Monday, November 30, 2015

SHEKH ISSA PONDA AACHIWA HURU


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.

********
Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu  lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo  alitoa  uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu  katika mashitaka mawili yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .


Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya Mwaka 2002.

Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi,  kumfutia kesi ya jinai  Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013  kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Hata hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye aliletwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao waliliambia gazeti hili kuwa wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kufunguliwa makosa matatu ya uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa gereza la Segerea Dar es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la Magereza uliamua kumuamisha Ponda kutoka Gereza la Segerea na kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.

Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa gofu mjini Morogoro.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi  wa Serikali, Bernard Kongola, alidai  kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa  na wakili wa kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.

Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.

Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.

Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

Oktoba 18 mwaka 2012, Ponda na wenzie 49 walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Mara ya kwanza   wakikabiliwa na makosa matano, kosa la kwanza ni la kula njama, kujimilikisha mali, kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang'ombe  Markas,wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali , Tumaini Kweka .Mahakama pia iliwafunga dhamana ya Ponda na mshitakiwa wa pili tangu 0ktoba 18 Mwaka 2012 hadi siku Kesi hiyo iliyotolewa hukumu Mei 9 Mwaka 2013.

Mei 9 mwaka 2013 Hakimu Mkazi Victoria  Nongwa akitoa hukumu yake katika kesi hiyo ya Ponda na wenzake alisema anawaachiria huru washitakiwa 49  kwasababu upande wa jamhuri  umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yao na kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu  la kuingia kwa jinai na kwamba na anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu pia jamhuri ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.

Sheikh Ponda alikataa rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mei 9 mwaka 2013 ambapo alishinda rufaa yake.

Hata hivyo siku Chache baada ya Kufungwa Kifungo hicho cha nje Mei 9 mwaka 2013, Ponda alikwenda Mkoani Morogoro na kufanya mkutano ambao alidai wa Kutenda makosa ya jinai ambao alikamtwa  Agosti Mwaka 2013 na kuwekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa Kesi Mahakama ya Kisutu Na.144/2013 ikafutwa na DPP na ndipo akafunguliwa kesi hiyo Mkoani Morogoro ambayo imetolewa hukumu Leo na kuachiwa huru.

Bilioni 4 za sherehe za uhuru kupanua barabara ya Mwenge-Moroco yenye urefu wa kilomita 4.3

index 
Sehemu  ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni  nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.PICHA NA IKULU.

…………………………………………………………………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
  Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja.

Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.  Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
  Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.Dar es Salaam.

30 Novemba,2015

RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR

sa1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR

sa2 sa3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis. Picha na OMR

MKUU WA MKOA WA TANGA ATEMBELEA MIRADI YA MAJI KATIKA JIMBO LA MLALO

 Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akizungumza na wananchi wa jimbo la mlalo wakati Mkuu wa mkoa wa Tanga alipotembelea mradi wa maji wa  jimbo hili na wakatiwa sherehe ya kumpongeza, katika hafla fupi ilifanyika maeneo ya Mlalo Mkongoloni mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza atembelea wilaya ya Lushoto na kuangalia miradi ya maendeleo ya Serikali ikiwepo maabara na mradi wa maji wilayani Lushoto Mkoani Tanga  baada ya kabla ya hafla fupi ya Mbunge wa jimbo la Mlalo iliyofanyika maeneo ya Mlalo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisalimiana na wananchi wa jimbo laMlalo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika jombo la Mlalo kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mariam Juma, Mbunge wa jimbo la Mlalo ndugu Rashid Shangazi na diwani wa jimbo la Kwemshasha Anuari Kiwe.
Baadhi ya wananchi na madiwani wa jimbo la Mlalo waliokusanyika kwaajili ya kukubali wito wa Mbunge wa Mlalo,Rashid Shangazi mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kukagua mradi wa maji katika jimbo la Mlalo, na Mbunge wa jimbo hilo kufanyiwa sherehe ya kumpongeza hafla hiyo iliyofanyika katika jimbo hilo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

MBUNGE WA JIMBO LA ILALA MUSSA ZUNGU ATEKELEZA AHADI ALIYOITOA WAKATI WA KAMPENI

  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ nyaraka za  Pikipiki  Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA  KHAMISI MUSSA)
 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za Pikipiki Dar es Salaam leo.   
 Zungu amesema  ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa mgombea  Urais Dk John Pombe Mgufuli  kupitia Chama cha Mapinduzi  CCM  ili iwasaidie kuongeza  kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa  vya michezo Zungu ameongeza na kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya  wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye maeneo mnayouzia samaki,  Nitatekeleza hilo  kabla ya mwezi wa kumi na mbili ili mfanye  biashara kwa uhuru.

WAKULIMA ZAIDI YA 300 WA MKOA WA MTWARA WAJIUNGA NA NSSF

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeandikisha wakulima wa Korosho zaidi ya 300 mkoani mtwara kwenye kampeni ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo ilifanyika mahususi ili kuwafikia watu ambao wako kwenye sekta  isiyo rasmi.

Kampeni hiyo yenye malengo ya kufikia umma wa Watanzania ambao haujafikiwa na elimu ya Hifadhi ya jamii, Kuwaandikisha kujiunga na NSSF ili kuongeza wigo wa wanachama na pia  Kupata mrejesho  wa huduma zetu kutoka kwa wanachama wa mfuko.Imemaliza mkoani Mtwara na itaendelea kwenye mikoa mingine.NSSF inaendelea kuwasihi Watanzania waendelee kujiunga na NSSF.
Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kulia), akiwapa maelezo kuhusu huduma zitolewazo na NSSF wakulima wa Kijiji cha Msijute, Kata ya Mayanga, mkoani Mtwara, kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘NSSF Kwanza’, ambayo inaendelea kwa kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi.
 Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akiwapa maelezo wakazi wa kijiji cha Msijute jinsi ya kujiunga na Huduma ya mafao ya Matibabu bure  kwenye kampeni maalumu ya kuwaelimisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara juu ya faida za Hifadhi ya Jamii kupitia NSSF.
Wakazi wa Kijiji cha Msijute kata ya Mayanga Mkoani Mtwara wakijiandikisha NSSF ili kuweza kujipatia mafao bora kutoka NSSF yakiwemo mafao ya matibabu bure kwa wanachama na familia zao.

NHIF YAKABIDHIWA KITUO CHAKE DODOMA

mi01Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akionesha ufunguo wa kituo hicho baada ya kukabidhiwa na baadae alikikabidhi rasmi katika uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
mi1Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Michael Mhando akikagua Kituo cha Kisasa cha Matibabu kilichopo katika Hospitali ya Mkoa Dodoma. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka huu.
mi2Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
Makadhiano hayo yalifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa NHIF, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradi huo wa kampuni ya Nosuto
Associates.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianze
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa fedha, Mipango na Uwekezaji wa NHIF Bw. Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.

MAPACHA WANNE WALITEKA JIJI LA DAR ES SALAAM

 Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Rwiza Mbutu akiwa jukwaani wakati wa shoo ya uzinduzi baada ya kujiunga tena katika Bendi ya  mapacha Wanne
 
 
 
 
 Chazi Baba kulia akiwa na Josee Mara wakiwa katika shoo iliyo wavutia wadau wakati wa uzinduzi wa nyimbo yao ya usiku wa kuachwa iliyozinduliwa hivi karibuni baada ya kusambaratika.
 Mpenzi wa Bend ya Mapacha wanne Fredicto Mupao ‘mwana tarime’ akimwagia mapesa mwimbaji wa Bend ya Mapacha wanne Kalala Jonia (kulia) katika ukumbi wa Mango Gaden wakati wa usiku wa nyimbo ya kuachwa iliyo zinduliwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam 
 Rwiza Mutu akiwa Jukwaani
 Mdau achanganyikiwa kwa kumwagia mapesa Mwimbaji wa Bend wa ya Mapacha wanne, KalalaJunia baada ya kuvutiwa na kipaji cha uimbaji wa mwimbaji huyo nakujikuta anamwagia mapesa
 Kuanzia kulia ni Chazz Baba, Haridi Chokora, Kalala Junia, Josee Mara
Kuanzi kulia ni Haridi Chokora, Kalala Jnia, Chazz Baba, Josee Mara