Tuesday, December 29, 2015

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK

Kampuni
ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika
mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa facebook, www.facebook.com/TigoTanzania  kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 
27 mwaka huu hapa Tanzania.
 
Kutokana 
na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook 
imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha 
ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na 
Facebook, ambapo wateja wanaweza  kutumia  Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza 
kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.
 
Ukurasa 
wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza 
na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za  kampuni.
 
Hivi 
karibuni, Tigo Tanzania imejishindia tuzo 
mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua 
mashirikana watu binafsi katika uongozi. 

Tuzo hizo ni ya Ubora wa  bidhaa (The Hall of Fame in Brand Excellence),
na Matumizi Bora yaMitandao ya  Kijamii KatikaMauzo    ( Best use of Social Media in Marketing).
 
Tigo 
Tanzania inaongoza katika soko la mawasiliano na imekuwa mstari wa mbele katika 
mitandao ya kijamii ambapo wateja wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa haraka.

Hii 
imeufanya mtandao kuaminika sana na wateja na kutumika kama mwendelezo wa huduma 
kwa  wateja.
 
Kuhusu 
Facebook Mkurugenzi wa Tigo Bwana Diego Gutierrez anasema. “Jukwaaletula Facebook 
na Twitter (Tigo TZ) limekuwa kitendea kazi muhimu ambacho kinatumika kujifunza 
kutoka kwa wateja wetu na jamii kwa jumla ambao wanakitumia. 

Tunajivunia kwakuweza 
kuyafikia mafanikio haya, na tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa na  imani nasi.
  
Tigo imedhamiria kubadilisha mtindo wa maisha wa kidijitali  
kwa kuwaletea wateja wetu ubunifu wa teknolojia maridhawa. Hivikaribuni, 
tumezindua teknolojia ya 4G LTE hapa Tanzania ambayo ni intaneti iliyo na kasi kuliko
zote pamoja na ofa ya aina ya simu yaTechno Y3 Smartphone inayotumia lugha ya Kiswahili.

No comments: