Monday, December 14, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA NHC LAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA 711 KAWE

k1
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam, Nyumba hizi ziko kwenye majengo 8 yenye ghorofa 18 kila moja ambayo yanatarajiwa kuchukua watu  1000 kwa  na huu ni utangulizi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua watu 15,000.
Watu wanaohitaji kununua nyumba hizo wanatakiwa kufika ofisi za NHC Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga au wanaweza kutembelea kwenye mtandao wa shirika hilo kwa maelezo zaidi ili kununua nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya shirika hilo Upanga.
k4
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
k17
Meneja wa Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na Monica Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya Monifinace Investment Group Limited wakati wa uzinduzi huo.
k18
Meneja  wa Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara NHC katika uzinduzi huo kulia ni Mwita Makenge Mkurugenzi wa Kampuni ya Wegmar Limited na kushoto ni William Genya Meneja Maendeleo ya Biashara NHC .
k19
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu katikati na  Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakimsikiliza Linley Kapya kutoa Benki ya NBC wakati alipokuza akizungumza jambo katika uzinduzi huo.
k5
Meneja wa Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na kuelezea jinsi mradi huo utakavyokuwa na mambo muhimu yaliyopo katika mradi huo huku akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
k06
Baadhi ya wafanyakazi wakipozi kwa picha wakati wa hafla hiyo
k6
Meneja  wa Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akifafanua jambo mbele ya waalikwa  wakati alipokuwa akiuelezea mradi huo.
k07
Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa 711 wa Kawe jijini Dar es Salaam.
k7
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Arden Kitomari akifafanua mambo mbalimbali wakati akiuelezea mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
k08
Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa mbalimbali wa Shirika la Nyumba NHC
k8
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakifuatilia video zilizokuwa zikionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa wakati wa uzinduzi uliofanyika Makao Mkuu wa shirika hilo Upanga.
k10
Baadhi ya wageni waalikwa kutoa taasisi mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
k12
Kutoka kulia ni Meneja wa Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Masoko wa NHC Bw. Aden Kitomari wakimsikiliza Taji Liundi aliyekuwa MC wa uzinduzi huo.
k14k15k16
Wageni mbalimbali walihudhuraia uzinduzi huo.
Post a Comment