Showing posts with label taarifa. Show all posts
Showing posts with label taarifa. Show all posts

Monday, October 31, 2011

APPOINTMENT OF DR. MARINA A. NJELEKELA AS EXECUTIVE DIRECTOR OF MUHIMBILI HOSPITAL




DR. MARINA A. NJELEKELA

This is to inform the general public that the Muhimbili National Hospital Board of Trustees has appointed Dr. Marina Aloyce Njelekela as the Executive Director of the Hospital with immediate effect. Before her appointment, Dr. Njelekela was a Senior Lecturer and Head of the Department of Physiology at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS).

Dr. Njelekela has worked with MUHAS since 2001 and prior to that, she had worked at Kisarawe District Hospital as a Medical Officer and at the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) as a Registrar until 1998 when she went for further studies in Japan.

Dr. Marina Njelekela holds a Doctor of Medicine Degree from the Univeristy of Dar es Salaam, and a PhD in Human and Environmental Studies from Kyoto University, Japan. Her area of specialization was Pathogenesis of Lifestyle Related Diseases in Developing countries.

As a team player, Dr. Marina Njelekela led the Medical Women Association of Tanzania (MEWATA) for six years. During her two terms as a MEWATA leader, she was in the forefront of health awareness among women and the general public, especially on Breast Cancer Awareness and Screening Campaigns that were conducted in Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, and Manyara.

She is also well known for her role in advocacy campaigns and has brought to light the real extent of the problem of breast and cervical cancers in Tanzania that led to significant improvement on the prevention and management of Cancers in the country.

Dr. Njelekela sits on various Boards, including the Aerial Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiatives (AGPAH) and Management Development for Health (MDH). She is a recipient of various awards in academia and social services, including the prestigious Martin Luther King Drum Major Award for Justice that was bestowed on her by the US Embassy in January 2010 for her efforts to improve women’s access to health care services.

Thursday, October 13, 2011

Prince Charles Kutembelea Tanzania



THE PRINCE OF WALES AND THE DUCHESS OF CORNWALL TO TOUR COMMONWEALTH AND GULF COUNTRIES
The British Government has asked The Prince of Wales and The Duchess of Cornwall to undertake official visits to South Africa and Tanzania from 2nd November to 9th November 2011 at the invitation of President Zuma and President Kikwete. The Prince of Wales will also visit Gulf countries on 31st October and 1st November. In Kuwait HRH will celebrate the 50th anniversary of Independence and 20th anniversary of liberation as the guest of the Amir and the Crown Prince. The Prince of Wales will stop briefly in Qatar for discussions with the Emir before departing for the Commonwealth countries.
Their Royal Highnesses’ Commonwealth tour will focus on trade and investment promotion to support Britain’s economic recovery and strengthen the economies of our partners; employment opportunities and development issues; education and practical support for disadvantaged young people; sustainability issues in the run-up to the Durban Climate Summit later in November; and shared heritage and conservation of traditional livelihoods and wildlife. In Tanzania the Royal visit will be part of the celebrations for the 50th anniversary of Independence. Bilateral ties including economic cooperation will also be to the fore in Kuwait and Qatar.
In both Commonwealth countries there will be a strong focus on The World Wildlife Fund’s (WWF) work to protect endangered species and fragile ecosystems. The Prince of Wales has recently become President of WWF UK. In South Africa Their Royal Highnesses will visit the Mandela Foundation in Johannesburg to see the legacy of former President Mandela.
The work of the Department for International Development (DFID) will assume particular prominence in South Africa and Tanzania given the UK Government’s commitment to the development of both countries.

JK aongoza mazishi ya Penza

Mzee Athumani Janguo akimzika rafiki yake mzee Penza leo jioni
Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga Khamisi Mgejja akimzika bwana Penza

Nape Nnauye akishiriki katika Mazishi ya Penza
Rais Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Juma Penza jioni hii
Waombolezaji wakiwasili kwenye makaburi ya kisutu kwaajili ya maziko ya mkongwe huyo
Rais Kikwete akiwa na wajukuu wa marehemu Juma Penda kwenye makaburi ya Kisutu jioni hii

********************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, jioni ya leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011 ameungana na waombolezaji kumzika mwanahabari mkongwe, Ndugu Juma Fugame Penza katika makaburi ya Kisutu, mjini Dar es Salaam.

Ndugu Juma Penza alifariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 63.

Marehemu Penza ambaye amekuwa katika tasnia ya habari kwa karibu miongo minne iliyopita na miongoni mwa walioshiriki mazishi yake katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam ni pamoja na viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alichokifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 20.

Katika salamu za rambirambi ambazo Mheshimiwa Rais Kikwete amempelekea Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Wilson Mukama na kupitia kwake kwa familia na ndugu wa marehemu, Mheshimiwa Rais amemwelezea Hayati Penza kama mwandishi wa habari aliyefanya kazi zake kwa weledi na uzalendo akiongozwa na misingi imara ya taaluma yake na uzalendo kwa nchi yake.

“Nilimfahamu binafsi Ndugu Penza wakati tulipofanya kazi pamoja katika Chama cha Mapinduzi. Hakuna shaka kuwa Marehemu Penza aliitumia taaluma yake ipasavyo, akiongozwa na weledi wa kazi hiyo na uzalendo kwa nchi yake. Kamwe, hakupata kutumia ujuzi wa kazi yake kugawa wananchi kwa misingi ya aina yoyote ile.”

Katika maisha yake, marehemu Juma Fugame alishikilia nafasi za uandamizi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na kuwa Kaimu Mhariri wa Mazageti ya Serikali ya Daily na Sunday News, Kaimu Mkuu wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) kabla ya kujiunga na utumishi wa CCM.

Katika utumishi huo, Marehemu Penza alipata kuwa Mwandishi wa Habari wa Katibu Mkuu wa CCM, Mzee Rashid Mfaume Kawawa ambaye pia ni marehemu, Mwandishi wa Habari wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee John Malecela, Mkurugenzi wa Redio Uhuru na Afisa Mwandamizi wa masuala ya habari na vyombo vya habari katika makao makuu ya Chama.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,DAR ES SALAAM.

13 Oktoba, 2011



Monday, October 03, 2011

JK, Museveni kuharakisha ujenzi wa reli ya Tanga-Musoma-Uganda

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo ikulu jijini Dare s Salaam leo mchana.Rais Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
************
TANZANIA na Uganda zimekubaliana kuharakisha ujenzi wa reli ya Tanga-Musoma-Uganda ili kuhitimisha ndoto ya miaka mingi ya Mwanzilishi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilieleza kuwa hayo ndiyo yalikuwa maamuzi makuu yaliyofikiwa jana, katika mkutano kati ya Rais, Jakaya Kikwete na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kupanua bandari za Tanga na Musoma katika Tanzania, na kujenga bandari mpya nchini Uganda ili kuhudumia reli hiyo mpya kati ya nchi hizo mbili.

Rais Museveni ambaye amefanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania aliwasili jana asubuhi na kupokea na mwenyeji wake Rais Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kiongozi huyo wa Uganda ameondoka kurejea nyumbani baada ya mazungumzo na mwenyeji wake.

Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamekubaliana kuharakisha ujenzi wa reli hiyo kama njia ya kufungua mlango wa tatu wa Uganda kupitishia bidhaa zake kutoka na kwenda kwenye Bahari ya Hindi. Milango mingine inayotumiwa na Uganda kusafirisha bidhaa kutoka na kwenda Bahari ya Hindi ni bandari za Dar es Salaam na Mombasa, Kenya.

Katika kuhakikisha uamuzi wake wa kuharakisha ujenzi huo unaanza katika muda mfupi iwezekanavyo, viongozi hao wawili wameunda kikosikazi cha kusimamisha suala hilo. Kikosi kazi hicho kitaundwa na mawaziri wa wizara za usafirishaji na uchukuzi, fedha na mambo ya nje kwa kila nchi.

Chini ya mpango huo, bidhaa zitasafirishwa kwa reli kutoka Bandari ya Tanga hadi Bandari ya Musoma na kuwekwa kwenye pantoni maalum ya (wagon ferry) reli kutoka Bandari ya Musoma hadi bandari mpya ya Uganda kwa kuvushwa Ziwa Victoria.

Viongozi hao wamefanya uamuzi wa kuharakisha ujenzi huo kwa sababu ya faida za reli hiyo kwa chumi za nchi zote mbili lakini pia kwa kujua kuwa bila usimamizi wa karibu wa Tanzania na Uganda itachukua miaka mingi zaidi kwa reli hiyo kuweza kujengwa.

Wazo la kujenga reli ya kuunganisha Uganda na Bandari ya Tanga kupitia Bandari ya Musoma liliasisiwa miaka mingi tokea awamu ya kwanza ya uongozi wa Tanzania, lakini kwa namna moja ama nyingine, utekelezaji wa wazo hilo umekumbana na changamoto mbalimbali.

Katika mkutano wao wa leo, viongozi hao pia wamejadili masuala mengine yanayohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala mengine ya kikanda na kimataifa.
SOURCE: IKULU

Tuesday, September 27, 2011

Chadema Igunga: Pepople's Powerrrrrrr


Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Nkinga wa kuwania kiti cha Ubunge cha jimbo la Igunga baada ya kuwasili na Helkopta jana.Picha na Fidelis Felix

IGP Mwema apata ajali


IGP Said Mwema ((Pichani aliyenyoosha mkono) amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea jana (Pichani) iliyotokea barabara ya Kivukoni front mbele ya ofisi za takwimu na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa majira ya saa 8 mchana. Gari ya IGP ilikuwa inatokea magogoni iligongana na gari dogo (Saloon) T 960 AYK gari ya IGP iliumia sana upande wa mbele kushoto.
Picha na: DEUSDEDIT MOSHI WA DM.PHOTO SOLUTIONS (TZ)

Monday, September 26, 2011

Rais Kikwete arejea nchini


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda muda mfupi baada ya kuwasili kutoka New York Marekani ambapo pamoja na mambo mengine alihutubia baraza la Umoja wa Mataifa. Kushoto no Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick
(picha na Freddy Maro).

Friday, September 23, 2011

Michael Sata ni Rais mpya wa Zambia

Kiongozi wa upinzani Micheal Sata ametangazwa kuwa rais mpya wa Zambia mapema hii leo baada ya uchaguzi uliokumbwa na vurugu zilizosababisha vifo vya watu wawili.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ilisema Sata alishinda asilimia 43 ya kura dhidi ya asilimia 36 za rais anayeondoka Rupiah Banda licha ya kuwa vituo 7 kati ya 150 vya upigaji kura nchini humo vilikuwa bado vinaendelea kuhesabu kura hizo.

Tume hiyo ya uchaguzi ilisema kuwa idadi ya wapiga kura katika maeneo hayo ni ndogo ikilinganishwa na kura laki moja elfu 88 zilizo watofautisha wagombea hao wawili. Wagombea wengine 8 waligawanya kura zilizosalia.

Jaji mkuu Ernest Sakala alimtangaza Micheal Chilufya Sata kuwa rais aliyechaguliwa wa jamhuri ya Zambia.

Punde baada ya kutolewa tangazo hilo muda mfupi baada ya saa sita usiku kuamkia leo, wafuasi wa Sata walimiminika barabarani katika mji wa Lusaka wakisherehekea huku wakipiga honi za magari.

Polisi ya kupambana na fujo ilikuwepo ikitazama wafuasi hao wakisherehekea.

Ilisema kuwa watu wawili waliuawa hapo jana katika vurugu zilizozuka baada ya wafuasi wa Sata kulalamikia utaratibu na udanganyifu katika zoezi la kuhesabu kura hizo.

Waangalizi wanasema hawajapata ushahidi wa kuthibitisha tuhuma hizo za udanganyifu huku waangalizi wa Umoja wa Ulaya wamekilaumu chama cha Banda MMD, kwa kutumia vibaya rasilimali za serikali, zikiwemo vyombo vya habari na magari wakati wa kampeni.

Hii ilikuwa ni mara ya nne kwa Sata kugombea wadhifa wa rais na ushindi wake unakifanya chama chake cha Patriotic Front kuwa chama cha tatu pekee kuingia uongozini tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo mwaka 1964.

Chama cha Banda ambacho Sata alikuwa mwanachama hadi mwaka 2001 kufuatia mzozo wa uongozi, umekuwa uongozini kwa miongo miwili.

Licha ya kuwa kiongozi huyo mpya ni mwenye umri wa miaka 74, mvuto wake ulikuwa zaidi kwa vijana nchini humo na watu wasiokuwa na ajira, wanaoona kuwa wametengwa kutoka biashara ya uchimbaji madini ya shaba nchini humo iliyoufanya uchumi wa nchi hiyo kuwa mojawapo ya unaofanya kazi vizuri Afrika.Biashara hiyo imesaidia kuundwa nafasi laki moja za ajira nchini Zambia na serikali imejenga madaraja, viwanja vya ndege hospitali kutoka fedha zinazopatikana kwa uchimbaji madini ya shaba.

Sata alikuwa gavana wa jimbo na waziri bungeni, alishindwa kwenye uchaguzi mnamo mwaka 2001 na pia mwaka 2006 kwa Levy Mwanawasa wa chama hicho cha MMD. Na baadaye mwaka 2008 wakati Mwanawasa alipofariki kutokana na kiharusi, Sata alishindwa na Banda ambaye aliyekuwa makamu wa rais wa Mwanawasa, kwa tofauti ndogo ya kura kwenye uchaguzi maalum uliofanyika.

Rais Kikwete akisalimiana na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika maongezi mafupi na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil jijini New York ambako wote wanahudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtabulisha Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue kwa kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil
kwa kina hebu watembelee
http://mawasilianoikulu.blogspot.com/2011/09/rais-kikwete-akisalimiana-na-kiongozi.html

Wednesday, September 21, 2011

Ubalozi wa Marekani wadhamini wasanii washiriki wa tamasha la Mtemi Milambo


Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.
Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.
Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru
Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.
Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.
Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.
Aksanteni kwa kunisikiliza.
Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.
www.chiefpromotions.or.tz
0755 638 004/0655 638 004

MAGONJWA YASIYO AMBUKIZI YANAONGEZA UMASKINI-TANZANIA


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani katika majadiliano ya kufatufa njia muafaka na zenye gharama nafuu za kuudhibiti na kutibu magonjwa yasiyo ambukizi.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete. Waziri wa Afya na maendeleo ya jamii kutoka Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Mhe. Juma Duni Haji, amesema , magonjwa yasiyo ambukizi yanaendelea kuwa mzigo mkubwa hususani kwa familia maskini.
Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wamekutana kwa siku(jumatatu na jumanne) mbili kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu magonjwa manne ambayo si ambukizi. Magonjwa hayo ni Kansa, Kisukari, Ugonjwa wa Moyo na Ugonjwa wa Mapafu.
“Gharama za kutibu magonjwa haya ni mkubwa mno. Karibu kila familia ambayo imeathirika na moja ya magonjwa haya inatumia asilimia 40 ya kipato chao kugharamia matibabu. Haya ni magonjwa yanayosababisha familia nyingi kuwa maskini” akasema Waziri Duni ambaye ni kati ya mawaziri watatu walioambatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 66 wa Umoja wa Mataifa ambao unaanza siku ya jumatano..
Mkutano wa Kilele kuhusu magonjwa yasiyo ambukizi ni kati ya mikutano kadhaa ya kilele ambayo inafanyika kabla ya Mkutano Mkuu.
Kutoka na gharama kubwa ya kutibu magonjwa hayo, Waziri Juma Duni amesema, Tanzania inasisitiza umuhimu wa magonjwa hayo kuingizwa katika ajenda za Kimataifa za Maendeleo.
Akasisita kuwa ongezeko la magonjwa yasiyo ambukizi kumesababisha changamoto kubwa katika mfumo uliopo wa utoaji wa huduma za afya.
Akizungumzia uzoefu wa Tanzania , Waziri amesema serikali ilizindua mwaka 2009 mkakati wa kitaifa kuhusu magonjwa yasiyo ambukizi. Mkakati huo unalenga pamoja na mambo mengine kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya pamoja na utudhibiti wa magonjwa hayo.
Aidha akaainisha kwamba kama nchi, Tanzania inakabiliwa na changamoto mbili kwa pamoja. Changamoto hizo ni kukabiliana kwanza, na magonjwa yasiyo ambukizi na ya pili ni kukabiliana na magonjwa ambukizi.
Kutokana na changamozo hizo, Waziri Duni anasema kuwa si vema basi aina moja ya ugonjwa ikatiliwa mkazo na kupewa kipaumbele dhidi ya ugonjwa mwingine kwa kuwa yote yanashabihiana.
Aidha amezitaja changamoto nyingine zinazoikabili Tanzania kuwa ni ongezeko la kansa ya shingo ya uzazi, ongezeko la wagonjwa wa kisukari wa asilimia tano, uvutaji wa sigara kwa asilimia 10, ongezeko la watu wenye utizo wa kupita kiasi, unywaji wa pombe na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya sickle –cell kila mwaka.
Mwishoni wa Mkutano huo, viongozi wa kuu wa nchi na serikali walipitisha tamkio la kisiasa ambalo licha ya kukiri kwamba magonjwa hayo manne ni changamoto ya katika karne ya 21.Pia wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ( WHO)na wadau wengine kuandaa taarifa itakayowasilishwa kwa viongozi hao katika Mkutano Mkuu wa 67 wa Umoja wa Mataifa.
mwisho

Tuesday, September 20, 2011

Rais Kikwete apata tuzo,pia ashiriki shughuli mbalimbali New York

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe baada ya kuipokea. Nyuma ya Mh. Membe ni Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Maajar
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh. Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku. (Picha kwa hisani ya Ikulu)

Dk Kafumu akikampeni Igunga


Mgombea ubunge jimbo la Igunga mkoani Tabora, kwa tiketi ya CCM, Dk Dalaly Peter Kafumu akihutubia mkutano wa kampeni jana katika kata ya Mwisi jimboni humo.

Chadema wawashabikia waliomvamia DC



Wanachama wa CHADEMA mjini Igunga, jana walijawa na furaha kubwa wakati wakiwapokea wabunge wao waliokamatwa hivi karibuni na kuwekwa rumande mjini Igunga na baadae kuhamishiwa kituo cha polisi mkoani Tabora kwa kosa la kumsukasuka mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario. Wabunge hao ni Sylivester Kasulumbai, mbunge wa Maswa Mashariki, Suzani Kiwanga, ambae ni mbunge wa viti maalumu.

Monday, September 19, 2011

Rais Ali Mohammed Shein awapa pole Mtambwe


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaun Takao,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni, akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofili na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.

Waziri wa Ardhi,Makaazi,maji na Nishati Mhe Ali Juma Shamuhuna,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwamamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni.

ATUHUMIWA KESI YA MELI WAPEWA DHAMANA BILA KUJUA TAREHE YA KWENDA TENA KORTINI


Watuhumiwa wa kesi ya mauajia ya meli ya Mv Spice iliyotokea Septemba 10 mwaka huu katika eneo la Nungwi Kisiwani Unguja Mjini Zanzibar na kuuwa watu zaidi ya 200,wakifikishwa Mahakama Kuu ya Zanzibar,wa mbele ni Nahodha Msaidizi wa meli hiyo Abdalla Moh'd Ali (30) katikati ni Yusufu Suleiman Jussa (47) ambaye ni mmiliki wa meli hiyo na mwisho ni Simai Nyange Simai (27) ni msimamizi wa bandari ya Malindi .Picha na Jackson Odoyo

****************************
Watuhumiwa watatu kati ya wanne waliofikishwa kwenye Mahakama Kuu Mjini Zanzibar wiki iliyopita wakikabiliwa na kosa la uzembe na kusababisha vifo vya watu 203 waliokuwa wakisafiri kwa Meli ya MV Spice Islander na kuzama katika bahari ya Hindi, Septemba 10 2011, wamepewa dhana na haikutaja siku ya kurejea tena Mahakamani hapo.

Watuhumiwa waliopewa dhamana ni Abdallah Mohammed Ali(30) mkazi wa Bububu, ambaye ni Afisa Mkuu wa Meli ya MV Spice Islander, Yussuf Suleiman Jussa(47), mkazi wa Kikwajuni ambaye pia ni Mmoja wa Wamiliki wa Meli na Msimamizi Mkuu wa Mizigo katika meli hiyo na Simai Nyange Simai(27) mkazi wa Mkele, ambaye ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mamlaka ya Usafiri Baharini anayehusika na usalama wa abiria melini.

Watuhumiwa hao, Ijumaa iliyopita walirejeshwa rumande baada ya kuzuka mabishano ya kisheria ya kutaka wapewe dhama ama wasipewe, ambapo Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar Mh. George Kazi, aliamuru warejeshwe rumande hadi leo Jumatatu atakapotoa uwamuzi wake.

Walipofikishwa Mahakamani hapo hii leo, Wakili wa Utetezi Bw. Hamidi Ali Saidi Mbwezeleni aliiomba Mahakama iwaachie huru watuhumiwa hao ili tume iliyoteuliwa na Rais kuchunguza chanzo cha kuzama kwa meli hiyo iendelee na kazi yake la sivyo tume isitishe kazi yake hadi pale kesi itakapomalizika.

Wakili huyo amesema kuwa kutakuwa na utata kama watuhumiwa wataendelea kubaki rumande kwani watakosa haki yao ya msingi katika tume iliyoundwa na Rais wa Zanzibar wakati ikiendelea na kazi yake endepo itataka kupata taarifa ama maoni kutoka kwa watuhumiwa hao hivyo wakiwa mahabusu watakosa haki yao ya kujieleza mbele ya tume hiyo.

Amesema hivi sasa inaonekana kuna makundi mawili yanayofanya kazi moja kwa maana ya Mahakama na Tume jambo ambalo alisema litakuwa na utata na lenye makusudio ya kuwalinda baadhi ya watu fulani.


Waziri Maghembe afanya ziara ya ghafla sokoni


Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akinunua sukari ya kilombero katika Soko la Kipati, Mbagala Jijini Dar es Salaam leo. Sukari hiyo ilikuwa ikiuzwa Shilingi 1,900 kwa kilo moja.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa Bwana Harshid Chavda mwakilishi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero kuhusu kiwango cha uzalishaji kwa siku na kiasi kinachouzwa kwa wasambazaji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kila siku wakati Waziri alipofanya ziara ya dharura katika ofisi za kiwanda hicho, Gerezani Jijini Dar es Salaam.

Sunday, September 18, 2011

Soko jingine laungua Mbeya


Soko hilo likiungua kwa moto ambao bado haujafahamika chanzo chake.

SOKO dogo lililopo eneo la Forest ya zamani, karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu Huria jijini Mbeya, limeteketea kwa moto jana usiku. Inadaiwa moto huo ulianza majira ya saa 3 za usiku na kudhibitiwa na zimamoto kabla ya kuleta madhara zaidi.

Tukio hili limetokea ikiwa ni siku moja kutoka soko lingine la Mwanjelwa eneo la SIDO kuteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa. Matukio haya yanayotokea jijini Mbeya yanaacha maswali mengi kwa wananchi kiasi cha kuhoji 'KUNANI MBEYA ?'

Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog

Dua wa kuwaombea wahanga wa Mv Spice Island


Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wilayani Arusha wakiwa katika dua ya pamoja katika ukumbi wa CCM mkoa wa Arusha ili kuwaombea marehemu na waathirika wa ajali ya meli ya MV Spice Island iliyotokea mjini Zanzibar wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 204 na kujeruhi zaidi ya 500,katika dua hiyo pia jumla ya shilingi milioni 3.6 ilichangishwa kama rambirambi ya ajali hiyo(Picha na Happy Lazaro).

Mambo ya vurugu Igunga


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) ambaye pia ni mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akimuonyesha afisa wa polisi kioo cha nyuma cha gari aina ya Toyota Prado T 888 ALL lililorushiwa mawe jana katika kijiji cha Nkinga kati na vijana wanaodhaniwa ni wafuasi wa Chadema. (Picha na Daniel Mjema)

TAWIRI YASHIRIKI MKUTANO WA KIMKAKATI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt. Eblate Mjingo ni miongoni mwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wanaoshiriki  mkuta...