Sunday, August 31, 2008

Mtuhumiwa wa ujambazi akamatwa Dar akiwa amevaa baibui





Na Festo Polea

MTU mmoja ambaye anadaiwa kuwa jambazi maarufu amekamatwa jijini Dar es salaam likiwa amevaa vazi la Baibui ili asijulikane kiraisi akiwa amebeba shoka mgongoni kwa ajili ya kujihami.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi alikamatwa juzi saa 1.30 usiku maeneo ya Kinyerezi Magengeni,jijini Dar es Salaam akiwa ajiandaa kufanya uhalifu.

Kova alisema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Kinyerezi Mwisho na kwamba alianza kufukuzwa baada ya jeshi la polisi kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa jambazi linalosakwa na polisi limeonekana katika eneo hilo likiwa limevaa baibui.

Alidai kuwa mtuhumiwa huyo akiwa katika mawindo yake juzi bila kujua kuwa anafuatiliwa, alipoona polisi alianza kukimbia na wananchi wakaanza kumfukuza k na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumpa mkong’oto na polisi walifika na kumuokoa.

Kamanda Kova alifafanua kuwa wakati mtuhumiwa anakamatwa alikuwa amevaa baibui na kwamba isingekuwa rahisi kutambua kuwa ni mwanaume.

“Jambazi hilo licha ya kuvaa baibui pia lilikuwa limeficha shoka mgongoni ambayo huitumia kufanikisha mipango yake,” alisema Kova.

Aliongeza kuwa baada ya jambazi hilo kukamatwa ilibainika kuwa amewahi husika katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani ya Morogoro na Pwani.

Katika hatua nyingine, wezi wanne ambao wanadaiwa kuiba magari, wamekamatwa jijini wakiwa katika harakati za kubadilisha namba za gari hayo mali.

Kamanda Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 10.30 jioni kwenye baa ya Super Min Wailer, wilayani Temeke ambako waliiba gari hilo siku moja kabla ya kukamatwa.

Mke wa Rais


Mke wa Rais Salma Kikwete(kushoto)akibadilishana mawazo na Mke wa Rais wa Marekani Laura Bush kwenye ikulu ya nchini hiyo The White House alipomtembela Laura jana.Rais Kikwete na Mkewe wapo nchini Marekani kwa Mwaliko Rasmi wa Rais George Bush.

Rais Kikwete White House



Rais Jakaya Kikwete akikaribishwa rasmi na Rais George Bush kwenye ofisi Maalum ya Rais wa Marekani Oval Office alipomtembela Rais Bush jana Washington DC.
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa na Rais George Bush wa Marekani mandhari ya ikulu ya Marekani,White House,wakati Rais Kikwete alipomtembelea Rais Bush Ijumaa asubuhi jijini Washington D.C.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Bush.Picha na Freddy Maro/Ikulu

Tuesday, August 26, 2008

Obama gives thumbs-up to wife's speech



By DARLENE SUPERVILLE,

Associated Press Writer Tue Aug 26, 12:48 AM ET
DENVER - It was Michelle Obama's speech, but her husband said it highlighted one of his attributes — one he says voters should want in a president.

"Now you know why I asked her out so many times, even though she said no," Barack Obama, the Democratic presidential nominee-in-waiting, told delegates by satellite Monday night after she delivered the first major speech of the Democratic convention.

"You want a persistent president," he said.

In her speech, Michelle Obama told cheering delegates jammed into the Pepsi Center and a nation watching on television that she and the possible future president have shared their hopes and dreams, and their struggles, too.

Afterward, their daughters — Sasha and Malia — joined her on stage and Stevie Wonder's "Isn't She Lovely" blared from the convention hall. Microphone in hand, the girls began smiling and waving at their father after his familiar face popped up on a large screen erected on stage.

Monday, August 25, 2008

Big Brother Africa III


Mimi kutoka Ghana


Lucille Kutoka Namibia


Sheila Kutoka Kenya


Hazel Kutoka malawi


Tawana kutoka Botswana



Huyu ndiye mwakilishi wa Tanzania mwaka huu katika shindano la Big Brother Africa III,
anaitwa Latoya Lyakurwa, kutoka Arusha Tanzania...kazi imeanza ndani ya nyumba!!!!

Sunday, August 24, 2008

Sherehe za birthday ya Mandela





Mke wa sasa Nelson Mandela, Mama Graca Machel (kushoto) akimpiga busu mke wa zamani wa Mandela, Winnie Mandela (kulia), kwenye sherehe za kusherekea birthday ya 90 ya mume wao. Naona wanapatana vizuri tu. Je, wana-share siri za kumfurahisha mzee?

Obama amtambulisha Biden


Barack Obama selects Sen. Joe Biden of Delaware to be his vice presidential running mate

By LIZ SIDOTI and NEDRA PICKLER , Associated Press
August 23, 2008

WASHINGTON - Barack Obama named Sen. Joe Biden of Delaware as his vice presidential running mate early Saturday, balancing his ticket with a seasoned congressional veteran well-versed in foreign policy and defense issues.

Obama announced the pick on his Web site with a photo of the two men and an appeal for donations. A text message went out shortly afterward that said, "Barack has chosen Senator Joe Biden to be our VP nominee."

Biden, 65, has twice sought the White House, and is a Catholic with blue-collar roots, a generally liberal voting record and a reputation as a long-winded orator.

Across more than 30 years in the Senate, he has served at various times not only as chairman of the Foreign Relations Committee but also as head of the Judiciary Committee, with its jurisdiction over anti-crime legislation, Supreme Court nominees and Constitutional issues.

In selecting Biden, Obama passed over several other potential running mates, none more prominent than former first lady Hillary Rodham Clinton, his tenacious rival in dozens of primaries and caucuses. Clinton issued a statement Saturday praising Obama's decision and calling Biden "an exceptionally strong, experienced leader and devoted public servant."

Obama's campaign arranged a debut for the newly minted ticket on Saturday outside the Old State Capitol in Springfield, Ill.

Obama's decision leaked to the media several hours before his aides planned to send a text message announcing the running mate, negating a promise that people who turned over their phone numbers would be the first to know who Obama had chosen. The campaign scrambled to send the text message after the leak, sending phones buzzing at the inconvenient time of just after 3 a.m. on the East Coast.

Hundreds of miles to the west, carpenters, electricians, sound stage gurus and others transformed the Pepsi Center in Denver into a made-for-television convention venue.

Friday, August 22, 2008

Mtoto wa Rais Aoa


Rais Jakaya Kikwete akimuaga mkwewe Bi.Arafa Mohamed pamoja na mtoto wake Ridhwani Kikwete muda mfupi baada ya mtoto wake kufunga ndoa na Bi Arafa katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo majira ya alasiri kuelekea Magharibi.

Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhwani Kikwete(Kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Mkewe Bi Arafa Muda mfupi baada ya Ridhwani kufunga ndoa katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo hii Majira ya alasiri Kuelekea Magharibi.

Katuni ya Kenya

Wednesday, August 20, 2008

Waheshimiwa Wabunge wakiyarudi


Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Joel Bendera akicheza na Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania,Celine Njuju,muziki ulioporomoshwa na African Stars 'Twanga Pepeta International'mjini Dodoma,wikiendi.
Mbunge wa Viti Maalumu,Anna Lupembe(kushoto)akicheza muziki wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta International)na Mbunge wa Mbinga Magharibi,John Komba wakati wa hafla iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania mjini Dodoma,wikiendi

Mbunge wa Mbinga Magharibi,John Komba akicheza muziki wa African Stars 'Twanga Pepeta International' akiwa ameshika ungo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Zain Tanzania mjini Dodoma, wikiendi.

Bweni laungua


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Bigwa inayomilikiwa na Masita wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro,wakiangalia baadhi ya vitu vyao vilivyoungua moto uliotokea jana na kuunguza mabweni mawili ya Shule hiyo.Picha na Mdau John Nditi/TSN Morogoro.

Rais Mwanawasa afariki kweli


RAIS wa Zambia Levy Mwanawasa (59), amefariki dunia nchini Ufaransa ambako amekuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mstuko.
Kifo cha Mwanawasa ambaye ni kipenzi cha nchi za Magharibi kutokana na msimamo wake katika mapambano dhidi ya ufisadi, kimetokea miezi takriban miwili baada ya kuzushiwa kifo.
Makamu wa Rais wa Zambia, Rupia Banda, amenukuliwa na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) akithibitisha kutokea kwa kifo cha Rais Mwanawasa.
Banda alifafanua kwamba kutokana na kifo hicho cha Rais Mwanawasa, nchi itakuwa katika maombelezo ya siku saba za msiba huo mzito.
Mwanawasa pia atakumbukwa kutokana na msimamo wake wa kuwa mmoja wa viongozi wa Afrika wanaomkosoa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, kutokana na matendo yake ya ukiukaji demokrasia na utawala bora.
"Ndugu zangu wananchi, kwa majonzi na masikitiko makubwa napenda kuarifu watu wa Zambia kwamba, Rais wetu Dk Levy Patrick Mwanawasa, amefariki leo asubuhi (jana)," alisema Makamu wa Rais Banda kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo na kuongeza:
"Pia ningependa kuarifu kwamba, maombelezo ya kitaifa ya kifo cha Rais yatafanyika kwa muda wa siku saba."
Kwa mujibu wa Katiba ya Zambia, Banda ndiye ambaye anatarajiwa kukaimu madaraka hayo ya Rais hadi utakapoitishwa uchaguzi.
Mwanawasa aliweza kujijengea heshima miongoni mwa Wazambia, baada ya kuwezesha utajiri wa madini ya shaba kunufaisha raia wake wengi.
Pia anaheshimiwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na nchi fadhili za Magharibi, ambazo ziliamua kuongeza msaada wa mabilioni ya dola kwa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.
Uamuzi wa IMF na nchi fadhili za Magharibi kuongeza msaada kwa Zambia, unatokana na juhudi nzito za Mwanawasa katika kuendesha kampeni nzito dhidi ya ufisadi, ikiwa ni za kwanza tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1964 kutoka kwa Waingereza.
Miongoni mwa watu waliokumbwa na operesheni hiyo ya ufisadi, ni Rais aliyemrithi Frederick Chiluba.
Hivi karibuni, baada ya kutokea hali ya tete ya nchini Zimbawe baada ya kuvurugika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi, Mwanawasa alimshutumu Mugabe akisema anataka kuleta balaa jingine la machafuko barani Afrika.

Historia fupi ya Mwawasa

Mwanawasa alizaliwa Mufurira, eneo la Ukanda wa Shaba, Septemba 3,1948 na kuanza kuibuka katika siasa wakati akiwa Makamu wa Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zambia, ambacho kilifanya maandamano kadhaa kuunga mkono harakati za ukombozi wa nchi ya Afrika Kusini.
Baada ya kuhitimu chuo mwaka 1973, taratibu Mwanawasa alianza kujiimarisha kama mwanasheria anayeshimika katika kipindi cha miaka 20 iliyofuata.
Katika moja ya kesi maarufu, alifanikiwa kumtetea makamu wa zamani wa rais, Christon Tembo na wenzake walioshtakiwa kwa makosa ya uhaini mwaka 1989, akiwa amewaokoa katika hukumu ya kifo kama wangepatikana na hatia.
Akiwa mmoja wa waasisi wa chama cha Movement for Multi- Party Democracy (MMD), Mwanawasa alimsaidia Frederick Chiluba kumshinda Rais Kenneth Kaunda katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Zambia mwaka 1991.
Mwishoni mwa miaka ya 1991 aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Zambia, lakini akajiuzulu miaka mitatu baadaye kutokana na kushindwa kuvumilia matumizi mabaya ya ofisi na rushwa iliyokuwa imekithiri wakati wa utawala wa Chiluba.
Wakati akiendelea kuwa mwanachama wa MMD, Mwanawasa aliendelea na shughuli zake kwenye jumuiya ya wanasheria hadi mwaka 2001.
Mwanawasa alinusurika katika ajali ya gari Desemba mwaka 1991 na akalazwa hospitalini kwa miezi mitatu. Ajali hiyo mbaya ilimfanya atembee kwa kuchechemea na kuzungumza kwa shida.
Baada ya kuitwa kurejea MMD kwa kutumia vikao vya pembeni na Chiluba, Mwanawasa aligombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2001.
Kwa mshangao wa kila mtu, Mwanawasa alikorofishana na Chiluba mara baada ya kuapishwa na akaanza kampeni ya kusafisha rushwa, kampeni ambayo ilidaiwa kuwa ya kutafuta mchawi dhidi ya serikali ya zamani.
Mwezi Aprili, 2006, Mwanawasa alikumbwa na kiharusi, lakini akapona mapema baada ya kutibiwa nchini Uingereza.
Miezi mitatu baadaye, alimshinda mpinzani wake wa kisiasa Michael Sata na kurejea madarakani kwa kipindi cha pili, akiwa ameshinda kwa kura chache.
Tofauti na aliyemtangulia, Mwanawasa alipata mafanikio makubwa katika maendeleo. Chini ya utawala wa Mwanawasa, Zambia imekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi, huku wawekezaji wa nje wakiwekeza mabilioni ya fedha.
Mwanawasa alikuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika mwaka 2007 na alisifiwa kwa juhudi zake zisizo na kikomo katika kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka nchiniZimbabwe baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 2008.
Mwanawasa ameacha mke Maureen Luchendo Mwanawasa na watoto sita.
- Reuters

Tuesday, August 19, 2008

Mwalimu wa dini wake 86, watoto 170




DUNIANI kuna mambo. Mwalimu wa dini ya Kiislamu nchini Nigeria, Mohamed Bello Abubakar (84) pichani juu na wake zake,ambaye alimejitokeza na kutafuta rekodi ya kuwa na wake wengi, amewataka wanaume kutoiga tabia yake hiyo.

Bello Abubakar mwenye wake 86 pamoja na zaidi ya watoto 170 anaoishi nao katika mji wa Niger alieleza kupitia shirika la habari la BBC kuwa si vyema kwa wanaume wengine kuiga mfano wake, kwa kuwa uwezo alio nao ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

“Mwanauame mwenye wake 10 anaweza kupata kiharusi na kufa, lakini kwa nguvu niliyopewa na Allah nimeweza kuwadhibiti wake zangu 86 bila matatizo. Nimekuwa siwatafuti mimi, ila wamekuwa wakija wenyewe kwangu. Nimekuwa nikiamini kuwa Mungu ndiye amekuwa akiwaleta na sina namna zaidi ya kuwaoa,” alieleza.

Aliongeza kwa kusisitiza kuwa kwa kadiri ajuavyo, hakuna adhabu yoyote iliyoelezwa katika kitabu Kitakatifu cha Koran kwa kuwa na wake zaidi ya wanne na kwua uwezo wake unatokana na nguvu ya uponyaji aliyopewa na Mungu.

“Kwa uelewa wangu katika Koran Tukufu, haijaweka ukomo na inategemea nguvu zako na kadiri uwezo unavyoruhusu, Mungu hakueleza adhabu yoyote kwa mjwanaume mwenye wake zaidi ya wanne, lakini ameelez wazi adhabu kwa wabakaji na wazinzi,” alieleza alipokuwa akijibu swali kuhusu madai ya mamlaka za kiislamu nchini humo, kuwa mtu huruhusiwa kuwa na wake wasiozidi wanne, ambao atatakiwa kuhakikisha anawahudumia vyema.

Baadhi ya wanawake wa Bello, ambao wengi wao wana umri mdogo kuliko baadhi ya mabinti zake waleieleza kuwa walikutana na mwanamme huyo walipokwenda kwake kwa ajili ya kuomba usaidizi kutokana na maradhi kadhaa.

“Mara tu nilipokutana naye ugonjwa wa kichwa ulipotea,” alieleza Sharifat Belo Abubakar, mwanamke aliyekutana na Abubakar akuwa na miaka 25, wakati mwanamme huyo alipokuwa na miaka 74.

“Mungu alinieleza kuwa ni wakati wangu wa kuwa mke wake, Sifa kwa Mungu kuwa sasa imetimia na imekuwa mkewe. Nilipomuona mara ya kwanza niliapa kwua siko tayari kuolewa na mzee huyu na ulipofika wakati alinieleza wazi kuwa ni agizo kutoka kwa Mungu,” alieleza mwanamke mwingine, Ganiat Mohamed Bello, ambaye mama yake aliwahi kumpeleka kwa Bello Abubakar kwa ushauri alipokuwa akisoma shule ya Sekondari.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumaliza shule alioana na mwanaume mwingine lakini muda si mrefu walitaliliana na alipokwenda kwa mzee huyo ambaye kwa kipindi cha miaka 20 ya uhai wake alikuwa akimuita baba hakuwa na namna zaidi ya kutekeleza agizo kutoka kwa Mungu.

“Kwa sasa ni mhongoni mwa wanawake wenye furaha duniani. Unapoolewa na mwanaume mwenye wake 86 unajua kabisa kuwa anaelewa namna ya kuwatunza,” alisisitiza.

Lakini maisha yake na wake zake hayana utaratibu maalum. Wake zake hao hawafanyi kazi na wanaishi zaidi ya wanne katika kila chumba na hana njia ya wazi kuhusu namna anavyoitunza familia yake kubwa. Hataki kueleza namna anavyoweza kupata fedha za kutosha kuweza kuwatumza wanawake hao.

Suala la kustaajabisha zaidi ni kuwa kamwe hajawahi kuwaruhusu wake zake wala watoto wake kutumia dawa ya aina yoyote wanapopatwa na maradhi mbali mbali kw akusema kuwa haamini iwapo kuna magonjwa kama Malaria duniani na kuwa wanapougua humweleza Mungu na Mungu huondoa maradhi yote.

Mmoja miongoni mwa wake zake, Hafsat Belo Mohammed alieleza kuwa watoto wake wanne walifariki, “waliugua na tukamweleza Mungu, Mungu akasema kwua wakati wao umefika.”

Lakini Bello Mohammed amekuwa akieleza kuwa Mtume Muhamad amekuwa akizungumza naye moja kwa moja na kumweleza mambo yote ambayo amekuwa akiyafanyia kazi.

Imeandaliwa na Andrew Msechu kwa msaada wa BBC

Monday, August 18, 2008

Rais apoke ripoti ya Epa kimyakimya


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea rasmi ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account–EPA)kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu iliyofanya uchunguzi huo,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Johnson Mwanyika katika halfa fupi iliyofanyika leo(Jumatatu,Agosti 18,2008)Ikulu,Dar Es salaam.Wengine katika picha ni wajumbe wa timu iliyofanya uchunguzi huo,Mkuu wa jeshi la polisi nchini,Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea.Picha na Freddy Maro/Ikulu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiipitia ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account-EPA)muda mfupi baada ya kukabidhiwa na mwenyekiti wa timu iliyoongoza uchunguzi huo Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Johnson Mwanyika.Wengine katika timu hiyo ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea.Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo hii.

Rais apoke ripoti ya Epa kimyakimya

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatatu, Agosti 18, 2008) amepokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payments Accounts - EPA) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amekabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson P.M. Mwanyika.

Mwanasheria Mkuu huyo alifuatana na wajumbe wengine wa Timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hosea.

Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.

Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.

Timu hiyo iliundwa na Rais Kikwete Januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Wakati anaunda Timu hiyo, Rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

Rais aliunda Timu hiyo baada ya kuwa amepitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2005/06 za EPA katika Benki Kuu Tanzania (BOT), uliofanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kampuni hiyo ya Ernst and Young iliombwa na Serikali kuifanya kazi hiyo. Iliianza Septemba, 2007 na kumalizika Desemba, mwaka huo huo, 2007.

Rais Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo Januari 7, mwaka huu, 2008 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, Rais aliitolea maamuzi Taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda Timu ya Mwanyika.


Imetolewa na

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

18 Agosti, 2008

Friday, August 15, 2008

Dereva wa daladala apiga mwanafunzi, azirai



KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kisutu, Pili Jackson (17), jana majira ya asubuhi alijikuta akipata kipigo kutoka kwa dereva wa daladala, Michael Hassan (40) linalofanya safari zake Gongolamboto hadi Kivukoni, hali iliyomfanya azirai.

Dereva huo anayeendesha basi hilo lenye namba T156 ADV aina ya Toyota DCM, alijichukulia sheria mkono majira ya saa mbili asubuhi baada ya kutokea majibizano kati yake na dereva wakigombea kukaa eneo la mbele karibu na dereva ambapo hakukuwa na siti zaidi ya benchi dogo.

Mwanafunzi huyo alizimia kutokana na kipigo kilichomsababishia kudondokea siti moja wapo ndani ya gari hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akielezea tukio hilo alisema lilitokea jana majira ya saa mbili asubuhi maeneo ya Ukonga Mombasa, baada ya mwanafunzi huyo kupanda katika daladala hilo baada ya kuzuiwa na kondakta, hali iliyosababisha majibizano kati yao habari na Festo Polea.

Barabara ya Mandela


Fundi wa shirika la umeme nchini (TANESCO) Josiah James akichimba shmo jipya la kuweka nguzo ili kupisha upanuzi wa barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam hivi karibuni hakika mkandarasi aliyekabidhiwa barabara hii anaonekana ni mtaalamu wa kujenga mitaro, maana wameanza na mitaro kibaooo.Picha na Zacharia Osanga

Tuesday, August 12, 2008

Watoto shuleni


Maisha ya skuli si mchezo kuna milima na mabonde, kuna miteremko vile vile hebu cheki hivi vijamaa vimejificha sijui vinaogopa nini, bila shaka vimetoroka kabla ya kuruhusiwa na mwalimu

Sunday, August 10, 2008

usafiri Dar


Hebu cheki Dar es salaam kila mtu yuko bize, kila mtu na jambo lake kila mtu anatafuta pesa, hata hivyo wapo baadhi wanafuatilia mambo ya watu, hapa ni kati kati ya jiji kila mtu anahangaikia usafiri sijui mwenzangu msomaji una maoni gani

kalaji


Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Mwananchi Communications wakigongeana glasi mara baada ya kushuhudia uzinduzi wa sura mpya ya mojawapo ya bidhaa za kampuni hiyo, ya gazeti la Mwananchi (picha ya Fidelis Felix

Thursday, August 07, 2008

msiba wa Kapteni Mazula







MAELFU ya waombolezaji katikati ya wiki hii walijitokeza kwa wingi katika kanisa la katoliki usharika wa St Martha mikocheni kuusindikiza mwili wa marehemu Kapt George Mazula

Miongoni mwa sifa za Marehemu Kapt Mazula ni kutumia muda wa masaa 17,640 kuruka na ndege angani wakati wote wa uhahi wake alioishi hapa duniani.

Mbali na kukumbukwa katika mengi lakini pia Kapt Mazula atakumbukwa kwa tija na ufanisi katika kazi huku akiweka mbele masilahi ya taifa kuliko kutafuta faida zake binafsi.

Katika uhai wake aliweza kutumia masaa 3,300 kuendesha ndege ndogo yenye uwezo wa kubeba watu 19,masaa 7,340 watu wasiozidi 50 na zaidi ya masaa 7,000 ndege za B737.

Marehemu Kapt Mazula alipata matatizo ya mgongo ambayao yalisababisha apelekwe India kwa matibabu ,mnamo julai 8 mwaka huu aliweza kufanyiwa upasuaji na kupata nafuu jambo lililopelekea aweze kurudishwa nchini julai 20.

Hali yake iliendelea vizuri hadi julai 30 mwaka huu alipoanza kupata mtatizo ya pumu kabla ya roho yake kutwaliwa agosti mosi majira ya saa nne asubuhi akiwa nyumbani kwake.

Marehemu Kapt Mazula amewaacha watoto wake wawili Brayan Mazula na George -Junior mazula wanaoishi nchini marekani pamoja na mke wake Hariety Mazula.

Akisoma wasifu wa marehemu Kapt Mazula mtoto wake Georgejunior anasema marehemu alizaliwa mwaka 1949 katika eneo la bwiru mkoani Mwanza,yeye akiwa ni mtoto wa nne kuzaliwa kutoka kwa wazazi wake Arbogasti na Maria Mazula.

Anasema alisoma katika shule ya msingi Tabora, kabla ya kuhamia shule ya Kangululi wilayani ukerewe mkoani mwanza.

anasema katika masomo yake ya sekondari Marehemu Mazula alisoma katika shule ya musoma collegge na baadaye mwaka 1970 alijiunga na shule ya sekondari ya Aga Khan Boys kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Georgemazula anasema mwaka 1973 Kapt Mazula alijiunga na benki ya taifa ya biashara alikofanya kazi kabla ya kujiunga na chuo cha urubani Saroti kilichopo nchini Uganda. Habari hii ya Peter Edson na picha zote ni za Perez Mwangoka wa Mwananchi.

Wednesday, August 06, 2008

Paschal Mayalla apata ajali



Pascal Mayalla akiwa katika chumba cha wagonjwa Daraja la kwanza katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako amelazwa kwa matibabu baada ya kupata ajali ya pikipiki juzi jioni katikati ya Ihumwa na Nzuguni nje kidogo ya mji katika barabara ya iendayo Morogoro. Kwa mujibu wa maelezo yake, amevunjika mkono wa kushoto ambao hauna mawasiliano na mwili uliosababishwa na kushituka kwa uti wa mgongo. Hata hivyo amepewa rufaa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo atapelekwa leo kwa matibabu zaidi. Picha na Jube Tranquilino.

Monday, August 04, 2008

hafla ya kuzaliwa rasmi zain



Baadhi ya wasanii wa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Umoja kutoka Afrika Kusini, wakicheza wakati wa hafla ya kubadilisha jina la kibiashara la Celtel kuwa Zain kwenye Uwanja wa Karimjee, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Sunday, August 03, 2008

Nasreem Karim Miss Vodacom


Miss Vodacom Tanzania 2008 nasreem Karim akifurahia ushindi na mshindi wa pili Sylvia Mashuda(shoto) na wa Tatu Pendo Laizer muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa Mwaka huu.

Hawa jamaa Wazee wa Ngwasuma wakisakata rhumba



Braza Chammeleone naye alikuwapo



Hawa hapa wakaingia Top Five





Twanga nao walikuwapo



Hebu cheki walivyopendeza