Sunday, November 28, 2010

Mke wa Mzee wa Mshitu apata nondooz


Mdau Eric Anthony ambaye ni Mhariri wa Habari wa HABARILEO (Jumamosi na Jumapili) akipozi na Mzee wa Mshitu, Yahya Charahani,kwenye ukumbi wa Mlimani City ambako Eric alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Taaluma za Maendeleo (Mipango na Utawala) wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.Picha ya John Bukuku.


Mzee wa Mshitu au Yahya Charahani wa Blogu hii akimvisha mkewe shada la maua baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika sanaa na elimu muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada hiyo na mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Balozi Fulgence Kazaura mahafari hayo alifanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana /Picha na Jackson odoyo

Wednesday, November 24, 2010

Baraza jipya la mawaziri

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI



OFISI/WIZARA
WAZIRI

NAIBU WAZIRI

1.Ofisi ya Rais



1. WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe

2. WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira


2.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

Hawa Ghasia

3.Ofisi ya Makamu wa Rais


1.Muungano

Samia Suluhu

2.Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa


4.Ofisi ya Waziri Mkuu


1.Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi

2.Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu


5.Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)


George Huruma Mkuchika

1.Aggrey Mwanri

2.Kassim Majaliwa


6.Wizara ya Fedha

Waziri

Mustapha Mkulo

Manaibu

1. Gregory Teu

2. Pereira Ame Silima

7.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Shamsi Vuai Nahodha

NAIBU
1.Balozi Khamis Suedi Kagasheki

8.Wizara ya Katiba na Sheria

Celina Kombani


9.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Bernard K. Membe

NAIBU

Mahadhi Juma Mahadhi

10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11.Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. Mathayo David Mathayo

NAIBU

1. Benedict Ole Nangoro

12.Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

NAIBU

1. Charles Kitwanga

13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna Tibaijuka
Goodluck Ole Madeye

14.Wizara ya Maliasili na Utalii

Ezekiel Maige

15. Wizara ya Nishati na Madini

William Mganga Ngeleja

NAIBU

1. Adam Kigoma Malima

16. Wizara ya Ujenzi

Dr. John Pombe Magufuli

NAIBU

Dr. Harrison Mwakyembe

17. Wizara ya Uchukuzi

Omari Nundu

NAIBU

Athumani Mfutakamba

18. Wizara ya Viwanda na Biashara

Dr. Cyril Chami

NAIBU

Lazaro Nyalandu

19.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru Kawambwa

NAIBU

Philipo Mulugo

20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Haji Hussein Mpanda

NAIBU
Dr. Lucy Nkya

21.Wizara ya Kazi na Ajira

Gaudensia Kabaka

NAIBU
Makongoro Mahanga

22.Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Sophia Simba

NAIBU

Umi Ali Mwalimu

23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo

Emmanuel John Nchimbi

NAIBU

1. Dr. Fenella Mukangara

24.Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Samuel John Sitta

NAIBU

1. Dr. Abdallah Juma Abdallah

25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Prof. Jumanne Maghembe

NAIBU
1. Christopher Chiza

26. Wizara ya Maji

Prof. Mark James Mwandosya

NAIBU
Eng. Gerson Lwinge

Sunday, November 21, 2010

Choo cha kwetu uswazi


Kwa wale wenzangu na mimi ambao ama wamewahi au wanaendelea kuishi katika vyumba vya kupanga katika maeneo yetu ya uswahilini, bila shaka wanazielewa ipasavyo adha wanazozipata na hususan pale unapowadia muda wa kwenda msalani.

Lakini kwa wale waliobahatika kuzaliwa katika familia zilizoneemeka hapa duniani, watakuwa hawanielewi ninapozungumzia adha ya vyoo vya uswahilini. Kwao vyoo ni vya kutumia maji ambayo husukuma uchafu kwa ustaarabu wa hali ya juu. Hakuna bughudha wala kinyaa chochote kwa watu hawa pindi waingiapo msalani. Hebu cheki choo hiki kilichopo karibu kabisa na katikati ya jiji Magomeni hapa halafu unambie.

Mzee Boziboziana mchawi wa Nzawisa ndani ya Bongo



Mwanamuziki kutoka nchini Congo, Bozoboziana (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Meneja wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta,Asha Baraka (wa pili kulia) walipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.Boziboziana yupo nchini kwa mafunzo maalumu kwa bendi ya Twanga katika kujitayarisha na soko la kimataifa.Picha na Venance Nestory.

Saturday, November 20, 2010

Dk Muterea afariki dunia



DK Absalom Mutere amezikwa leo mchana katika makaburi ya huko Musanda, Mumias, Kakamega Kenya. Alifariki ghafla akiwa safarini nchini Zambia ambako alikwenda kwaajili ya masuala yake ya kitaaluma. Dk ay Profesa Mutere ninamkumbuka sana kwa staili yake ya ufundishaji na kwa nondo zake alizotupatia katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino hasa darasa la Masters 2009.
Hakika fani ya mawasiliano ya Umma imepoteza gwiji lake ambaye alikuwa ni mtu asiyekuwa na mikwara na wala kinyongo hata kidogo, kufundisha kwake ilikuwa kama ni maji asipokunywa anakuwa na kiu.
***************************************


Mutere was educated in the UK, Uganda, Kenya and the USA. He held a BA in Political Science, MA in Journalism (Kent State University, USA), and a PhD from the University of Amsterdam.

He passed away on Tuesday 9 November in Lusaka, aged just 54. He leaves behind a wife, Chalwa Mutere, and two daughters, Ayanda and Julia, from a previous marriage.

He also leaves behind a rugby fraternity that will mourn his departure while celebrating his enormous contribution to the sport.

----------------------------------------------------------------------------
It is with humble acceptance of God’s will that we announce the passing away of Dr Absalom “Bimbo” Mutere in Lusaka, Zambia.

Loving husband of Chalwa Mutere. Father of Ayanda and Julia Mutere. Son of the late Prof Festo Abby Mutere and Mrs Melcah Ephalinah Mutere. Brother of Matilda Mutere, the late Anna Mutere, the late Jacqueline Mutere, Gillian Mutere and Flora Okuku. Brother-in-law of Greg Pirio and Tony Okuku, and uncle to several.


Body arrived in Nairobi on Wednesday, Nov 17, 2010. Friends, relatives and professional colleagues meet daily at Nairobi Railway Club.



Fundraiser took place on Tuesday, Nov 16, 2010 at same venue at 6pm. Burial on Saturday, Nov 20, 2010 at Musanda, Mumias, Kakamega County.



We will miss you terribly.

“A good name is better than precious ointment; and the dayof death than the day of one’s birth.” - Ecclesiastes 7:1.

Tuesday, November 16, 2010

Vodacom gets US $4.8 million to expand M-Pesa services


Vodacom Tanzania is to receive a 4.8 million US dollars grant from the Bill & Melinda Gates Foundation to augment financial inclusion in Tanzania through increased usage of its mobile money service, Vodafone M-PESA.
Vodacom Managing Director, Dietlof Mare, said that the grant aims to and will improve the lives of Tanzanians as Vodacom believes that financial inclusion is possible through the use of Vodafone M-PESA.
The grant, about 7.2 billion Tanzanian shillings, will be used to enhance and improve Vodafone M-Pesa services that a customer receives from an agent, Mare said.
“Vodacom will use the money to increase the awareness and service benefits of Vodafone M-Pesa specifically to those living in remote parts of the country”, he noted.
“Tanzania has a highly dispersed population of around 40 million, which severely restricts access to financial services. Today only two million Tanzanians have access to a bank account while over 18 million are mobile phone users,” he said.
Research in Kenya and Tanzania shows that many people find M-PESA provides a safe and affordable way to store and send money to friends, family and business associates.
According to Mare, Vodacom has been singled out to receive the grant because the company laid the groundwork for the uptake of mobile money transfer services in the country and has invested greatly in the technology.
To date over 5.3 million people have already registered to use Vodafone M-PESA in Tanzania.
Although it is ideally suited for those without access to financial services, it is the banked community that has been the quickest to take advantage of the convenience, security and efficiency it offers.
With funding from the Bill & Melinda Gates Foundation through the Financial Services for the Poor initiative, Vodacom will extend this service to reach the wider “unbanked” community.
This grant was announced on November 16 by Melinda French Gates at the Global Savings Forum in Seattle, Washington, as a part of the foundation’s $500 million pledge to expand access to savings accounts and help the world’s poor build financial security.
The pledge included a package of six grants, totaling $40 million, from the foundation’s Financial Services for the Poor initiative, to support projects and partnerships that will bring quality, affordable savings accounts and other financial services to the doorsteps of the poor in the developing world.
“Savings doesn’t just help people mitigate the risks posed by a medical emergency or a bad crop,” said Gates at the foundation-hosted event.
“It also gives them the ability to marshal their resources to build something better for themselves and their children. It allows them to fund their own businesses, to look ahead with confidence. Savings helps families to take the giant leap from reacting to events to planning for a healthier, happier future.”

Mbunge wetu Mary Mwanjelwa akiapa bungeni


Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa akiapa, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, November 15, 2010

Pinda umechakachuaa hahahahaha


Waziri Mkuu aliyemaliza muda wake, Mizengo Pinda akifurahia jambo na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa walipokutana nje ya ukumbi wa Pius Msekwa bungeni jana mjini Dodoma. Pinda alikwenda kujumuika na wabunge wenzake wa CCM waliokuwa na kikao cha kumteua mgombea wa Naibu Spika kwa tiketi ya chama chao. Picha na Edwin Mjwahuzi

Saturday, November 13, 2010

Spika mpya mama Makinda


MHESHIMIWA ANNE MAKINDA NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE BAADA YA KUMSHINDA MH. MGOMBEA MABERE NYAUCHO MARANDO KATIKA UCHAGUZI WA KUMPATA SPIKA MPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.


Idadi ya kura zilizopigwa = 327
Idadi ya kura zilizoharibika = 9

Mabere Marando amepata kura 53
Anna Makinda amepata kura 265

Wednesday, November 10, 2010

CCM WAFANYA MAPINDUZI WAWAPITISHA MAKINDA, ANNA ABDALLAH, KATE KAMBA USPIKA

Anna Makinda
Anna Abdallah
Kate Kamba
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.

Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.

Uzinduzi wa TV ya Sony 3D


Mkurugenzi Mkuu wa Sony Osamu Miura (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mauzo Afrika Mashariki Dinakaran Munaswamy (wa pili kulia) wakizindua TV ya Sony 3Djijini Nairobi leo.

Managing Director, Sony Gulf Mr. Osamu Miura(right) accompanied by a Sony model unveil the Sony 3D TV.

Managing Director, Sony Gulf Mr. Osamu Miura (second left) and East Africa Head of sales Mr. Dinakaran Munaswamy (second right) unveil the 3D Sony TV accompanied by Sony models.

Makamu wa Rais



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi Makamu wa Rais (Mazingira), wakati alipofika ofisini hapo kusaini kwa mara ya kwanza na kuanza kazi rasmi Nov 08. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel.( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Sunday, November 07, 2010

Rais Kikwete aapishwa aanza ngwe




RAIS Jakaya Kikwete jana aliapishwa kuiongoza Tanzania kwa kingine cha miaka mitano ijayo na kutoa wito kwa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali yake katika kuimarisha demokrasia na kudumisha amani nchini.
Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu Augustino Ramadhan katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete ambaye alipata ushindi wa asilimia 61.17 ambayo ni chini zaidi ya ushindi aliopata mwaka 2005, alisema wapinzani waliifanya CCM kujituma zaidi na mahali pengine kulazimika kufanya kazi ya ziada wakati wa kusaka ushindi.
"Siwezi kuacha kuwatambua wagombea wenzangu sita tuliowania nafasi ya uongozi wa juu kabisa wa nchi yetu, nawashukuru kwa kutuchangamsha wakati wa kampeni, mmetufanya tujitume zaidi na mahali pengine tufanye kazi ya ziada.

Thursday, November 04, 2010

Vodacom yatangaza zawadi za Mwanza Cycle Challenge



Vodacom Tanzania imetangaza zawadi zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki mashindano ya baiskeli ambayo yatafanyika Jijini Mwanza mwezi huu yanayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza naWaandishi wa Habari, Jijini leo, katika makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi.

“Mashindano haya yameboreshwa kwa upande wa zawadi, ubora na viwango,” alisema.

Aidha alifafanua kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa siku mbili yaani Novemba 12 na 13 mwezi huu na kwamba tarehe 12 itakuwa maalumu kwa mashindano ya walemavu ambao watashindana kilometa 15 kwa wanaume na 10 kwa wanawake. Na tarehe 13 Novemba yatafanyika mashindano ya kilomita 196 kwa wanaume, 80 kwa wanawake ambapo kwa upande wa walemavu ni Kilometa 15 kwa walemavu wanaume na Kilomita 10 kwa walemavu wanawake.

Akitangaza zawadi hizo kwa washiriki wa mbio za kilometa 150 Mtingwa alisema mshindi wa kwanza atajipatia shilingi 1,500,000, wa pili kiasi cha 1,000,000, wa tatu 700,000, ambapo mshindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atajipatia shilingi 500,000 kila mmoja. Aidha kwa upande washindi wa 11 hadi 20 kila mmoja atajinyakulia kitita cha 250,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 90,000 kila mmoja.

Kwa upande wa mbio za mita 80 kwa wanawake mshindi wa kwanza pia atajipatia zawadi ya shilingi milioni 1,100,000, wa pili 800,000, mshindi wa tatu 600,000, wakati washindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atazawadia kiasi cha shilingi 350,000 kila mmoja. Vilevile washindi watakaoshika nafasi ya 11 hadi ya 20 katika mbio hizo watapewa jumla ya 130,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 70,000 kila mmoja.

Mbali na hayo Mtingwa alibainisha kwamba kwa upande wa mbio za kilometa 10 ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu alisema washindi wa kwanza wawili kila mmoja atajipatia jumla ya shilingi 400,000.

Kwa washindi wa pili wawili nao watajishindia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja, washindi wa tatu wawili kila mmoja atapewa kiasi cha 150,000 kila mmoja wakati washindi wa nne wane hadi wa kumi watajipatia kitita cha 70,000 kila mmoja.

Wednesday, November 03, 2010

TEMCO: Wakuu wa mikoa na wilaya waliisaidia CCM kampeni



Mwenyekiti wa kamati ya uangalizi wa uchaguzi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (TEMCO) Profesa Rwekaza Mukandala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya awali ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambapo ripoti hiyo inaeleza kuwepo kwa mapungufu kwa baadhi ya maeneo ingawa inaeleza ulikuwa huru, kulia ni makamu mwenyekiti Temco Maryam Abubakar. Picha na Said Powa

*********************************************************************************

TIMU ya Waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu (Temco) imetoa tathmini yake ya awali kuhusu uchaguzi huo uliofanyika Oktoba31, ikionyesha kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya walikisaidia chama tawala katika kampeni zake.
Temco pia imeonyesha kuwepo kwa dalili za kuvunjwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi kutokana na baadhi ya vyama kutoa mabango mengi na vifaa vingine vya kampeni hizo vyenye gharama kubwa.
Katika taarifa yake hiyo ya awali mbele ya wanahabari jana Temco kupitia mkwenyekiti wake, Profesa Rwekaza Mukandala imetaja kuwepo kwa vitendo vilivyotishia uvunjifu wa amani na vurugu ikibainisha kuwa vyama vya CCM, Chadema na Cuf kuhusika.
“Mambo yasiyofaa yaliyobainishwa na timu ya waangalizi wa Temco si mageni, lakini yameonekana kuchukua nafasi kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu,”alisema Profesa Mukandala na kufafanua:
Wakuu wa mikoa na wilaya walitumia rasilimali za taifa kama magari katika kampeni za urais kumsaidia mgombea anayetetea nafasi yake.”
Mwenyekiti huyo wa Temco aliongeza kuwa mara kadhaa katika kampeni zake mgombea urais huyo alitumia nafasi yake kama kiongozi wa nchi kutoa au kubadili uamuzi wa serikali kama ahadi kwa wapiga kura ili kujipatia wapiga kura jambo ambalo wagombea wengine hawakuweza kulifanya.
Temko ilitembelea majimbo 135 kati ya 223 ikiacha majimbo ya uchaguzi ambayo wagombea wake walipita bila kupingwa na kutoa alama A mpaka E kwa majimbo.
Mukandala alisema kuwa mgombea kutoa ahadi si jambo baya lakini kutoa ahadi au uamuzi kutumia madaraka aliyonayo mtu ili kuvuna wapiga kura syo jambo sahihi.
Wakati wa kampeni za kuwania urais, ubunge na udiwani kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumapili iliyopita, vyama vya upinzani vililalamikia baadhi ya wagombea nafasi hizo kutumia nyadhifa zao kutoa ahadi kwa lengo la kuvuna wapigakura.
Akizungumzia uvunjaji sheria ya gharama za uchaguzi, mwenyekiti huyo wa Temco alisema kuwa, “Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza kufanyika chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi uliolenga kudhibiti matumizi makubwa ya fedha, lakini kumekuwepo na vifaa vingi vya gharama kubwa kwa vyama vikubwa hasa chama tawala CCM.”...
Imeandikwa na Exuper Kachenje: SOURCE: MWANANCHI

Nyalandu aibuka na ushindi mnono



MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweza tena kurejea madarakani baada ya kuibuka na jumla ya kura 46,869 ikiwa ni asilimia 91 ya kura zote.

Nyalandu ambaye amekuwa mgombea ubunge wakwanza nchini kutumia helkopta katika kampeni aliwabwaga wapinzani wake Msaghaa Kimia kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipata kura 3,544 wakati Sizimwe Kanyota wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 550.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa jana, Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Iliminata Mwenda alisema jumla ya wapigakura waliojiandikisha walikuwa 90,045 wakati waliopiga kura ni 46,869 katika jimbo hilo.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nyalandu alisema kuwa wananchi wa Singida Kaskazini wamempa heshima kubwa kwa kuonyesha kumwamini na kuwa yuko tayari kuendeleza mambo aliyoyafanya kipindi kilichopita na kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.

Rais wa awamu ya saba wa Zanzibar


Rais Jakaya Kikwete, akimpongeza Rais wa Mpya wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya kuapishwa kuwa rais wa saba wa visiwa hivyo katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Amani Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar awamu ya saba,Dk Ali Mohamed Shein, akiapa kuwa rais wa visiwa hivyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Aman Unguja jana, anayeshuduhua kushoto ni aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume.

Rais wa Zanzibar awamu ya saba,Dk Ali Mohamed Shein, kiapa kuwa rais wa visiwa hivyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Aman Unguja jana, anayeshuduhua kushoto ni aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume.

Tuesday, November 02, 2010

Mtikisiko kufanyika Mbeya na Iringa





TAMASHA la Mtikisiko linalotarajiwa kufanyika katika mikoa ya Iringa na Mbeya, litafanyika Novemba 6 kwa Mbeya, Uwanja wa Sokoine, wakati Iringa litafanyika Novemba 13, huku kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzanzania, ikidhamini kwa Sh Milioni 22.

Tamasha hilo limeandaliwa kwa mara ya nne mwaka huu na Ibony Entertainment ya mkoani Iringa na kupewa jina la ‘Bata Mrefu’, kwa nia ya kuwakutanisha viijana na wapenzi wa mambo ya burudani, huku pia likiwakutanisha vijana na kujadiliana vitu vinavyowakabili.

Akizungumza na Gazeti hili, Mwakilishi wa tamasha hilo, kutoka Ibony, Leah Mbeyale, alisema kwamba tamasha hilo litashirikisha wasanii mbalimbali, wakiongozwa na bendi inayotamba kwa sasa, The African Stars Twanga Pepeta.

Pia kutakuwapo na michezo mingine, ikiwamo Pool table na masumbwi, huku wakiamini kwamba onyesho la mikoa miwili, litatumika kama sehemu ya kufurahia burudani za tamasha hilo lenye mguso mkubwa kwa mashabiki wa burudani.

Kwa mujibu wa Leah, tamasha hilo la Mtikisiko, limepiga hatua kubwa baada ya kufanikiwa kuongeza mikoa ya kufanya tukio hilo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuongeza hamasa kwa wote watakaohudhuria.

“Tangu lianzishwe tamasha hili, limekuwa na mguso mkubwa mkoani Iringa, kitu kilichotuongezea hamasa na hamu ya kuona mikoa mingine wanapata fursa ya kusherehekea tukio hilo lenye dira na mguso kwa wadau wote wa Mbeya na Iringa.

“Wadau waje kwa wingi, kwani kiingilio ni cha chini kabisa, Sh 5,000 huku ulinzi ukiwa wa kutosha wakati wote wa tamasha hilo, Novemba 6 huko Mbeya na hata Iringa pia kila kitu kitawekwa sawa ili kuwapatia kitu kizuri wadau wa mambo ya burudani kutoka kwetu,” alisema Leah.

Naye Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, alifurahia kudhamini tamasha hilo, huku akisema kwamba litakuwa maalumu kwa wadau wao, kuifahamu vyema Vodacom na kusherehekea pia miaka 10, tangu kuanzishwa kwake.

“Siku zote Vodacom inapenda kushirikiana na wadau wake katika mambo yote, huku wakiamini kwamba ndio fursa pekee ya kuwatumikia na kujitangaza kwao katika kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa,” alisema Kiswaga.

Ukiacha Twanga Pepeta, pia wasanii wengine wa Bongo Fleva, akiwamo Juma Nature, Temba, Chege, Niki wa 2, Barnabas, Loma, Izo B na wengineo, ambao wote kwa pamoja watahakikisha kwamba mambo yanakwenda vyema, huku waandaaji wakitafuta uwezekano wa Joseph Mbilinyi, Mr Two, aliyeshinda ubunge, anakuwapo kwenye tamasha hilo la Mbeya.