Wednesday, June 29, 2011

PRESIDENT JAKAYA KIKWETE MEETS BILL GATES

President Dr. Jakaya Kikwete (2nd-L) and Vice President, Dr. Mohammed Gharib Bilal, in a group photo with the Chairman of Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates (L) and his wife, Melinda gates, who is the Co-Chair, shortly after the president had talks with him at State House in Dar es Salaam Wednesday June 29, 2011. (Photo; State House)
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (R) meets with the Co-Chair of Bill and Melinda Getes Foundation, Bill Gates at State House in dare s Salaam Wednesday June 29, 2011. (Photo; State House)

Ziara ya CCM mkoani Mtwara, Lindi

Nape akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano huo kwenye uwanja wa fisi. Picha zote za Bashir Nkoromo wa Nkoromo Daily Blog kwa
Habari zaidi waweza kubonya hapaUpate tukio hilo kwa kina.

Katibu wa Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma (kushoto) akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake na Nape kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza ngoma ya kikundi cha uhamasihaji cha vijana wa Newala, baada ya msafara wake kuwasili mjini Newala, Juni 27, 2011

Tuesday, June 28, 2011

Shaggy in the house


Wasichana wa kabila la kisukuma wakimkaribisha Shaggy katika viwanja vya Bujoro kabla ya kusimikwa kuwa chifu wa kabila hili.


Wasichana wa kabila la kisukuma wakimkaribisha Shaggy katika viwanja vya Bujoro kabla ya kusimikwa kuwa chifu wa kabila hili.
Chifu Mark Bomani akiteta jambo la Shaggy alipokuwa katika vwanja kwa Bujora ambapo kulikuwa na ngoma za msimu wa mavuno ambazo huchezwa ndani ya siku nane wakisherekea mafanikio ya mavuno.


Kutoka kushoto ni Shaggy akisaliiana na Mark Bomani mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege wa jijijni Mwanza.

Mwandishi Bora Tuzo ya CNN atoka Kenya


KENYAN FATUMA NOOR NAMED
CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST 2011
Fatuma Noor from Kenya has been awarded the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2011 Awards Ceremony.

Fatuma Noor, who works for The Star Kenya, won for her investigative three-part series on the ‘Al-Shabaab’, which was chosen from among 1407 entries from 42 nations across the African continent.

The series tells the story of the young men who give up their freedom abroad to return and fight for the ‘Al-Shabaab’ in one of the world’s most dangerous places on earth – Somalia.

Fatuma Noor was one of the 27 finalists at the Awards ceremony on Saturday evening and was a winner in the category ‘General News Award (Print).’

The Awards, which rotate location each year in tribute to their pan-African credentials, were held at a Gala ceremony hosted by CNN and MultiChoice at The Sandton Sun Hotel, Johannesburg, South Africa yesterday evening, Saturday 25th June.
Nolo Letele, Executive Chairman MultiChoice South Africa and Parisa Khosravi, Senior Vice President of international newsgathering for CNN Worldwide presented Fatuma Noor with the Award.

Fatuma said: “I want to thank my mum and my boss Catherine, who believed in me when no one else did. There was a time in my life when I thought about giving up, but with this Award I'm not giving up any time soon”

Chair of the judging panel, journalist and media consultant Joel Kibazo said: “The judges were impressed with the high quality of entries to the competition this year, and this intrepid young journalist has shown great courage and determination in going the extra mile to tell this fascinating story. Fatuma Noor’s three-part series on the Al-Shabaab provides a detailed and personalised portrait of the young men who leave their comfortable western lives to join one of the world’s most ruthless militant groups in Somalia.”

Tuesday, June 21, 2011

Madawati ya Saruji darasani


HIVI karibuni asasi ya kiraia ya Twaweza kupitia programu yake ya Uwazi,ilifanya utafiti katika jiji la Dar es Salaam na kubaini upungufu mkubwa wa madawati katika shule za serikali.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliohusisha sampuli ya shule za msingi 40 katika manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni, karibu nusu ya shule hizo hazina madawati ya kutosha, hali inayowalazimu wanafunzi kukaa sakafuni.

Na hata katika shule zilizo na madawati, wanafunzi wanalazimika kukaa watano katika dawati moja ambalo kimsingi linapaswa kukaliwa na wanafunzi wasiozidi watatu.

“Katika takribani nusu ya shule(18 kati ya 40), hapakuwa na madawati ya kutosha kwa wanafunzi wote, wengi wanalazimika kukaa chini…..,” inasema sehemu ya ripoti ya utafiti.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukosefu wa madawati ni tatizo kubwa katika Shule ya Msingi Kunduchi ambapo, robo tatu ya wanafunzi 1,931 katika shule hiyo hawana madawati. Pichani unaweza kuona ubunifu wa aina yake wa madawati ya saruji yaliyojengewa ndani ya darasa kama suluhisho la tatizo hilo.

Monday, June 06, 2011

MAHAKAMA YAMUACHIWA HURU MBOWE, YEYE AELEZEA JINSI ALIVYOCHUKULIWA NA NDEGE HADI ARUSHA


HATIMAYE Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameachiwa huru jana kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, huku wafuasi wake waliokuwa wamefurika mahakamani hapo wakimbeba juu kwa furaha nje ya mahakama hiyo.

Hatahivyo,mahakama hiyo pia imemkataa mdhamini wake wa awali Julius Margwe, kuendelea kumdhamini ,na kukubali mdhamini mwingine baada ya kuwa na shaka na mwenendo wa mdhamnini huyo,ambapo Diwani wa kata ya Elerai wa CHADEMA,John Bayo alijitokeza na kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Akizungumza Mahakamani hapo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa, alisema kuwa kutokana na mdhamini huyo kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo, ikiwa ni pamoja na mdhamini huyo kukabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso, hivyo mahakama imeamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

Alisema kuwa mbali na kueleza uongo Mahakamani hapo kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, bado mahakama haina sababu naye sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.

Kuhusu Mbowe Hakimu huyo alikiri kuwa ni kweli mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie kikao cha bunge la bajeti na ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.

“Ila sasa mtaendelee na vikao vyenu vya bunge kama tulivyosema awali, ila wadhamini wenu lazima waje mahakamani kila kesi itakapotajwa na tunaondoa amri ya kukamatwa na sasa utaendelea na dhamana yako ya awali,” alisema Magesa.

Saturday, June 04, 2011

Maandalizi Kikao cha Bunge la Bajeti

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BUNGE LA TANZANIASimu Na. 022 2112065


Fax Na. (255) 022 2112538


E-mail: tanzparl@parliament.go.tz


(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (KATIBU WA BUNGE)Unapojibu tafadhali taja:

Ofisi ya Bunge


S.L.P. 9133


DAR ES SALAAM
Kumb. EB.155/172/01/300 31 Mei, 2011

YAH: WANAHABARI KWA AJILI YA BUNGE LA BAJETI


____________________
Tunayo furaha kukujulisha kuwa, Mkutano wa Nne wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza rasmi mjini Dodoma tarehe 7 Juni, 2011. Mkutano huu utakuwa wa Bajeti hivyo macho na masikio ya watu wengi yatakuwa yameelekezwa Dodoma kwa ajili ya kupata kile ambacho Serikali imekiandaa na kitakachopitishwa na Bunge kwa ajili ya mwaka wa fedha 2011/12.Kama ilivyo kawaida tunategemea chombo chako kitatuma Wanahabari Dodoma kwa ajili ya habari za Mkutano huo.Ofisi ya Bunge kila mara imekuwa ikitamani kupata toka kwako Wanahabari wenye uzoefu na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya Bunge zikiwemo kanuni na taratibu zinazotawala chombo uendeshaji wa chombo hiki.Aidha, ili kuwa na uratibu mzuri wa shughuli za utoaji Habari za Bunge, mwaka 2008 Wanahabari waliamua kuunda umoja wao kwa ajili ya kuwaunganisha katika shughuli hizi. Umoja huo uitwao Bunge Press Association of Tanzania (BUPAT) pamoja na mambo mengine unalenga kuwajengea uwezo Wanahabari na uwelewa mpana wa masuala ya Bunge.Ni nia ya Ofisi ya Bunge kuuendeleza umoja huo ili hatimaye kujenga kada ya Wanahabari waliobobea katika utoaji wa Habari za Bunge. Katika kutekeleza azima hii, ofisi inaandaa mpango wa mafunzo utakaojumuisha semina, warsha na ziara za mafunzo katika Mabunge mbali mbali kwa Wanahabari husika.Ni kwa misingi hiyo basi tumeona ni vyema tukapata ushirikiano wako katika hili na hivyo kukuomba kuwa kuanzia sasa unapoteua Wanahabari kwa ajili ya kwenda Bungeni wakidhi vigezo vifuatavyo:
  1. Wawe wamehudhuria Mikutano angalau mitatu

  2. Wawe na Press card inayotolewa na Idara ya Habari – Maelezo

  3. Wawe nadhifu, waadilifu na wenye nidhamu


Ili kutuwezesha kufanya maandalizi ipasavyo (vitambulisho, nyaraka, n.k) tutashukuru ukitupatia majina ya Wanahabari watakaohusika angalau siku nne kabla ya kuanza Mkutano wenyewe.Tunatanguliza shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wako katika jambo hili.Pamoja na salaam toka ofisi za Bunge.


J.S. Mwakasyuka


Kny: KATIBU WA BUNGE


Friday, June 03, 2011

NHC kubomoa ofisi zao za Upanga

SHIRIKA LA NYUMBA LINAPENDA KUWAJULISHA WAPANGAJI WOTE KWAMBA KUANZIA TAREHE 01 JULAI, 2011 OFISI YA SHIRIKA LA NYUMBA ILIYOKO UPANGA ITAHAMISHIWA PLOT NO. 568/48 MTAA WA SAMORA, JENGO LA MATSALAMAT, GHOROFA YA KWANZA.

AIDHA HUDUMA ZOTE ZINAZOHUSU WAPANGAJI ZITATOLEWA KWENYE OFISI MPYA KUANZIA JULAI 01, 2011. WATEJA WATAENDELEA KULIPIA KODI YA PANGO KWENYE OFISI ZETU ZILIZOPO MTAA WA NKRUMAH.

TAWI LA UPANGA NI KUBWA KULIKO MATAWI YOTE YA SHIRIKA NA LINAHUDUMIA WAPANGAJI WENGI HIVYO NI VYEMA KUWA NA OFISI AMBAYO WATEJA WETU WATAPA HUDUMA ZENYE UBORA ZAIDI.

TUMEONA NI VYEMA KUWAARIFU WAPANGAJI WETU MAPEMA ILI KUWAONDOLEA USUMBUFU USIOKUWA WA LAZIMA.

KWA KUONA UMUHIMU WA SUALA LA MAKAZI SHIRIKA LIMEONA NI VYEMA KUTUMIA KIKAMILIFU THAMANI YA ARDHI ILIYOPO KATIKA ENEO HILI ILI KUWEZA KUWAPATIA WANANCHI MAKAZI ZAIDI.

JENGO LITAKALOJENGWA HAPA LITAKUWA NA SEHEMU ZA KUISHI TAKRIBAN 200 HIVYO WATU 1000 WATANUFAIKA KUISHI KATIKA ENEO HILI LITAKALOKUWA NA MIUNDOMBINU MUHIMU NA HUDUMA ZINGINE ZA KIJAMII KAMA VILE MADUKA, SEHEMU ZA KUCHEZA WATOTO, SEHEMU ZA KUEGESHA MAGARI NA KADHALIKA. HII NI KATIKA KUTEKELEZA AZMA YA KILIBADILISHA KABISA ENEO LA UPANGA.

KWA SASA ENEO LA UPANGA LINA WAPANGAJI 4,772 NA MAKUSANYO YA MWEZI NI ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA AMBAPO NI KARIBU ASILIMIA 40 YA MAKUSANYO YA KODI KATIKA MIKOA YOTE.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Ziara ya CCM Rukwa hebu cheki umati

Nape akisalimia wananchi , Kata ya Kabwe wilaya ya Nkasi baada ya kuwasili eneo hilo kwa ajili ya mkutano wa hadhara juzi.
Wananchi wa Kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wakimshangilia Nape wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo. Picha za Bashir Nkoromo wa gazeti la Uhuru.

Thursday, June 02, 2011

Maadhimisho wiki ya maziwaBaadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi za Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiandama kwenye barabara ya Kawawa kuadhimisha kilele cha wiki ya uhamasishaji unywaji wa maziwa.Picha na Zacharia Osanga