WAZIRI WA MAMBO YA NJE,BALOZI AUGUSTINE MAHIGA ATEMBELEA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA NA LAKI LAKI ARUSHA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia Kaaya(kulia) akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(kushoto)katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku |
Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi akizungumza jambo mbele Waziri Augustine Mahiga aliyefika katika kituo hicho tangu ateuliwe kushika wadhifa huo. |
Baadhi ya watumishi wa AICC |
Mkuu wa mawasiliano serikalini,Mindi Kasiga akiongoza kipindi cha maswali kwa waandishi wa habari. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa ,Balozi Augstine Mahiga amesema eneo la Laki Laki lililopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa taasisi za kimataifa utaifanya Tanzania kung’ara duniani.
Balozi Mahiga alisema hayo Desemba 19 baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo na Kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC .
Eneo hilo litajengwa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari(MICT)Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR) na taasisi zingine na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Akiwa kwenye kituo cha AICC alipokea taarifa za mradi wa ujenzi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kilimanjaro International Convention Center kitachovuta dunia Tanzania.
Pia Waziri alizungumzia hali ya kisiasa nchini Burundi kuwa inaigusa Tanzania na kuwa atawasiliana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera kuandaa kuandaa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
Comments