Wednesday, December 30, 2015

RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ATEUA MAKATIBU WAKUU, MANAIBU MAKATIBU WAKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JIONI HII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam jioni ya leo December 30, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kumkabidhi  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akishuhudia.
PICHA NA IKULU














Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue
  1. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)
  1. Ofisi ya Makamu wa Rais
            Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
            Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)
  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)
  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)
  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)
  1.  Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Katiba na Sheria
Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)
  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)
  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
  2. Job D. Masima (Katibu Mkuu 
  3. Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU


30 Desemba, 2015

No comments: