkuu Theophil Makunga, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow na mzee wa Mshitu.

Kutoka kushoto Joyce Bazira, wa nne kutoka kushoto Mary Mwanjelwa, Mhariri Mtendaji, Theophil Makunga, wa pili kutoka kulia Evelyn Mpasha na wa kwanza kulia Bujaga Izengo Kadago Mahafali hayo yamefanyika jana Malimbe Campus Sain Augustine University of Tanzania (Saut).

Mzee wa Mshitu Yahya Charahani akiwa amekula nondooozz za Masters of Arts in Mass Communications (MA Mass Communications) jana wengine katika picha hiyo ni Mhariri wa Mwanaspoti, Frank Sanga, Mhariri wa Makala Hawra Shamte.

Kutoka shoto ni Abdul Njaidi, fred Maro na Eveline Mpasha katika picha ya pamoja mara baada ya kula nondozzz zao za uzamili katika mawasiliano ya umma ( Master of Mass Communication) katika wa mahafali ya 11 ya chuo kikuu cha Mt. Augustino (SAUT) ambapo Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

Friday, November 27, 2009

Five students for Youth Leadership Program in the U.S.


U.S. Embassy Public Affairs Officer Ilya Levin with five secondary school students and a teacher who are to travel to the United States for a four-week study tour under the Youth Leadership Program. The four-week program, sponsored by the American people through U.S. Department of State, will take place in Denver and Washington D.C. from November 29 through December 22, 2009.
From left: Mustapha Said Rashid (form 1V) - Makong’onda Day Sec. School – Masasi; Kornel Rainery Mbele (form IV) - Hagati Secondary School – Mbinga, U.S. Embassy PAO Levin; Kassimu Lukindo Sengasu – District Secondary Education Officer, Muheza, Tanga; Herieth Heriel Ringo (form III) – Kaloleni Secondary School- Arusha; Mwajuma Ali Ali (form III) - Nungwi Secondary School – Zanzibar, and Agnes Kassian Machaninga (form IV) - Philip Mangula Secondary School- Njombe. (Photo courtesy of the American Embassy)

Sunday, November 22, 2009

Busta Rhymes ndani ya Tamasha la Fiesta





Tamasha kubwa la burudani la Fiesta 2009 limefanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam ambapo mwanamuziki wa Hip Hop kutoka nchini Marekani, Busta Rhymes na wasanii wa hapa nchini walitumbuiza na kukonga nyoyo za mshabiki waliofurika kama nyuki.
Katika onyesho hilo busta alionesha uwezo mkuwa wa kuliteka jukwaa wakiwemo na hata mashabiki kwa kiasi kikubwa, mbali ya kamuzi hilo Busta ameisifu Tanzania na watu wake akisema ni watu wazuri wakarimu na kuongeza kuwa amefurahishwa sana na umati wa watu uliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta One Love 2009.

Friday, November 20, 2009

Madaktari wapya haaao IMTU






Wanafunzi wa Chuo kikuu Cha Madaktari IMTU cha Dar es Salaam, wakiapa kiapo cha utii wa utekelezaji wa maadili ya taaluma hiyo, kabla ya kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu digrii ya udaktari na upasuaji, wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam juzi, Picha nyingine inamuonyesha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Jumanne Maghembe akiwa na Maprofesa wengine wa chuo hicho.Picha na Said Powa.

Thursday, November 19, 2009

Kombe la dunia lawasili nchini






Kombe la Dunia la fifa na Coca-Cola limewasili jioni hii na kupelekwa moja kwa moja kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kombe hilo liliwasili nchini majira ya saa 10:30 jioni na kupokelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendela kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa.

Kombe hilo lilopo kwenye safari ya kuelekea Afrika Kusini ilikuwa hapa nchini kwa siku mbili, leo walitakuwa visiwani Zanzibar na kesho Jumamosi ilitakuwa uwanja wa Taifa na kushudia na mashabiki mbalimbali wa mchezo wa soka hapa nchini.

Watu waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege walibaki wakiduwa wasijue nini kinaendelea baada ya ndege kuwasili, na kushitukia tayari limeshangia kwenye magari maalumu yalioandaliwa na msafara kuanza ukiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Helkopta.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea kombe hili Rais Jakaya Kikwete alisema kuwasili kwa taji hilo ni jambo la kihistoria, imeleta changamoto kubwa kwenye maendeleo ya michezo hapa nchini.

"Kutwaa Kombe la Dunia ni ndoto ya kila mchezaji na kufika kwa taji hili Tanzania ni bahati ya pekee kwa kutimiza malengo yetu ya soka," alisema.

Rais alisifu uteuzi wa vijana kwenye timu taifa ya Tanzania kwani unasaidia kuibua vipaji vipya ambao wataweza kusaidia nchi siku za usoni.

Wednesday, November 18, 2009

Nnauye ahadharisha wauza 'unga' kufadhili vyama



MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye, amesema vitendo watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kufadhili vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu, vinasababisha serikali inayoingia madarakani kutekeleza matakwa ya wafadhili hao.

Nape alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizundua Chama Kuweka na Kukopa cha Upendo Group ambapo alisema serikali inayochaguliwa kwa njia hiyo itakuwa ya wauza madawa ambao maamuzi yao hayawezi kuleta maendeleo kwa wananchi.

“Hao wauza unga wanapopata nafasi ya kukifadhili chama cha siasa kisha chama hicho kikafanikiwa kuingia madarakani kwa nguvu za pesa zao, serikali ya chama hicho haitakuwa na uwezo wa kuwachukulia hatua watu hao na badala yake, itafanya maamuzi kwa muujibu wa wafadhili hao,”alisema Nnauye.

“Tukumbuke waswahili walisema “anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua tuni ya muziki, wafadhili wa aina hiyo wakifanikiwa kukiweka chama madarakani kwa njia fedha zao, wanaweza kuichagulia serikali mambo ya kufanya kwa mgongo wa fedha zao,” alisema.

Kwa muda sasa, kumekuwa na hoja kuwa vyama vya siasa nchini, vinategemea kupata fedha za kampeni kutoka kwa wafadhili wao bila kujali nyanzo vya fedha hizo na athari zake kwa taifa.

Hata hivyo Nape ambaye alitoa Sh1.2milioni ili kukiwezesha upendo group kufungua saccos yao alisema vyama vya siasa visivyo kuwa makini na watu hao kuna siku vitajutia. Imeandikwa na Jackson Odoyo.

Mama Kikwete ziarani Singida


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akiwa amebeba kibuyu mara baada ya kukabidhiwa na wanawake wa kabila la wataturu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika mkoa wa Singida. Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.Picha na Juma Kengele - Ikulu

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) akisalimiana na mtoto Neema Jackson mwenye umri wa miaka miwili wakati alipotembelea Hospitali ya wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kufungua wodi ya watoto.

Monday, November 16, 2009

Kikwete: Wazee hawana nafasi 2010


Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa kama akijaliwa kupata kipindi cha pili cha kuliongoza taifa la Tanzania, atafanya jitihada kubwa kuubadilisha uongozi wa Tanzania kuwa uongozi wa vijana.

Rais Kikwete pia amesema kuwa vijana ndiyo Tanzania ya kesho, na kama Tanzania haikuwekeza vya kutosha katika vijana na maendeleo yao, basi itakuwa haiwekezi katika hali yake ya baadaye.

Akizungumza jana mjini Dar Es Salaam na vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika wanaoshiriki katika Mpango wa Kulea Uongozi wa Afrika wa African Leadership Initiative, Rais Kikwete amesema kuwa anauthamini Mpango huo.

Amewaambia vijana hao ambao wanashiriki katika Mpango huo unaodhaminiwa na Askofu Mkuu (mstaafu) wa Kanisa la Anglikan Desmond Tutu wa Afrika Kusini kuwa kwa kadri miaka inavyokwenda ni lazima rika la wazee lipishe lile la vijana.

Rais amewaambia vijana hao kwenye mkutano wao katika Hoteli ya Southern Sun mjini Dar Es Salaam: “Kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, kama nitajaliwa na nikapata bahati ya kuchaguliwa tena, nitahakikisha kuwa naubadilisha uongozi wa Tanzania kwa kuufanya uongozi wa vijana zaidi.”

Ameongeza: “Wale viongozi wa rika langu lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi, na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”

Amesisitiza: “Vijana ndiyo matumaini ya nchi hii katika miaka inayokuja, na kama hatukuwekeza katika vijana wetu, basi ni dhahiri kuwa hatuwekezi ipasavyo katika miaka ijayo ya taifa letu.”

Akijibu maswali ya vijana hao kutoka nchi mbali mbali za Afrika zikiwamo Tanzania, Nigeria, Kenya, Afrika Kusini na Uganda, Rais Kikwete amewaeleza vijana hao jinsi gani alivyojikuta anaingia katika siasa.

Akijibu swali kuhusu maendeleo ya karibuni katika siasa za Zanzibar, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba vyama vya siasa katika Zanzibar vimeamua kuachana na siasa na mazoezi ya zamani na kuanza ukurasa mpya. Taarifa ya Ikulu Press ya leo.

Katikati ya jiji la Dar




Eneo hili lipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam ni karibu sana pia na maeneo muhimu ya soko kuu kabidha la bidhaa nchini, lakini hebu cheki maji yanavyotitika h

Sunday, November 15, 2009

Mo Ibrahim: Viongozi Afrika si makini




MMILIKI wa taasisi ya Mo Ibrahim amesema matatizo yote yanayoikumba nchi za bara la Afrika, ikiwemo vita, njaa na magonjwa, yanatokana na viongozi wake kutokuwa makini na kutofuata misingi ya utawala bora.
“Viongozi wetu wengi si makini na pia hawafuati misingi ya utawala bora na kutokana na haya ndio maana bara hili bado lipo nyuma kiuchumi na linasumbuliwa na matatizo ya njaa, magonjwa na vita,” alisema mmiliki huyo, Mo Ibrahim jijini Dar es Salaam juzi katika hafla maalum ya muziki ikiwa ni sehemu ya maadalizi ya mkutano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Milimani City.
Katika mkutano uliokutanisha viongozi mbalimbali kutoka nchi za bara la Afrika, pamoja na mambo mengine walijadili masuala mbalimbali yakiwemo ya mabadiliko ya hali ya hewa, kilimo na maendeleo ya nchi za Afrika.
Mo Ibrahim, ambaye ni milionea alifafanua kwamba viongozi wa nchi za Afrika ni wepesi wa kuzungumza lakini si watendaji katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya wananchi wanaowaongoza.
Alisema kutokana na hali hiyo, Afrika inaonekana ni bara masikini na lenye matatizo mengi ikiwa ni pamoja na vita, njaa na magonjwa. Imeandikwa na Sadick Mtulya.

Siku ya kisukari duniani





Baadhi ya wakzi wa jiji la Dar es Salaam, wakipimwa msukumo wa damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Kisukari duniani, yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja leo. Picha na Zacharia Osanga

Spika Sitta Mkutanoni UN Marekani


Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa wa kudumu wa umoja wa mataifa toka Tanzania Dr. Augustine P. Mahiga mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jana. Spika yupo marekani kuhuduria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU mkutano unaofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akihudhuria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York marekani jana. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Switzand Pascale Bruderer Na Spika wa Bunge la Africa Kusini Max Sisulu.



Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akihudhuria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York marekani jana. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Switzand Mhe. Pascale Bruderer Na kulia ni Mbunge toka wa la Viet Nam Mhe. Ngo Quang Xuan

maafa ya mafuriko


Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya mkondoa wilaya ya Kilosa mkoani wakivua nyuma ya majengo ya shule hiyo baada ya kukumbwa na mafuliko yalisababaisha wanafunzi kukosa masomo kwa siku tatu. Picha na Juma Mtanda

Kwa wale wapenda ulabu tu











Hii imetokea huko Iran ambako Pombe ni kitu haramu! hii ni operation iliyofanyika mitaani ya kuharibu vitu vyote vya aina ya kilevi ilikufanya watu wasilewe. Jamani hapom mpo?Tukio hili limechangiwa sana na imani za KIDINI!!!!!!!

Friday, November 13, 2009

Maafa ya Same katika picha







SIMANZI na vilio jana vilitawala kwenye mazishi ya watu 2O waliofariki dunia kwa kufunikwa na kifusi kilichoporomoka mlimani na kufukia nyumba zao usiku wa manane katika Kata ya Mamba Miamba, wilayani Same, Kilimajaro.
Gazeti hili lilishuhudia watu zaidi ya 1,000 waliokusanyika katika msiba huo mkubwa wakiwa wamefunikwa na simazi, huku wakilia kwa uchungu kutokana na kupoteza ndugu zao katika mkasa huo wa kutisha.
Asilimia kubwa ya watu walionyesha masikitiko yao, hasa kwa familia ambayo imepoteza watu 15 na kati ya hao wanne hawajapatikana mpaka sasa.
Wanachi hao waliiomba serikali iwasaidie kutafuta miili ya watu hao na ikiwezekana watumie kikosi cha mbwa ili kubaini mahali ilipo.
Elineema Shambi, mmoja wa ndugu wa wanafamilia 15 waliofariki dunia na ambaye alinusurika kwa vile alikuwa amekwenda mjini Moshi kwa shughuli za kibiashara, alisema kwa majonzi kwamba amepoteza mke na watoto wake wanne ambao walifukiwa na kifusi hicho.
Alisema alikwenda mjini Moshi kununua bidhaa za kuuza, na kesho yake asubuhi alipigiwa simu na kuondoka mara moja. Alieleza kuwa alipofika alikuta nyumba yake imefunikwa kabisa kiasi cha kutoonyesha kama kulikuwa na nyumba na mwili wa mkewe ulikuwa haujapatikana hivyo akasaidia kuutafuta na kuupata pamoja na miili ya watoto wake.
Alifahamisha kuwa yeye ni mmoja kati ya ndugu wa watu 15 waliofariki katika tukio hilo la kutisha.
Akisimulia juu ya maporomoko hayo, alisema, dalili za mlima huo kuporomoka zilianza kuoneka mwaka jana kwa kuwa kulikuwa na ufa, hata hivyo hakueleza kwamba ni kwa nini hawakuhama katika eneo.
Akiunga mkono maelezo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega alibainisha kuwa wananchi wa Kata ya Mamba Miamba walishaona dalili za kuporomoka kwa mlima ulioua watu 20, tangu mwaka jana, lakini hawakuchukua tahadhari.IMeandikwa na Daniel Mjema na Rehema Matowo kutokea Same.