Wednesday, July 01, 2026

RAIS DKT. SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.



Viongozi, wafanyabiashara pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 30 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza historia ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 1, 2026, ameongoza Maadhimisho ya Miaka 30 ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwasili katika ukumbi huo, Rais Samia alitembelea maonesho maalumu yaliyoandaliwa na TRA na kupata maelezo kuhusu historia ya mamlaka hiyo, mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 30 pamoja na mchango wake katika kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.

Maadhimisho hayo yamewakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi za umma na binafsi, wadau wa kodi pamoja na washirika wa maendeleo kwa lengo la kuadhimisha mafanikio ya TRA tangu kuanzishwa kwake na kujadili mikakati ya kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Kwa kipindi cha miaka 30, TRA imeendelea kuwa mhimili muhimu katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, hatua iliyowezesha Serikali kugharamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, miundombinu, maji na huduma nyingine za kijamii.

Maadhimisho hayo pia yametoa fursa ya kutafakari mafanikio yaliyofikiwa, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuifanya TRA iendelee kuwa taasisi imara, bunifu na inayotoa huduma bora kwa walipakodi, sambamba na kuimarisha uchumi wa Taifa.

RAIS DKT. SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya M...